Home » » Mbunge wa viti maalum mkoa wa Singida, Mlata ashiriki zoezi la usafi Manispaa ya Singida

Mbunge wa viti maalum mkoa wa Singida, Mlata ashiriki zoezi la usafi Manispaa ya Singida

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

IMG_1128
Mbunge wa viti maalum mkoa wa Singida, Martha Mosses Mlata, akishiriki kutekeleza agizo ya rais Dk. John Pombe Magufuli la Watanzania wote kufanya usafi katika maeneo yao, kama sehemu ya maadhimisho ya sherehe za Uhuru kutimiza miaka 54, kwa kufanya usafi kwenye chuo cha wasioona cha mjini hapa. Pamoja na kufanya usafi chuoni hapo, Mlata alitoa msaada wa vifaa mbalimbali ikiwemo viti vya plastiki 150.Thamani ya msaada huo, ni zaidi ya shilingi 6.3  milioni.
IMG_1124
IMG_1132
IMG_1142
Mbunge wa viti maalum mkoani Singida, Martha Mosses Mlata, akikabidhi msaada wa vifaa mbalimbali wenye thamani ya zaidi ya shilingi 6.3 milioni kwa uongozi wa Chuo cha wasioona cha mjini hapa. Msaada huo ni sehemu ya maadhimisho ya sherehe za Uhuru kutimiza miaka 54.(Picha na Nathaniel Limu).
Na Nathaniel Limu, Singida
MBUNGE wa viti maalum (CCM) mkoani Singida,Martha Mosses Mlata, (9/12/2015) ametumia zaidi ya saa tatu kufanya usafi katika Chuo cha Watu Wasioona kilichopo Manispaa ya Singida.
Mlata ambaye alifuatana na baadhi ya wana CCM wa Manispaa ya Singida, alifanya usafi huo ikiwa ni kutekeleza agizo la Rais Dk.John Pombe Magufuli kama sehemu ya maadhimisho ya sherehe za kutimiza miaka 54 ya Uhuru.
Mbunge huyo alisema kuwa anamuuga mkono Rais Magufuli kwa kuhimiza usafi wa mazingira kitendo ambacho pamoja na mambo mengine,kitapunguza uwezekano wa kutokea kwa magonjwa ya mlipuko ukiwemo kipindupindu
“Tabia hii ya kufanya usafi kwenye maeneo yatu na yale mengineyo, inapaswa iwe endelevu kutokana na faida zake kuwa nyingi.Pia mazingira yakiwa masafi,yanapelekea kuvutia zaidi”,alisema mbunge Mlata.
Pamoja na kufanya usafi sehemu mbalimbali za chuo hicho ikiwemo maeneo ya vyoo,Mlata alitoa msaada wa vifaa mbalimbali vikiwemo vya kufanyia usafi, viti 150 vya plastiki na mazulia.Vifaa hivyo vina thamani ya zaidi ya shilingi 6.3 milioni.

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2011. Singida Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogz za Mikoa