Wazazi manispaa ya Singida watakiwa kujenga utamaduni wa kuzungumza na watoto wao juu ya Ukimwi na namna ya kujikinga.



 Mkufunzi wa mafunzo juu ya UKIMWI na namna bora ya kujikinga na maambukizi ya virusi vinavyosababisha ugonjwa hatari wa UKIMWI, Dk. Elia Petro akiwajibika darasani.

 Baadhi ya wanafunzi wa shule za msingi na sekondari katika manispaa ya Singida,wanaohudhuria mafunzo juu ya madhara yatokanayo na UKIMWI.Mafunzo hayo yanaendeshwa na Kituo cha vijana cha mjini Singida,kinachomilikiwa na kanisa la Pentekoste (FPCT).

Kituo cha vijana mjini Singida kinachomilikiwa na kanisa la Pentekoste (FPCT) mjini Singida.(Picha zote na Nathaniel Limu).
Na Nathaniel Limu.
 Jumla ya wanafunzi zaidi ya 100 wa shule za msingi na sekondari katika manispaa ya Singida, wanahudhuria mafunzo juu ya UKIMWI na namna bora ya kujikinga na ugonjwa huo hatari ambao hadi sasa, hauna kinga wala chanjo.
Wanafunzi hao kwa sasa wapo mapumziko hadi Januari shule zitakapofunguliwa.
Mafunzo hayo yanatolewa na kituo cha vijana Singida kinachomilkiwa na kanisa la Pentekoste (FPCT) la mjini Singida.
Mratibu wa mafunzo hayo Peter Samweli, amesema wanafunzi hao ni wale wenye umri wa miaka 12 hadi 15, na awamu ya kwanza ya mafunzo hayo, yalihudhuriwa na wanafunzi  60.
Amesema awamu ya pili inayoendelea hivi sasa, ina wanafunzi 40 ambao pamoja na kujifunza juu ya UKIMWI wenyewe, pia wanafundishwa namna bora ya kujikinga na ugonjwa huo.
Peter amesema vile vile wanafundishwa juu ya athari za madawa ya kulevya, ulevi na namna nzuri ya kujikinga na mimba za utotoni.
Katika hatua nyingine, Peter ametoa wito kwa wazazi na walezi, kujenga utamaduni wa kuzungumza na watoto wao, mara kwa mara juu ya ugonjwa wa UKIMWI na namna nzuri ya kujikinga.
Amewataka wahakikishe watoto wao wanakuwa na ufahamu mkubwa wa athari za UKIMWI, madawa ya kulevya, mimba za utotoni na ulevi, ili waweze kujikinga na mambo hayo ambayo ni hatari kwa maisha yao.

Wazazi manispaa ya Singida watakiwa kujenga utamaduni wa kuzungumza na watoto wao juu ya Ukimwi na namna ya kujikinga.



 Mkufunzi wa mafunzo juu ya UKIMWI na namna bora ya kujikinga na maambukizi ya virusi vinavyosababisha ugonjwa hatari wa UKIMWI, Dk. Elia Petro akiwajibika darasani.

 Baadhi ya wanafunzi wa shule za msingi na sekondari katika manispaa ya Singida,wanaohudhuria mafunzo juu ya madhara yatokanayo na UKIMWI.Mafunzo hayo yanaendeshwa na Kituo cha vijana cha mjini Singida,kinachomilikiwa na kanisa la Pentekoste (FPCT).

