CHAGUA AMANI RAI KATIKA KURA ZA MAONI SINGIDA MJINI‏

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Chagua Amani Rai Jimbo la Singida Mjini.

Maziku amaliza mgogoro wa Nyalandu na wenzake, waendelea na mchakato kuomba kura kwa wananchi

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

KATIBU
Katibu wa CCM mkoa wa Singida, Mary Maziku akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumaliza mgogoro wa wagombea Ubunge Jimbo la Singida Kaskazini.
maziku
Katibu wa CCM Mkoa wa Singida, Mary Maziku akiwa ofisini kwake.
MONKO
Mgombea Ubunge Jimbo la Singida Kaskazini, Jastine Monko akizungumza na waandishi wa habari nje ya jengo la CCM Mkoa wa Singida baada ya kumaliza tofauti zao.
nyalandu
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akizungumza na waandishi wa habari nje ya viwanja vya CCM Mkoa wa Singida, mara baada ya kikao cha maridhiano baina yake na wagombea wenzake saba kumalizika na kuondoa tofauti zao.
GARI
Wagombea wa Ubunge Singida Kaskazini wakipanda gari kuendelea na mchakato kwa kuomba kura kwa wananchi baada ya kumaliza kikao na Katibu wa CCM Mkoa Mary Maziku.(PICHA ZOTE NA HILLARAYSHOO,  SINGIDA).
Na Hillary Shoo, SINGIDA
Hatimae mgogoro uliokuwa ukifukuta kwa wagombea saba wa nafasi ya Ubunge Jimbo la Singida Kaskazini kutaka kugomea kuendelea na mchakato wa kura za maoni umemalizika na sasa wagombea hao wanaendelea na zoezi.
Hatua hiyo ya wagombea saba kutaka kugomea ilidaiwa ni kutokana na mgombea mwenzao Lazaro Nyalandu kukiuka taratibu za mchakato huo, na hivyo kuonekana kana kwamba anabebwa na viongozi wa Wilaya ya Singida vijijini.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana , Katibu wa CCM Mkoa wa Singida Mary Maziku alisema baada ya kikao cha kuwakutanisha pande zote mbili , kila moja alikuwa na malalamiko yake, lakini baada ya kikao cha pamoja cha zaidi ya saa moja, walimaliza suala hilo.
Maziku alisema kuwa kilichotokea ni siasa za kupakana matope, kuchafuana , kudharauliana na kejeli za hapa na pale miongoni mwa wagombea hao.
Aidha alisema baada ya kusikiliza malalamiko ya wagombea saba Justine Monko, Yohana Sintoo, Amos Makiya, Alon Mbogo, Sabasaba Manase, Michael Mpombo na Mungwe Athuman,dhidi ya Nyalandu  ambaye nae alikuwa na malalamiko yake, walikubaliana kimsingi kuondoa tofauti zao kwa kuwa wote ni wana CCM.
“Hawa saba walikuwa wakimlalamikia Nyalandu lakini na yeye alikuwa akiwalalamikia hawa, sasa baada ya ya kukaa pamoja tumeona hakuna haja ya kuendelea na malumbano kwa kuwa wote wameonekana kuwa na makosa madodo madogo ambayo hayana mashiko bali ni siasa za kawaida kwenye chaguzi mbalimbali.” Alisistiza Maziku.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa kikao hicho, Waziri wa maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu alisema hana tatizo na mgombea yeyote na kwamba madai ya wagombea wenzake kumlalamikia ni dalili za kuanza kushindwa.
“Mimi niwaambie waandishi wa habari nimefanya mambo mengi katika Jimbo hili la Singida Kaskazini na wananchi watanipima kwa kazi sio maneno, na nina uhakika wa kupata zaidi ya aslimia 90 ya kura za maoni.”Alijigamba Nyalandu huku akionesha kujiamini sana.

NDOTO YA WEMA SEPETU KUWA MBUNGE YAYEYUKA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Haikuwa bahati yake. Safari ya Wema Sepetu kuelekea bungeni imefikia tamati.

