Home » » RAIS MAGUFULI AOMBOLEZA POLISI WALIOKUFA AJALINI SINGIDA

RAIS MAGUFULI AOMBOLEZA POLISI WALIOKUFA AJALINI SINGIDA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Rais John Magufuli.
Rais John Magufuli, amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Inspekta Jererali, Ernest Mangu, kufuatia vifo vya askari watatu waliopoteza maisha katika ajali ya gari iliyotokea juzi katika kijiji cha Isuna, wilayani Ikungi mkoani Singida.
 
Askari waliopoteza maisha katika ajali hiyo ni Inspekta Miraji Mwegelo, Sajenti Elias Mrope na Sajenti Gerald Mtondo.
 
Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari jana na Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Gerson Msigwa, Rais amesikitishwa na vifo vya askari hao, ambao wamekutwa na mauti wakiwa wanatekeleza majukumu yao ya kazi.
 
“Kupitia kwako Mkuu wa Jeshi la Polisi, natoa pole nyingi kwa familia za askari waliopoteza maisha, ndugu, jamaa na marafiki pamoja na askari wote wa jeshi hilo ambao wameguswa kwa namna ya pekee na msiba huu,” ilieleza taarifa hiyo.
 
Rais Magufuli pia amewatumia salamu za pole askari walioumia katika ajali hiyo, akiwamo Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarabi Mkoa wa Singida, Mratibu wa Polisi, Peter Magira na kuwaombea wapone haraka ili waendelee na majukumu yao ya kila siku.
CHANZO: GAZETI LA NIPASHE

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2011. Singida Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogz za Mikoa