Home » » USHAWISHI UTUMIKE KUVUTIA WATU CHF, SI KUWALAZIMISHA.

USHAWISHI UTUMIKE KUVUTIA WATU CHF, SI KUWALAZIMISHA.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
KATIBU Tawala wa Mkoa wa Singida, Festo Kang’ombe ametaka kuwepo na nguvu ya ushawishi katika kupata wanachama wa Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) na si kuwalazimisha wananchi na kusababisha wakimbilie porini kwa sababu za michango.
Alisema hivyo wakati akifungua mkutano wa siku ya wadau katika wilayani hapa, ikiwa ni sehemu ya upitishaji wa mchakato wa kutungwa kwa sheria ndogo na kutengenezwa hati kwa lengo la kuwezeshwa kuendeshwa kwa mpango wa CHF wilayani humo.
Mchakato huo unaokwenda hatua kwa hatua, unatarajiwa kukamilishwa wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani.
Alisema, pamoja na uzuri wa mpango huo ambao ni wa hiari, wananchi wanatakiwa kushawishiwa na si kulazimishwa kwa kutumia mabavu, ili wajiunga na CHF.
Kang’ombe alisema, wilaya ya Mkalama si ngeni katika utekelezaji wa mpango wa CHF na kwamba muitikio mkubwa utakaowezesha kuimarisha huduma za afya wilayani hapo utatokana na nguvu za hoja na wala si hoja za nguvu.
Alisema, wilaya hiyo mpya ilikuwa awali ikitekeleza mpango huo chini ya wilaya ya Iramba na ilionesha mafanikio makubwa tangu kuanzishwa kwake mwaka 2004 ndio maana wilaya nyingi zilifika kujifunza.
Kang’ombe alisema, alipokuwa Ofisa Mipango katika wilaya ya Kahama walifika kujifunza uendeshaji wa CHF, safari ambayo pia iliwafikisha Igunga na Mbinga.
Alisema, taifa lenye wagonjwa haliwezi kusonga mbele na uwekaji wa nguvu za pamoja utawezesha matatizo ya sekta ya afya yaliyopo kwa sasa kuondoka.
 CHANZO ; HABARI LEO.

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2011. Singida Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogz za Mikoa