NSSF YASHIRIKI SIKU YA WAFANYAKAZI DUNIANI – MKOANI SINGIDA


Na Mwandishi Wetu, Singida

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Bw. Masha Mshomba, amewataka wafanyakazi wa Mfuko huo kuendelea kutoa huduma bora na kufanya kazi kwa bidii ili kuhakikisha Mfuko unatimiza malengo uliyojiwekea.

Akizungumza katika hafla ya kuwapongeza wafanyakazi na wanamichezo wa NSSF walioshiriki maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Kitaifa (Mei Mosi), Bw. Mshomba alisema huduma bora kwa wanachama na wadau ndiyo msingi wa mafanikio ya taasisi yoyote ya umma ikiwemo Mfuko wa NSSF.

“Tunao wajibu wa kuhakikisha kila mwanachama anahudumiwa kwa weledi na kwa wakati. Hili linawezekana tu endapo kila mmoja wetu atajituma zaidi na kuweka mbele maslahi ya Mfuko,” alisema Bw. Mshomba.

Hafla hiyo ilifanyika Aprili 30, 2025, mkoani Singida kuelekea siku ya Mei Mosi, ikiwa ni sehemu ya kuwatambua na kuwapongeza wafanyakazi waliofanya vizuri katika maeneo mbalimbali ndani ya Mfuko, katika michezo na ushiriki katika Wiki ya Usalama Mahala pa Kazi.

Alisema NSSF itaendelea kuboresha mazingira ya kazi ili kuongeza ufanisi na ari kwa wafanyakazi, lakini akasisitiza kuwa jitihada binafsi za kila mtumishi ndizo msingi wa mafanikio ya pamoja.

“Pamoja na juhudi tunazozifanya kuboresha mazingira ya kazi, tunahitaji kuona bidii na ubunifu zaidi kutoka kwenu – hasa katika eneo la ukusanyaji wa michango. Hili ni eneo muhimu linalobeba ustawi wa Mfuko,” aliongeza.

Katika hotuba hiyo, Bw. Mshomba alitoa pongezi kwa timu ya mpira wa kikapu ya NSSF kwa kushika nafasi ya tatu, na Bi. Agnetha Bimbiga aliyefanya vizuri katika mbio za riadha kwa kuwa mshindi wa pili katika mbio za mita 800 na 3,000 na  kushika nafasi tatu katika mbio za mita 1,500.

“Haya ni mafanikio makubwa. Yameleta heshima kwa Mfuko na yanapaswa kuwa chachu ya kujituma zaidi hata katika maeneo ya kazi,” alisema.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Usimamizi wa Rasilimali Watu na Utawala wa NSSF, Bw. Ekwabi Mujungu, alisema hafla hiyo ni sehemu ya kujenga mshikamano na kuimarisha utendaji wa watumishi na Mfuko kwa ujumla.

“Mafanikio tunayoyaona leo ni matokeo ya kazi ya pamoja na mshikamano miongoni mwa wafanyakazi. Ni muhimu kuendeleza hali hii ili kufikia malengo ya Mfuko,” alisema Bw. Mujungu.

NSSF ilishiriki kikamilifu katika maadhimisho ya Mei Mosi yaliyofanyika kitaifa katika Uwanja wa Bombadia, Singida, ambapo mgeni rasmi alikuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassani. Pia wafanyakazi wote wa NSSF walishiriki maadhimisho hayo katika kila mkoa Nchini.
















SINGIDA WAASWA KUTEKELEZA ZOEZI LA UBORESHAJI DAFTARI KWA WELEDI


Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Dkt Zakia Mohamed Abubakar leo ametembelea mafunzo ya Waandishi Wasaidizi na Waendesha Vifaa vya Bayometriki watakao husika na zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura katika Halmashauri ya Singida Vijijini mkoani Singida na kuzungumza nao wakati wa mafunzo yao ya siku mbili yaliyoanza leo Septemba 22 na kumalizika kesho Septemba 23, 2022.