Kituo cha vijana mjini Singida kinachomilikiwa na kanisa la Pentekoste (FPCT) mjini Singida.(Picha zote na Nathaniel Limu).
Na Nathaniel Limu.
 Jumla ya wanafunzi zaidi ya 100 wa shule za msingi na sekondari katika manispaa ya Singida, wanahudhuria mafunzo juu ya UKIMWI na namna bora ya kujikinga na ugonjwa huo hatari ambao hadi sasa, hauna kinga wala chanjo.
Wanafunzi hao kwa sasa wapo mapumziko hadi Januari shule zitakapofunguliwa.
Mafunzo hayo yanatolewa na kituo cha vijana Singida kinachomilkiwa na kanisa la Pentekoste (FPCT) la mjini Singida.
Mratibu wa mafunzo hayo Peter Samweli, amesema wanafunzi hao ni wale wenye umri wa miaka 12 hadi 15, na awamu ya kwanza ya mafunzo hayo, yalihudhuriwa na wanafunzi  60.
Amesema awamu ya pili inayoendelea hivi sasa, ina wanafunzi 40 ambao pamoja na kujifunza juu ya UKIMWI wenyewe, pia wanafundishwa namna bora ya kujikinga na ugonjwa huo.
Peter amesema vile vile wanafundishwa juu ya athari za madawa ya kulevya, ulevi na namna nzuri ya kujikinga na mimba za utotoni.
Katika hatua nyingine, Peter ametoa wito kwa wazazi na walezi, kujenga utamaduni wa kuzungumza na watoto wao, mara kwa mara juu ya ugonjwa wa UKIMWI na namna nzuri ya kujikinga.
Amewataka wahakikishe watoto wao wanakuwa na ufahamu mkubwa wa athari za UKIMWI, madawa ya kulevya, mimba za utotoni na ulevi, ili waweze kujikinga na mambo hayo ambayo ni hatari kwa maisha yao.

Mgana Msindai apania kufufua michezo mkoani Singida na kuwataka wadau kutoa ushirikiano.



Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Singida, Mgana Izumbe Msindai akizungumzia kufufua michezo wakati akihutubia wakazi (hawapo kwenye picha) wa kata ya Aghondi jimbo la Manyoni magharibi. Mkutano huo wa hadhara ulifanyika katika kijiji cha Kamenyange.Wa kwanza kulia ni mbunge wa jimbo la Manyoni magharibi, John Paulo Lwanji na anayefuata ni mwenyekiti wa CCM wilaya ya Manyoni.(Picha na Nathaniel Limu).
Mwenyekiti wa CCM Mkowa wa Singida Mgana Izumbe Msindai, amedai kwamba CCM, serikali ya Mkoa na wadau mbalimbali,  kwa pamoja watashirikiana ili kufufua michezo kwa lengo la kurejesha heshima ya mkoa katika sekta ya michezo.
Msindai maarufu kwa jina la CRDB benki inayomjali mteja, ameyasema hayo wakati akizungumza na wana-CCM na wananchi kwa ujumla wa kata ya Aghodi, Kata ya Sajaranda jimbo la Manyoni Magharibi.
Amesema mkoa wa Singida katika miaka ya nyuma, ulikuwa ukifanya vizuri sana kwenye mashindano ya michezo mbalimbali, ikiwemo mchezo wa mpira wa miguu, netiboli na riadha.
Msindai amesema lakini katika miaka ya hivi karibuni, michezo mkoani Singida imeporomoka kwa kasi ya  kutisha.
Amesema tatizo la kuporomoka kwa michezo ni lazima litafutiwe ufumbuzi wa kudumu, kwa vile michezo ina faida nyingi.
Kwa hali hiyo, amesema mlango wa ofisi yake utakuwa wazi wakati wote kwa mtu/watu wenye maoni, ushauri na mapendekezo ya namna nzuri, itakayosaidia.

Serikali Wilayani Singida yazindua awamu ya pili ya kampeni ya Vita dhidi ya Jangwa.



Mkuu wa wilaya ya Singida Mwalimu Queen Mlozi akizindua upandaji miti katika kijiji cha Kitope manispaa ya Singida.
Mkuu wa wilaya ya Singida mwalimu Queen Mlozi akishiriki kampeni ya kupanda miti ili kuokoa wilaya hiyo isikumbwe na balaa la Jangwa.


Mtoto Juma Sungi wa darasa la tatu katika shule ya msingi ya Mwankoko manispaa ya Singida akishiriki kampeni ya kupanda miti kwa lengo la kunusuru manispaa hiyo isigeuke jangwa.

