Home » » Tunamwonea bure Jaji Warioba

Tunamwonea bure Jaji Warioba

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Nchi hii kwa kweli ina visa sijawahi kuviona mahali kwingine katika dunia hii. Ni nchi ya ajabu na sijui ilikuwaje nikaishi humu.
Kuna mambo mengi yanayotokea na kunilazimisha baadhi ya nyakati kulaani kwa nini nimekuwa Mtanzania, yaani inachosha sana.
Hivi sasa kuna hizi harakati za kutafuta Katiba mpya hapa nchini. Iliundwa tume maalumu ya kutusaidia kupata katiba hiyo.
Watu kutoka makundi mbalimbali wakateuliwa, wakiwamo wanasiasa kutoka chama tawala cha CCM na hata vyama vya upinzani. Makundi mengine nayo yakashirikishwa ipasavyo. Baada ya kumaliza kazi yake, tume hiyo iliyokuwa ikiongozwa na Mzee Joseph Warioba ilikabidhi rasimu zake kwa Serikali na kwa wananchi kwa jumla.
Sasa kioja kimeanza kutoka kwa wanasiasa hasa wale wa CCM ambao kila siku wanamsimanga mzee wa watu bila sababu yoyote.
Kila siku Mzee Warioba yuko midomoni mwao wakimlalamikia kwa hili ama lile.
Utafikiri kuwa maoni yaliyomo kwenye rasimu yaliandaliwa na Mzee Warioba chumbani. Tume ilikuwa na wajumbe kibao tena wengine ni kutoka CCM, lakini mzigo wote ni Warioba, kila mtu Warioba kama vile yeye ndiye aliyetengeneza rasimu hiyo.
Kama CCM hawakubali mawazo ya wananchi waliyotoa kwa wajumbe wa tume, basi wasimwonee Warioba pekee, wawe pia wanawataja wajumbe wengine tunaojua kuwa nao ni CCM wa damu.
Huyu mzee kaitumikia nchi hii kwa uadilifu mkubwa, jamani aachwe apumzike kwa amani. Kwa nini tumchoshe?
Chanzo;Mwananchi

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2011. Singida Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogz za Mikoa