21 WAJERUHIWA WAKITOKA HARUSINI

MTU mmoja amekufa na wengine 21 kujeruhiwa, baada ya basi dogo aina ya Coaster walilokuwa wakisafiria kutoka Shinyanga kwenye harusi, kurejea nyumbani kwao Morogoro kupinduka katika kijiji cha Ikugha wilayani Ikungi kwenye barabara kuu ya Singida - Dodoma.
Mkuu wa Wilaya ya Singida, Queen Mlozi akizungumza kwenye hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida, walikolazwa majeruhi, alisema kuwa ajali hiyo ilitokea juzi majira ya saa 8.00 mchana.
Alisema kuwa ajali ilitokea baada ya Coaster hiyo, kuhamia upande wa kulia wa barabara, kukwepa uharibifu uliotokana na kungâ™oka mkanda wa chuma kwenye eneo hilo la daraja, hivyo kusababisha kugongwa kwa nyuma na basi la Zuberi lililokuwa likipita kwa kasi.
Jina la dereva wa basi hilo la Zuberi, lenye namba za usajili T 983 ABU, lililosababisha Coaster hiyo kupoteza mwelekeo na kupinduka mara tatu, halijafahamika.
Jina la aliyekufa kwenye ajali na majeruhi, hayakuweza kupatikana mara moja. Ajali hiyo imetokea kipindi ambacho kikosi cha usalama barabarani, kimeimarisha doria sehemu mbalimbali nchini.
Walioshuhudia ajali hiyo, walisema kuwa mwendo kasi na uzembe wa madereva, bado ni kikwazo kwa usalama barabarani.
Chanzo:Habari Leo
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

MH. NYALANDU ATANGAZA RASMI NIA YA KUWANIA URAIS 2015


Mbunge wa Singida Kaskazini, Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu ametangaza rasmi kuwania Urais wa Tanzania katika uchaguzi mkuu mwakani.

Amesema amechukua uamuzi huo baada ya kuona kwamba anao uwezo wa kuiongoza Tanzania, katika harakati za kuwafikisha kwenye maendeleo endelevu wanayotaka Watanzania.

Amesema, yuko tayari kushindanishwa na Watanzania wengine watakaoona kuwa wanafaa kuwa Rais, lakini akisema kwanza kila atakayejitokeza itabidi kazi zake zipimwe kwa moto na endapo zitayeyuka hafai.

Nyalandu ambaye alitangaza uamuzi huo kwenye Uwanja wa Michezo wa Ilongelo jimbo la Singida Kaskazini, alisema, yeye anaingia kwenye kinyang'anyiro akiwa kifua mbele kutokana na kuamini kwamba amekwishafanyakazi zilizotukuka.

"Kazi zangu nilizofanya zinajulikana na ninaziamini kwamba ni nzuri, hivyo yeyote atakayetaka urais apimanishwe na mimi kwa kupimwa kazi zetu kwa moto", alisema Nyalandu

Itakapofika siku ya siku, nitaenda Dodoma nikisindikizwa na wana Singida Mashariki, na wengine wengi kutoka pembe zote za Tanzania, kwenda Dodoma kuchukua fomu ya kuwania kuteuliwa kugombea Urais kwa tiketi ya CCM", alisema.

Mkutano huo wa jimbo ambao ulipambwa na shamrashamra mbalimbali zikiwemo za wasanii wakiwemo kina Rose Mhando, ulifurika maelfu ya wananchi waliohamasika kumsikiliza Nyalandu.

 Waziri wa Maliasili na Utalii, Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazalo Nyalandu alisalimia wananachi baada ya kuwasili na mkewe Faraja Kota kwenye Mkutano wa jimbo uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Michezo wa Ilongelo, jimboni humo (Picha na Bashir Nkoromo theNkoromo Blog)
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazalo Nyalandu alisalimia wananachi baada ya kuwasili na mkewe Faraja Kota kwenye Mkutano wa jimbo uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Michezo wa Ilongelo, jimboni humo
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazalo Nyalandu alisalimia wananachi baada ya kuwasili na mkewe Faraja Kota kwenye Mkutano wa jimbo uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Michezo wa Ilongelo, jimboni humo
 Mwimbaji wa muziki wa Injili, Frola Nkone akiimba kutumbuiza wakati wa mkutano huo
Mwanamuziki wa muizki wa Injili, Rose Mhando akiimba kutumbuiza wananchi katika mkutano huo wa Nyalandu
Wasanii wa kikundi cha Makomandoo cha mjini Singida wakitumuiza wakati wa mkutano huo
Wadau wakifurahia burudani wakati wa mkutano huo wa Nyalandu

 Steve Nyerere ambaye ni Msanii na Kamanda wa Umoja wa Vijana wa CCM, akizungumza kabla ya kumwaga vimbwanga vyake vya kuingiza sauti za viongozi mbalimbali wakati wa mkutano huo wa Nyalandu.
KABLA YA MKUTANO

