MFANYABIASHARA ATEKWA,POLISI WAMUOKOA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.


POLISI mkoani Singida inashikilia watu watatu, akiwemo mganga wa tiba asilia kutoka Tanga, kwa tuhuma za kumteka nyara mfanyabiashara mkazi wa Manyoni.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Singida, Geofrey Kamwela alidai utekaji huo ulifanyika Machi 21, mwaka huu saa 9.30 alasiri mjini Manyoni.
Wanaoshikiliwa ni Saidi Mgolola (Pesambili) (49) ambaye ni mganga wa tiba za asili, Faraji George (35) ambaye ni mfanyabiashara wa Dodoma na Michael Peter (26), mkazi wa Moshi.
Kwa mujibu wa Kamanda, siku ya tukio, watuhumiwa wakiwa kwenye Toyota Prado T.242 CBM, walifika dukani kwa Mathew Dominic (Cheupe) ambaye ni mfanyabiashara, na kujitambulisha kuwa maofisa usalama wa taifa kutoka makao makuu Dar es Salaam.
"Walimtaka aongozane nao hadi kwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa, mjini Singida kwa ajili ya mahojiano zaidi.
Alikubali kwa sharti kwamba aondoke na mkewe, Selina Mathew," alisema Kamanda.
Ilidaiwa badala ya kuelekea barabara ya Singida, walielekea Dodoma lakini kutokana na polisi kupata taarifa mapema, walikamatwa Bahi kwenye kizuizi cha barabarani.
Alisema chanzo cha utekaji huo kinadaiwa kuwania mali ya mfanyabiashara huyo.
Chanzo:Habari Leo 

Queen Mlozi ashiriki operasheni ya kuondoa mawe makubwa yaliyokuwa yakitumiwa kuteka magari barabara kuu ya Singida-Dodoma

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

DSC07404
Mkuu wa wilaya ya Singida,Queen Mlozi akipasua jiwe kubwa ili liweze kupandishwa kwenye lori kwa lengo kuondolewa kando kando ya barabara kuu ya Singida-Dodoma eneo la kijiji cha Kisaki manispaa ya Singida. Mawe hayo makubwa kwa kipindi kirefu yametumiwa na watu wanaodhaniwa ni majamabazi watekaji wa malori na kupora mali na fedha.
DSC07402
Mkazi wa kijiji cha Kisaki manispaa ya Singida, Juma akipasua jiwe kubwa lililokuwa likitumiwa na majambazi kwa ajili ya kuteka magari na kisha kupora abiria.
 DSC07393
Askari Polisi, Jeshi na baadhi ya wakazi wa kijiji cha Kisaki manispaa ya Singida,wakipandisha jiwe kubwa kwenye lori. Zoezi hilo la kuondoa mawe makubwa kando kando ya barabara kuu ya Singida yaliyokuwa yakitumiwa na watu wanaodhaniwa ni majambazi katika kuteka magari na kupora abiria. Mawe hayo mwishoni mwa mwaka jana yalitumika kuteka gari la chuo cha SUA Morogoro na kisha maiti ndani ya sanduku.
 Mo Blog

News: Wafanyabiashara watekwa na maafisa usalama feki

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

DSC001791
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Singida, SACP Geofrey Kamwela, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) ofisini kwake.
Na Nathaniel Limu, Singida
WAFANYABIASHARA wa Manyoni mjini mume na mke,wametekwa na watu watatu waliojifanya kuwa ni maafisa usalama wa taifa makao makuu jijini Dar-es-salaam.
Waathirika wa utekaji huo ni Methew Dominik @ Cheupe (46) na mke wake Selina Methew (42).
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Singida, SACP Geofrey Kamwela amesema tukio hilo limetokea juzi saa tisa alasiri Manyoni mjini.
Amesema Faraja George (35) mfanyabiashara wa Dodoma mjini,mganga wa tiba asilia na mkazi wa mkoa wa Tanga,Saidi Mgolola @Pesa mbili (49) Michael Peter  na Michael Peter (26) mkazi wa Moshi mjini na dereva wa gari lililotumika katika utekaji huo.
Amesema siku ya tukio watuhumiwa wakiwa na gari T.242 CBM aina ya toyota prado,walifika dukani kwa Methew baada ya kudai kuwa wao ni maafisa usalama taifa,walimwamuru mwenye duka kuwa wanamhitaji Singida mjini kwa ajili ya mahojiano.
“Methew aliwaomba maafisa hao bandia kuwa aambatane na mke wake huko kwenye mahojiano hayo.Baada ya waathirika hao kuingia ndani ya gari,gari hilo badala ya kuelekea Singida mjini,lilibadili na kuelekea Dodoma”,amesema.
Kamwela amesema bahati nzuri polisi Manyoni mjini walipata taarifa ya tukio hilo mapema na wakawasiliana na wenzao wa Bahi mkoani Dodoma ambao walifanikiwa kuwanasa watuhumiwa hapo kwenye kizuizi.
Amesema uchunguzi wa awali umebaini kuwa chanzo cha tukio hilo,ni watuhumiwa kutaka kumwibia mali mfanyabiashara hiyo Methew.Uchunguzi zaidi bado unaendelea.
Kamwela amesema kuwa mara upelelezi utakapokamilika,watuhumiwa watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma inayowakabili.
Mo Blog

Tundu Lissu akabiliwa na changamoto ya michango

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.


