WATU SITA WAFARIKI KWA AJALI YA LORI KIJIJI CHA KATIKA KIJIJI CHA KIJOTA, SINGIDA.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

 Mmoja wa majeruhi akipatiwa matibabu ya mkono katika hospitali ya Mkoa wa Singida mara baada ya kupata ajali ya lori iliyoua watu 6 katika kijiji cha Kijota Singida.
 Mmoja wa majeruhi akiwa amelazwa huku akiendelea kupatiwa matibabu ya mkono katika hospitali ya Mkoa wa Singida mara baada ya kupata ajali ya lori iliyoua watu 6 katika kijiji cha Kijota Singida.
Baadhi ya ndugu na jamaa wa majeruhi wa ajali ya lori iliyoua watu sita wakiwa nje ya wodi za wagonjwa katika hospitali ya Mkoa wa Singida.


Watu sita wamefariki dunia huku wengine 42 wakijeruhiwa baada ya lori lenye namba za usajili T.806 AEL aina ya scania mali ya Abdalla Mussa (39) mfanyabiashara mkazi wa Mwenge mjini Singida, kuacha njia na kupinduka katika Kijiji cha Kijota, Singida.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida ACP Debora Magiligimba amesema ajali hiyo imetokea Agosti 27 mwaka huu saa 1.30 usiku katika kijiji cha Kijota wakati likitokea mnadani katika kijiji cha Mtinko Singida vijijini, likielekea Singida mjini.

ACP Magiligimba ametaja chanzo cha ajali kuwa ni uzembe wa dereva wa lori hilo Jumanne Kidanka (32) Kamanda huyo amesema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva ambaye hakuwa makini akiwa anaendesha lori hilo lililosheheni abira na mizingo mingi.

Amewataja waliofariki katika ajali hiyo kuwa ni Haji Jumanne (35), Mikidadi Mohammed (40) wote wawili wakazi wa kijiji cha Mrama na Musa Salimu (30) mkazi wa kijiji cha Mwakiti.

ACP Magiligimba amewataja wengine kuwa ni Allen Mwangu (38) mkazi wa wilaya ya Ikungi, Lucas Stephano (40) mkazi wa kijiji cha Mrama na Sharifa Omari (19) mkazi wa kijiji cha Ilongero.

Ameongeza kuwa majeruhi 20 wamelazwa katika hospitali ya Mkoa wa Singida, kumi wamelazwa hospitali ya misheni ya Mtinko na wanne ambao hali zao ni mbaya, wamelazwa katika hospitali ya misheni ya Hydom mkoani Manyara.

Ameeleza kuwa baadhi ya majeruhi walipatiwa matibabu na kurejea makwao huku wengine waliolazwa wamevunjika mikono, miguu na sehemu mbalimbali ya miili yao.

“Hawa wenye hali mbaya ni Fadhili Jumanne (33) mkazi wa Kibaoni mjini Singida, Mikidadi Hamisi, Jafari Hamisi na Idrisa Ibrahimu, wote wamevunjika miguu. Miili ya marehemu imehifadhiwa kwenye hospitali misheni Mtinko”, amesema.

DC MTATURU AMWAGA VIFAA VYA MICHEZO KWA TIMU 69 ZINAZOSHIRIKI MASHINDANO YA IKUNGI ELIMU CUP 2017

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.


Mkuu wa Wilaya ya Ikungi mhe Miraji J. Mtaturu akifungua mipira aliyoigawa kwa timu zote shiriki za mashindano ya mpira wa miguu maarufu kama "IKUNGI ELIMU CUP 2017"
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi mhe Miraji J. Mtaturu akionyesha moja ya mipira aliyoigawa kwa timu shiriki kwenye mashindano ya mpira wa miguu maarufu kama "IKUNGI ELIMU CUP 2017"

Baadhi za jezi zilizotolewa kwa ajili ya timu zote shiriki kwenye mashindano ya mpira wa miguu maarufu kama "IKUNGI ELIMU CUP 2017"
Na Mathias canal, Singida

Takribani timu 69 zinazoshiriki  mashindano ya mpira wa miguu maarufu kama “IKUNGI ELIMU CUP 2017” zimekabiziwa jezi pamoja na mipira kwa ajili ya utimilifu wa kuwa na vifaa vya michezo kwenye mashindano hayo jambo ambalo limeibua hisia chanya kwa kila timu kutaka kuibuka mshindi.

Akitoa vifaa hivyo vya michezo kwa ajili ya ushiriki wa timu hizo, Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu alisema kuwa Ofisi yake kwa ushirikiano mkubwa na wadau wa elimu na wananchi kwa ujumla wamechangia vifaa hivyo vya michezo ikiwa ni sehemu ya kuongeza chachu ya hamasa katika mashindano na kufikisha zaidi ujumbe wa umuhimu wa waanchi kuchangia mfuko wa elimu.

Mashindano hayo yanayoshadihishwa na kauli mbiu isemayo CHANGIA, BORESHA ELIMU IKUNGI yanafanyika katika vijiji vyote 101 ambapo katika Jimbo la Singida Magharibi lenye kata 15 kila Kata itatoa timu mbili na Jimbo la Singida Mashariki lenye Kata 13 kila kata itatoa timu tatu hivyo kuwa na timu 69 zitakazopambana na kupatikana timu tatu bora.

Mhe Mtaturu alisema kuwa kunzishwa kwa mashindano hayo ni kusudio la kuifanya jamii kujihusisha na shughuli za maendeleo kwa kushirikiana na serikali, kuibua vipaji vya michezo katika Wilaya ili kukuza ajira na kufanya vijana waachane na utumiaji wa madawa ya kulevya.

Sababu zingine ni Kuunganisha jamii kuwa kitu kimoja hatimaye vijana na wananchi kuimarisha upendo, ajira na afya sambamba na kudumisha amani na mshikamano.

