DC MSAMBYA ATAKA WATAALAMU WA KODI MGODINI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

MKUU wa Wilaya ya Ikungi mkoani Singida, Manju Msambya, ameiagiza Halmashauri ya Wilaya hiyo kupeleka wataalamu wa kodi na kuweka viwango vya ushuru katika mgodi wa machimbo ya dhahabu ya Muhintiri.
Akizungumza na viongozi na watendaji wa Halmashauri hiyo, Msambya, alisema ili kuiwezesha Halmashauri hiyo ni vema viongozi hao wakaweka wataalamu wa kodi watakaokusanya mapato ya ndani, ili waweze kukamilisha baadhi ya miradi badala ya kuendelea na utamaduni wa kutegemea fedha za Serikali kuu.
Aidha, alisema eneo la machimbo hayo lina mzunguko mkubwa wa fedha, hivyo kuhitaji kuangaliwa na kuhakikisha ulinzi na usalama wa wananchi na mali zao unakuwa wa uhakika na kuongeza kuwa, mgodi huo bado haujawa rasmi hivyo ni vema kufuatilia mapato.
Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Celestine Yunde, alimwagiza mkaguzi wa ndani kukagua miradi ya maendeleo iliyopo vijijini na kuwasilisha taarifa.
Chanzo:Tanzania Daima

UTUMISHI YAFANYA KIKAO KAZI KWA VIDEO CONFERENCE NA MIKOA YA SINGIDA,ARUSHA NA DODOMA


Naibu Katibu Mkuu Utumishi Bw.HAB Mkwizu (kulia) akifungua kikao kazi kwa njia ya Ki-elektroniki (video conference)kilichojumuisha Utumishi na Mikoa ya Singida, Arusha, Dodoma na Tume ya Mipango katika ukumbi wa Utumishi mapema leo.
Naibu Katibu Mkuu Utumishi Bw.HAB Mkwizu (kulia) akifuatilia mada wakati wa kikao kazi kilichofanyika kwa njia ya Ki-elektroniki (video conference) kati ya Utumishi na Mikoa ya Singida, Arusha, Dodoma na Tume ya Mipango katika ukumbi wa Utumishi mapema leo.
Afisa Utumishi Mwandamizi wa Ofisi ya Rais-Utumishi Bi.Sakina Mwinyimkuu akiwasilisha katika kikao kazi kilichofanyika kwa njia ya Ki-elektroniki (video conference) kati ya Utumishi na Mikoa ya Singida, Arusha, Dodoma na Tume ya Mipango katika ukumbi wa Utumishi mapema leo. Wengine ni viongozi wa Ofisi ya Ris Menejimenti ya Utumishi wa Umma wakifuatilia mada.
Baadhi ya viongozi na watumishi wa Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma wakifuatilia mada wakati wa kikao kazi kilichofanyika kwa njia ya Kielektroniki (video conference) kati ya Utumishi na Mikoa ya Singida, Arusha, Dodoma na Tume ya Mipango katika ukumbi wa Utumishi mapema leo.
Afisa Utumishi wa Ofisi ya Rais-Utumishi Bi.Magreth Ngondya (kushoto) akiwasilisha mada katika kikao kazi kilichofanyika kwa njia Ki- elektroniki (video conference) katika kikao kazi kati ya Utumishi na Mikoa ya Singida, Arusha, Dodoma na Tume ya Mipango katika ukumbi wa Utumishi mapema leo. Wengine ni viongozi wa Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma wakifuatilia mada.


Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

WALIMU WAKOSA VYOO

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

WALIMU wa Shule ya Sekondari ya Kata ya Mandewa katika Halmashauri ya Manispaa ya Singida hawana vyoo kwa miaka nane sasa, halia ainayowalazimu kutumia vyoo vya wanafunzi.
Kufuatia hali hiyo, Rais wa Shirikisho la Wachimbaji wa Madini Tanzania (FEMATA), John Bina, ameingilia kati na kutoa sh. 500,000, lori 10 za mchanga na vifaa kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa vyoo hivyo.
Akizungumza juzi kwenye mahafali ya nne wa kidato cha nne kwenye shule hiyo, Bina ambaye alikuwa mgeni rasmi alionekana kuguswa na hali hiyo na kuamua kuendesha harambee ya papo kwa hapo.
Mara baada ya Bina kuanzisha harambee hiyo, Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Tawi la Singida, Emmanuel Kingu alitoa mifuko 20 ya saruji, mwenyekiti wa kamati ya shule alitoa mifuko 10 ya saruji na Diwani wa viti maalum wa Kata hiyo, Sara Alute alitoa mifuko miwili.
Mapema katika taarifa ya shule, pamoja na mambo mengine mkuu wa shule hiyo, Magreth Misanga alisema shule hiyo inakabiliwa na tatizo la ukosefu wa vyoo vya walimu.
Misanga alisema shule hiyo iliyoanzishwa mwaka 2006 kwa michango ya nguvu za wananchi na hadi sasa ni miaka nane hawana vyoo vya walimu na hivyo kujikuta wakitumia vyoo vya kantini ya shule pamoja na watu wengine.
Shule hiyo ina wanafunzi 381, ambapo kati yao wavulani ni 204 na wasichana 177.
Chanzo:Tanznia Daima

MAAMBUKIZI YA VVU YAPUNGUA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

TANZANIA imefanikiwa kupunguza viwango vya maambukizi mapya ya Virusi vya Ukimwi (VVU) kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto kutoka asilimia 26 mwaka 2009 hadi kufikia asilimia 15 mwaka 2012.
Hayo yalibainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk. Parseko Kone, wakati wa uzinduzi wa mpango wa ushirikiano ili kupunguza VVU na vifo vya wajawazito na watoto, iliyofanyika mjini Singida juzi.
Dk.Kone alifafanua kwamba pamoja na mafanikio hayo, serikali hivi sasa inalenga kutokomeza kabisa maambukizi hayo.
Mkuu wa Mkoa huyo pia alipokea msaada wa vifaa mbali mbali vilivyotolewa na Watu wa Marekani kupitia Shirika ka misaada la USAID kama sehemu ya Mpango wa dharura wa Rais wa Marekani wa kupambana na Ukimwi (PEFER).
“Ni katika utekelezaji wa mkakati huo wa kitaifa, leo nitazindua mkakati wa tokomeza maambukizi mapya ya VVU toka kwa mama kwenda kwa mtoto kwa mkoa wa Singida,”alisema.
Kwa mujibu wa Dk.Kone, takwimu zinaonesha kwamba hapa nchini kati ya wajawazito 100,000 wanaojifungua, 454 hufariki kutokana na matatizo wakati wa mimba au uzazi na watoto 26 hufariki dunia kati ya watoto 1,000 wanaozaliwa kila mwaka.
Awali, Mkurugenzi wa Tunawajali, Dk.Gottlieb Mpangile akitoa maelezo ya mradi huo, pamoja na kukabidhi msaada wa vifaa vyenye thamani ya sh. milioni 155, alivitaja vituo vitakavyonufaika na msaada huo kuwa ni hospitali za Mtakatifu Gasper, Caroluos, Misheni ya Kilimatinde na Kiomboi, Manyoni, Makiungu, Iambi, vitoa vya afya Ndago, Ikungi na Sokoine.
Alisema kuwa nia ya Tanzania ni kupunguza vifo vya akina mama wakati wa uzazi, jambo alilosema linawezekana.