Mkuu wa wilaya ya Singida mwalimu Queen Mlozi akionyesha miche ya miti maji ambayo amedai kuwa inatumika kuvuna mbao na pia kutengenezea sabuni.(Picha zote na Nathaniel Limu).
Na Nathaniel Limu.
Serikali wilayani Singida imepiga marufuku mara moja uvunaji ovyo wa misitu, kwa madai kwamba uvunaji wa aina hiyo, unatishia wilaya hiyo kugeuka jangwa.
Mkuu wa wilaya hiyo mwalimu Queen Mlozi, ametoa agizo hilo la kupiga marufuku, wakati akizindua awamu ya pili ya kampeni ya vita dhidi ya jangwa katika wilaya hiyo.
Amesema kumekuwa na uvunaji wa ovyo wa msitu usiokuwa na uwiano na upandaji wa misitu, unachochewa kwa kiasi kikubwa na biashara ya mkaa.
Mlozi amesema hivi sasa kuna malori mengi kutoka wilaya ya Arusha na Manyara, ambayo yanasafirisha mamia kwa mamia ya magunia ya mkaa kutoka Wilaya ya Singida, biashara ambayo inataka kuacha wilaya yetu kuwa jangwa, haikubaliki na hatutaki iendelee ni lazima tuikomeshe.
Mkuu huyo wa wilaya amesema kuanzia sasa, vizuizi viwekwe kwenye sehemu husika  ili kuyakamata malori hayo ya mkaa na wahusika wachukuliwe hatua kali za kisheria.
 Awali Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi ya Ant desert environment scheme Kitanto Said, alisema katika awamu hii ya pili ya kampeni dhidi ya jangwa, wanatarajia kupanda miti zaidi ya elfu moja.

Club Ya Waandishi Singida Kukumbwa Na Mgogoro


 Baadhi ya wanachama wa Singpress wakiwa mkutano mkuu na kufikia uamuzi wa kusamehe madeni kwa wenzao walioazima vifaa vya klabu
 Katibu mtendaji wa Singpress, Bw. Abby Nkungu akieleza kwa wadau wa habari safari ndefu ya kalbu hiyo iliyoanzishwa mwaka 2002
Singida
Desemba 12,2012.
MGOGORO mkubwa unaiandama Klabu ya wanahabari mkoa Singida (Singpress), kufuatia mwenyekiti wake Seif Takaza kuruhusu baadhi ya wanachama kufutiwa madeni yenye thamani ya Sh. 1,961,600.
Madeni dhidi ya wanachama hao ambao huko nyuma pia waliwahi kula fedha za waandishi, yametokana na kuazima vitendea kazi, vilivyotolewa masaada na baraza la habari nchini (MCT).
Vifaa hivyo vilivyotolewa kwa klabu zote nchini miaka minne iliyopita ni kamera aina ya sonny kwa ajili ya video na picha mnato (zote digitali), kompyuta za mezani na kinasa sauti kimoja.
Bei ya kukodi kwa siku ilikuwa Sh. 2,500 (kinasa sauti) Sh. 3,000 (picha mnato) na Sh.5,000 (video), wakati kompyuta haikuwa kwenye mpango wa kuazimishwa, lakini ilikuwa kwa mmoja wa viongozi, zaidi ya miaka miwili.
Kamera mbili ikiwemo ya video na picha mnato pia kompyuta, vilikuwa vipya wakati vinaazimwa, lakini viliporejeshwa vilikuwa havifai, wakati kinasa sauti mpaka sasa hakijulikani kilipo.
Katika mkutano huo, mwandishi wa jeshi la polisi mkoa Singida, Shabani Msangi, Paschal Tantau na wadaiwa sugu, walijipanga vema kudhoofisha jitihada ya uongozi uliotaka madeni hayo yalipwe.
Kufuatia mvutano mkali uliosababisha wajumbe wengi kutoka nje kwa hasira, mwenyekiti Takaza alivuruga zaidi alipoamuru upigaji kura na wajumbe wachache waliokuwa ndani, wakashinda.
Mkutano huo pia ulipitisha deni la Sh. 200,000 za pango alizokuwa anazodaiwa mwanachama Jumbe Ismaelly na Sh. 56,000 dhidi ya fundi mlango wa chuma Evarest Thomas, wazirejeshe mara moja.
Wanachama waliofutiwa madeni hayo na kiasi chao ni Doris Meghji (Sh. 90,000), Elisante Mkumbo (Sh. 25,000), Jumbe Ismaelly (Sh.1,231,600), Hillary Shoo (Sh. 615,000) na fundi mlango Evarist Thomas (56,000).
Waliofutiwa madeni hayo baadhi ni wadaiwa sugu, baada ya miaka ya nyuma kula fedha za rambirambi na mwingine kula fedha za umoja wa waandishi na wafanyakazi wa vyombo vya habari nchini (AJM).
Aidha tabia ya wanachama wakorofi kupenda vurugu hadi kuchangia madeni hayo kufutwa, inaweza kuiingiza klabu kwenye mgogoro mkubwa, baada ya kutulia tangu uongozi mpya uingie madarakani 2011.



