HII NDIO SINGIDA AIRPORT.


 Hili ni bango utakalokutana nalo ukiwa unaelekea uwanja wa ndege wa Singida uliopo maeneo ya Sabasaba.
 Hii ni ofisi ya wahudumu wa uwanja wa ndege wa Singida.
Maandhari ya uwanja wa ndege wa Singida unapoingia.Hapo ndipo ndege zinapotuwa na kupaa.
Helicopter ikijiandaa kutua kwenye uwanja wa ndege wa Singida.
PICHA KWA HISANI YA CHUMA BLOG

Azimia Na Kulazwa Hospital Baada Ya TFD Kukamata Bidhaa Bandia Dukani Kwake...!



Kaimu meneja wa mamlaka ya chakula na dawa kanda ya kati(TFDA), Aberl Deule akizungumza na waandishi wa habari (hawapo kwenye picha) juu ya zoezi la kukagua bidhaa katika maduka ya wilaya ya Manyoni.

Moto ukiwa umewaka kuteketeza bidhaa zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni tano ambazo ni sumu na zile ambazo muda wake wa kutumika umekwisha.Bidhaa hizo zilikamatwa na TFDA katika baadhi ya maduka ya wilaya ya Manyoni.

Bidhaa ambazo zina sumu na zilizokwisha muda wake zilizokamatwa na TFDA kabla hazijateketezwa kwa moto.

Kaimu meneja wa TFDA kanda ya kati, Aberl Deule (wa kwanza kulia) akitoa maelekezo kwa muuza duka wa Manyoni mjini.

                       (Picha na habari, Nathaniel Limu).

Mamlaka ya Chakula na Dawa Kanda ya Kati (TFDA) imeteketeza bidhaa mbali mbali zenye thamnai ya zaidi ya shilingi milioni tano zikiwemo zile ambazo muda wake wa kutumika umeisha.

Bidhaa hizo ni pamoja na soda, juice, biskuti (muda wake wa kutumika uliishapita) na maziwa ya unga ya watoto wadogo aina ya Lactogen (18 na 2) ambayo ni bandia.

Bidhaa zingie zilizoteketezwa ni tani moja ya vipodozi hatari kwa matumizi ya binadamu yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni tatu.

Vipodozi hivyo vyenye kemikali za hydroquinone na zebaki, hutumiwa kubadilisha rangi ya ngozi (kujichubua).

Akizungumza muda mfupi baada ya kuteketeza bidhaa hizo, Kaimu Meneja TFDA Kanda ya Kati Aberl Deule, amesema msako wa ukaguzi wa kuangalia ubora na usalama wa chakula, dawa na vipodozi, ulianza Novemba 13 hadi 17 wilayani Manyoni.

Amesema msako huo ambao ni endelevu, ulifanyika katika maeneo 52 ya Manyoni mjini na Itigi, ambayo ni pamoja na viwanda vya kutengeneza vyakula, kuuzia vyakula, maduka ya vipodozi, maduka ya dawa za binadamu na yale ya dawa za mifugo.

Katika hatua nyingine, Kaimu Meneja huyo amewataka wananchi kuhakikisha wanatumia bidhaa ambao hazijaisha muda wake na zile ambazo  hazina sumu.
Kwa upande wa wafanyabiashara, Deule amewataka muda wote wahakikishe wanampatia mteja bidhaa zenye ubora, zisizokuwa na sumu na zile ambazo muda wake wa kutumika, haujaisha.

Amesema “Wafanyabiashara mnaojishughulisha na biashara za chakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba, hakikisheni majengo yenu yanasajiliwa na TFDA. Hakikisheni pia  bidhaa, mnazozalisha au kuuza ni salama kwa afya ya binadamu na bora”.

Deule amewataka wajenge utamaduni wa  kukagua bidhaa zao ili kubaini kama kuna bidhaa zilizopitwa muda wa matumizi na wajiepushe kuuza vipodozi vyenye viambato vya sumu.
Imedaiwa kuwa mfanyabiashara aliyefahamika kwa jina moja la Anord wa Manyoni mjini,  amelazwa katika hospitali  ya wilaya, muda mfupi baada ya shehena ya biadhaa zisizokuwa salama kwa matumizi ya binadamu, kukamatwa dukani kwake.