DSC07452
Kaimu mkuu wa shule ya sekondari Unyahati jimbo la Singida, Mboya David akiwa ofisini kwake akitekeleza majukumu yake.
DSC07453
Meza ya mkuu wa shule ya sekondari ya Unyahati jimbo la Singida mashariki linaloshikiliwa na CHADEMA.
DSC07457
Kutokana na ofisi ya mkuu wa shule ya sekondari ya Unyahati jimbo la Singida mashariki kutokuwa na kabati za kutunzia nyaraka imelazimika kutumia viti vya plastiki kutunza nyaraka mbalimbali.
DSC07463
Mwalimu Mboya David kaimu mkuu wa shule ya sekondari ya kata Unyahati jimbo la Singida mashariki ambalo mbunge wake ni Tundu Lissu aliyejipatia umaarufu kwa hoja zake bugeni, akikagua choo cha nyasi chenye matundu nane kinachotumiwa na wanafunzi wavulana 173 wa shule hiyo.
DSC07469
Wanafunzi wa kidato cha kwanza shule ya sekondari Unyahati jimbo la Singida mashariki,wanaketi kwenye  viti vya plastiki na kuandikia kwenye mapaja yao kutokana na kukosa madawati.(Picha na Nathaniel Limu). 
DSC07471
.Shule za sekondari jimboni kwake zipo hoi kwa madawati na vyoo
Na Nathaniel Limu, Ikungi
SHULE ya sekondari ya Unyahati iliyopo kijijini kwa mbunge wa jimbo la Singida Mashariki (CHADEMA),Tundu Lissu inakabiliwa na changamoto nyingi, ikiwemo ya uhaba mkubwa wa vyoo hali inayochangia wanafunzi kutumia choo cha nyasi.
Kaimu mkuu wa shule hiyo, Mbaya David amesema kuwa kutokana na wazazi/walezi wa jimbo hilo kuwa kwenye mgomo wa kuchangia wala kushiriki miradi yao ya maendeleo mbalimbali ikiwemo ya sekta ya elimu,hali hiyo imechangia mwaka jana walimu wa shule hiyo na wanafunzi kuchimba choo ambacho wakati wa masika, kilidumbukia kutokana na kuwa chini ya kiwango.
“Jimbo hili ukitamka jambo la michango au watu kushiriki utekelezaji wa miradi, huwezi kueleweka.Wazazi/walezi wameishaambiwa kuwa serikali ina fedha nyingi ya kugharamia miradi yote na wao kama wananchi, hawahusika kabisa na jukumu hilo”amesema.
Kwa hali hiyo, amesema ili shule isije ikafungwa kwa kukosa choo, shule imeamua ijenge choo cha muda ambacho ni cha nyasi.
David amesema pamoja na changamoto ya choo zipo zingine ikiwemo ya wanafunzi wa kidato cha kwanza kutumia viti vya plastiki darasani na hali hiyo inachangia waandikie juu ya mapaja yao.
Kaimu mkuu huyo wa shule, alitaja changamoto zingine kuwa shule hiyo haina kabisa nyumba za walimu kitendo kinachochangia wapange katika kijiji cha Ikungi kilichopo umbali wa kilomita nne. Hali hiyo inachangia mwalimu kutembea kilomita nane kwa siku kwenda shuleni.
“Hapa kwetu hatuna jengo la utawala jambo linalosababisha tubadilishe matumizi ya vyumba viwili vya madarasa na kuwa ofisi za walimu.Tunakabiliwa na upungufu mkumbwa wa samani ikiwemo makabati kitendo kinachotulazimisha kutumia viti vya plasitiki kuhifadhia nyaraka mbalimbali”, amesema Divid.
Kuhusu vyumba vitatu vya maabara, David amesema kuwa hali ni mbaya mno kwa sababu hata kutenga eneo lenyewe la kujenga vyumba hivyo halijatengwa.
Kwa mujibu wa uongozi wa shule hiyo ingawa shule hiyo imejengwa kijijini kwa Tundu Lissu, lakini toka ianzishwe miaka saba iliyopita mbunge huyo hajaweza kutembelea shuleni hapo.
Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana shuleni hapo, hakuna ndugu wa karibu na mbunge Tundu anayesoma shuleni hapo. Hata hivyo mbunge Tundu Lissu, amealikwa kwenye harambee ya kuchangia maendeleo ya shule ya kijijini kwao.
Juhudi za kumpata Tundu aweze kuzungumzia changamoto za shule hiyo zilikwama baada ya kumtumia ujumbe kwa njia ya simu hakujibu na alipopigiwa, hakupokea.
Hivi karibuni mkuu wa wilaya ya Ikungi, Manju Msambya amesema kuwa kabla ya mwaka 2010 wakazi wa jimbo hilo walikuwa mstari wa mbele katika kujenga shule za sekondari za kata na kata mbili zilijenga sekondari mbili. Baada ya uchaguzi mkuu wa 2010 mambo yalibadilika baada wananchi kukatazwa kuchangia maendeleo yao.

