MISS SINGIDA 2012 KUJULIKANA JUNI MOSI.


Mratibu wa Miss Singida mkoani Singida Aunt Borah Lemmy akizungumza na mwandishi wa habari wa MO BLOG (hayupo kwenye picha) juu ya maandalizi ya shindano la kumsaka Miss Singida 2012.
Miss Singida 2011 Lizpbeth Pertti (katikati) na kulia ni mshindi wa pili Nyange Warioba na kushoto ni mshindi wa tatu Esther Gidion. (Picha zote na Nathaniel Limu).


Na Nathaniel Limu.
Shindano la kumsaka Miss Singida 2012 Redds, linatarajiwa kufanyika Juni Mosi mwaka huu kwenye ukumbi wa mikutano wa Aque vitae mjini Singida.
Akizungumza na mwandishi wa habari wa MO BLOG ofisini kwake, Mratibu wa Miss Tanzania mkoani Singida Aunt Borah Lemmy, amesema maandalizi yote muhimu yanaendelea vizuri ikiwemo warembo kuendelea kujisajili.
Amesema warembo mbali mbali waliopania kuwania nafasi hiyo, wanaendelea kuchukua fomu ambazo zinatolewa bure.
Aunt Borah amesema kwa sasa hawezi kutaja majina ya warembo ambao wamejisajili, lakini atafanya hivyo muda ukifika.
 Aidha ametoa wito kuwa warembo ambao watajikagua vizuri na kubaini kuwa wana sifa zote zinazohitajika, wafike kwa wingi kwenye salon yake kuchukua fomu na kuzijaja.
Mtaribu huyo amesema anatarajia kupata washiriki wasiopungua watatu kutoka kila wilaya ya Manyoni na Iramba.
Aunt Borah ameongeza kuwa shindnao la mwaka huu, litapambwa na burudani kabambe itakayotolewa na malkia wa mipasho nchini Bi.Khadija Kopa.
Aunt Borah huku kitabasamu pia amesema Katibu wa uenezi na itikadi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Nape Mnauye, atakuwa  mgeni rasmi kwenye shindano hilo .
Mratibu huyo alimeja viingilio kuwa vitakuwa  shilingi 10,000 kwa viti vya kawaida na 20,000 kwa viti vya VIP.
Alisema pamoja na shindano hilo kudhaminiwa na Redds, pia litadhaminiwa na kampuni ya Mohammed Enterprises Ltd ambayo Mkurugenzi wake Mkuu ni Mbunge wa jimbo la Singida mjini Mh. Mohammed Gullam Dewji.
Miss Singida wa mwaka jana (2011) Lizpbeth Pertti kutoka Itigi wilayani Manyoni hakuweza kushiriki miss kanda ya kati kwa kile akilichodaiwa ni kuwa na mimba. 
Kwa hisani ya Mo Blog

MKUU WA MKOA WA SINGIDA AMUAHIDI JK UTENDAJI BORA KUFUATIA UTEUZI WA WAKUU WA WILAYA.


