Home » » KUPATA DAWA MKALAMA IMEKUWA VIGUMU

KUPATA DAWA MKALAMA IMEKUWA VIGUMU

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
KAIMU Mganga Mkuu wa Wilaya ya Mkalama mkoani hapa, Ephraim Kaphilimbi amesema agizo jipya la serikali la kutonunua dawa nje ya Bohari Kuu ya Dawa (MSD) limeongeza ugumu wa upatikanaji wa dawa katika wilaya yake.
Aidha, alisema muda MSD inaochukua kujibu maombi yao ni tatizo kubwa katika kuhakikisha kwamba hospitali zote za serikali wilayani humo zina dawa za kutosha.
Alikuwa akijibu hoja za wananchi na wadau wa afya waliokuwa wakisema kwamba ukosefu wa dawa, na kuzuiwa kupata matibabu katika hospitali mbili za misheni wilayani ni kikwazo kwao katika kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii.
Miongoni mwa waliolalamikia tatizo hilo ni madiwani Mohamed Juma, Ramadhani Mohamed na kiongozi wa dini maarufu kwa jina Shehe Jumanne.
“Ukosefu wa dawa ni tatizo kubwa na suala hili ni kubwa kwa kuwa limeanzia mbali ni suala la kitaifa,” alisema Kaimu Mganga Mkuu huyo na kuongeza kwamba sehemu kubwa ya mkanganyiko wa sasa wa dawa ni kutokana na maagizo hayo kwamba dawa zote zinunuliwe MSD.
Alisema, serikali inasema imeingiza fedha MSD moja kwa moja, lakini dawa hazifiki wilayani na majibu ya maswali kwanini hazijaja huwa yanakatisha tamaa.
Kwa maelezo yake, kutokana na mazingira hayo kwa sasa, Halmashauri haziruhusiwi kununua dawa nje ya maagizo ya serikali.
Alisema, pamoja na dawa kuwa tatizo wilaya hiyo inakabiliwa na ukosefu wa hospitali ya wilaya na zile zinazodhaminiwa zimesimamisha huduma za CHF kutokana na kuidai Halmashauri ya Mkalama fedha nyingi.
Hata hivyo, ilifafanuliwa katika kikao hicho kwamba ukosefu wa dawa ni tatizo kwa kuwa halmashauri husika zinaweza kukopa dawa NHIF wakati wanafanya kukamilisha mipango ya kusubiri dawa za MSD.
CHANZO ; HABARI LEO.

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2011. Singida Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogz za Mikoa