Na Mo Blog

Tunamwonea bure Jaji Warioba

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Nchi hii kwa kweli ina visa sijawahi kuviona mahali kwingine katika dunia hii. Ni nchi ya ajabu na sijui ilikuwaje nikaishi humu.
Kuna mambo mengi yanayotokea na kunilazimisha baadhi ya nyakati kulaani kwa nini nimekuwa Mtanzania, yaani inachosha sana.
Hivi sasa kuna hizi harakati za kutafuta Katiba mpya hapa nchini. Iliundwa tume maalumu ya kutusaidia kupata katiba hiyo.
Watu kutoka makundi mbalimbali wakateuliwa, wakiwamo wanasiasa kutoka chama tawala cha CCM na hata vyama vya upinzani. Makundi mengine nayo yakashirikishwa ipasavyo. Baada ya kumaliza kazi yake, tume hiyo iliyokuwa ikiongozwa na Mzee Joseph Warioba ilikabidhi rasimu zake kwa Serikali na kwa wananchi kwa jumla.
Sasa kioja kimeanza kutoka kwa wanasiasa hasa wale wa CCM ambao kila siku wanamsimanga mzee wa watu bila sababu yoyote.
Kila siku Mzee Warioba yuko midomoni mwao wakimlalamikia kwa hili ama lile.
Utafikiri kuwa maoni yaliyomo kwenye rasimu yaliandaliwa na Mzee Warioba chumbani. Tume ilikuwa na wajumbe kibao tena wengine ni kutoka CCM, lakini mzigo wote ni Warioba, kila mtu Warioba kama vile yeye ndiye aliyetengeneza rasimu hiyo.
Kama CCM hawakubali mawazo ya wananchi waliyotoa kwa wajumbe wa tume, basi wasimwonee Warioba pekee, wawe pia wanawataja wajumbe wengine tunaojua kuwa nao ni CCM wa damu.
Huyu mzee kaitumikia nchi hii kwa uadilifu mkubwa, jamani aachwe apumzike kwa amani. Kwa nini tumchoshe?
Chanzo;Mwananchi

WANAWAKE WASISITIZWA KUWAKUMBUKA WENZAO WALIOKO MAGEREZANI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


 Mtoto Njiti akiwa amebebwa na mama yake.
WANAWAKE Mkoani Singida wamehimizwa kujenga tabia ya kuwakumbuka wanawake wenzao waliofungwa na walioko mahabusu gerezani ili waendelee kuaminiwa kuwa bado ni sehemu muhimu ya wanawake mkoani humu.

Wito huo umetolewa hivi karibuni na Mwenyekiti wa umoja wa wanawake kanisa la Free Pentekoste church Tanzania (UWW-FPCT) tawi la Singida mjini, Lessi Jaredi muda mfupi baada ya kutoa msaada wa vitu mbali mbali kwa wanawake wanatumikia adhabu jela na wale walioko mahabusu katika gereza la wilaya ya Singida.Msaada huo ulikuwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya wananwake duniani.

Amesema wanawake waliopo magerezani, hawajapoteza utu wao na wala sio kwamba hawana msaada tena katika kuchangia maendeleo ya mkoa wa Singida na taifa kwa ujumla.
Baadhi ya watoto waliozaliwa kabla ya kufikia umri wa kuzaliwa (Njiti) ambao wamelazwa katika hospitali ya mkoa mjini Singida.

“Wanawake hawa ni wenzetu, ndugu zetu na watoto wetu, wapo gerezani kwa lengo la kusaidiwa kurekebisha baadhi ya mienendo na tabia zao tu.  Kwa hali hiyo, tunapaswa kuwapenda,kuwathamin na kuwajali, ili kuondoa uwezekano wao wasianze kuhisi kwamba, wametengwa au sio sehemu muhimu ya jamii”,alifafanua Mwenyekiti huyo.

Akisisitiza zaidi, Lessi amesema wanawake hao waliopo gerezani wakitembelewa na hasa na wanaweke wenzao na kukpewa misaada, kitendo hicho kitawatia moyo na kamwe hawatakata tamaa katika maisha yao.