Mkuu wa mpya wa wilaya ya Singida mwalimu Queene Mlonzi akiapa mbele ya mkuu wa mkoa wa Singida Dk.Parseko Vicent Kone.
Mkuu wa wilaya mpya ya Ikungi Manju Salum Msambya akiapa mbele ya mkuu wa mkoa wa Singida Dk.Parseko Vicent Kone.
Mkuu wa mkoa wa Singida Dk.Parseko Vichent Kone (wa pili kutoka kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na wakuu wapya wa wilaya ya Singida muda mfupi baada ya kuwaapisha.
Baadhi ya viongozi wa serikali na vyama vya siasa mkoani Singida waliohudhuria kuapishwa kwa wakuu wapya wa wilaya za mkoa wa Singida.
Mwenyekiti wa CHADEMA manispaa ya Singida John Kumalija akimpongeza mkuu mpya wa wilaya ya Manyoni Fatuma Taufiq muda mfupi baada ya kuapishwa.
Mkuu wa wilaya mpya ya Mkalama Mussa Chang’a akiwa kwenye picha na aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Iramba Grace Mesaki. (Picha zote na Nathaniel Limu).
Na Nathaniel Limu
Mkuu wa mkoa wa Singida Dk. Parseko Kone amempongeza rais Jakaya Kikwete kwa kuupa mkoa huo timu kabambe ya wakuu wa wilaya ambayo, amedai itasaidia pamoja na mambo mengine mkoa kujitosheleza kwa chakula.
Dk. Kone ametoa pongezi hizo muda mfupi baada ya kuwaapisha wakuu wa wilaya ya Manyoni Fatuma Hassan Taufiq, Mussa Chang’a wa wilaya mpya ya Mkalama, Mwalimu Queene Mlonzi wa Singida, Manju Salum Msambya wa wilaya mpya ya Ikungi, Mkuu wa wilaya ya Iramba Yahaya Nawanda ambaye hata hivyo hakuwepo kwenye hafla hiyo ya kuapishwa.
Amesema wakuu hao wa wilaya anawafahamu vizuri sana uwezo wao wa kuchapa kazi ambao kwa ushirikianao na wananchi na wadau wengine wa maendeleo mkoa utapaa kimaendeleo.
Kwa upande wa wakuu wa wilaya hao, mkuu wa wilaya mpya ya Mkalama Chang’a, amesema amefarijika mno na kitendo cha kuteuliwa na anakiona kuwa ni deni kubwa ambalo malipo yake ni kuwatumikia kikamilifu wakulima na wakazi wa Mkalama.
Amesema atahakikisha kilimo katika wilaya hiyo kinakuwa cha tija zaidi na masoko ya uhakika kwa mazao yao yanapatikana. 

Baraza Kuu NHC Lafanyika Singida

Meneja wa NHC Tawi la Mkoa Singida, Mariam Kambi, pamoja na wajumbe wengine wakiwa wamesimama tayari kumpokea mgeni rasmi
Wafanyakazi wa NHC Mkoa Singida wakiimba wimbo maalumu wa shirikaa hilo, kabla ya kufunguliwa kwa mkutano huo, leo mjini Singida
Sehemu ya wajumbe wa mkutano wa Taifa wa baraza kuu la wafanyakazi wa NHC, wa siku mbili leo na kesho unaofanyika mjini Singida
Naibu katibu mkuu wizara ya ardhi,nyumba na maendeleo ya makazi,Maria Bilia akifungua mkutano wa siku mbili wa baraza kuu
 Mkurugenzi mkuu wa NHC, Nehemia Mchechu akimkaribisha mgeni rasmi Naibu katibu mkuu, wizara ya ardhi nyumba na maendeleo ya makazi
Singida
Mei 12, 2012.
MKUTANO wa baraza la kuu la wafanyakazi wa shirika la nyumba nchini umefuguliwa leo mjini Singida na NAIBU katibu mkuu wizara ya ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi nchini, Bi. Maria Bilia, katika ukumbi wa Lake Hill Singida Motel.
Baraza kuu la NHC litafanyika kwa siku mbili, leo na kesho jumapili mkuu wa mkoa Singida Dk. Parseko Kone anatarajia kufunga.
Na Elisante John

AANGUKA KIZIMBANI BAADA YA HUKUMU NI MSHTAKIWA ALIYEKIRI KUUWA KISA ALINYIMWA MAKANDE YA HARUSI.


