Home » » WALIMU SHULE ZA MSINGI IRAMBA WATISHIA KUFANYA MAANDAMANO IWAPO HATAREJESHEWA MAKATO YAO.

WALIMU SHULE ZA MSINGI IRAMBA WATISHIA KUFANYA MAANDAMANO IWAPO HATAREJESHEWA MAKATO YAO.




Mwenyekiti wa chama cha walimu Tanzani (CWT) mkoa wa Singida Allan Jumbe akizungumza na waandishi wa habari wakati akitoa salamu zake za mwaka mpya wa 2012.
Jengo la CWT mkoa wa Singida. (Picha zote na Nathaniel Limu).
Na Nathaniel Limu.
Walimu wote wa shule za msingi wilayani Iramba mkoa wa Singida wameonya kwamba iwapo hawatarejeshewa zaidi ya shilingi 27 milioni walizokatwa kimakosa  kama malipo ya pango la nyumba miaka kumi iliyopita, watafanya maandamano makubwa na ya aina yake kushinikiza marejesho hayo.
Wamedai kwamba kama hawatarejeshewa fedha hizo hadi mwishoni mwa mwezi huu, wataacha kufanya kazi na kwenda makao ya wilaya ambayo ni New Kiomboi, na kufanya maandamano hayo.
Akitoa salaam za CWT za mwaka mpya wa 2012 kwa walimu wote wa mkoa wa Singida kupitia vyombo vya habari Mwenyekiti wa Chama cha walimu Tanzania (CWT) mkoa wa Singida Allan Jumbe amefafanua kuwa zaidi ya miaka kumi iliyopita, walimu wengi wa wilaya ya Iramba, walikatwa kwa makosa fedha za pango la nyumba (house rent).
 Jumbe amesema wakati wanakatwa fedha hizo, walimu hao walikuwa wamepanga nyumba za watu binafsi na walikuwa wakilipa pango la nyumba hizo kwa fedha zao.
Hawakuwa wamepanga nyumba za serikali kwa hiyo hawakustahili kukatwa fedha za pango na mwajiri wao.
Katika hatua nyingine, Mwenyekiti huyo ametumia fursa hiyo kumshukuru Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Manyoni, kwa madai kwamba kwa kipindi chote cha mwaka jana, hapakuwa na tatizo.
Habari kwa hisani ya Mo Blog

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2011. Singida Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogz za Mikoa