“Nitumie fursa hii kuwahimiza wanawake wa jimbo la Singid mjini na wa mkoa wetu wa Singida kwa ujumla, tujenge utamaduni wa kuadhmisha siku ya wanawake duniani, kwa kuwatembelea wanawake wenzetu walioko magerezani, haspitali na wenye matatizo mbali mbali, ili makundi hayo yaweze kutembua kwamba tunayajali na kuyathamini”,amesema.

Katika hatua nyingine, Mwenyekiti huyo pia amewahimiza wanawake kuwatembelea wanawake walioko katika hospitali mbali mbali baada ya kujifungua watoto na hasa wale ambao watoto wao hawakufikisha umri wa kuzaliwa (njiti).

Mwenyekiti wa Umoja wa wanawake wa kanisa la Free Pentekoste Church Tanzania (UWW-FPCT) tawi la Singida, Lessi Jaredi akimwombea mtoto Njiti ili Mungu aweze kumsaidia kuongeza uzito stahiki ambao utatoa fursa kwa wao kupewa ruhusa ya kurejea nyumbani kwao.

Amesema wanawake hao wanapaswa kufarijiwa mara kwa mara, sio tu na ndugu zao, bali na wanawake wengine kwa sababu wanalazwa muda mrefu wakisubiri watoto wao wafikishe uzito unaotakiwa.

“Sisi leo (jana 8/3/2014) wanachama wa UWW FPCT, tumetembelea wanawake sita walioko hospitali ya mkoa ambao wamejifungua watoto njiti. Tumebaini kwamba wana kazi kubwa ya kuhakikisha watoto wao njiti, wanafikisha uzito unaotakiwa.  Kazi hiyo ambayo ni pamoja na kuwalisha kikamilifu ili kupata uzito stahili, inawalazimu kukaa hospitalini kwa mud amrefu”,alifafanua.

Akifafanua zaidi, alisema watoto hao licha ya kuhifadhiwa kwenye chumba chenye joto, pia wapo wengine ambao wanalazimika kupakatiwa kifuani na mama zao, ili kuuunganisha ngozi ya kifuani ya mama na ya mtoto, kwa lengo mtoto njiti,apate joto la mama yake aweze kukua na kuongeza uzito.
Mhasibu wa Umoja wa wanawake wa kanisa Free Pentekoste Church Tanzania (UWW-FPCT) tawi la Singida, Joyce Gunda,akikabidhi msaada kwa mgonjwa aliyelazwa katika hospitali ya mkoa mjini Singida.Msaada huo ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya wanawake duniani mwaka huu.
Mwenyekiti wa Umoja wa wanawake wa kanisa la Free Pentekoste Church Tanzania (UWW-FPCT) Lessi Jaredi, akikabidhi msaada kwa mmoja wa wanawake waliojifungua watoto hawajafikia umri (Njiti) wa kuzaliwa.Msaada huo ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya wanawake duniani mwaka huu.
Picha na mtandao wa Singida yetu

Mama mlemavu wa ngozi ashikiliwa kwa kumuua mwanawe

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Kamanda wa Polisi mkoa wa Singida, Geofrey Kamwela
 
Polisi mkoani Singida inawashikilia wanawake wawili akiwamo mlemavu wa ngozi (albino), kwa mauaji ya mtoto Daud Richard (2.5), kwa imani za kishirikiana.
 
Kamanda wa Polisi mkoa wa Singida, Geofrey Kamwela (pichani), alisema kuwa tukio hilo lilitokea juzi saa 1:30 asubuhi katika kijiji cha Nkalankala tarafa ya Nduguti, wilaya Mkalama.
 
Aliwataja wanaoshikiliwa kuwa ni bibi wa mtoto huyo, Neema Paulo (35) na mama wa marehemu, Hidaya Omari (20).
 
Alisema kuwa uchunguzi wa awali umebaini kabla ya kufikwa na mauti, mtoto huyo alinyongwa shingoni, kuchunwa ngozi sehemu zake za siri na wauaji kutoweka nazo, kisha mwili wake kutumbukizwa ndani ya kisima kilichokuwa na maji.
 
Kamwela alisema kuwa mwili wa mtoto huyo baadaye ulionekana baada ya kuelea juu ya maji na wananchi kutoa taarifa polisi.
 
"Mauaji haya yanahusishwa na imani ya kishirikina kutokana na kuchunwa ngozi na kunyofolewa sehemu za siri...lazima pia tuwashikilie wanawake hawa, walikuwa wapi wakati mtoto kama huyu mdogo anatoweka nyumbani!, hata ndugu wengine pia watahojiwa," alisema Kamwela.
 
Kufuatia tukio hilo Kamwela alisema kuwa mama wa mtoto huyo ambaye ni mlemavu wa ngozi na bibi wa marehemu kwa pamoja watafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.
 