"Unaona sasa tabia ya kuingiza wanachama bila kufuatiliwa wasifu wao huko walikotokea imeanza kutugharimu...klabu ilishatulia, ona vurugu hizi, mtu anasema hadi anagonga meza utadhani amegombana, mimi najiuzulu ,"alisema mmoja wa viongozi wanaounda kamati ya utendaji.

Singpress yagawanyika, mkutano mkuu wautaka uongozi wa zamani kukabidhi ofisi ndani ya wiki mbili.




Katibu wa klabu ya waandishi wa habari (Singpress) mkoa wa Singida Bw. Abby Nkungu akitoa taarifa yake ya utekelezaji kwa kipindi cha mwaka uliopita.(Picha na Nathaniel Limu).
Na Nathaniel Limu. 
Mkutano Mkuu wa mwaka wa Klabu ya Waandishi wa habari (Singpress) Mkoani Singida, umeagiza uongozi wa zamani wa Klabu hiyo, kukabidhi ofisi katika kipindi cha wiki mbili, vinginevyo uchukuliwe hatua kali zikiwemo za kisheria.
Mkutano huo uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa halmashauri ya Wilaya ya Manyoni mjini, Umeagiza uongozi huo uandikiwe barua rasmi ya kuupa muda wa wiki mbili kuanzia tarehe ya barua husika.
Akitoa pendekezo hilo mbele ya mkutano huo mkuu, Shabanj Msangi, amesema pamoja na muungano wa jumuiya ya vilabu vya waandishi wa habari nchini (UTPC), kuridhia uongozi wa sasa kuingia ofisini bila makabidhiano, uamuzi huo ni kinyumbe na katiba ya Singpress.
Baada ya mvutano mkali kwa upande uliokuwa unapendekeza juu ya hatua ya kukabidhi rasmi ofisi na upande uliokuwa ukidai kwamba hatua hiyo haina mashiko au tija, zilipingwa kura na upande uliokuwa unataka uongozi wa zamani uliokuwa  chini ya uenyekiti wa mchungaji Emmanuel Barnaba ukabidhi ofisi, ulishinda.
Katika hatua nyingine, mkutano huo katika hali isiyokuwa ya kawaida, uliamua kusamehe deni la shilingi milioni 2,217, 600 ambalo walikuwa wanadaiwa wanachama waliokodisha vifaa vya klabu ikiwemo kamera.
Baadhi ya wanachama walidai kwamba kutokana na udhaifu mkubwa ulionyeshwa na uongozi uliopita, basi madeni hayo ambayo yameacha  vifaa vilivyokodishwa  kuharibika  na kupelekea visitumike  tena, basi madeni yafutwe na wasidaiwe wanachama hao.
Wanachama hao waliokodisha vifaa hivyo,walikodishwa vikiwa vipya havijatumika kabisa na vimekaa mikononi mwao hadi vikaharibika na havitegenezeki tena.
Baada ya mvutano huo mkali kudumu zaidi ya nusu saa, upande uliopendekeza madeni hayo yafutwe na yasionekane kwenye kumbukumbu za Klabu, ulishinda.
Mapendekezo hayo yawaligawa wananchama wa Singpress katika vipande viwili na baadhi walidai kuwa kitendo cha kusamehe madeni hayo ni sawa na kuifanya Singpress kuwa ni shamba la bibi.
Uamuzi huo uliendelea kulaumiwa kwa madai kwamba msamaha wa aina hiyo usiokuwa na tija, utakuwa endelevu kwa vile wakopaji au watumiaji wa mali ya Klabu watakuwa wanautumia katika kuihujumu Klabnu kiuchumi.
Wadaiwa hao na madeni yao kwenye mabano ni  Doris Mehgji, (90,000/=), Elisante Mkumbo (25,000/=), Jumbe Ismail (1,431,600), Hillary Shoo (615,000) na Evarist Thomas (56,000).
Hata hivyo Hillary Shoo kwa sasa sio mwanachama wa Singpress.  


