Home » » DC MSAMBYA ATAKA WATAALAMU WA KODI MGODINI

DC MSAMBYA ATAKA WATAALAMU WA KODI MGODINI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

MKUU wa Wilaya ya Ikungi mkoani Singida, Manju Msambya, ameiagiza Halmashauri ya Wilaya hiyo kupeleka wataalamu wa kodi na kuweka viwango vya ushuru katika mgodi wa machimbo ya dhahabu ya Muhintiri.
Akizungumza na viongozi na watendaji wa Halmashauri hiyo, Msambya, alisema ili kuiwezesha Halmashauri hiyo ni vema viongozi hao wakaweka wataalamu wa kodi watakaokusanya mapato ya ndani, ili waweze kukamilisha baadhi ya miradi badala ya kuendelea na utamaduni wa kutegemea fedha za Serikali kuu.
Aidha, alisema eneo la machimbo hayo lina mzunguko mkubwa wa fedha, hivyo kuhitaji kuangaliwa na kuhakikisha ulinzi na usalama wa wananchi na mali zao unakuwa wa uhakika na kuongeza kuwa, mgodi huo bado haujawa rasmi hivyo ni vema kufuatilia mapato.
Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Celestine Yunde, alimwagiza mkaguzi wa ndani kukagua miradi ya maendeleo iliyopo vijijini na kuwasilisha taarifa.
Chanzo:Tanzania Daima

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2011. Singida Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogz za Mikoa