Home » » WALIMU WAKOSA VYOO

WALIMU WAKOSA VYOO

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

WALIMU wa Shule ya Sekondari ya Kata ya Mandewa katika Halmashauri ya Manispaa ya Singida hawana vyoo kwa miaka nane sasa, halia ainayowalazimu kutumia vyoo vya wanafunzi.
Kufuatia hali hiyo, Rais wa Shirikisho la Wachimbaji wa Madini Tanzania (FEMATA), John Bina, ameingilia kati na kutoa sh. 500,000, lori 10 za mchanga na vifaa kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa vyoo hivyo.
Akizungumza juzi kwenye mahafali ya nne wa kidato cha nne kwenye shule hiyo, Bina ambaye alikuwa mgeni rasmi alionekana kuguswa na hali hiyo na kuamua kuendesha harambee ya papo kwa hapo.
Mara baada ya Bina kuanzisha harambee hiyo, Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Tawi la Singida, Emmanuel Kingu alitoa mifuko 20 ya saruji, mwenyekiti wa kamati ya shule alitoa mifuko 10 ya saruji na Diwani wa viti maalum wa Kata hiyo, Sara Alute alitoa mifuko miwili.
Mapema katika taarifa ya shule, pamoja na mambo mengine mkuu wa shule hiyo, Magreth Misanga alisema shule hiyo inakabiliwa na tatizo la ukosefu wa vyoo vya walimu.
Misanga alisema shule hiyo iliyoanzishwa mwaka 2006 kwa michango ya nguvu za wananchi na hadi sasa ni miaka nane hawana vyoo vya walimu na hivyo kujikuta wakitumia vyoo vya kantini ya shule pamoja na watu wengine.
Shule hiyo ina wanafunzi 381, ambapo kati yao wavulani ni 204 na wasichana 177.
Chanzo:Tanznia Daima

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2011. Singida Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogz za Mikoa