Akizungumza na Waandishi hao Wasaidizi na Waendesha Vifaa vya Bayometriki Dkt Zakia aliwataka kuzingatia mafunzo wanayopewa, dhamana waliyopewa ya kuendesha zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa weledi. Mafunzo hayo ni maandalizi ya Uboreshaji wa Dafrati la Kudumu la Wapiga Kura unaoitaraji kuanza Septemba 25, 2024 hadi Oktoba 1 mwaka huu.
Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Dkt Zakia Mohamed Abubakar leo ametembelea mafunzo ya Waandishi Wasaidizi na Waendesha Vifaa vya Bayometriki watakao husika na zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura katika Halmashauri ya Singida Vijijini mkoani Singida na kuzungumza nao wakati wa mafunzo yao ya siku mbili yaliyoanza leo Septemba 22 na kumalizika kesho Septemba 23, 2022.
Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Dkt Zakia Mohamed Abubakar (kulia) akiangalia mafunzo kwa vitendo yaliyokuwa yakifanywa na waandishi wasaidizi na Waendesha vifaa vya Bayometriki (BVR) wakati alipotembelea mafunzo yao leo Septemba 23, 2024 katika Shule ya Sekondari Mwanamwema Shein iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Singioda Vijijini mkoani Singida. Mkoa wa Singida na Dodoma wanataraji kuanza uboreshaji septemba 25 hadi Oktoba mosi mwaka huu.
Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Dkt Zakia Mohamed Abubakar (kushoto) akiangalia mafunzo kwa vitendo yaliyokuwa yakifanywa na waandishi wasaidizi na Waendesha vifaa vya Bayometriki (BVR) wakati alipotembelea mafunzo yao leo Septemba 23, 2024 katika Shule ya Sekondari Mwanamwema Shein iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Singioda Vijijini mkoani Singida. Mkoa wa Singida na Dodoma wanataraji kuanza uboreshaji septemba 25 hadi Oktoba mosi mwaka huu.
Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Dkt Zakia Mohamed Abubakar (kulia) akiangalia mafunzo kwa vitendo yaliyokuwa yakifanywa na waandishi wasaidizi na Waendesha vifaa vya Bayometriki (BVR) wakati alipotembelea mafunzo yao leo Septemba 23, 2024 katika Shule ya Sekondari Mwanamwema Shein iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Singioda Vijijini mkoani Singida. Mkoa wa Singida na Dodoma wanataraji kuanza uboreshaji septemba 25 hadi Oktoba mosi mwaka huu.

Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Dkt Zakia Mohamed Abubakar (kulia) akiangalia mafunzo kwa vitendo yaliyokuwa yakifanywa na waandishi wasaidizi na Waendesha vifaa vya Bayometriki (BVR) wakati alipotembelea mafunzo yao leo Septemba 23, 2024 katika Shule ya Sekondari Mwenge iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Singida mkoani Singida. Mkoa wa Singida na Dodoma wanataraji kuanza uboreshaji septemba 25 hadi Oktoba mosi mwaka huu.
Waandishi wasaidizi na Waendesha vifaa vya Bayometriki (BVR) wakisikiliza jambo wakatio wa mafunzo.


Sehemu ya washiriki wa mafunzo ya Waandishi wa Saidizi na Waendesha vifaa vya Bayometric (BVR) wakila kiapo cha kujitoa uanachama na kiapo cha kutunza siri muda wote wa utekelezaji wa majukumu yao.

Sehemu ya washiriki wa mafunzo ya Waandishi wa Saidizi na Waendesha vifaa vya Bayometric (BVR) wakila kiapo cha kujitoa uanachama na kiapo cha kutunza siri muda wote wa utekelezaji wa majukumu yao.

Sehemu ya washiriki wa mafunzo ya Waandishi wa Saidizi na Waendesha vifaa vya Bayometric (BVR) wakila kiapo cha kujitoa uanachama na kiapo cha kutunza siri muda wote wa utekelezaji wa majukumu yao.


Mafunzo yakiendelea

"FANYENI KAZI KWA BIDII KWA MAENDELEO YA TAIFA" DAS PETER MASINDI

Katibu Tawala wilaya ya Mkalama Ndugu Peter Masindi amewataka watumishi wilayani Mkalama kuwa wazalendo na kufanya kazi kwa bidi katika kuwaenzi mashujaa wa nchi waliopigana kwa ajili ya taifa la Tanzania.
Kauli hiyo ametoa Julai 25, 2024 kwa niaba ya Mkuu wa wilaya ya Mkalama wakati wa zoezi la usafi liliofanyika katika hosipitali ya wilaya ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku ya Mashujaa nchini.
Serikali inaleta fedha nyingi kwa ajili ya kutekeleza miradi, tuwajibike pamoja katika kuhakikisha fedha hizi zinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa. Kila mmoja katika nafasi yake atimize wajibu wake, huwezi kuwa shujaa kama ukishindwa kutimiza wajibu wako, kwa kufanya hivi tutakuwa tumewaenzi Mashujaa wetu” DAS Masindi.
Katibu Tawala Peter Masindi amewasisitizia watumishi kuwahudumia wananchi kwa kutumia lugha nzuri pindi wanapokuwa wanatoa huduma kwa wananchi, kulinda maadili ya kazi pamoja na kudumisha amani na umoja baina yao “Tuache ubabe, tuache ufalme kwa kutumia ofisi zetu za serikali, bali tuwatumikie watanzania kwa lugha nzuri” DAS Masindi
Aidha Katibu Tawala Ndugu Peter Masindi amekumbusha watumishi na wananchi wilayani Mkalama kuhusu suala la kulinda maadili ya nchi yetu kwa kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia, vitendo vya ulawati na ushoga katika jamii zetu
“Ndugu zangu Tuhakikishe maadili ya watoto wetu yanajengwa na sisi wazazi, yanajengwa na sisi jamii iliyopo leo, tuhahitaji jamii yenye utuvuli , amani kwa ajili kufikia maendeleo ya taifa letu,hakikisha mtoto anaenda shule, huo ndio Ushujaa unaostahili” DAS Masindi