Mashindano hayo yanataraji kufika ukomo Septemba 19, 2017 huku zawadi zikitaraji kutolewa kwa washindi watano ambapo mshindi wa kwanza atapatiwa zawadi ya Kombe, Seti ya jezi, Mipira miwili na kitita cha shilingi 1,000,000/= , na mshindi wa pili atapatiwa Seti ya jezi, Mipira miwili na shilingi 750,000/=.

Mshindi wa tatu atapatiwa Mipira miwili na shilingi 450,000/= , Mshindi wa nne atapatiwa Mpira mmoja na Shilingi 200,000/= huku mshindi wa tano akipatiwa Mpira mmoja na Shilingi 100,000/=.

Aidha, kutakuwa na zawadi zingine kwa timu yenye nidhamu, Zawadi ya mfungaji bora, Zawadi ya Kipa bora, Zawadi ya mchezaji bora, huku wachezaji wengine 30 wakichaguliwa kuingia kambini kufundishwa mbinu za uchezaji bora.

Katika taarifa ya Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu wakati wa uzinduzi wa ligi hiyo mbele ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida Dkt Angelina M. Lutambi aliyemuwakilisha Mkuu wa Mkoa huo Mhe Dkt Rehema Nchimbi, alisema kuwa Idara ya elimu katika Wilaya hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo upungufu wa nyumba za walimu, Upungufu wa Walimu, Maabara ya Masomo ya sayansi kwa shule za sekondari, pamoja na vifaa vya kujifunzia na kufundishia.

Hivyo Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi kwa ushirikiano na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya hiyo walianzisha mfuko wa elimu wilaya kwa mujibu wa sheria ndogo ya Halmashauri Wilaya ya Ikungi ya mwaka 2014 ambayo ilitolewa katika tangazo la serikali Na. 222 la tarehe 11 Julai, 2014 ili kuweza kukabiliana na changamoto za elimu ambazo zinaathiri mafanikio ya elimu katika Wilaya hiyo.

Kuanzishwa kwa mfuko wa elimu kumepelekea pia kufunguliwa kwa akaunti ya mfuko katika Benki ya NMB tawi la Ikungi kwa jina la Mfuko wa Elimu wa Wilaya ya Ikungi (Ikungi District Education Funds) akaunti Namba 52510000554.

Hata hivyo Mhe Mtaturu alitoa Rai kwa wadau wa elimu kuchangia mfuko wa elimu ili kukuza ufanisi wa elimu katika Wilaya hiyo ambao kwa kiasi kikubwa unategemea zaidi upatikanaji wa rasilimali fedha na nguvu kazi kutoka kwa wadau, wananchi, Taasisi, Mashirika, Makampuni mbalimbali yaliyopo ndani na nje ya nchi.



MBAO FC YAJAZWA MILION 140 YA UDHAMINI NA KAMPUNI YA GF TRUCKS & EQUIPMENT LTD

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Mkurugenzi wa Mtendaji kampuni ya GF Trucks & Equipment Imrani Karmali na Mwenyekiti wa Mbao Fc Solly Zephania Njashi wakionyesha hati ya makubaliano ya Mkataba ikiwa ni mkataba wa udhamini wa timu hiyo kwa mwaka mmoja wenye thamani ya Milioni 140 sambamba na basi la wachezaji.

 
Mwenyekiti wa Mbao Solly Zephania Njashi akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuingia makubaliano ya udhamini wa mkatabwa mwaka mmoja na na kampuni ya GF Trucks & Equipments wenye thamani ya Milioni 140, kushoto ni Mkurugenzi wa Mtendaji kampuni ya GF Trucks & Equipment Imrani Karmali 
Afisa Masoko wa Kampuni ya GF Trucks & Equipments Kulwa Bundala akizungumza na wanahabari baada ya kuingia mkataba na timu ya Mbao Fc wenye thamani ya Milioni 140 kwa mwaka mmoja.
Mkurugenzi wa Mtendaji kampuni ya GF Trucks & Equipment Imrani Karmali na Mwenyekiti wa Mbao Solly Zephania Njashi wakionyesha jezi za Mbao zitakazotumikia mwaka huu.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

UONGOZI wa klabu ya Mbao Fc umeingia mkataba wa mwaka mmoja wenye thamani ya milioni 149 na kampuni ya GF Trucks & Equipments ikiwa ni udhamini wa timu hiyo kutoka Jijini Mwanza.

Kampuni hiyo imeridhishwa na maendeleo ya timu hiyo na kuamua kuwapatia udhamini kwani hawajawahi kushiriki katika udhamin i wa soka la Kiwango cha ligi kuu.

Mkataba huo uliosainiwa mbele ya waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Imrani Karmali amesema kuwa mkataba huo ni wa kihistoria kwani unaenda kuleta na kukuza maendeleo ya mpira wa miguu nchini.
Karmal amesema kuwa, madhumuni makubwa ni kukuza vipaji vya mpira wa miguu na wanatarajiwa kuisaidia Mbao Fc kufikia malengo yao msimu huu, " tunafahamu usafiri umekuwa ni tatizo kwa klabu nyingi ndogo za Ligi Kuu na hicho kimetupelekea kuanza na basi msimu huu ambapo katika mkataba wa milioni 140 utajumuisha sambamba na basi hilo la wachezaji lenye thamani ya milioni 70,".

"uwezo waliouonesha katika ligi kuu na hata kuingia fainali ya kombe la FA ulituhamasisha kuifuatilia kwa ukaribu sana na tuna imani kwa msaada wetu Mbao itaendelea kufanya vizuri na si hao tu bali hata ajira kwa vijana zitaongezeka,"amesema Karmali.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Mbao Fc, Solly Zephania Njashi ameusifu mkataba huo na kusema kuwa utazidi kuleta chachu ya maendeleo katika klabu yao na hata kupunguza gharama za mahitaji kwa wachezaji.