SOURCE: NIPASHE

Wasichana 35 wafukuzwa shule kwa mimba, utoro

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
BODI ya Shule ya Sekondari Munkinya, Kata ya Dung’unyi wilayani Ikungi, Singida imewafukuza shule wanafunzi 35 kwa sababu za utoro, mimba na ukosefu wa nidhamu.
Mkuu wa Shule hiyo, Joseph Kilinga, alisema wanafunzi hao walifukuzwa kati ya mwaka 2010 hadi mwaka huu.
Alifafanua kwamba katika kipindi hicho jumla ya wanafunzi 21 walifukuzwa shule kwa utoro, wakati utovu wa nidhamu uliwafukuzisha wanafunzi wanne na wengine watatu walifukuzwa kwa mimba.
 Chanzo;Tanzania Daima

NEWS: WAFUNGWA MIAKA 1O JELA KWA KUSABABISHA KIFO CHA MWANAFUNZI WAKATI WA KUTOA MIMBA.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

DSC07094
Aliyekuwa tabibu msaidizi wa Dispensari ya Tumaini mjini Singida, (wa mbele) Godlisten Raymond (37) na mfanyabiashara wa mbuzi na biashara ya kusaga nafaka (wa tatu mbele) Adamu Shaban Hole (46) mkazi wa kijiji cha Kitandaa tarafa ya Sepuka wilaya ya Ikungi,wakisindikizwa na askari polisi kwenda gerezani kuanza kutumikia adhabu ya kila mmoja kifungo cha miaka 10 baada ya kupatikana na hatia ya kumtoa mimba mwanafunzi na kusababisha kifo chake.
DSC07095
Mfanyabiashara wa Mbuzi na kusaga nafaka katika kijiji cha Kintandaa Adamu Shaban Hole (46) (mbele mwenye kofia baraghashia) na aliyekuwa tabibu msaidizi katika dispensari ya Tumaini mjini Singida, Godlisten Raymond (37) aliyefunika uso,wakisindikizwa gerezani kwenda kuanza kutumikia kifungo cha miaka 10 baada ya kutiwa hatiani na mahakama kuu kanda ya kati kwa kosa la kumpa mimba mwanafunzi na kuitoa na kusababisha kifo chake.Mwanafunzi huyo Hamida Athumani (16) alifariki dunia siku chache kabla ya kufanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi.(Picha na Nathaniel Limu).7
Na Nathaniel Limu, Singida
MAHAKAMA Kuu kanda ya kati iliyomaliza vikao vyake hivi karibuni mjini Singida,imewahukumu aliyekuwa tabibu msaidizi wa dispensari ya Tumaini Godlisten Raymond (37) adhabu ya kutumikia jela miaka 10 baada ya kupatikana na hatia ya kujaribu kutoa mimba kwa njia isiyo sahihi kwa  mwanafunzi na kusababisha kifo chake.
Mshitakiwa Godlisten anadaiwa kumtoa mimba mwanafunzi wa shule ya msingi Kintandaa tarafa ya Sepuka wilaya ya Ikungi, Hamida Athumani (16) septemba saba mwaka 2006 na alifariki dunia septemba 17 mwaka huo huo wa 2006, siku chache kabla ya kufanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi.
Pia katika kesi hiyo,mfanyabiashara wa mbuzi na kusaga nafaka mkazi wa kijiji cha Kitandaa tarafa ya Sepuka wilaya ya Ikungi,Adamu Shabani Hole (46),naye amepewa adhabu ya kutumikia jela miaka 10 baada ya kupatikana na hatia ya kumpa mimba mwanafunzi Hamida Athumani (16) na kisha kushiriki kutoa mimba hiyo na kusababishia kifo mwanafunzi huyo.
Ilidaiwa mahakamanai hapo kuwa mshitakiwa wa pili ambaye ni mfanyabiashara ya mbuzi,Adamu,katika kipindi hicho hicho,aliweza kumpa mwanafunzi mwingine Rukia Juma aliyekuwa akisoma darasa moja na Hamida (marehemu).
Rukia baada ya kutolewa mimba na washitakiwa,aliweza kulazwa katika hospitali ya mkoa mjini hapa,na aliweza kunusurika kufariki dunia baada ya kupatiwa matibabu.
Kabla ya kutolewa kwa adhabu hiyo,mwendesha mashitaka wakili wa serikali mkuu mfawidhi kanda ya Singida,Neema Mwanda,aliiomba mahakama hiyo itoe adhabu kali ya kifungo cha maisha jela kwa washitakiwa,ili iwe fundisho kwao na watu wengine wanaotarajia kuwatoa mimba wasichana wadogo na kisha kusababisha vifo vyao.
“Vitendo vya watu wazima kufanya mapenzi na wanafunzi na kisha kuwapa ujauzito,havikubaliki kabisa,kwa sababu zinaharibu maisha ya wanafunzi husika na wakati mwingine vinasababisha vifo.Pia madaktari na tabibu wasaidizi wenye tabia ya kutoa mimba kwa njia isiyo salama,nao wanakwenda kinyume na sheria za taaluma zao”,amesema Mwanda.
Kwa upande wake wakili wa kijitegemea kutoka Dodoma mjini.Deus Nyabiri aliyekuwa anamtetea mshitakiwa wa kwanza,Godlisten,aliiomba mahakama hiyo impe adhabu nafuu mteja wake ikizingatia kuwa kosa hilo ni la kwanza kwake na pia anategemewa na familia yake na ya wazazi wake ambao kwa sasa,wana umri mkubwa.
Naye wakili wa kujitegemea wa mjini hapa,Raymond Kimu aliyekuwa akimtetea mshitakiwa wa pili,Adamu,aliiomba mahakama hiyo impe adhabu nafuu mteja wake na kiwezekana imwachie huru,kwa madai kuwa baada ya kuwapa mimba wanafunzi wawili waliokuwa darasa la saba,mke wake amemkimbia na familia yake imemtega.
Akitoa adhabu hiyo,jaji Cresentia  Makuru, amesema kwa mazingira ya kawaida,kosa walililofanya  washitakiwa,hawastahili huruma ya mahakama.
Amesema vitendo vya wasichana wadogo kupoteza maisha kwa kutolewa mimba kwa njia isiyo salama,licha ya kusababisha vifo vyao,pia vinachangia ndoto za wazazi kwa watoto wao,kupotea.
Aidha,jaji Makuru amesema katiba ya nchi,inatamka wazi kwamba uhai wa mtu ni lazima uheshimiwe na kulindwa.Hata sheria za kimataifa nazo zimetamka hivyo hivyo.