Chanzo:Tanzania daima

FUNDI RADIO AFA BAADA YA KUZIDIWA GESTI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

FUNDI radio maarufu mjini hapa, Daniel Mosha (53), amefariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya Mkoa baada ya kuugua ghafla akiwa anafanya mapenzi na mwalimu mmoja katika nyumba ya kulala wageni iitwayo Cheyo.
Tukio hilo limetokea jana majira ya saa 11:00 alfajiri katika nyumba hiyo iitwayo Cheyo chumba namba nne, wakati fundi huyo akijivinjari na mpenzi wake huyo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACP), Geofrey Kamwela, alisema fundi huyo alifariki Oktoba 14 mwaka huu saa 10.30 jioni katika hospitali ya Mkoa alikokimbizwa baada ya kuzidiwa akiwa gesti.
Aidha, Kamanda Kamwela alisema kuwa Oktoba 13 mwaka huu majira ya jioni, marehemu akiwa nampenzi wake wa muda mrefu, Serafine Lucian (56), mwalimu wa shule ya Msingi Manguanjuki manispaa ya Singida, walipanga chumba namba nne kwa ajili ya mapumziko ya usiku mzima.
"Ilipofika alfajiri saa saa 11 Oktoba 14 mwaka huu, mwanaume huyo alianza kuugua ghafla huku akikoroma na ndipo mwalimu Serafine, aliamka na kumwita meneja wa nyumba hiyo na kumweleza juu ya hali ya mpenzi wake," alisema.
Alisema meneja pamoja na mwalimu huyo, walifanya juhudi za kumkimbiza hospitali ya Mkoa ili kuokoa maisha yake lakini mambo yaliendelea kuwa magumu.
Hata hivyo, Kamanda Kamwela, alisema uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa katika chumba walichopanga wapenzi hao, pamoja na vitu vingine zilikutwa paketi tupu za pombe kali aina ya viroba vilivyotumika.
"Tunaendelea na uchunguzi ili kujua kama kuna mtu au watu wanaohusika na kifo hicho cha fundi radio, lakini tunamshikilia mwalimu huyo kwa uchunguzi zaidi, ili pamoja na mambo mengine kuchunguza iwapo kuna mtu au watu waliohusika na kifo hicho,” alisema Kamwela.
Chanzo:Tanzania Daima

BAADA YA DIAMOND KUPANDA KWENYE STAGE NA NGUO ZA JESHI, JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA (JWTZ) LATOA TAARIFA







JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA
KURUGENZI YA HABARI NA UHUSIANO

Simu ya Upepo   : “N G O M E”            Makao Makuu ya Jeshi,
Simu ya Mdomo : DSM  22150463       Sanduku la Posta 9203,
Telex                     : 41051                        DAR ES SALAAM, 20 Octoba, 2014
Tele Fax                : 2153426
Barua pepe       : ulinzimagazine@yahoo.co.uk
Tovuti                  : www.tpdf.mil.tz
                  
Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linatoa taarifa kwa wananchi wote kuwa ni kosa kisheria kumiliki au kuvaa sare za JWTZ kwa mtu yeyote asiyehusika.
          Aidha,  kumeonekana matukio kadhaa ya baadhi ya vikundi, ama mtu mmoja mmoja kumiliki au kuvaa sare za JWTZ.  Inakumbushwa kuwa kwa yeyote atakayeonekana amevaa ama kumiliki sare hizo sheria itachukua mkondo wake. 

  
Imetolewa  na  Kurugenzi  ya  Habari  na  Mahusiano
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
S.L.P  9203,   Dar es Salaam,  Tanzania.


Kwa Mawasiliano zaidi: 0783 - 309963


Chanzo: Pamoja Blog
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

TAARIFA FUPI YA MAFANIKIO YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA SERIKALI MKOANI SINGIDA KIPINDI CHA 2005 - 2014‏

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dokta Parseko Vicent Kone
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dokta Parseko Vicent Kone.
Katibu Tawala Mkoa wa Singida Bw. Liana Hassan.
Katibu Tawala Mkoa wa Singida Bw. Liana Hassan.
Jengo la OPD katika Hospitali Mpya ya rufaa ya Mkoa wa Singida.
Jengo la OPD katika Hospitali Mpya ya rufaa ya Mkoa wa Singida.
Jengo la utambuzi wa Magonjwa katika Hospitali Mpya ya rufaa ya Mkoa wa Singida.
Jengo la utambuzi wa Magonjwa katika Hospitali Mpya ya rufaa ya Mkoa wa Singida.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