Njashi ameishukurui kampuni ya GF Trucks & Equipments kwa mkataba huo na kuwaahidi mashabiki na wapenzi wa Mbao kuwa mwaka huu wataendelea kufanya vizuri na kuendelea kusalia katika Ligi kuu msimu ujao.

Baada ya kusaini mkataba huo, kampuni ya GF Trucks & Equipments i iliwakabidhi mfano wa jezi zitakazovaliwa na timu ya Mbao tayari zikiwa zimeshaweka nembo ya kamouni hiyo.
 

POLISI SINGIDA WAUA MTU MMOJA AKIDAIWA KUWA JAMBAZI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Mkazi wa kijiji cha Shiponga, Hanang Mkoani Manyara anayedaiwa kuwa jambazi, Hamisi Athumani (32), amefariki dunia baada ya kupigwa risasi kiunoni na askari polisi wakati akiwa katika harakati ya kutoroka.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani hapa, ACP Debora Magiligimba, amesema tukio hilo limetokea Agosti 25 mwaka huu saa nane mchana, huko katika kijiji cha Mgori tarafa ya Ngimu wilaya ya Singida.

Amefafanua kuwa Hamisi (marehemu) alipigwa risasi na askari polisi wakati akijaribu kuwatoroka mara baada kuonyesha bunduki aina ya rifle yenye namba 7358 na risasi zake tano.

Amesema bunduki hiyo iliyokuwa imekatwa mtutu na risasi zake tano zilikuwa zimefichwa kwenye soksi, vitu hivyo vilikuwa vilihifadhiwa kwenye mfuko wa sandarusi, na kufichwa chini ya jiwe.

ACP Magiligimba amesema Agosti 23 mwaka huu, mtuhumiwa alikamatwa na wananchi wa kijiji cha Ngamu, na kufikishwa katika kituo cha polisi cha kijiji hicho kwa tuhuma ya kujihusisha na matukio ya ujambazi.

“Kesho yake mtuhumiwa alihojiwa na kukiri kujihusisha na matukio ya ujambazi wa kutumia silaha katika mikoa mbalimbali. Pia aliahidi kuwapeleka askari kuwaonyesha mahali alikoificha silaha anayoitumia kwenye matukio hayo ya ujambazi,” amesema ACP Magiligimba.

Kamanda huyo amesema Agosti 25 mwaka huu saa sita mchana, askari polisi wakiwa na mtuhumiwa, walikwenda katika pori la kijiji cha Mgori mahali alipokuwa ameficha bunduki hiyo aina ya rifle.

“Mara tu baada ya kuwaonyesha askari hao silaha hiyo na wakati askari wanaendelea kufanya upekuzi katika eneo hilo, mtuhumiwa alijaribu kutoroka askari kwa kukimbia” amesema na kuongeza.

“Askari mmoja alifyatua risasi tatu hewani akimtaka asimame, lakini hakutii. Ndipo alipompiga risasi moja iliyompata sehemu ya kiunoni”.

Amesema jereha hilo la risasi lilisababisha mtuhumiwa Hamisi avuje damu nyingi, na hivyo kufariki dunia wakati akikimbizwa hospitali ya mkoa kwa matibabu.

“Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida linaendelea kutoa wito kwa wananchi waote kutoa taarifa zitakazosaidia kubaini wahalifu katika maeneo yao ili hatua ziweze kuchukuliwa kudhibiti vitendo vya kihalifu,” amesema kamanda huyo.

Chanzo Kijukuu

YALIYOJIRI KWENYE UZINDUZI WA MFUKO WA ELIMU WILAYANI IKUNGI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.


Jumamosi iliyopita, Agost 19,2017 Wilaya ya Ikungi mkoani Singida ilizindua rasmi “Mfuko wa Elimu Ikungi” ulioanzishwa wilayani humo kwa lengo la kusaidia utatuzi wa kero za elimu ikiwemo uhaba wa maabara, madarasa, vyoo pamoja na nyumba za waalimu.

Katika uzinduzi huo, pia zilifanyika shughuli kadhaa ikiwemo uzinduzi wa ligi ya soka ya “Ikungi Elimu Cup 2017” yenye lengo la kuhamasisha wananchi pamoja na wadau mbalimbali kuchangia Mfuko wa Elimu Ikungi, uzinduzi wa zoezi la ufyatuaji wa matofali ambapo kila Kata wilayani Ikungi imeazimia kufyatua matofali elfu kumi.

Karibu kwa dakika chache kutazama yaliyojiri kwenye uzinduzi huo ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt.Rehema Nchimbi ambaye aliwakilishwa na Katibu Tawala mkoani humo Dkt.Angeline Lutambi huku mwenyeji wake akiwa ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi na mlezi wa Mfuko wa Elimu Ikungi, Mhe.Miraji Jumanne Mtaturu. Tazama video hapo chini.

MABAO 19 YATUPIWA MECHI ZA UFUNGUZI LIGI KUU

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


Matola aanza kwa kuiwezesha Lipuli kutoa onyo, mabao 19 yatupiwa mechi 

WAKATI jumla ya mabao 19 yamefungwa kwenye mechi za raundi ya kwanza ya ligi hiyo iliyoanza juzi na kuendelea jana, Yanga imeendeleza rekodi ya Ligi Kuu Bara baada ya kulazimisha sare dhidi ya vijana wa Suleiman Matola, Lipuli FC ya Iringa.
Tangu msimu wa 2010/11, haijawahi kutokea mechi za ufunguzi za ligi hiyo kuchezwa bila kuwapo na mechi hata moja yenye matokeo ya sare, jambo ambalo kama mechi hiyo ya jana timu mojawapo ingeshinda basi ingekuwa ni rekodi mpya.

Aidha, mabao 19 yaliyofungwa katika mechi za ufunguzi msimu huu yamevunja rekodi ya magoli yaliyofungwa katika mechi za ufunguzi msimu uliopita uliokuwa na mabao 12 kwenye mechi zake za raundi ya kwanza.