Hiyo ni baada ya kushindwa kuwashawishi wanachama wa CCM mkoani mkoani Singida kumpa dhamana ya kuwawakilisha kwenye viti maalum vya ubunge.
Wema ameshindwa kupita kwenye kura za maoni za ubunge huo kwa kupata kura 90 tu. Aliyeongoza kwenye kinyang’anyiro hicho ni Aysharose Mattembe (311), Martha Mlata (235) na Diana Chilolo (182).
Wema amekubali kushindwa na kudai kuwa ushiriki wake umempa ujasiri zaidi.
“Nilivyoamua kugombea viti maalum, nilijua kuna kupata na kukosa. Awamu hii nimekosa, ila dunia bado inazunguka,” ameandika kwenye kwenye Instagram.
“Nawapongeza walioshinda. Nawashukuru mlioniunga mkono, Mungu aendelee kuwabariki kwa mapenzi yenu juu yangu, yananipa moyo. Nawashukuru pia wote mlionipinga maana mmeniongezea ujasiri na nina nguvu mpya ya kuthubutu upya,” ameongeza.
“2015 ni mwaka wa kipekee kwenye muamko wa vijana Tanzania. Bigger things loading.. Most of all Nilizaliwa nikiwa katika Chama Cha Mapinduzi na nitakufa nikiwa ndani ya Chama Cha Mapinduzi…. Safari yangu ya Siasa ndo kwanza inaanza.”

MWIGULU HABARI NYINGINE HUKO IRAMBA MBIO ZA UBUNGE NDANI YA CCM,JAIRO NA WENZAKE WAJITOA,MWIGULU KUSHINDA KWA KISHINDO

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Mwigulu Nchemba akiondoka Viwanja vya Shelui mara baada ya Mkutano wa Kampeni Kumalizika.Mwigulu Nchemba akisalimiana na Wananchi wake Kata ya Shelui wakati wa Mkutano wa Kampeni ya kura ya Maoni za UBunge kuwania kuteuliwa kupeperusha Bendera ya CCM Wilaya ya IrambaMwigulu Nchemba akilakiwa na Wananchi wake kijiji cha Tulya wilayani Iramba wakati wa kampeni za Kura ya Maoni ya kuwania Ubunge ndani ya CCM.
Mwigulu Nchemba akifurahia mwenendo wa kampeni za kura ya maoni na Wananchi wake.
MWigulu NChemba akiwa na Wagombea wenzake kabla hawajajitoa kwenye mbio hizo za kura ya Maoni ya kuwania Ubunge Jimbo la Iramba kwa tiketi ya CCM,Wagombea kuanzia kushoto ni Juma Kilimba,Davd Jairo Kitundu,Amon Gunda na Mwigulu Nchemba.Mwigulu Nchemba akizungumza na wananchi wa kata ya Mbelekesye kuhusu mambo mbalimbali ya Maendeleo aliyowafanyia ikiwamo kuwasha Umme Zaidi ya vijiji 48 ndani ya miaka 5,Ujenzi wa maabara na zahanati kwa kila kata ,Ujenzi wa barabara za kuunganisha kila kijiji,Uchimbaji wa visima kwa Zaidi ya Vijiji 50 n.k.Hivyo anaomba ridhaa ya kuendelea kuwatumikia wananchi kwa miaka 5 ijayo.Vijana wakimshangilia Mbunge wao kwa kazi alizofanya hivyo kumuunga mkono kwenye kura za maoni iliaweze kuteuliwa tena kuwawakilisha Bungeni kwa miaka 5 ijayo.Wananchi wakiwa wamemshikilia Mbunge wao Mh.MWigulu Nchemba iliasalimiane nao wakati wakura za Maoni.Mwigulu amekuwa akishangiliwa sana na Wananchi wa Iramba na wengi wanaonekana kumuunga mkono kutokana na alivyoweza kuibadilisha Taswira ya Jimbo la Iramba kimaendeleo na katika Sura ya Nchi.

MAGUFULI ATAKIWA KUVUNJA MFUMO WA SASA WA CCM.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Dk. John Magufuli.

Kanisa la Christian Mission Fellowship Tanzania, limesema ili Watanzania warejeshe imani kwa serikali yao, kuna umuhimu wa anayegombea nafasi ya urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli, avunje mfumo uliopo sasa ndani ya chama hicho.
 
Makamu Askofu Mkuu wa kanisa hilo, Donald Mhango, akizungumzia uteuzi wa CCM uliompa ushindi Dk. Magufuli, alisema mfumo unaotakiwa kuvunjwa ni ule unaosababisha baadhi ya viongozi kujihusisha na ufisadi, rushwa, kutowajibika ipasavyo kwenye nafasi za kazi, wanaosababisha taifa hasara na kutowajibishwa kwa mujibu wa sheria.
 
Askofu Mhango alisema Watanzania wengi wanatarajia Dk. Magufuli ,atatumia ujasiri alionao kuwaondoa madarakani wale wote wanaotuhumiwa kuliingizia taifa hasara, hali ambayo imeendelea kudidimiza hali za wananchi na kuendelea kuwa maskini.
 