HATARI: MAJAMBAZI WAVAMIA MSAFARA WA MAITI SINGIDA WAPORA ZAIDI YA MILIONI 19 NA KUVUNJA NA KUSACHI JENEZA


 
Gari aina ya Land Cruiser mali ya chuo cha SUA cha mjini Morogoro kama linavyoonekana baada ya kupigwa mawe na watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi nje kidogo ya mji wa Singida.


Mhudumu wa chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya mkoa mjini Singida ambaye jina lake halikuweza kutambuliwa mara moja, akiliweka sawa jeneza baada ya kufanyiwa ukarabati baada ya kubomolewa na majambazi na kulisachi. (Picha na Nathaniel Limu).

---

---
Watu wasiofahamika idadi yao na ambao wanadhaniwa kuwa ni majambazi, wamevamia gari lililokuwa linasafirisha maiti kutoka Morogoro mjini hadi mkoa wa Mara na kupora zaidi ya shilingi milioni 19.8.

Baada ya kumaliza zoezi la uporaji huo, majambazi hayo yalishusha jeneza na kisha kulifumua na kuanza kulisachi.

Jeneza hilo lilikuwa limebeba mwili wa mwanafunzi Munchari Lyoba, mwanafunzi wa mwaka wa tatu aliyekuwa anasomea elimu ya biashara kwenye chuo cha SUA.

Amesema gari hilo lilibeba viongozi wa wanafunzi sita na viongozi wengine wanne akiwemo dereva.

Akizungumza na waandishi wa habari nje ya chumba cha kuhifadhi maiti cha hospitali ya mkoa wa Singida, mkuu wa msafara huo Makarang Nouna, amesema tukio hilo limetokea Disemba 6 mwaka huu saa 7.30 usiku, na lilihusisha gari Land Curise lenye namba za usajili SU 37012 na lilikuwa likiendeshwa na Kalistus Malipula.


Amesema tukio hilo la kinyamana la kusikitisha, limetokea katika barabara kuu ya Dodoma – Mwanza nje kidogo ya mji wa Singida kwenye kona maarufu kwa jina la Mohammed Trans.

Amesema walipofika eneo la tukio, walikuta mawe makubwa yamepangwa kukatisha barabara, kitendo kilichosababisha washindwe kupita, na hivyo kutoa mwanya kuvamiwa na kundi kubwa la vijana ambao walibeba bunduki mbili aina ya gobore, marungu, mashoka na mawe.

Makaranga amesema walichofanya kwanza ni kupiga kioo cha gari letu kwa mbele, na baadaye kumparaza kwa panga usoni dereva wetu Kalistus Malipula.

Baada ya hapo walivunja vunja vyoo vyote na kutuamuru kutoa kila kitu ambacho tulikuwa nacho.





Akifafanua zaidi, amesema kwa upande wake yeye ameporwa shilingi milioni mbili ambazo zilikuwa kwa ajili ya kugharamia msafara huo, jumla ya shilingi milioni 8.8 ambazo zilichangwa na wanafunzi kama rambi rambi kwa mwenzao, na shilingi milioni tisa ambazo wasindikizaji walikuwa nazo zikiwa ni posho.