Idadi hiyo ya mabao imepatikana baada ya matokeo ya Simba kushinda 7-0 dhidi ya Ruvu Shooting, Mwadui kuifunga Singida United 2-1 na Prisons kuitandika Njombe Mji 2-1.

Matokeo mengine ni Azam kuifunga Ndanda bao 1-0, Mbeya City kushinda bao 1-0 dhidi ya Majimaji, Mbao kuichapa Kagera Sugar bao 1-0, Mtibwa kuifunga Stand United 1-0 kabla ya jana Yanga kulazimishwa sare ya bao moja kwa moja.

Katika mechi ya jana ambayo ilipigwa kwenye Uwanja wa Uhuru, Yanga ambao walikuwa wanatafuta ushindi hasa baada ya watani zao wa jadi, Simba kuanza kwa kishindo cha ushindi wa bao 7-0 dhidi ya Ruvu Shooting, jana walikosa maarifa ya kuipenya ngome ya Lipuli iliyokuwa chini ya Asante Kwasi, aliyejiunga na timu hiyo msimu huu akitokea Mbao FC.

Wageni, Lipuli ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao katika dakika ya 44 kupitia kwa mshambuliaji wa zamani wa Azam FC na JKT Ruvu, Seif Abdallah, aliyepiga shuti upande wa kulia wa Uwanja lililoenda moja kwa moja nyavuni na kumshinda golikipa Youthi Rostand.
Bao hilo lilidumu kwa dakika moja tu kutokana na Thaban Kamusoko kuisawazishia timu yake kwa kichwa akiunganisha nyavuni mpira wa kona uliochongwa na Ibrahim Ajibu.

Baada ya bao hilo, liliwafanya wachezaji wa Lipuli kumzinga mwamuzi Hans Mabena kufuatia mpira uliopigwa na Kamusoko kugonga mwamba wa juu na kuangukia ndani huku wachezaji wakidhani mpira huo uliangukia nje ya goli.
Pamoja na Yanga kufanya mashambulizi mfululizo, Lipuli walikuwa imara na kufanikiwa kuwabana Yanga wasipate bao la pili.

Hata hivyo, Lipuli ilipata pigo baada ya beki wake Kwasi kupewa kadi ya pili ya njano iliyomfanya kutolewa kwa nyekundu zikiwa zimebaki dakika mbili mpira kumalizika.

Baada ya mpira kumalizika mashabiki wa Yanga walionekana kuwatolea maneno machafu wachezaji wa Lipuli huku wakiwatuhumu kwa vitendo vyao vya kujiangusha mwishoni mwa kipindi cha pili.

Katika mchezo huo kiungo wa Yanga, Kabamba Tshishimbi alishindwa kuonyesha makeke yake kama alivyofanya kwenye mchezo dhidi ya Simba baada ya kubanwa na viungo wa Lipuli Sahaban Zuberi na Mussa Nampaka.

Imeandaliwa na Faustine Feliciane na Adam Fungamwango

WANAFUNZI WENYE MIMBA SASA KUANZA KUSAKWA MASHULENI.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Fadhil Nkurlu amesema kamati ya ulinzi na usalama imekamilisha utaratibu wa kuwasaka wanafunzi wenye mimba ili kuchukua hatua.
Aliitoa kauli hiyo juzi akiwa Kata ya Ntobo katika Halmashauri ya Msalala wakati wa makabidhiano ya mradi wa maendeleo ya jamii wa ADP Busangi uliokuwa ukitekelezwa na shirika la World Vision Tanzania kwa kuishirikisha wananchi.

Alisema pamoja na mafanikio ya mradi huo, Nkurlu ambye pia ni Mkuu wa Wilaya hiyo, alisema kwa sasa tayari utaratibu wote kupitia kamati zote za ulinzi na usalama za mji, Msalala na Ushetu zimekaa na kukubaliana kuwasaka shule hadi shule wasichana watakao kuwa na mimba.

“Baada ya kukubaliana kitakaochofuata ni kuwakamata na wale watakaobainika hatua kali zitachukuliwa, Serikali haiwezi kutumia fedha nyingi kwa ajili ya watoto kwenda shule lakini yanafanyika mambo kinyume,” alisema.

Kaimu mkurugenzi wa shirika hilo, Johnson Robinson alisema utekelezaji wa mradi huo umeiinua sekta ya elimu.
 
Chanzo Kijukuu

MTUHUMIWA WA UJAMBAZI AFARIKI KWA KUPIGWA RISASI WAKATI AKITOROKA MKOANI SINGIDA.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

 
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida ACP Debora Magiligimba akionyesha bunduki aina ya rifle iliyokuwa ikimilikiwa na mtuhumiwa wa ujambazi Hamisi Athumani (32) mkazi wa Shiponga-Hanang mkoa wa Manyara anayedaiwa kuitumia kwenye matukio ya ujambazi. 
Picha/habari na Nathaniel Limu

 

Mkazi wa kijiji cha Shiponga – Hanang Mkoani Manyara anayedaiwa kuwa jambazi, Hamisi Athumani (32), amefariki dunia baada ya kupigwa risasi kiunoni na askari polisi wakati akiwa katika harakati ya kutoroka.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani hapa, ACP Debora Magiligimba, amesema tukio hilo limetokea Agosti 25 mwaka huu saa nane mchana, huko katika kijiji cha Mgori tarafa ya Ngimu wilaya ya Singida.

Amefafanua kuwa Hamisi (marehemu) alipigwa risasi na askari polisi wakati akijaribu kuwatoroka mara baada kuonyesha bunduki aina ya rifle yenye namba 7358 na risasi zake tano.

Amesema bunduki hiyo iliyokuwa imekatwa mtutu na risasi zake tano zilikuwa zimefichwa kwenye soksi, vitu hivyo vilikuwa vilihifadhiwa kwenye mfuko wa sandarusi, na kufichwa chini ya jiwe.