Mshitakiwa Juliana Ibrahimu akitolewa nje ya chumba cha mahakama kuu baada ya kuzirai kutokana na kuhukumiwa kutumikia jela miaka mitatu baada ya kukiri kosa la kuuwa bila kukusudia.
Askari polisi wa kike wakimpunguzia nguo mshitakiwa Juliana Ibrahimu ili waweze kupepea upepo aweze kuzinduka baada ya kuzirai kutokana na kuhukumiwa adhabu ya kwenda jela miaka mitatu kwa kosa la kuuwa jirani yake Maria Musa, bila kukusudia.(Picha zote na Nathaniel Limu).
Mwanamke mkazi wa kijiji cha Musimihi tarafa ya Ilongero wilaya ya Singida, Juliana Ibrahimu (52),ameanguka kizimbani na kisha kuzirai na kupoteza fahamu, baada ya kuhukumiwa na mahakama kuu  kanda ya Dodoma, kutumikia jela miaka mitatu.
Mahakama kuu kanda ya Dodoma inayoendelea na vikao vyake mjini hapa, ilimhukumu Juliana hukumu hiyo,baada ya kukiri kosa la kumuua jirani yake, Maria Musa, bila kukusudia kwa madai ya kunyimwa makande kwenye sherehe ya harusi.
Mshitakiwa Juliana, alihukumiwa adhabu hiyo pamoja na mtoto wake Pendo Yohana, ambaye naye atatumikia jela miaka mitatu kwa kukiri kosa hilo.
Baada ya washitakiwa hao kusomewa shitaka hilo la mauaji ambalo walilitenda agosti tano mwaka 2006, wote kwa pamoja, bila hofu kila moja kwa wakati wake alikiri kosa hilo .
Awali mwanasheria wa serikali Ahmed Seif, alidai mbele ya mrajisi wa mahakama hiyo, Renatus Rutatinisibwa, kuwa mnamo agosti tano mwaka 2006, muda usiofahamika,washitakiwa wote kwa pamoja, walimpiga Maria na kusababisha kifo chake siku 27 baadaye.
Alisema siku ya tukio, mshitakiwa Juliana akiwa amefuatana na mtoto wake Pendo, walikwenda nyumbani kwa marehemu (Maria) kumuliza ni kwa nini aliwanyima makande kwenye sherehe ya harusi (harusi hiyo iifanyika 4/8/2006).
Seif alisema marehemu aliwajibu kuwa hawezi kujibu swali hilo na kwamba mwenye uwezo wa kulijibu swali hilo , ni Dilu Mohammed.
Alisema washitakiwa walikasirishwa na jibu hilo liliyotolewa na marehemu na ndipo walipoanza kumshambulia.
Baada ya kutolewa kwa uhukumu hiyo, mshitakiwa wa kwanza,Juliana akiwa bado yupo kizimbani, alidondoka chini na mrajisi Rutatinisibwa, akaamuru atolewe nje kwenda kupepewa upepo.
Kwa hisani ya Mo Blog

WARATIBU ELIMU WAAGIZWA KUSIMAMIA KIKAMILIFU UTOAJI TAALUMA MKOANI SINGIDA.




Afisa elimu wa halmashauri ya wilaya ya Singida Bw.Patrick Mwaluli akitoa taarifa yake kwenye maadhimisho ya siku ya taaluma ya halmashauri hiyo.
Baadhi ya walimu wakuu wa shule za msingi na wakuu wa shule za sekondari katika halmashauri ya wilaya ya Singida waliozawadiwa simu za vingajani kwa kufanya vizuri katika taaluma.(Picha zote na Nathaniel Limu).
Afisa elimu mkoa wa Singida, Yusuph Kipengere, amewaagiza waratibu elimu kata, kuongeza kasi ya kuratibu na kusimamia kikamilifu utoaji taaluma, ili lengo la mkoa la kufaulisha mtihani wa kitaifa wa kumaliza elimu ya msingi kwa asilimia 85 lifanikiwe.
Kipengere ameto agizo hilo juzi wakati akizungumza kwenye kilele cha maadhimisho ya siku  ya taaluma wilaya ya Singida, yaliyofanyika Sepuka kilomita 27 magharibi ya Singida mjini.
Alisema jukumu la mratibu elimu wa kata, ni kuhakikisha kila mwalimu katika kata yake anatekeleza ipasavyo majukumu yake kwa mujibu wa mkataba wake wa kazi.
Katika hatua nyingine, Kipengere alitumia fursa hiyo kuupongeza uongozi wa elimu wilaya ya SIngida, kwa uamuzi wake wa kupongeza shule na walimu waliofanya vizuri katika utoaji taaluma mwaka jana.
“Utaratibu huu ni mzuri mno, binadamu ukimpongeza na kumpa zawadi hata iwe ndogo namna gani, hujisikia kuheshimiwa sana,na hivyo ataongeza juhudi zaidi katika utendaji wake wa kazi.  Naziomba wilaya zingine nazo ziige mfano huo”,alisema.
Halmashauri ya wilaya ya Singida, ina jumla ya shule za msingi 192 na shule za sekondari 61, kati ya hizo, shule 2 za msingi ni za binafsi na shule tano za sekondari ni za binafsi.