“Pia tumeporwa simu zetu zote za mikononi, viatu, laptop na mabegi yote ya nguo zetu”amesema.

Makaranga ambaye amesema anafanya kazi za kiutawala katika chuo cha SUA, amewataja walioumizwa zaidi ni pamoja nay eye, dereva Malipula na kiongozi wa wanafunzsi Idd Idd na kutibiwa katika hospitali ya mkoa na kuruhusiwa.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Singida Mwalimu Queen Mlozi, ambaye aliwasiliana na uongozi wa SUA Morogoro kwa ajili ya shughuli ya kutuma gari jingine na ukarabati wa jeneza, amesema kuwa kwa ushirikiano wa jeshi la polisi na kamati ya ulinzi na usalama, watahakikisha watu waliofanya unyama huo, wanakamatwa mapema iwezekanavyo ili waweze kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria.

Jamii yaombwa kusaidia makundi maalumu yasiyojiweza.


Mkuu wilaya Iramba-Singida, Yahaya Nawanda akikabidhi msaada wa madaftari kwa mwanafunzi Hilda Samwel (12) uliotole na vikundi vitatu vya jumuiya ya kuweka na kukopeshana (SELC).
Na Nathaniel Limu
Mkuu wa wilaya Iramba mkoani Singida, Yahaya Nawanda ameitaka jamii kusaidia makundi yasiyojiweza, wakiwemo watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi, ili kujenga moyo wa upendo baina yao.
Nawanda alisema hayo wakati akikabidhi vifaa mbalimbali vya shule msingi, kwa ajili ya wanafunzi wa shule sita  za watoto wanaoishi kwenye mazingira hatarishi, wilayani humo.
Msaada huo ulitolewa na vikundi vitatu vya jumuiya ya kuweka na kukopeshana(SELC), ambavyo kila mwanachama huchangia Shilingi mia tatu, kwa ajili ya kusaidia makundi mbalimbali yasiyojiweza, wilayani Iramba.
Alibainisha kuwa, msaada siyo lazima iwe kitu chenye thamani kubwa, bali waweza kuwa hata wenye thamani ndogo, lakini utakuwa umewaondoa wahitaji kutoka hatua moja hadi nyingine, kulingana mahitaji yao.
Msaada huo uliojumuisha sare za shule, madaftari, rula na kalamu, ulitolewa kwa wanafunzi 74 wa shule sita za msingi katika kata ya Kiomboi, ikiwemo Kiomboi hospitali, Salala, Lulumba shule ya msingi na Sekondari, Igumo, Kiomboi Bomani na Kizega.
Vikundi hivyo vitatu vinavyounda jumuiya hiyo ambavyo kila kimoja kina wanachama 30 ni Msweki, Loelya na Umoja, ambavyo kwa pamoja vimeshirikiana kutoa msaada huo wenye thamani ya Sh. 395,000.
Mapema akisoma risala ya vikundi hivyo kwa mgeni rasmi, katibu wa Msweki, Johari Manguli alisema wamelazimika kutoa msaada huo kutokana na wanafunzi hao kufiwa na wazazi wao wote wawilina wengine mzazi mmoja.
Aidha Johari aliomba wadau, wafadhili na mashirika yenye uwezo kujikita zaidi kusaidia makundi mbalimbali yenye matatizo, wakiwemo watoto waliofiwa na wazazi wao na wale wanaoishi kwenye mazingira hatarishi.
Hata hivyo baadhi ya wazazi na walezi katika hafla hiyo waliofiwa na waume wao,pia wanafunzi waliopoteza wazazi wao, walieleza kwa masikitiko tabu na shida wanazopata katika kukabaliana na maisha ya kila siku.
DC Iramba Yahaya Nawanda akimkabidhi mwanafunzi Jacob David (11) wa shule msingi Kiomboi hospitali msaada wa madaftari uliotole na vikundi vitatu vya jumuiya ya kuweka na kukopeshana (SELC).
 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2011. Singida Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogz za Mikoa