ACP Magiligimba amesema Agosti 23 mwaka huu, mtuhumiwa alikamatwa na wananchi wa kijiji cha Ngamu, na kufikishwa katika kituo cha polisi cha kijiji hicho kwa tuhuma ya kujihusisha na matukio ya ujambazi.

“Kesho yake mtuhumiwa alihojiwa na kukiri kujihusisha na matukio ya ujambazi wa kutumia silaha katika mikoa mbalimbali. Pia aliahidi kuwapeleka askari kuwaonyesha mahali alikoificha silaha anayoitumia kwenye matukio hayo ya ujambazi”, amesema ACP Magiligimba.

Kamanda huyo amesema Agosti 25 mwaka huu saa sita mchana, askari polisi wakiwa na mtuhumiwa, walikwenda katika pori la kijiji cha Mgori mahali alipokuwa ameficha bunduki hiyo aina ya rifle.

“Mara tu baada ya kuwaonyesha askari hao silaha hiyo na wakati askari wanaendelea kufanya upekuzi katika eneo hilo, mtuhumiwa alijaribu kutoroka askari kwa kukimbia” amesema na kuongeza;

“Askari mmoja alifyatua risasi tatu hewani akimtaka asimame, lakini hakutii. Ndipo alipompiga risasi moja iliyompata sehemu ya kiunoni”.

Amesema jereha hilo la risasi lilisababisha mtuhumiwa Hamisi avuje damu nyingi, na hivyo kufariki dunia wakati akikimbizwa hospitali ya mkoa kwa matibabu.

“Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida linaendelea kutoa wito kwa wananchi waote kutoa taarifa zitakazosaidia kubaini wahalifu katika maeneo yao ili hatua ziweze kuchukuliwa kudhibiti vitendo vya kihalifu”, amesema kamanda huyo.

UVCCM MKOANI SINGIDA WAMPONGEZA DC IKUNGI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Umoja wa Chama cha Mapinduzi UVCCM mkoani Singida umempongeza Mkuu wa Wilaya ya Ikungi mkoani humo Mhe.Miraji Mtaturu kwa kuanzisha michuano ya Ikungi Elimu Cup 2017 ili kuhamasisha wananchi na wadau mbalimbali kuchangia utatuzi wa changamoto za elimu kupitia Mfuko wa Elimu Ikungi.

Mwenyekiti wa UVCCM mkoani Singida, Jimson Mhagama (pichani) alitoa pongezi hizo jana Agosti 19,2017 kwenye uzinduzi wa michuano hiyo uliofanyika kwenye uwanja wa shule ya sekondari Ikungi mkoani Singida ambapo mgeni rasmi alikuwa Katibu Tawala mkoani Singida, Dkt.Angeline Lutambi aliyemwakilisha Mkuu wa mkoa huo Dkt.Rehema Nchimbi.

Uzinduzi wa michuano hiyo, ulikwenda sambamba na uzinduzi wa zoezi la ufyatuaji wa matofali kwa ajili ya ujenzi wa maabara uliokwama tangu mwaka 2009 katika shule ya sekondari Ikungi hii ikiwa ni uzinduzi rasmi wa zoezi kama hilo kwenye kata zote wilayani Ikungi ambapo kila Kata imepewa jukumu la kufyatua matofali elfu kumi kwa ajili ya ujenzi wa madarasa na nyumba za waalimu.

Katika zoezi hilo, walijitokeza wadau pamoja na viongozi mbalimbali wakiwemo madiwani, wenyeviti wa halmashauri, jeshi la polisi, Tanesco na wanachi ambao walimuunga mkono Mkuu wa wilaya ya Ikungi, Mhe.Mtaturu aliyekabidhi mifuko 100 ya simenti na wao wakachangia fedha taslimu zaidi ya shilingi 800,000 na ahadi zaidi ya shilingi 1,900,000, ahadi za simenti mifuko 194 na mchanga wa moramu malori matano kutoka kwa mdau wa maendeleo wilayani Ikungi Hussein Sungita.

IKUNGI UNITED WAJINOA KUELEKEA MICHUANO YA "IKUNGI ELIMU CUP 2017" MKOANI SINGIDA.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Fundi akichomelea vyuma kwa ajili ya kufunga nyavu ikiwa ni marekebisho ya mwisho katika uwanja wa shule ya Sekondari Ikungi, wilaya ya Ikungi mkoani Singida kwa ajili ya maandalizi ya michuano ya ligi ya mpira wa miguu ya Ikundi Elimu Cup 2017 wilayani Ikungi.
Kauli mbiu katika mashindano hayo ni " Changia, Boresha Elimu Ikungi.

Na George Binagi, BMG
Mashindano hayo yatashirikisha timu mbalimbali kutoka Kata 28 wilayani Ikungi yakilenga kuhamasisha wananchi na wadau wengine wa elimu kushiriki katika kutatua changamoto za elimu ikiwemo uhaba wa madarasa, nyumba za waalimu, maabara pamoja na vyoo vya shule.

Hii ni baada ya Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe.Miraji Jumanne Mtaturu kuteuliwa kuwa mlezi wa mfuko wa elimu wilayani humo na hivyo kuamua kuanzisha michuano hiyo ili kuleta chachu kwa wananchi na wadau mbalimbali kuchangia masuala ya kielimu.

Jumamosi timu ya soka ya Ikungi United na inakuwa ikimenyana na timu ya Puma ambapo mchezo huo utatanguliwa na mchezo kati ya madiwani wa halmashauri ya manispaa ya Singida dhidi ya madiwani wa halmashauri ya Wilaya ya Ikungi.

Katika mchezo huo wa awali timu ya madiwani kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Ikungi itaongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu huku timu ya madiwani wa halmashauri ya Manispaa ya Singida ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhe.Elias Tarimo.