“Naamini Dk. Magufuli ameinuliwa kwa kusudi maalum. Kikubwa tunachotarajia afanye ni kuvunja mfumo wa serikali ili kurudisha imani ya Watanzania ambayo siyo siri kwamba imetoweka. Kwa sasa taifa limegawanyika vipande vipande, vikiwamo vya udini, ukabila na tofauti za kiuchumi,” alieleza Askofu Mhando.
 
Alitaja sababu kubwa iliyowafanya wananchi kukosa imani kwa serikali yao kuwa ni viongozi wengi kuhusishwa na kashfa mbalimbali za kukosa uadilifu ikiwamo za rushwa na kutowajibika, kiasi cha baadhi yao kushuhudiwa wakiitwa mizigo lakini wakiendelea kuachwa wabaki madarakani.
 
Hata hivyo Askofu Mhando alisema ili serikali ya awamu ya tano ifanikiwe kubomoa mifumo hiyo ya kiutawala, ni lazima kila Mtanzania kwa imani yake amuombe Mungu ili aingilie kati
SOURCE: NIPASHE

NATOSHA KUVAA VIATU VYA UBUNGE WA DEWJI SINGIDA MJINI- HASAN MAZALA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

fomu
Mjumbe Mkutano Mkuu wa CCM Manispaa ya Singida, Hasan Mazala akionesha vijana fomu yake ya kuwania ubunge Jimbo la Singida Mjini jana kwenye ukumbi wa mikutano wa CCM Mkoani Singida.
kwa nguvu
Mazala akiwaasa vijana kufanya kazi kwa nguvu katika jimbo hilo.
nimenyooka
Mkinipa nafasi ya kuwatumikia mambo yatanyooka namna hii.
ninao uwezo
tuko imara
Mgombea wa nafasi ya Ubunge Jimbo la Singida Mjini Hassan Philipo Mazala akisistiza jambo kwa vijana waliomsindikiza kuchukua fomu.
pamoja
vijana
Baadhi ya vijana wakiwa katika picha ya pamoja na Hassan Mazala nje ya jengo la makao makuu ya CCM Mkoa wa singida mara baada ya kuchukua fomu.(PICHA ZOTE NA HILLARY SHOO).
Na Hillary Shoo, SINGIDA
MJUMBE wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa (MNEC) Manispaa ya Singida,Hassan Mazala amechukua fomu ya kuwania Ubunge Jimbo la Singida Mjini ..
Akizungumza na kundi la Vijana wa CCM kwenye ukumbi mdogo jana, Mazala amesema kuwa amefungua ukurasa mpya wa maisha yake kwa kuwania nafasi hiyo iliyoachwa wazi na Mohammed Dewji aliyestaafu.
‘Nimejipima nikaona ninaweza kuvaa viatu vilivyoachwa wazi na Dewji kwani katika kipindi chote alichukuwa Mbunge nilishirikiana nae katika kuyatekeleza yale yote aliyonituma kama msaidizi wake wa karibu.” Alisema Mazala.
“Nimekuwa Kiongozi kwa muda mrefu katika ngazi mbalimbali kuanzia kwenye vijiji ,Kata, Wilaya, Mkoa na sasa Taifa, hivyo nina uwezo wa kutosha na nimekomaa kisiasa katika kufanya kazi hii ya Ubunge bila wasiwasi wowote pale alipoachia Dewji” Alisisitiza.
Aidha alisema anazifahamu changamoto zinazolikabili Jimbo hilo kwani ametembea kona zote na kujionea hali halisi ya wananchi wanavyojishigulisha na shughuli za kijamii.
“Nina Moyo wa dhati kabisa wa kuwatumikia, ninaombeni mnibebe, najua yamesemwa mengi sana juu yangu katika kipindi ambachio nimlikuwa nafanya kazi na MO, lakini yapuuzeni hayo kwani hayana ukuweli wowote ni chuki binafsi tu.” Alisema huku akishangiliwa na kundi la vijana linalojiita team Mazala.
Hata hivyo Mazala ambaye ana uwezo mkubwa wa kutawa jukwaa alisema kamwe hatawaanguisha wananchi wa Jimbo hilo huku akitumia misamiati Zimwi likujualo, Usiache mbachao na mwokoto kuni porini huota moto pamoja.
Akitangaza kutogombea tena Ubunge mapema Julai 08 mwaka huu mjini Singida Dewji alimsifu Mazala kwa kusema kuwa ni mchapa kazi, mwaminifu, mwadilifu na ana moyo wa kujitolea kwani aliweza kusimamia kazi zake zote bila ya matatizo yoyote.
“Na pia ninapenda kumshukuru kipekee mtu mmoja ambaye bila yeye mafanikio yangu ya kiuongozi niyoyopata hapa Singida yasingeweza kufanikiwa vizuri bila ya yeye.” Alisema Dewji katika taarifa yake hivi karibuni.