DKT. KONE ATOA ONYO LA KUTOKUPOKEA WALIMU WASIO NA WITO MKOANI SINGIDA.




Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Parseko Kone akizungumza kwenye kilele cha mahafali ya tano ya chuo cha walimu mjini Singida. Kulia ni Mkuu wa chuo hicho cha walimu Didas Monyo.
Mkuu wa chuo cha walimu cha Singida mjini Didas Monyo akitoa taarifa yake kwenye mahafali ya tano ya chuo hicho. Kulia ni Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Parseko Kone.
Baadhi ya wanachuo wa chuo cha ualimu cha Singida mjini waliohudhuria mahafali ya tano.
Bango la chuo cha ualimu na shule ya sekondari ya Singida iliyopo mjini Singida. (Picha zote na Nathaniel Limu).
Na.Nathaniel Limu.
Serikali ya mkoa wa Singida imedai kwamba haina nafasi kabisa ya kupokea walimu ambao hawana maadili ya ualimu kwa hofu kwamba wanamadhara makubwa katika ustawi wa sekta ya elimu.
Akizungumza kwenye mahafali ya tano ya chuo cha ualimu cha Singida mjini, Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Parseko Kone  amesema  kupokea walimu ambao hawana maadili ya ualimu, kuna hasara nyingi tena kubwa, zikiwemo kushusha taaluma na kuchangia kuharibu maadii ya wanafunzi.
 Kuhusu wahitimu walimu tarajiwa hao 559, Dkt. Kone amesema anafahamu kuwa watakuwa wamechagua au kuchaguliwa kwenda kufanya kazi ya ualimu katika mikoa mbali mbali ya Tanzania , ikiwemo mkoa wa SIngida.
Awali mkuu wa chuo cha ualimu Singida Didas Monyo, alitaja changamoto mbali mbali zinazokikabili chuo hicho, kuwa ni pamoja na upungufu wa vitabu vya kufundishia (kiada) na uhaba mkubwa wa maji.
 Kwa mujibu wa mwalimu Monyo chuo hicho kina wanahcuo 1,610, kati yao wapo wa mwaka wa kwanza 1051 na wa mwaka wa pili ambao ndio wahitimu ni 559.
Kwa hisani ya Mo Blog

Picha Za Jamii Ya Wahadzabe


Bw.
Abel Matayo, mkazi wa kitongoji Kipamba, kata Mwangeza, Iramba, wa
jamii ya Kihadzabe akiaga familia tayari kwa safari kuwinda
 Mmoja wa Wahadzabe, Abel Matayo akivuta sigara nyumbani kwake Kipamba, kata Mwangeza kabla ya kuelekea kuwinda porini.
Mhadzabe
akivuta kasi kusaka wanyama pori, lakini wanalalamika pori lao
kuvamiwa na jamii ya wafugaji, hasa Wasukuma na Wadaatoga, kiasi cha
kuharibu mazingira yao kwa kufyeka misitu ovyo kusaka mashamba na eneo
la malisho.

Na Elisante John Wa Mjengwa Blog

Singida Walivyoadhimisha Siku Ya Habari


DAS wilaya Iramba Singida, Yahaya Anania, akikabidhi sehemu ya msaada wa thamani ya zaidi ya Milioni moja


Wahadzabe wakisubiri msaada kutoka kwa klabu ya wanahabari mkoa Singida(SINGPRES0, walipotembelea ili kutoa msaada
Seif Takaza (kushoto), Mwenyekiti wa klabu ya wanahabari mkoa Singida akikabidhi sehemu ya msaada wa kibinadamu kwa katibu tawa