Ufunguzi wa mashindano hayo utatanguliwa na shughuli ya ufyatuaji matofali ambapo kila Kata wilayani Ikungi imetakiwa kufyatua matofali yasiyopungua 10,000 ili kusaidia ujenzi wa madarasa, nyumba za waalimu na vyoo vya shule.
Mwl.Seth Raban Mwakalasya ambaye ni mjumbe wa kamati ya maandalizi ya ligi ya ligi ya soka ya Ikungi Elimu Cup 2017 yanayotarajiwa kuanza katika wilaya ya Ikungi mkoani Singida, Jumamosi Agosti 19 katika uwanja wa shule ya sekondari Ikungi.
Timu ya soka ya Ikungi United Sports Club ikifanya mazoezi katika uwanja wa shule ya msingi Ikungi jioni ya leo
Ikungi United Sports Club wakifanya mazoezi katika uwanja wa shule ya msingi Ikungi jioni ya leo
Ikungi United Sports Club watamenyana na timu ya Puma katika mchezo wa ufunguzi wa mashindano ya Ikungi Elimu Cup 2017
Timu ya Ikungi United Sports Club ikiwa kwenye mazoezi hii leo jioni
Nahodha wa timu ya Ikungi United Sports Club, Lazaro John Francis (pichani) amesema maandalizi yao yako vizuri na kwamba michuano ya Ikungi Elimu Cup 2017 itakuwa na ushindani mkubwa hivyo wapenzi wa soka wategemee soka la kuvutia kwenye michuano hiyo
Kocha wa timu ya soka ya Ikungi United Sports Club, Danny Ayoub amesema kikosi chake kimejipanga vyema na kwamba michuano itaweza kuiwezesha timu yake kusonga mbele kimichezo nchini ikifuata nyayo za kaka zao Singida United.
Kikosi cha Ikungi United Sports Club kikiwa kwenye tathmini fupi baada ya mazoezi ya hii leo jioni
Kocha wa kikosi cha Ikungi United Sports Club akitoa tathmini fupi baada ya mazoezi ya timu hiyo jioni ya leo ikiwa ni maandalizi ya kuelekea kwenye michuano ya Ikungi Elimu Cup 2017 katika wilaya ya Ikungi mkoani Singida ambapo michuano hiyo itafunguliwa jumamosi Agosti 19,2017 huku mgeni rasmi akiwa ni Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mhe.Dkt.Rehema Nchimbi.
Kauli mbiu katika mashindano hayo ni " Changia, Boresha Elimu Ikungi.

MAANDALIZI YA IKUNGI ELIMU CUP 2017 YAPAMBA MOTO

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

Na Mathias Canal, Wazo Huru Blog

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu Jana Agosti 16, 2017 ametembelea na kukagua uwanja utakaotumika kwa ajili ya Mashindano ya ligi ya mpira wa miguu Wilayani Ikungi Mkoani Singida Maarufu kama “IKUNGI ELIMU CUP 2017” 

Mhe Mtaturu akiwa ameongozana na Viongozi Mbalimbali katika Wilaya hiyo amezuru katika Uwanja wa shule ya Sekondari Ikungi ili kujionea Hatua za mwisho za maandalizi ya mashindano hayo.

Akizungumza na Mtandao wa www.wazo-huru.blogspot.com Mhe Mtaturu alisema kuwa mashindano hayo yataanza kurindima Siku ya Jumamosi Agosti 19 huku yakiwa na dhamira ya kuwafikia zaidi ya wananchi 5000 katika Wilaya hiyo.

Mashindano hayo yatakayofunguliwa na Mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe Dkt Rehema Nchimbi na kuzikutanisha timu mbalimbali kutoka Kata zote 28 na vijiji 101 katika Wilaya ya Ikungi huku yakiongozwa na kauli mbiu ya “ Changia, Boresha Elimu Ikungi”.

Mechi ya ufunguzi itakuwa ni kati ya timu ya Kata ya Ikungi na Timu ya Kata ya Puma ambapo kabla ya kufunguliwa kwa mashindano hayo kutakuwa na mchezo dhidi ya Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Singida waatakaovaana vikali na Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi.

Katika mchezo huo wa awali Timu ya Madiwani kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Ikungi itaongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji J. Mtaturu huku timu ya Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Singida ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhe Elias Tarimo.

Katika ufunguzi wa mashindano hayo kutakuwa na zoezi la Uzinduzi wa zoezi la ufyatuaji matofali ambapo kila Kata imetakiwa kufyatua  matofali 10,000 ikiwa ni sehemu ya kuhimiza utatuzi wa Changamoto mbalimbali Wilayani Ikungi ikiwemo Upungufu wa nyumba za walimu, Vyumba vya madarasa, Ofisi za walimu, Maabara, Thamani mbalimbali, Matundu ya vyoo vya walimu na wanafunzi.

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu aliteuliwa kuwa mlezi wa mfuko wa Elimu kuhakikisha anahamasisha wananchi na wadau wachangie ili kufanikisha kuboresha miundombinu ya elimu katika wilaya ya Ikungi.

Mtaturu Alisema kuwa Uzinduzi  wa ufyatuaji matofali umeanzishwa kwa ajili ya majukumu muhimu kusaidia sekta ya Elimu ikiwa ni pamoja na kuendeleza ujenzi wa maabara uliokwama toka mwaka 2009.

Mtaturu alisema kuwa katika ufunguzi wa mashindano hayo pia kutakuwa na zoezi la kukabidhi zawadi kwa shule ya sekondari Ikungi iliyofanya vizuri katika matokeo ya kidato cha sita na kupelekea kuongoza kikanda kwa wanafunzi 16 kupata Daraja la kwanza.

Kuanza kwa mashindano hayo ya “IKUNGI ELIMU CUP 2017” ni utekelezaji wa Wazo la kuanzisha Mfuko wa Elimu lilitokana na kikao cha wadau wa elimu kilichoitishwa na Mkuu huyo wa Wilaya mwezi Disemba, 2016 na kubaini changamoto zinazoikabili sekta ya elimu ikiwemo kushuka kwa ufaulu wa wanafunzi kuanzia elimu ya msingi mpaka Sekondari.