KDU wakamata majangili zaidi ya 600

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
KIKOSI cha Kuzuia Ujangili (KDU)KIKOSI cha Kuzuia Ujangili (KDU) Kanda ya Kati, kimefanikiwa kukamata majangili 692 na meno ya tembo 195 katika Operesheni Tokomeza Ujangili iliyofanyika wilayani Manyoni, Singida kuanzia mwaka 2009 hadi 2012.
Kaimu Meneja wa Hifadhi ya Pori la Akiba la Rungwa, Batholomeo Mganga, alisema hayo wakati wa kumkabidhi baiskeli ya miguu mitatu mlemavu, Yohana Pangarasi, mwanakijiji wa Imalampaka, Manyoni.
Mganga alisema katika kipindi hicho tembo 168 wenye uzito wa kilo 166 waliuawa na majangili hao kinyume cha sheria.
Hata hivyo Kaimu Meneja wa KDU alisema mwaka 2009 licha ya kukamatwa kwa majangili 116, tembo 16 waliuawa wakati mwaka 2010 majangili 172 walikamatwa wakiwa na meno ya tembo manne yaliyokuwa na uzito wa kilo 23.5
Chanzo;Tanzania Daima

Chama cha waandishi Wanawake chatoa msaada wa Mizinga 80 ya Nyuki

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

DSC07053
Katibu wa chama cha waandishi wanawake (Women in Media Organization - WMO) tawi la mkoa wa Singida, Awila Silla, akitoa taarifa yake ya msaada wa mizinga 80 kwa vikundi vinne vya wafuga nuki wanawake kutoka wilaya ya Singida na Ikungi.
 
DSC07075
 
Mkuu wa mkoa wa Singida, Dk.Parseko Kone, akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi msaada wa mizinga ya nyuki kwa vikundi vinne vya Wanawake wafuga Nyuki.Kushoto ni mkuu wa wilaya ya Singida, Queen Mlozi na kulia ni mwenyekiti wa WMO Evarista Lucas.
DSC07082
 
Mkuu wa mkoa wa Singida, Dk.Parseko Kone (wa pili kulia) akikabidhi mzinga wa Nyuki kwa wawakilishi wa vikundi vinne vya wafuga Nyuki wa wilaya ya Singida na Ikungi.Wa kwanza kulia ni Afisa Maliasili mkoa wa Singida,Charles Kidua.
DSC07087
 
