Home » » MAGUFULI ATAKIWA KUVUNJA MFUMO WA SASA WA CCM.

MAGUFULI ATAKIWA KUVUNJA MFUMO WA SASA WA CCM.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Dk. John Magufuli.

Kanisa la Christian Mission Fellowship Tanzania, limesema ili Watanzania warejeshe imani kwa serikali yao, kuna umuhimu wa anayegombea nafasi ya urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli, avunje mfumo uliopo sasa ndani ya chama hicho.
 
Makamu Askofu Mkuu wa kanisa hilo, Donald Mhango, akizungumzia uteuzi wa CCM uliompa ushindi Dk. Magufuli, alisema mfumo unaotakiwa kuvunjwa ni ule unaosababisha baadhi ya viongozi kujihusisha na ufisadi, rushwa, kutowajibika ipasavyo kwenye nafasi za kazi, wanaosababisha taifa hasara na kutowajibishwa kwa mujibu wa sheria.
 
Askofu Mhango alisema Watanzania wengi wanatarajia Dk. Magufuli ,atatumia ujasiri alionao kuwaondoa madarakani wale wote wanaotuhumiwa kuliingizia taifa hasara, hali ambayo imeendelea kudidimiza hali za wananchi na kuendelea kuwa maskini.
 
“Naamini Dk. Magufuli ameinuliwa kwa kusudi maalum. Kikubwa tunachotarajia afanye ni kuvunja mfumo wa serikali ili kurudisha imani ya Watanzania ambayo siyo siri kwamba imetoweka. Kwa sasa taifa limegawanyika vipande vipande, vikiwamo vya udini, ukabila na tofauti za kiuchumi,” alieleza Askofu Mhando.
 
Alitaja sababu kubwa iliyowafanya wananchi kukosa imani kwa serikali yao kuwa ni viongozi wengi kuhusishwa na kashfa mbalimbali za kukosa uadilifu ikiwamo za rushwa na kutowajibika, kiasi cha baadhi yao kushuhudiwa wakiitwa mizigo lakini wakiendelea kuachwa wabaki madarakani.
 
Hata hivyo Askofu Mhando alisema ili serikali ya awamu ya tano ifanikiwe kubomoa mifumo hiyo ya kiutawala, ni lazima kila Mtanzania kwa imani yake amuombe Mungu ili aingilie kati
SOURCE: NIPASHE

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2011. Singida Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogz za Mikoa