Balozi asema Rais Magufuli ameipaisha Tanzania kimataifa

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mwigulu Nchemba (kushoto) na mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Singida, Martha Mlata wakikabidhi zawadi ya boga kubwa lenye kilo zaidi ya 7 Balozi wa China nchini, Dk Lu Youqing. (Na Mpigapicha Wetu).
SERIKALI ya China imeiunga mkono serikali katika mkakati wake wa kutoa elimu bure, ikisisitiza kuwa chini ya uongozi wa Rais John Magufuli, Tanzania inasifika duniani.
Katika kuunga mkono elimu bure, ubalozi wa nchi hiyo nchini umetoa msaada wa madawati 400 yenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 28 kwa shule mbalimbali za msingi katika wilaya ya Iramba mkoani Singida.
Balozi wa China hapa nchini, Dk Lu Youq’ng alisema msaada huo ni moja ya juhudi za nchi yake kuiunga mkono Serikali ya Tanzania katika kutoa elimu bure. “Wakati mimi nimechangia madawati 300, Kampuni inayochimba madini hapa ya Sun Shine Group imechangia madawati 100 ili kuniunga mkono,” alifafanua.
Akikabidhi madawati hayo katika mikutano mitatu tofauti kwenye mji wa Kiomboi, Shelui na Misigiri, Balozi Youq’ng alisisitiza umuhimu wa Tanzania kuwekeza kwenye elimu kuwaletea wananchi wake maendeleo ya kweli.
“Hata kama nchi ni maskini kiasi gani, lazima elimu itiliwe mkazo; tena iwe ni elimu bora na elimu bora haiwezi kuja kwa wanafunzi kukaa chini. “Madawati ni moja ya mambo ambayo yanamjengea mwanafunzi mazingira mazuri ya kujifunzia,” alisema.
Aliongeza, “kutokana na umuhimu huo, ndio maana mbunge wenu aliponijia na kuniomba msaada wa madawati, sikusita hata kidogo. Nilijua anafanya hivyo ili kuisaidia jamii yake kuboresha elimu”. Aliyeomba msaada huo ni Mbunge wa Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba.
Aidha, balozi huyo amewapongeza wakazi wa mkoa wa Singida kwa kumchagua Dk Magufuli kuwa Rais na kuongeza kusema kuwa chini ya uongozi wake sasa Tanzania inasifika duniani kote. “Nitahakikisha nchi yangu inaendelea kusaidia maendeleo ya nchi hii kwa kuwa urafiki wetu ni wa enzi na enzi,” alisema.
Awali, Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mathew Mtigumwe alisema kuwa mkoa unathamini msaada huo kwa kuwa umepunguza kwa kiasi kikubwa upungufu wa madawati 4,016 ambayo wilaya hiyo ilikuwa nao.
Chanzo Gazeti La Habari Leo

UWANJA WA NDEGE SINGIDA NI 'JIPU' NANI WA KULITUMBUA?