Mkuu wa mkoa wa Singida,Dk.Parseko Kone, (wa pili kulia walioketi) akiwa kwenye picha ya pamoja na wanakikundi wa ufugaji nyuki kutoka wilaya ya Singida na Ikungi.Wa kwanza kulia ni mwenyekiti wa WMO Evarista Lucas.Kushoto ni afisa maliasili mkoa Charles Kidua na anayefuata ni mkuu wa wilaya ya Singida,Queen Mlozi.(Picha na Nathaniel Limu).
Na Nathaniel Limu, Singida
CHAMA cha Waandishi wa Wanawake (Women in Media Organization – WMO) mkoani Singida kimetoa msaada wa miziga 80 ya nyuki ya kisasa, kwa vikundi vine vya wanawake wa halmashauri ya Singida na Ikungi.
Mizinga hiyo ya kisasa iliyotengenezwa na SIDO ndogo mjini hapa, inakadiriwa kuwa na thamani ya zaidi ya shilingi milioni kumi.
Hayo yamesemwa hivi karibuni na Katibu wa WMO mkoani Singida, Awila Sill wakati akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi mizinga hiyo ya kisasa iliyofanyika kwenye viwanja vya SIDO mjini Singida.
Amesema vikundi hivyo ni kutoka vijiji vya Masweya na Muhintiri vya wilaya ya Ikungi na Ilongero na Nduamughanga vya halamashauri ya wilaya ya Singida.
Awila ambaye ni mwandishi wa habari wa gazeti la mwananchi na the citizen mkoani hapa, alisema mizinga hiyo kila moja una uwezo wa kutoa/kuzalisha lita 20 na bei ya lita moja kwa sasa ni shilingi 10,000.
“Wanakikundi wote,tumeishawapatia mafunzo ya ufugaji bora wa nyuki.Kwa hiyo tunayoimani kuwa mbele ya safari,wanakikundi hawa watanufaika na msaada huu na kwa vyo vyote,watajikomboa kiuchumi”,amesema Awila.
Katika hatua  nyingine, Katibu huyo alitumia fursa hiyo kuishukuru serikali kupitia wizara ya maliasili na utalii kitengo cha mfuko wa misitu nchini kwa kukipatia WMO ruzuku ya zaidi ya shilingi 14.4 milioni.
Kwa upande wake mgeni rasmi katika hafla hiyo, mkuu wa mkoa wa Singia, Dk. Parseko Vicent Kone, ameziagiza halmashauri za wilaya na manispaa, kuongeza juhudi katika kuendelea kuibua vikundi vingi zaidi vya ufugaji nyuki.
Aidha, ameziagiza kuwaondoa mara moja wavamizi wa misitu na hasa kwenye misitu ya vijiji vya Mgori, Minyughe, Mlilii, Sekenke/Tulya, Wembere, Chaya na maeneo mengine yaliyoharibiwa.
“Halmashauri mnalo jukumu la kuzuia ukataji miti ya asili kwa ajili ya kukaushia tumbaku, wakulima wa tumbaku wanapaswa kupanda miti kwa ajili ya matumizi yao”,amesema Dk.Kone.

Hatari: Mkulima akamatwa na Bhangi misokoto 888 yenye uzito gramu 44

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

DSC001791
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Singida,SACP Geofrey Kamwela.
Na Nathaniel Limu, Singida
JESHI la Polisi mkoa wa Singida linamshikilia Mariamu Songeraeli (32) mkulima mkazi wa kijiji cha Nselembwe wilaya ya Iramba kwa tuhuma ya kumiliki madawa ya kulevya aina ya bhangi misokoto 88 yenye uzito wa gramu 44.
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Singida,SACP Geofrey Kamwela amesema mtuhumiwa Mariamu amekamatwa juzi saa 11.30 jioni nyumbani kwake katika kijiji cha Nselembwe kata ya Shelui wilaya ya Iramba.
Amesema askari polisi waliokuwa kwenye doria siku ya tukio,walipata taarifa kutoka kwa raia wema kwamba mtuhumiwa Mariamu anajihusisha na biashara haramu ya kununua na kuuza bhangi.
Kamwela amesema askari hao waliweza kwenda nyumbani kwa mtuhumiwa na kuipekua na kisha kuikuta misokoto hiyo ya bhangi ikiwa chumbani kwake,imefichwa kwenye mfuko wa rambo.
“Tunamshikilia mtuhumiwa kwa uchunguzi zaidi,ili kujua ni wapi anakoitoa bhangi hiyo na watu anaoshirikiana nao katika bishara hiyo haramu,baada ya uchunguzi huo kukamilika,atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma inayomkabili”,amesema.
Aidha,Kamwela ametumia fursa hiyo kuwashukuru na kuwapongeza raia wema kwa kutoa taarifa sahihi za uhalifu na wahalifu,na kuwaomba waendelee na moyo huo huo,kwa madai kwamba suala la usalama ni la wananchi wote kwa ujumla.
Chanzo Mo Blog
 
 

ABIRIA WAKWAMA SINGIDA

ABIRIA waliokuwa wanasafiri  kutoka Dodoma kuelekea  mikoa  ya kanda ziwa,  magharibi  na  nchi jirani,  leo asubuhi wamekwama kwa zaidi ya saa nne  katika eneo la Kijiji cha Kisaki umbali wa Kilomita 10  kabla ya kufika Singida mjini baada ya madereva wa malori kufunga barabara .