UJENZI WA BOMBA LA MAFUTA GHAFI: MRADI WENYE FURSA KEDEKEDE WATANZANIA WANAPASWA KUZICHANGAMKIA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Hivi Karibuni, Rais wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli na Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda kwa pamoja waliweka jiwe la msingi la Ujenzi wa Bomba la Mafuta Ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Tanga Tanzania. Katika Makala hii pamoja na mambo mengine Mwandishi Said Ameir wa Idara ya Habari- MAELEZO anaeleza kwani nini mradi huu ni kipimo cha utayari na ujasiri wa watanzania katika kuchangamkia fursa.

Mradi huu unaojulikana kama Mradi wa Bomba la Kusafirisha Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) unatekelezwa kwa ubia kati ya washirika wa sekta binafsi na sekta za umma za nchi za Tanzania na Uganda.

Washirika hao ni Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Kampuni ya Taifa ya Petroli ya Uganda (UNOC), Kampuni ya Mafuta ya Total ya Ufaransa, Kampuni ya TULLOW yenye makao makuu yake London nchini Uingereza na Kampuni ya China National Offshore Oil Company (CNOOC).

Bomba ambalo litagharimu dola za kimarekani 3.5 bilioni, sehemu yake kubwa yaani kilomita 1,115 kati ya kilomita 1,445 litajengwa katika ardhi ya Tanzania na kupita mikoa 8, wilaya 24 na vijiji 184.

Kutokana na hali hiyo, inaelezwa kuwa, mradi huu wakati wa ujenzi na utakapokamilika, utatoa na fursa nyingi za kiuchumi ambazo zitasaidia sana kuchangamsha shughuli za kiuchumi hivyo kuchangia ukuaji uchumi na kuinua kiwango cha maisha ya watanzania kwa namna mbalimbali.

Mradi huu ni mfano wa ushirikiano kati ya nchi za Tanzania na Uganda na kwa upande mwingine ni mfano mzuri wa ushirikiano kati ya sekta binafsi na sekta za umma katika nchi hizi. 
Katika hatua mbalimbali za utekelezaji wake, mradi huu utahitaji ushiriki wa sekta binafsi katika nchi zote mbili na wakati mwingine hata taasisi nyingine za umma ambazo zinatoa huduma zitakazohitajika na mradi.

Kwa hiyo, wakati tukisifia kuwa ni mfano wa mradi wa ubia wa sekta ya umma na sekta binafsi katika nchi zetu, watanzania hawana budi kuelewa kuwa wana wajibu mkubwa wa kuzitumia vyema fursa za mradi huu.

Kwa Tanzania, mradi huu unaweza kuonesha picha halisi ya ushirikiano wa sekta hizo kwa kuzingatia namna makampuni na taasisi za humu nchini zitakavyoweza kushiriki na kufanikisha mradi huu.

Kwa maana nyingie ni mradi ambao unaweza kutumika kupima utayari, umakini, uwezo na ujasiri wa watanzania katika kuchangamkia fursa za kiuchumi.

Kama alivyoeleza Rais Magufuli wakati wa sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi kuwa katika mradi huu, Serikali imesamehe mambo mengi ili uweze kutekelezwa kwa kuishirikisha Tanzania. Wataalamu wa nchi walichambua na kupembua hadi kubaini kuwa kusamehe huko kutafidiwa na fursa nyingi zitakazoletwa na mradi huu.

Kwa maana hiyo bila ya watanzania kuchukua hatua madhubuti za kuhakikisha wanazitumia kadri itakavyowezekana fursa hizo uamuzi huo wa Serikali kusamehe hivyo ilivyovisamehe hautakuwa na maana yeyote.

Kuja kwa mradi huu Tanzania, watanzania hawana budi kuipongeza Serikali chini ya Rais John Pombe Magufuli kwa jitihada kubwa kwa kutumia ushawishi wa kisiasa, kidiplomasia, uchumi na ukaribu wa viongozi wa nchi hizo mbili pamoja na hoja nyingine hadi kufanikisha mradi huu kuja Tanzania.

Jitihada hizi ni kielelezo cha dhamira ya kweli iliyonayo Serikali ya Awamu ya Tano ya kutafuta kila aina ya fursa za kiuchumi ambazo zitasaidia kutimiza ahadi zake kwa watanzania ya kujenga Tanzania yenye uchumi imara.

Serikali imejitwika mzigo mkubwa wa kushiriki katika kutekeleza mradi huu mkubwa wa aina yake lakini imefanya hivyo kwa kuamini kuwa watanzania wako tayari na wako imara kuupokea kwa hali na mali.

Imeelezwa mara kwa mara kuwa mradi huu utaliingizia taifa mapato makubwa, utaleta tekinolojia na utalaamu na fursa za kiuchumi ambazo watekelezaji wake kwa kiwango kikubwa ni kutoka sekta binafsi. Kwa mnasaba huo, Serikali hapa imefanya zaidi ya wajibu wake ambao ni wa kujenga mazingira mazuri ya kuvutia uwekezaji.

Wale wahenga wa Cambrigde walisema“give us the tools and lets finish the job” na hivi ndivyo ilivyofanya Serikali kwa mradi huu. Imeleta mradi na kufungua fursa tele ambazo watanzania wanapaswa kuzitumia kujenga kiuchumi wao binafsi na uchumi wa taifa.

Haitakuwa na maana hata kidogo katika ngazi ya serikali na katika ngazi ya Mtanzania mmoja mmoja kufika wakati fursa za mradi huu kuchukuliwa na wageni kwa sababu zozote na katika mazingira yeyote yale. Ikifikia hatua hiyo watanzania watakuwa wamewaangusha viongozi wao.