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
mfanyakazi  wa  kikosi  cha zimamoto na uokozi katika  uwanja  wa  ndege wa mkoa wa Singida akijiandaa  kwa kukifanyia majaribio  kifaa chake  cha  kuzimia moto wakati  ndege  iliyombeba balozi wa China nchini Dr  Lu Yong,ng ikiwasili katika  uwanja  huo jumapili ya May 29 wakati wa  ziara  yake wilayani Iramba
Hapa mfanyakazi  huyo akiwa pekee yake  huku akifanya kazi  tatu kwa  wakati mmoja kuelekeza ndege  hiyo ,kushika kifaa cha  kuzimia moto iwapo  hitirafu  itajitokeza na tatu kuweka gogo kwenye taili la ndege  baada ya kutua
Hapa  akielekea  kuelekeza eneo la  kutua
Hapa  akimwelekeza rubani wa  ndege hiyo huku  kulia kifaa kinachotumika kama gari la zimamoto na uokozi likiwa limeegeshwa kulia
Hapa  anakamilisha  kuelekeza eneo la  kutua anajiandaa kurudi  kuchukua kigogo kwenye gari  hili maalum ambalo kweli  bado mamlaka  ya  viwanja  vya ndege  vinapaswa  kulitazama   hili pasipo kusubiri majanga  ili  kuunda tume ya uchunguzi wa kitakachotokea
Ndege  ikiwa  imetua huku kifaa kinachotumika kama  gari la zimamoto na uokozi  kikiwa pembeni na mhudumu wa kifaa hicho  kushoto
Rubani  akimtazama  mfanyakazi  huyo mmoja anayefanya kazi  tatu kwa  wakati mmoja katika  uwanja wa ndege Singida
Hapa  akielekea  kuweka kigogo kwenye ndege  ushauri  wetu matukiodaimaBlog kwanza kwa kamati ya  ulinzi na usalama mkoa  wa Singida  kulitazama suala   hili la kiusalama kwa jicho la tatu kwani hatuombi jambo basi kutokea  ila ni  vema kinga  kuliko  tiba ,pili uongozi wa kiwanja  hicho  cha ndege kuongeza  wafanyakazi na hata  kuomba gari la kisasa katika uwanja  huo , tatu wizara  husika  kulitazama   hili na mwisho uongozi wa viwanja vya ndege nchini kutoka ofisini na kuzungukia  viwanja  vyote kikiwemo  hiki  cha Singida kuangalia changamoto  zake vinginevyo hili ni  jipu sasa ni nani wa  kujitolea  kulitumbua ?

TAASISI ZA SERIKALI ZILIZOUNGANISHWA NA MFUMO WA SIMU ZENYE ITIFAKI YA INTANETI ZATAKIWA KUTUMIA HUDUMA HIYO KUPUNGUZA GHARAMA YA MAWASILIANO.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Na. Aron Msigwa –MAELEZO.

Serikali kupitia Wakala ya Serikali Mtandao (e-Government Agency) imezitaka taasisi zote zilizounganishwa kwenye mfumo wa simu zenye itifaki ya intaneti (Internet Protocol (IP) ambazo zinatumia intaneti kuzitumia simu hizo katika mawasiliano yao kila siku ili kuboresha utendaji kazi na kupunguza gharama za mawasiliano Serikalini.
Meneja  Habari, Elimu na Mawasiliano wa Wakala hiyo Bi. Suzan Mshakangoto amesema  kuwa Serikali imeamua kusisitiza matumizi ya simu hizo ili kuziwezesha taasisi  za Serikali kuwa na mawasiliano yaliyo bora, salama na kupunguza gharama za mawasiliano.
Amesema kuwa Serikali kupitia Wakala ya Serikali Mtandao (eGA) imeunganisha taasisi za  Serikali 72 ambazo zinajumuisha Wizara, Idara  zina zojitegemeana na Wakala za Serikali na kuongeza kuwa taasisi hizo zimeunganishwa na Mtandao wa Mawasiliano wa Serikali yaani Government Communication Network (Govnet)’ unaowezesha mfumo wasimu hizo kufanya kazi kwa ufanisi.
  Kupitia mfumo wa simu hizi zenye itifaki ya intaneti mtumishi wa taasisi  iliyounganishwa anaweza kupiga simu kwenda taasisi nyingine ya nje ikawa kama amepiga simu ya ‘extension’ ndani ya ofisi moja Amesema Bi. Suzan.
Aidha, amesema Taasisi za umma zitanufaika moja kwa moja na simu hizo kwa kuwa, taasisi hizo zitaweza kubadilisha na taarifa kupitia mtandao mmoja tuwa Mawasiliano wa Serikali kwa usalama na uhakika. Pia simu hizo zitawawezesha watumishi wa taasisi mbalimbali kufanya mkutano kwa njia ya simu wakiwa kwenye ofisi zao na hivyo kuokoa muda na gharama za usafiri.

Hata hivyo amesema taasisi za umma zilizopo katika mtandao wamawasiliano wa Seikali zitaendelea kuwasilia na na taasisi zilizo nje ya mtandao huo kwa kupitia mtoa huduma wa simu za mezani (PSTN Provider) kama vile TTCL.

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2011. Singida Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogz za Mikoa