Zaidi ya malori 300 yaliegeshwa barabarani  kuanzia  saa 12 hadi saa 4 asubuhi, kuzuia  magari mengine yasipite ili kulishinikiza jeshi la polisi kudhibiti uhalifu wa mara kwa mara katika eneo hilo baada ya wenzao wawili kutekwa na majambazi, kujeruhiwa kisha kuporwa  fedha  na mali nyingine.

Madereva hao wamesema wamefikia uamuzi wa kufunga barabara ili kuwasilisha hisia zao kwa mamlaka  husika baada ya eneo  hilo na utekaji magari mara.
Wamesema mbali na kuporwa fedha na mali nyingine, pia wamekuwa akijeruhiwa kwa mapanga, pinde na silaha za moto kiasi cha kuhatarisha maisha yao lakini hakuna hatua zinazochukuliwa.

Madereva hao wamekubali kuendelea na safari  baada  ya Naibu Waziri wa Ushiriano wa Afrika   Mashariki Abdulla Juma Abdull aliyekuwa miongoni mwa watu walikwama eneo hilo,  kuahidi kuifikisha kero hiyo kwa mamlaka husika na ufumbufu wa kudumu kutafutwa haraka iwezekanavyo.

Kamanda wa polisi mkoa  wa Singida Geofrey Kamwela amesema polisi wanaendelea  na msako mkali dhidi ya watu waliofanya utekaji huo wa magari na kupora  madereva fedha pamoja na kuwajeruhi.


Hata  hivyo  ametoa wito  kwa wadau wote kushirikiana  kudhibiti uhalifu  badala ya  kufunga barabara na kuwategemea polisi  peeke ambao ni wachache na hawawezi kuwepo kila mahali penye uhalifu.
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

Serikali yashauriwa kuajiri Waganga wa Jadi kupunguza uhaba wa watumishi wa Afya

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

DSC06762
Kaimu meya mstahiki wa manispaa ya Singida, Hassan Mkata akizungumza kwenye kikao cha kawaida cha Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Singida kilichofanyika mkoani Singida.Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa manispaa ya Singida. Robert Mahili na kushoto ni Mwenyekiti wa CCM manispaa ya Singida,Hamisi Nguli.
DSC06736
Diwani wa kata ya Unyamikumbi,Mosses Ikaku, akichangia hoja katika kikao cha baraza la madiwani wa manispaa ya Singida kilichofanyika mjini Singida.
DSC06751
Afisa  Ardhi manispaa ya Singida, Angelus John  Camara,akitoa ufafanuzi juu ya sheria ya Ardhi mbele ya kikao cha baraza la Madiwani kilichofanyika mkoani Singida.
DSC06757
Baadhi ya madiwani wa manispaa ya Singida waliohudhuria kikao cha kawaida cha baraza la madiwani kilichofanyika mjini Singida.(Picha na Nathaniel limu).
Na Nathaniel Limu, Singida
KUTOKANA na uhaba mkubwa wa watumishi wa sekta ya afya katika vituo mbalimbali vya afya vikiwemo zahanati,serikali imeshauriwa kuajiri waganga wa jadi ili kupunguza uhaba huo.
Ushauri huo wa bure,umetolewa hivi karibuni na Diwani wa kata ya Unyambwa (CCM) Manispaa ya Singida,Shaban Satu wakati akichangia hoja ya diwani wa kata ya Unyamikumbi,Mosses Ikaku ambaye alidai zahanati ya kata yake imekuwa na mhudumu moja tu kwa kipindi kirefu.
Amesema uzoefu unaonyesha kuwa uhaba wa wahudumu wa afya una athari nyingi ikiwemo ya utoaji wa huduma usiokidhi mahitaji.
“Diwani mwenzetu ametueleza kwamba kwa muda mrefu amefikisha tatizo la uhaba wa wahudumu katika ngazi husika mara nyingi,lakini juhudi zake hazijazaqa matunda hadi sasa”,amesema.
Amesema endapo serikali imeshindwa kulitafutia ufumbuzi wa kudumu tatizo hilo,basi ni bora ikatoa nafasi kwa waganga wa jadi kuziba mapungufu hayo”,alifafanua.
Katika hatua nyingine,imedaiwa kuwa shule ya msingi ya kijiji cha Mwankoko,inakabiliwa na uhaba wa madawati 316.
Kaimu Mkurugenzi wa manispaa hiyo,Robert Mahili aliiomba serikali ya kijiji hicho kuongeza juhudi zaidi kuhamasisha wananchi kuchangia ununuzi wa madawati.
Amesema pia juhudi zilifanyika za za kuzishawishi benki ya NBC,CRDB,NMB na CIP,ili ziweze kusaidia kuondoa uhaba huo mkubwa wa madawati.
Kwa mujibu wa kaimu mkurugenzi,Mahili,manispaa hiyo inakabiliwa na uhaba mkubwa wa walimu 298.
 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2011. Singida Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogz za Mikoa