Martha Mlata Aendesha Harambee Ya Kuchangia Ujenzi Wa Msikiti Singida






Mbunge wa viti maalum (CCM) mkoa wa Singida,Martha Mlata (wa pili kushoto) akipokelewa na waumini wa msikiti wa Almasijidi Muhidini Baytulah wa kitongoji cha Mbuyu Senene kijiji cha Iguguno wilaya ya Mkalama,akipokelewa na waumini wa msikiti huo.,


Imamu wa msikiti wa Nuru Salama Unyankindi mjini Singida,Yahaya Mahiki akitoa nasaha zake kwenye hafla ya harambee ya kuchangia kumalizia ujenzi wa msikiti wa Almasijidi Muhidini Baytulah wa kitongoji cha Mbuyu Senene kijiji cha Iguguno wilaya ya Mkalama.


Mbunge wa viti maalum (CCM) mkoa wa Singida Martha Mlata akihutubia waumini wa kiislamu wa kijiji cha Igiguno wilaya ya Mkalama juzi waliohudhuria hafla ya harambee ya kuchangia umalizaji wa msikiti wa Almasijidi Muhidin Baytuhal.Kulia ni katibu wa wananwake wa msikiti huo Mama Mariamu na kushoto ni diwani wa kata ya Iguguno Bi Lyochi.



Baadhi ya waumini wa kiislamu waliohudhuria hafla ya kuchangia umalizaji wa msikiti wa Almasijidi Muhidin Baytuhal wa kitongoji cha Mbuyu Seenene wilaya ya Mkalama.Harambee hiyo ilikusanya zaidi ya shilingi milioni nne ambazo ni fedha taslimu na ahadi.
              
                       (Picha zote na Nathaniel Limu).

Inasikitisha : Watu watatu wa familia moja wafariki Dunia kwa kuangukiwa na nyumba



Mwandishi wetu, Singida Yetu

WATU watatu wa familia moja wamefariki duniani mkoani Singida baada ya kuangukiwa na nyumba.

Kamanda wa polisi mkoa wa Singida kamishina msaidizi Linus Sinzumwa amesema tukio  hilo limetokea jana majira  ya saa 10 alfajiri wakati  wanafamialia hao wakiwa wamelala.

Amewataja waliokufa kuwa ni baba wa familia hiyo Ramadhani   Amrani  (25) mkewe  Mariam Kondo  (23) na mtoto wao  Amrani Ramadhani  mwenye  umri wa miezi  saba wote wakazi wa eneo la Tambuka-Reli katika halshauri ya wilaya ya Manyoni mkoani Singida.

Kamanda Sinzumwa amesema siku ya tukio wanafamilia  hao walikuwa wamelala kwenye nyumba yao waliyojenga kwa tofali mbili na kuezeeka kwa miti na udogo mwezi mmoja uliopita.

Hata  hivyo amesema kutokana na  kile kinachosadikiwa kuwa kuzidishwa udogo juu,  miti iliyotumika kujengea nyumba hiyo ilivunjika, hali iliyosababisha udogo na kuta kuporomoka.

Kamanda Sinzumwa amesema  hali hiyo  ilisababisha wanafamilia hao watatu kukandamizwa na  kupondwa na miti, tofali na udogo hadi wakapoteza maisha yao  papo hapo.

Kufuatia  vifo hivyo jeshi la polisi mkoani Singida  limetoa wito kwa wananchi husani  wanaoishi kwenye nyumba za kienyeji maarufu kama tembe kuzifanyika ukarabati kabla ya mvua za masika.
Blogzamikoa

UHABA WA NYUMBA NA UPUNGUFU WA WALIMU WA SAYANSI KIKWAZO KIKUBWA KWA ELIMU KATA IPEMBE MKOANI SINGIDA.