 

“WAZAZI TUNA WAJIBU WA KUMLINDA MTOTO WAKIKE” DC MACHALI


Mkuu wa wilaya ya Mkalama Mhe. Moses Machali amefanya ziara ya kikazi kwa ajili ya kusikiliza na kutatua kero mbalimbali zinazowakabili wananchi wa Kijiji cha Nkinto kilichopo kata ya Nkito wilayani Mkalama.

Akizungumza wakati wa mkutano wa hadhara, Leo Julai 29,2024 Mhe. Machali amewataka wazazi wa Kijiji cha Nkinto na wilayani Mkalama kwa ujumla kuwa mstari wa mbele kupinga mimba za utotoni hasa kwa wanafunzi.

“Tunawajibu mkubwa wa kumlinda mtoto wakike, wananchi wenzangu tushirikiane pamoja kupambana dhidi ya tatizo la mimba mashuleni. Nawaomba sana mtoe ushirikiano pindi kesi za mimba zinapofika Mahakamani, wanaume achaneni na wanafunzi” Mhe. Machali

Mhe. Machali amesisitiza kuwa mzazi yeyote atayebainika kuwa chanzo cha kukwamisha Ushahidi mahakamani atachukuliwa hatua za kisheria “Mtendaji kuanzia leo ikiwa kuna mzazi anahusika nayeye achukulie hatua za kisheria” Mhe. Machali

Akijibu swali kuhusu changamoto ya maji iliyoibuka wakati wa mkutano huo wa hadhara, Mhe. Machali amesema tayari serikali imeshatenga fedha kwa ajili ya kuleta maji safi na hata wataalamu kutoka Mamlaka ya Bonde la Maji mkoa wa Singida wapo Kijiji Nkinto kufuatilia vyanzo vya maji.

“Niwahikishishie wananchi wa Kijiji cha Nkinto na vijiji vya Jirani kuwa tayari watalaamu wetu wako kazini nimeambatanao hapa, mwaka huu hautaisha mtakuwa mmepata Maji” Mhe. Moses Mahali

MHE. JAMES MKWEGA AZINDUA ZAHANATI YA IGENGU


Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama Mhe. James Mkwega amezindua zahanati ya Igengu ikiwa ni mpango wa serikali wa kuhakikisha kila Kijiji nchini kinakuwa na zahanati.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa zahanati hiyo Julai 20,2024 katika Kijiji cha Igengu, Mhe. James Mkwega ameishukuru serikali pamoja na kwataka wananchi wa Kijiji hicho kulinda afya zao.
 
“Serikali imefanya kazi kubwa, Rais Dkt. Samia kaleta Zahanati na kaleta Umeme. Nampongeza pia Mganga Mkuu wetu Dkt. Solomon Michael kwa kazi kubwa anayofanya lakini pia niwapongeze wananchi kwa kazi kubwa mliofanya. Niwasihi tulinde afya zetu, tuzingatie ushauri wa wataalamu wetu”Mhe. Mkwega
 
Akizungumza kwa niaba ya Mkuregenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama, Dkt. Solomon Michael amewataka wajawazito wa Igengu kufika kliniki mapema ili kuepusha madhara yanayoweza jitokeza wakati wa kujifungua.
Awali akisoma taarifa kuhusu ujenzi wa zahanati hiyo, Mtendaji wa kata ya Ibaga Ndugu Abdallah Mohamedi amesema zahanati hiyo imegharimu kiasi cha shilingi milioni 110 ikiwa ni fedha kutoka Serikali Kuu, Fedha za Jimbo pamoja na nguvu za wananchi



 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2011. Singida Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogz za Mikoa