Home » » Huduma ya Tigo 4G LTE yazinduliwa Singida, sasa ipo miji 23 nchini

Huduma ya Tigo 4G LTE yazinduliwa Singida, sasa ipo miji 23 nchini

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
 Meneja wa Kanda ya Kaskazini kutoka Tigo, Aidan Komba, akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani) kuhusu uzinduzi wa huduma ya 4G LTE mkoani Singida, kushoto ni Meneja Mauzo wa Mkoa wa Singida Raymond Royer.
Waandishi wa habari wakichukua matukio kwenye mkutano huo wa uzinduzi wa Huduma ya 4G LTE mkoani singida mapema leo.



Singida, Mei 22, 2017-Wateja wa Tigo mkoani Singida hivi sasa wanaweza kufurahia  kuunganishwa na huduma ya intaneti ya kasi kufuatia kampuni hiyo kupanua huduma yake ya 4G LTE katika mji huo uliopo katikati ya Tanzania. Teknolojia ya 4G ina takribani kasi ya mara tano zaidi ya teknolojia ya 3G ambayo inapatikana hivi sasa katika soko.
Kwa mujibu wa Meneja wa Tigo Kanda ya Kaskazini Aidan Komba ni kwamba upanuzi wa huduma hiyo unafuatia  mafanikio yaliyopatikana  baada ya kuizindua katika mji mingine mikubwa nchini.
Komba alisema  kwa kuifanya  huduma ya 4G kupatikana Singida, “Tigo  kwa mara nyingine tena imeonesha  kujikita kwake katika kuboresha  mabadiliko katika mtindo wa maisha ya kidijitali na inavyoongoza katika kutoa teknolojia ya kisasa  na ubunifu katika soko hili.”
Alitangaza kuanza kwa enzi mpya za kidijitali katika historia ya mawasiliano  ndani ya Singida akibainisha kwamba Tigo 4G LTE itahakikisha  kunakuwepo uwezo mkubwa na muhimu  katika kuwaunganisha wateja ndani ya mkoa huo.
“Singida  ni kituo  muhimu kibiashara kwa mikoa ya kati na kaskazini mwa Tanzania. Tunaamini kwamba wakazi wa Singida, jumuiya ya kibiashara na wadau wataufurahia  huduma Tigo 4G LTE na hivyo kuzifanya shughuli zao kwa njia ya mtandao kuwa rahisi zaidi.”
“Mawasiliano ya simu ni nguzo muhimu kwa jamii iliyoendelea. Kwa hiyo mtandao wa 4G utachangia katika maendeleo ya sekta mbalimbali zikiwemo elimu, fedha na huduma za afya na hali kadhalika kukuza  uchumi na biashara”, alisema  Komba.
“Kama mnavyojua, Tigo imekuwa mstari wa mbele  katika kuzisaidia jamii zinazotuzunguka, na mfano mzuri ukiwa ni uchimbaji wa visima 12  ambavyo tulivitoa kama msaada  kwa vijiji vya Singida mwaka jana,”  Komba alibainisha.
Aliongeza kwamba gharama ya vifurushi vya 4G LTE ni sawa na ile ya vifurushi vya 3G na kufafanua kuwa wateja wanachotakiwa  ni kuwa na kifaa  kinachowezesha 4G LTE  ama simu ya kisasa (Smartphone) au modemu ikiwa na kadi ya simu ya 4G LTE ili kuwawezesha kupata muunganisho na 4G LTE. Alieleza kuwa wateja wanaweza kubadilisha au kununua  kadi ya simu ya 4G LTE kutoka katika duka la Tigo la huduma kwa wateja  lililopo Singida Mjini.
Akizungumzia uwekezaji  katika mtandao,  Komba alisema kwamba Tigo imewekeza kwa kiwango kikubwa katika miundombinu ya kisasa, ikilenga  kusaidia katika maendeleo endelevu ndani ya mkoa.
Alihitimisha kwa kusema, “Mipango  imo njiani katika kupanua huduma  kwa ajili ya mikoa iliyobakia ili hatimaye kuisambaza nchi nzima.”
Kwa upande wake, Meneja wa mkoa wa Singida wa kampuni ya Tigo, Raymond Royer  alibainisha umuhimu wa  huduma ya 4G na mchango wake katika kuboresha  huduma za uwanda mpana wa simu za mkononi.
Royer alisema, “Katika kipindi cha hivi karibuni  kumekuwepo ongezeko kubwa la idadi ya wateja pamoja na matumizi ya data; simu za kisasa idadi yake imeongezeka kwa asilimia 90 na hivyo kubadilisha namna tunavyowasiliana.”
Aliongeza, “Kwa hiyo teknolojia ya Tigo 4G LTE inampatia mteja faida mbili za  data zilizo na kasi kubwa  na kupunguza ucheleweshaji. Ni nguvu ya mabadiliko  ambayo itaboresha mtindo wa maisha ya kidijitali kwa wateja wetu.”
Mtandao wa 4G LTE  unamaanisha kasi  kubwa katika kurambaza (Surf) na kupakua mada  kutoka katika intaneti na kupiga miito ya mawasiliano ya kuonana (Skype). Kwa kiwango kikubwa inaboresha  uzoefu wa wateja katika kutiririsha video au kufanya mikutano. Hali kadhalika  inaweza kuhifadhi zana nyingi kama vile mkutano wa video, muonekanao wa hali ya juu, blogu za video, michezo na kutiririsha  video kutoka katika mitandao ya kijamii.


Mwisho

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2011. Singida Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogz za Mikoa