Moja ya Majengo ya Shule yaliyojengwa na Mh. Mohammed Dewji Mbunge wa Singida Mjini.
Na. Nathaniel Limu
Kata ya Ipembe jimbo la Singida mjini inakabiliwa na uhaba mkubwa wa nyumba za kuishi walimu zipatazo 72 katika shule zake tatu ikiwemo moja ya sekondari.
Akitoa taarifa yake ya utekelezaji mbele ya  kikao cha baraza la madiwani wa manispaa ya Singida, diwani wa kata hiyo Twalib Kihara amesema shule ya msingi Ipembe inakabiliwa na upungufu wa nyumba za kuishi walimu 23, wakati shule ya  msingi Sumaye, pia ina upungufu wa nyumba 20.
Kihara amesema shule pekee ya sekondari ya kata hiyo, inahitaji nyumba za kuishi walimu 30, kwa sasa ina nyumba moja tu, na hivyo inakabiliwa na upungufu wa nyumba 29.
Katika hatua nyingine, Kihara ametaja baadhi ya changamoto zinazowakabili kuwa ni pamoja na upungufu wa walimu wa masomo ya sayansi katika shule ya sekondari Ipembe.
Diwani huyo mkongwe,alitaja changamoto zingine kuwa ni uhaba wa vitendea kazi na mwitikio mdogo wa jamii katika uchangiaji wa maendeleo.
Kwa mujibu wa diwani Kihara Kata ya Ipembe ni miongoni mwa kata 16 za manispaa na ina wakazi wapatao 2,833 kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2002.

ABIRIA ZAIDI YA 40 MKOANI SINGIDA WANUSURIKA KIFO BAADA YA BASI KUZIDIWA NA MZIGO.


Abiria zaidi ya 40 wamenusurika kufa baada ya basi dogo aina ya Costa lenye namba za usajili T.333 BNK lililokuwa linatoka Singida mjini  kwenda kijiji cha Ilunda wilayani Iramba, kupinduka katika eneo la kituo cha mabasi cha zamani kwa kile kilichodaiwa kuwa ni kuzidiwa na uzito wa mizigo iliyokuwa imepakiwa.
Picha mbalimbali zinazoonyesha basi hilo kupinduka.(Picha na Nathaniel Limu).
Picha na Mo Blog

HIKI NDICHO KIJIJI AMBACHO KIPO KATIKATI YA NCHI YA TANZANIA. TAZAMA HAPA


 Hapa ndio Sukamahela maeneo ya Manyoni, mkoani Singida, ambapo ndipo katikati kabisa ya nchi ya Tanzania. Alama yake iko kuleeee juu ya miamba hapo chini ambako ukaindalia kwa makini juu ya mwamba uliochomoza kulia pana alama kama ya nyani aliyesimama inayoashiria hivyo. 
PICHA NA MICHUZI BLOG

APENDEKEZA MAGARI 10 TU MSAFARA WA RAIS



Fidelis Butahe, Manyoni
MKAZI wa Kata ya Kintinku, Wilaya ya Manyoni, Hadija Ismail (58) amependekeza Katiba Mpya iwe na kifungu kinachosema misafara yote ya viongozi hususan Rais  iwe na magari yasiyozidi  10 ili kupunguza gharama za uendeshaji.

 Hadija alisema kuwa fedha zinazotumika kugharimia magari zaidi ya 30 yanayokuwa katika msafara mmoja wa Rais, zinaweza kujenga madarasa na kuwalipa fedha ya ziada walimu wanaoishi vijijini.

 
Akizungumza wakati akitoa maoni juu ya Katiba Mpya juzi, Hadija alisema  Katiba Mpya inatakiwa kueleza wazi suala hilo, kwa kuwa fedha za walipa kodi ndiyo zinazotumika kuendeshea magari hayo.
“Rais msafara wake unatakiwa kuwa na magari 10 tu, msafara wa Waziri Mkuu na Makamu wa Rais unatakiwa kuwa na magari matano matano,” alisema Hadija.
Alisema kuwa ni ajabu kwa viongozi wa Serikali kutumia magari mengi katika shughuli zao za kila siku wakati kuna baadhi ya vijiji, wananchi wanatumia jembe la mkono katika shughuli za kilimo.

“Mfano msafara mmoja unakuwa na magari 30, ukipiga hesabu ya gharama ya mafuta kwa magari 20, labda kutoka Dodoma mpaka Singida, zinatosha kabisa kununulia trekta la kilimo” alisema Hadija.
Pia Hadija alisema kuwa viongozi wote wanaochaguliwa na wananchi wanatakiwa kukaa madarakani kwa vipindi viwili tu na siyo kama ilivyo sasa ambapo wapo wabunge wenye miaka zaidi ya 30 bungeni.
“Diwani na mbunge nao wanatakiwa kuwa na vipindi viwili tu vya kugombea kama ilivyo kwa Rais” alisema.

Chanzo: Mwananchi

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2011. Singida Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogz za Mikoa