Home » » Polisi Singida yapiga marufuku maandamao ya UKAWA kupinga ushindi wa Rais mteule Dk. Magufuli

Polisi Singida yapiga marufuku maandamao ya UKAWA kupinga ushindi wa Rais mteule Dk. Magufuli

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
RPC
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Singida, Thobias Sedoyeka akizungumza na waandishi wa habari juu ya kupinga maandamano ya vyama vinavyounda Katiba ya Wananchi (UKAWA) kupinga matokeo ya tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kumtangaza Rais Mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. John Pombe Magufuli.
Na Hillary Shoo, SINGIDA
JESHI la polisi Mkoani Singida limepiga marufuku maandamano yanayotarajiwa kuandaliwa na kufanyika chini ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) ya kupinga ushindi wa Rais Mteule John Magufuli katika Wilaya zote za Mkoa huo.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo, Kamanda wa Polisi (ACP) Thobias Sedoyeka alisema kuwa polisi wamepata taarifa za kiintelijensia kuwa (kesho) leo kuwa vyama hivyo chini ya mwavuli wa UKAWA, viko katika mipango ya chini kwa chini ili kufanya maandamano ya kupinga matokeo hayo ya Urais.
“Uchunguzi huo unaonesha kuwa maandamano hayo yatashirikisha makundi mbalimbali ya watu hususan zaidi vijana na kupita sehemu mbalimbali za Miji kabla ykuhitimishwa katika ofisi za CHADEMA Mkoa wa Singida.” Alisema Kamanda Sedoyeka.
“Sisi Jeshi la polisi Mkoani Singida tunasema kuwa maandamano hayo ni batili na hatuyaruhusu kwa namna yoyote ili huku tukiwataka viongozi wa vyama hivyo kutofanya hivyo kamwe na badala yake watumie njia stahiki za utawala wa kisheria ikiwemo kwenda kwenye vyombo ambavyo vinawajibika kushughulikia malalamiko yao.” Alisisitiza.
SEDOYEKA
RPC Singida Thobias Sedoyeka.
Hata hivyo alionya vijana kutojihusisha na maandamano hayo na badala yake waendelee na kazi zao za uzalishaji mali kwani jeshi la polisi halitasita kutumia nguvu za ziada pale itakapobidi kitendo ambacho huenda kikaathiri utendaji kazi wao pamoja na watu wengine ambao hawatahusika na maandamano hayo.
Hata hivyo Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Singida, Shaban Limu alisema walipeleka barua kwa OCD wa Wilaya zote za Mkoa wa Singida juu wa kufanya maandamano hayo ya amani, lakini wamezuiwa kufanya hivyo na Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Singida.
Aidha Limu alisema hivi sasa wanawasiliana na makao makuu ya CHADEMA, kupinga amri hiyo ya Kamanda wa polisi Thobias Sedoyeka kwani kikatiba ni halali kufanya maandamano bila kuvunja sheria za nchi, kwani kazi ya polisi ni kuwalinda wakati wakiandamana.
limu
Mwenyekiti wa (Chama cha CHADEMA) Mkoa wa Singida, Shaban Limu akizungumza na waandishi wa habari Mkoani Singida juu ya hatua yao ya kupinga amri ya Kamanda wa polisi Mkoani humo Thobias Sedoyeka ya kuzuia maandamano yao kupinga ushindi wa Dkt. John Magufuli .
ofisi
Ofisi za CHADEMA Mkoa wa Singida (PICHA ZOTE NA HILLARY SHOO).
Mo Blog

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2011. Singida Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogz za Mikoa