Tamasha la Fiesta 2014 laiteka Singida, leo Jumapili kurindima mjini Dodoma


 Baadhi ya mwashabiki wa tamasha la Fiesta 2014 wakishangilia kwa hisia,wakati shoo ikiendelea jukwaani ndani uwanja wa Namfua mjini Singida.
 Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka kampuni ya No Fake Zone,Linah Sanga ambaye kwa sasa anatamba na wimbo wake wa Oletemba,akiimba jukwaani mbele ya umati wa watu wakati wa tamasha la Fiesta lililofanyika jana katika uwanja wa Namfua,kulia ni mmoja wa wacheza shoo wake akiwajibika jukwaani.
 Kundi mahiri la muziki wa kizazi kipya litambulikalo kwa jina la Makomando wakilishambulia jukwaa la Fiesta hapo jana ndani ya uwanja wa Namfua mjini Singida.
 Sehemu ya umati wa watu wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye jukwaa la Fiesta ndani ya Uwanja wa Namfua hapo jana mjini Singida.
 Mmoja wa mashabiki akishangilia huku akiwa amebebwa
 Msanii wa muziki wa bongofleva,Mr Blue a.k.a Kabyssal akiimba mbele ya umati wa wakazi wa mji wa singida waliojitokeza kwenye tamasha la Fiesta lililofanyika hapo jana ndani ya uwanja wa Namfua.
 Sehemu ya umati wa watu ndani ya tamasha la Fiesta mjini Singida hapo jana katika uwanja wa Namfua
10
 Ilikuwa ni shangwe tu ndani ya uwanja wa Namfua wakati tamasha la Fiesta likiendelea.
 Msaniii mwingine anaefanya vyema katika anga ya muziki wa bongofleva,kupitia kundi la WEUSI,Niki wa Pili akiwaimbisha mashabiki wake
 Shabiki kapagawa na yaliyokuwa yakijiri jukwaani.
 Badala ya kuwa watazamaji tu,nao pia walikuwa wakijimwaya mwaya taratiibu.
 Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka nyumba ya vipaji ya THT,Rachael akiwaimbisha mashabiki wake (hawapo pichani),wakati wa tamasha la Fiesta likendelea ndani ya uwanja wa Namfua mjini Singida hapo jana.
 Msanii mkongwe wa muziki wa kizazi kipya,Dully Sykes anaetamba na wimbo wake wa Togola akiwaimbisha mashabiki wake,kwenye tamasha la Fiesta ndani ya uwanja wa Namfua mjini Singida hapo jana.
 Mmoja wa wasanii mahiri wa muziki wa kizazi kizazi kipya atambulikae kwa jina kisanii Mwana-FA akiimba mbele ya umati wa wakazi wa Singida waliojitokeza kwenye tamasha la Fiesta 2014,lililofanyika jana ndani ya uwanja wa Namfua.
 Msanii Mwana-FA na Linah wakiimba kwa pamoja jukwaani,huku miluzi na makelele ya mashabiki yakiwa yametawala kila kona ya uwanja wakati wa tamasha la Fiesta likiendelea.
 Mashabiki wakishangilia
 
Wasanii mahiri wa muziki wa Bongofleva, Ney wa Mitego na Stamina wakilishambulia jukwaa kwa pamoja kupitia wimbo wao unajojulikana kwa jina la Huko kweni Vipi,ndani ya tamasha la Fiesta usiku wa kuamkia leo ndani ya uwanja wa Namfua mjini Singida.
Sehemu ya umati wa wakazi wa Singida wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri ndani ya tamasha la Fiesta.PICHA NA MICHUZI JR-SINGIDA.


Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2011. Singida Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogz za Mikoa