Singida,
Mei 04, 2012.
WANAHABARI mkoa Singida, kupitia klabu yao SINGPRESS,  wameungana na wanahabari wenzao duniani kwa kuadhimisha siku yao kwa kutoa msaada wa kibinadamu kwa jamii ya Wahadzabe wanaoishi kitongoji cha Kipamba, kata Mwangeza, wilayani Iramba.
Katika kuadhimisha siku hiyo, SINGPRESS imetoa msaada wa chakula na vifaa vya shule vyenye thamani ya zaidi ya Sh. Milioni moja.
Msaada huo ulikabidhiwa kwa mgeni rasmi, katibu tawala wa Wilaya Iramba, Yahaya Anania, kabla naye kumkabidi mwenyekiti wa kitongoji hicho, Edward Mashimba, ili kwa kushirikiana na wajumbe wa serikali ya kijiji, viwafikie walengwa waliokuwepo katika hafla hiyo.
Akipokea msaada huo, Anania aliwashukuru wanahabari, kutokana na kuithamini jamii hiyo, inayoishi maisha ya shida, kwa kuhamahama porini, huku chakula chao kikuu kikiwa ni mizizi, matunda na nyama pori, ambavyo hata hivyo hivi sasa imekuwa shida, kutokana na kuingiliwa na jamii ya wafugaji katika eneo lao.
Hata hivyo, katibu tawala huyo amesema serikali kwa kushirikianana wadau mbalimbali, imekuwa ikitoa misaada ili kuinusuru jamii na maisha ya shida.
Alisema tayari serikali imetenga eneo lo na kulifanya kuwa hifadhi maalumu, lakini pamoja na jitihada hizo, bado jamii ya wafugaji imeingilia makazi yao na kuanza kufyeka msitu ovyo katika makazi yao.
Kutokana na hali hiyo, katibu tawala huyo ameitaka jamii hiyo kuwafichua wote wanaoharibu mazingira, katika kipindi hiki ambacho taratibu zinaendelea kuwatoa wote waliovamia eneo lao.
Mapema mwenyekiti wa SINGPRESS, Seif Takaza, alimweleza mgeni rasmi kuwa, wanahabari wa Singida badala ya kuadhimisha siku yao mjini, walionelea vyema kwenda katika jamii hiyo ili watoe sauti yao ambayo itasikika katika jumuiya mbalimbali ndani na nje, waweze kusaidiwa.
“Sisi tumeona badala ya kuadhimisha siku hii mjini Singida, tumeona tuje kwenu tuwaletee hiki kidogo na jamii ingine ielewe matatizo yenu…..kuliko hivi mnavoishi miaka yote, lakini hakuna mabadiliko yoyote, naamini tutaungwa mkono na wengi,”alisema.
Msaada huo uliungwa mkono kwa kupigwa jeki na mfanyabiashara maarufu wa mjini Singida, Bw. Nagji, ambaye alijitolea katoni kadhaa za sabuni ya kufulia, Biskuti, madaftari na pipi, ili kuisaidia jamii hiyo.
Na Elisante John 

AJALI ILIYOHUSISHA MAGARI MATATU KWA MPIGO MKOANI SINGIDA.

Askari wa usalama barabarani mjini Singida, wakipima ramani sehemu ya ajali iliyohusisha Tipper T.733 BGX ambalo lilikuwa likiendeshwa na Adam Awadhi (amevunjika miguu yote) likitokea maeneo ya Mwenge kuja mjini kati kupitia barabara ya Singida – Arusha, liligonga kwa nyuma fuso.T.780 AFR. Fuso hilo  lilikuwa likielekea barabara ya Stanley Motel ambapo baada ya kugongwa liliangukia gari ndogo T.491 ARG.Dereva wa fuso lililokuwa limebeba sukari guru na dereva wa gari hilo amelazwa hospitali ya mkoa ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja.
Tipper T733 BGX  likiwa limegongana na fuso namba T780 AFR.
Baadhi ya wakazi wa Singida mjini wakishuhudia ajali iliyohusisha magari matatu jana  saa 9.20 alasiri.(Picha zote na Nathaniel Limu).
Kwa hisani ya Mo Blog
 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2011. Singida Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogz za Mikoa