NHIF YAKABIDHI MSAADA WA MASHUKA 200 KWA HOSPITALI YA MKOA MJINI SINGIDA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. DSC00136
Meneja wa NHIF mkoa wa Singida, Agnes Chaki (kushoto) akimkabidhi Mkuu wa wilaya ya Singida, Alli Amanzi msaada wa mashuka 200 kwa ajili ya hospital ya mkoa mjini hapa.(Picha na Nathaniel Limu).
DSC00132
Mkuu wa wilaya ya Singida,Alli Amanzi (kulia) akibadilishana mawazo na Meneja Mfuko wa taifa wa bima ya afya (NHIF) mkoa wa Singida, Agnes Chaki (katikati) muda mfupi kabla Meneja NHIF hajakabidhi mashuka 200 kwa hospitali ya mkoa mjini hapa.Kushoto ni Afisa uthibiti ubora wa huduma NHIF mkoani hapa, Dk.Edwin Mwangajilo.
Na Nathaniel Limu, Singida
HOSPTALI ya mkoa wa Singida iliyopo mjini hapa,inakabiliwa na uhaba mkubwa wa mashuka kitendo kinachochangia wagonjwa kutumia mashuka yao binafsi wakati wote wanapokuwa wamelazwa hospitalini hapo.
Hayo yamesemwa na Kaimu mganga mkuu wa mkoa wa Singida,Dk.Henry Mgetta, wakati akizungumza kwenye hafla ya makabidhiano ya msaada wa mashuka 200 yaliyotolewa msaada kwa hospitali ya mkoa na mfuko wa taifa wa bima ya afya (NHIF) mkoani Singida.
Alisema hospitali hiyo yenye vitanda 300 vya kulaza wagonjwa,inakabiliwa na uhaba wa mashuka 2,400 na magodoro 230.
“Hali ni mbaya mno,shuka 100 tulizonazo,ni chakavu na kwa ujumla nazo hazifai kwa matumizi ya binadamu.Wagonjwa wanaolazwa inawalazimu kutumia shuka zao binafsi jambo ambalo halikubaliki”,alisema Dk.Mgetta.
Alisema mbali na uhaba wa shuka na magodoro,hosptali hiyopia ina uhaba wa vitanda na hasa kwenye wodi ya wazazi, kitendo kinachochangia wajawazito wanne watumie kitanda kimoja.
“Natoa wito kwa wadau mbalimbali,waangalie uwezekano wa kuisaidia kwa hali na mali hospitali yetu hii na vituo mbalimbali,ili viweze kutoa huduma bora inayokidhi mahitaji ya wananchi”’alisema Dk.Mgetta.
Kwa upande wake Meneja wa NHIF mkoa wa Singida, Agnes Chaki,alisema kuwa wametoa msaada huo wa mashuka hayo baada ya kuombwa na serikali ya wilaya ya Singida.
Alisema majukumu ya NHIF,ni pamoja na kuhakikisha vituo vya kutolea huduma za afya zinajitosheleza kwa kuwa na mahitaji yote muhimu kwa kutoa misaada na vile vile mikopo ya kununulia dawa,vifaa tiba na uboreshaji wa majengo.
“Nina imani kituo cho chote cha afya,zahanati na hospitali,kinapokuwa na vitanda,mashuka na mambo mengine muhimu kwa wagonjwa wanaolazwa,kitendo hicho kitakuwa kinawajengea mazingira mazuri ya kuendelea na matibabu bila usumbufu wo wote”,alifafanua meneja huyo.
Chaki alisema NHIF itaendelea kutoa misaada mbalimbali kadri uwezo utakavyoruhusu kwa lengo la kusaidiana na serikali katika kuboresha utoaji wa huduma za afya.

DIAMOND PLATNUMZ KUPAMBA MKUTANO MKUBWA WA JIMBO LA SINGIDA MJINI VIWANJA VYA PEOPLE'S CLUB‏

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
11101348_827429087339981_3431616584413911623_n
 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2011. Singida Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogz za Mikoa