Hii kutokana na mazingira ambayo Serikali imeyaweka kuwawezesha watanzania kushiriki katika sekta ya mafuta na gesi asilia. Mbali ya kupitisha Sheria ya Local Content Act ya 2015 ambayo inasisitiza ushiriki wa watanzania lakini zaidi dhamira ya kweli ya kisiasa iliyonayo uongozi wa Serikali ya kuhakikisha kuwa watanzania wanafaidika ipasavyo na mradi huu.

Ni jambo la kutia moyo kuona kuwa baadhi ya Taasisi za Serikali na za sekta binafsi zimeshaanza maandalizi au zimejitokeza kuwaandaa watanzania kuchangamkia fursa hizo na kuhakikisha wanazitumia vyema.

Miongoni mwa taasisi hizo ni Jumuiya ya Watoa Huduma katika Sekta ya Mafuta na Gesi (ATOGS) ambayo inawakusanya pamoja watoa huduma katika sekta hiyo ambapo lengo lake kubwa ni kuhakikisha kuwa fursa za mradi huo zinatumika ipasavyo kwa manufaa ya muda mfupo na mrefu ya watanzania.

ATOGS, kama taasisi nyingine zitakazoelezwa baadae, imeonesha mfano wa utayari kwa kuwa na mpango mkakati wake ambao unalenga kuwawezesha watoa huduma wa humu nchini wanapata fursa hizo kwa kuwasaidia kwa namna mbali mbali tangu hatua za awali za kuwania fursa hizo hadi utekelezaji wake.

Makamu Mwenyekiti wa Taasisi hiyo Abdulsamad Abdulrahim katika moja ya mikutano na waandishi wa habari alisema taasisi yake imejipanga kuwajengea uwezo watoa huduma na kutoa wito watoa huduma hao kwa waliokuwa bado hawajajiunga wajiunge na taasisi hii kwa minajili ya kufaidika na uwezeshaji wao.

Halikadhalika, Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) nalo linaeleza kuwa limejidhatiti kuhakikisha kuwa watanzania watakaobahatika kupata fursa za kutoa huduma katika mradi huo hawashindwi kwa kukosa fedha za kutekeleza kandarasi zao.

“Hatutaki kusikia mtanzania amekosa fursa hii kwa sababu ya kukosa fedha …ukibahatika njoo kwenye Baraza tutakushauri… Serikali ina mifuko 17 yenye fedha za kutosha kukuwezesha” anaeleza Mkurugnezi wa uwezeshaji wa NEEC Bwana Edwin Chrisant.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF) Bwana Godfrey Simbeye aliwaambia waandishi wa habari kuwa taasisi yake imejipanga kuhakikisha kuwa mikataba ya kandarasi itakayofikiwa inazingatia maslahi ya pande zote na utekelezaji wake unafanyika kulingana na vipengele vya mikataba.

Dhamira hizi zilizoelezwa na taasisi hizi muhimu nchini, hapana shaka yoyote kuwa ni habari njema inayoashiria matumaini makubwa na kuonesha sasa watanzania wameamka na wamedhamiria kujenga Tanzania mpya kwa kila mmoja kwa nafasi yake kuyatumia mazingira yaliyopo kujenga uchumi wa taifa.

Kama kweli taasisi hizi zitatekeleza yale ziliyojipangia ikiwemo kuwapatia watoa huduma msaada wa kitaalamu, huduma za kisheria, kifedha, viwango na vigezo katika manunuzi, utaalamu, kuwaunganisha na wabia, kuwajengea uwezo vijana wasomi ili waweze kushika nafasi zitakuwa zimetoa msaada mkubwa kwa nchi.

Kwa hakika mradi huu kama ilivyoelezwa awali utakuwa kigezo muhimu kupima utayari, umakini na uwezo wa sekta binafsi kuchangamkia fursa zinapotokea na mafanikio ya ushiriki wa sekta hiyo huenda ukawa mwanzo mzuri wa kuupa mgongo utamaduni ulizoeleka wa watanzania kulalamika hususan kuilalamikia Serikali kuwa haiwapi fursa kama hizi.

Wahenga walisema “shike shike na mwenyewe nyuma” kwa hili Serikali zimefanya wajibu wake sasa mpira uko kwa wadau katika sekta binafsi kuucheza kwa zitumia fursa na ni vyema kukumbuka kuwa “mso matendo hula uvundo” hivyo watanzania wachangamkie fursa wasije wakajikuta karamu imekwisha ‘wakaramba vyungu.

 Ni vyema pia kutanabahisha kuwa fursa za mradi huu haziko kwa watoa huduma kama hao pekee ambao wao ni wafanyabiashara na wataalamu ambao tayari wanajielewa, wana uwezo na wako katika sekta hiyo hivyo tunaweza kusema wana angalau uzoefu.

Lakini ukweli hi kuwa fursa za mradi huu zimetapakaa kila mahala katika ngazi mbali mbali kuanzia wakulima wa jembe la mkono, wafugaji wadogo wadogo, mafundi mchundo, hadi vibarua wa ujenzi. Hivyo taasisi zinazohusika zinapaswa pia kuliangalia kundi hili kubwa na kuhakikisha linashiriki vyema.

Hii ni kwa sababu, inapozungumziwa ajira elfu kumi na ajira nyingine zaidi ya elfu thelathini nyingi zinawagusa watanzania wa kundi hili. Ikumbukwe kuwa kundi hili ambalo ndilo litakalokuwa karibu na mradi ndilo litakalokuwa la kwanza kulalamika pindi litakapokosa fursa na kujikuta halina namna ya kushiriki na kufaidika.

Utekelezaji mzuri na wenye ufanisi wa mradi huu kwa kushirikisha sekta binafsi nchini utakuwa kigezo cha kufungua milango kwa miradi mingine mikubwa ya aina hii humu nchini.



Watanzania hawana budi kumpongeza Rais Magufuli kwa jitihada zake za kujenga Tanzania Mpya yenye matumaini mapya. Hakika Tanzania yenye uchumi wa kati na ya viwanda inawezekana, kama kila mmoja atatimiza wajibu wake

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2011. Singida Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogz za Mikoa