Home » » BURUNDI YAWATAKA WATANZANIA KUMUUNGA MKONO RAIS MAGUFURI.

BURUNDI YAWATAKA WATANZANIA KUMUUNGA MKONO RAIS MAGUFURI.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Rais Pombe Magufuri.

SERIKALI ya Burundi na chama tawala cha nchi hiyo CNDD-FDD imewataka Watanzania kumuunga mkono Rais John Magufuli katika azma yake ya kusimamia nidhamu ya viongozi na kuleta maendeleo kwa taifa.

Mkuu wa Wilaya ya Kibago mkoani Makamba nchini Burundi, Juma Albert alitoa kauli hiyo akiongoza ujumbe wa watu watano wa kiserikali na chama tawala cha nchini humo, waliohudhuria maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), yaliyofanyika kimkoa kwenye kijiji cha Munzenze, wilayani Buhigwe mkoani hapa.

Albert alisema, Serikali ya Burundi na chama tawala cha CNDD- FDD imekuwa ikifuatilia mambo yanayofanywa na Rais Magufuli na kwamba, wanamuunga mkono kwa yale anayofanya ambayo yamekuwa na tija kwa uchumi wa Tanzania.

Alisema, Magufuli pia amekuwa akilenga kuimarisha uchumi wa nchi yake sambamba na ustawi wa jirani zake ikiwemo Burundi. Pamoja na hayo viongozi hao walitoa shukrani zao kwa wananchi wa Kigoma kuendelea kuwahifadhi ndugu zao katika kambi mbalimbali za wakimbizi, kufuatia mapigano ya wenyewe kwa wenyewe nchini mwao.

Akizungumza katika maadhimisho hayo, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kigoma, Dk Walid Kabouorou aliwataka viongozi wa upinzani kukubali kwamba uchaguzi umekwisha na CCM ndio mshindi.

Alisema, kutokana na hilo, hawana budi kuungana na kutekeleza Ilani ya CCM kwa kuhakikisha miradi ya maendeleo iliyopangwa kutekelezwa inafanikiwa. Awali, Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Issa Machibya aliwataka wananchi kupeleka watoto wao shule ili kuunga mkono mpango wa Serikali wa kuondoa ujinga kwa Watanzania kutojua kusoma na kuandika.

Alisema, kumekuwa na tabia ya kuwaficha watoto walemavu na kuwanyima haki yao ya kupata elimu, hivyo aliitaka jamii kuwafichua wote wenye kuendekeza ukatili huo dhidi ya wenye ulemavu.
 CHANZO: HABARI LEO

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2011. Singida Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogz za Mikoa