Home » » Wanachama wa CCM Singida, wajitokeza kuvaa viatu alivyoviacha Mgana Msindai vya nafasi ya uenyekiti CCM mkoa

Wanachama wa CCM Singida, wajitokeza kuvaa viatu alivyoviacha Mgana Msindai vya nafasi ya uenyekiti CCM mkoa

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

IMG_1998
Mwana CCM, Martha Mosses Mlata (kushoto) akirejesha fomu za kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Singida kwa Katibu msaidizi CCM mkoa wa Singida, Adamu Makulilo leo.Nafasi ya Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Singida,iliachwa wazi na Mgana Izumbe Msindai aliyetimkia CHADEMA baada ya kushindwa kwenye kura za maoni wakati wa kinyang’anyiro za kura za maoni (nafasi ya ubunge) ndani ya CCM.
IMG_2001
IMG_2008
Mwanyekiti wa jumuiya ya wazazi (CCM) mkoa wa Singida, Yusuph Mwandami Gwayoka (kushoto) akikabidhiwa fomu ya kugombea nafasi ya mwenyekiti wa CCM mkoa wa Singida na Katibu msaidizi CCM mkoa wa Singida, Adamu Makulilo.Picha na Nathaniel Limu.
Na Nathaniel Limu, Singida
MBUNGE wa viti maalum (CCM)  mkoa wa  Singida, Martha Mosses Mlata ni miongoni mwa wana CCM sita ambao wamejitokeza kuomba kuziba nafasi iliyoachwa wazi na Mgana Izumbe Msindai ya mwenyekiti wa CCM mkoa aliyetimkia CHADEMA muda mfupi baada ya kushindwa kwenye uchaguzi wa kura za maoni (CCM) kugombea ubunge.
Wana CCM wengine waliochukua fomu hadi leo jioni toka zoezi la uchukuaji fomu lianze Januari sita mwaka huu asubuhi,ni Juma Hassan Kilimba, Mohammed Hamisi Missanga, Narumba Barnaba Hanje, Shafii Juma Mtaturu na Yusuh Mwandami Gwayoka.
Katibu msaidizi wa CCM mkoa wa Singida,Adamu Makulilo,alisema hadi sasa aliyekuwa mbunge wa jimbo la Iramba Juma Hassan Kilimba,Martha Mlata na aliyemaliza muda wake wa ubunge wa jimbo la Singida magharibi mwaka jana,Mohammed Hamisi Missanga,wameisha rejesha fomu zao.
Adamu alisema zoezi hilo la utoaji wa fomu bado linaendelea na linatarajiwa kukoma januari 10 mwaka huu saa kumi jioni.
“Nitumie fursa hii kuwaomba wana CCM  wajitokeze kwa wingi na hasa wale watakaojipima na kubaini wanao uwezo wa kuvaa viatu vilivyoachwa na Mgana Msindai,ili kuleta upinzani wa kweli utakaosaidia CCM kupata mwenyekiti atakayemudu kasi iliyopo hivi sasa nchini.Ada ya fomu ni kama bure kabisa, kwa sababu tunatoza fomu ‘buku’ tu (shilingi 10,000)”,alisema katibu msaidizi huyo.
Akizungumza na mwandishi wa habari hii kwenye viwanja vya CCM mkoa,Mlata alisema kuwa safari hii ni zamu ya mwanamke kuongoza chama tawala mkoani hapa,na kwamba mwanamke huyo si mwingine isipokuwa ni yeye (Mlata).
Alisema amejikagua na kujitathimini na kubaini kwamba anao uzoefu wa kutosha kuwatumikia wana CCM na wananchi kwa ujumla katika nafasi hiyo ya mwenyekiti CCM mkoa.
“Kupitia nafasi mbalimbali nilizozipata ikiwemo ya ubunge wa viti maalum,nafahamu vyema Chama Cha Mainduzi kinavyoongozwa,nazijua changamoto ya chama chetu kuanzia ngazi ya chini ya tawi hadi mkoa.Kwa ukweli huo,mimi ni chaguo sahihi kupewa nafasi iliyoachwa wazi na kaka yangu Msindai”,alisema.
Mlata aliyesema endapo atafanikiwa kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa CCM mkoa wa Singida,atatumia nguvu zake zote amoja na wanachama wengine,kurejesha umoja na mshikamano miongoni mwa wana CCM,ili mkoa uendelee kuwa wa CCM chama cheye sera zinazotekelezeka.
“Nitashirikiana na wana CCM wenzangu kukiimarisha chama na kuhakikisha CCM inawajengea mazingira mazuri wananchama wake ili waweze kuboresha hali zao za kiuchumi.Tatizo linalosababisha mwanachama ye yote wa chama cho chote cha saisa kuhama hama,ni umaskini tu.Lakini mtu kama ana uwezo mzuri kiuchumi,huyo sio rahisi kumurubuni au kumdanganya”,alisema Mlata.
Kwa upande wake Yusuph Mwandami Gwayoka, alisema kuitia nafasi yake ya mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi mkoa,anayo uzoefu wa kutosha wa kumudu nafasi ya mwenyekiti CCM mkoa.
“Mimi nimejipanga vema kushindana na wana CCM wenzangu katika kuwania nafasi hii ya mwenyekiti wa CCM mkoa wa Singida. Niwaase tu wagombea wenzangu kwamba tunakwenda kushindana na wala hatuendi kugombana.Kwa hali hiyo,kabla na baada ya matokeo kutangazwa,tuendelee kudumisha umoja na mshikamano na ikiwezekana,ushirikiano tulio nao,tuuboreshe zaidi”,alifafanua Mwandami.
MO BLOG

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2011. Singida Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogz za Mikoa