Nyalandu na Mkewe Faraja Kota wakiingia kwenye Kanisa la KKKT  Usharika wa Ilongelo kwa ajili ya ibada maalum. Pamona nao ni watoto wao Sera na Christopher kabla ya kwenda Uwanjani kutangaza azma yake ya kuwania Urais 2015
Nyalandu na Faraja Kota wakiwa na watoto wao Sera na Christopher katika kanisa hilo 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro  Nyalandu akitoa neno la shukrani baada ya ibada maalum katika katisa la KKKT Usharika wa Ilongelo jimboni humo leo
Waziri Nyalandu akiwa na watoto wake wakati wa ibada maalum iliyofanyilka leo katika Kanisa la KKKT Usharika wa Ilongelo Jimbo la Singida Kaskazini
Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu akitoa sadaka wakati wa ibada maalum iliyofanyika leo katika Kanisa la KKKT Usharika wa Ilongelo jimboni humo
Mke wa NYalandu, Faraja Kota akipita baada ya kutoa sadaka kwenye kanisa hilo la KKKT Usharika wa Ilongelo
Mwimbaji wa nyimbo za Injili lkatika Kanisa la KKKT Usharika wa Ilongelo
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu akizungumza na viongozi wa shule ya Kiislam ambayo huhudumia watoto wa dini zote katika kata ya Ilongelo, shule hiyo ina watoto 74.
Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu akisalimia waumini kwenye Kanisa la FPCT  katika jimbo la Ilongelo alipofika kwa ajili ya ibada maalum
Waumini wakiwa katika kanisa la FPCT wakati wa ibada maalum aliyohudhuria Nyalandu leo
Nyalandu na Mkewe wakitoka katika Kanisa la FPCT baada ya kuhudhuria ibada maalum leo asubuhi. Picha zote na Bashir Nkoromo-theNkoromo Blog
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

CHADEMA YAKOMBA 350 KWA NYALANDU

 CHADEMA yakomba 350 kwa Nyalandu
 CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimefanya mkutano mkubwa na kujipatia wanachama wengi mahali panapodaiwa kuwa ngome ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Singida Kaskazini, jimbo linaloongozwa na Waziri wa Utalii na Maliasili Lazaro Nyalandu.
Katika mkutano huo uliofanyika juzi katika Kijiji cha Msange na kuhutubiwa na naibu katibu mkuu wa CHADEMA Zanzibar Salum Mwalimu, ambapo zaidi ya wanachama 350 walikabidhiwa kadi pamoja na kuapishwa kiapo cha uzalendo kwa ajili ya kuwajengea ujasiri.
Mwalimu aliwaambia wanachama hao kuwa kiapo hicho cha cha kuwajengea ujasiri, ni kwa ajili ya kujiunga na kundi la watanzania wanaopigania haki na matumaini ya taifa lao.
Alisema operesheni inayoendelea iliyopewa jina la Operesheni Delete CCM (ODC) imelenga kuwafikia watanzania wote na kuwapatia ujumbe wa namna sera na mikakati ya CCM ilivyoshindwa na kwamba kinastahili kuondolewa madarakani kuanzia katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Disemba 14 mwaka huu na mkuu mwakani.
“Ndugu zangu nimefurahi leo (juzi) nimefika katika jimbo linaloongozwa na Nyalandu ambaye ni mbunge wenu … nilikuwa natamani kufika hapa  ili nione mlivyo na  maendeleo kwa kuwa mbunge wenu ni mtu wa maraha nadhani anaweza kumshinda hata Rais Kikwete kwa kwenda nje kufanya utalii” alisema Mwalimu na kuongeza
“Nilijua wenzetu kwa namna mbunge wenu alivyo, ninyi mtakuwa na huduma bora za afya, elimu, barabara na maji kumbe hakuna kitu … lakini sasa nadhani meonyesha kuondoa CCM, nafikiri hali kama mbunge wenu ameiona, ni salamu tosha kwa chama chake kujiandaa na kufungasha virago katika ofisi za serikali ifikapo mwakani. 
Chanzo;Tanzania daima
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

WANAFUNZI WASOMEA SEBULENI KWA MWALIMU

 WANAFUNZI 173 wanaosoma darasa la awali katika Shule ya Msingi Minga, iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Singida, wanasomea kwenye sebule ya nyumba ya mwalimu kutokana na upungufu wa vyumba vya madarasa unaoikabili shule hiyo.

Mwalimu Mkuu Msaidizi wa shule hiyo, Gregory Manimo, alibainisha hayo kwenye mahafali ya nne ya kuwaaga wanafunzi 162 wa shule ya msingi Minga.

Alisema kwa sasa shule hiyo ina vyumba 10 vya madarasa wakati mahitaji ya vyumba ni 38, huku kukiwa na vyumba viwili vya madarasa vilivyofikia hatua ya kupauliwa, nyumba mbili za walimu, ofisi moja ya mwalimu mkuu na ofisi mbili za walimu.

“Shule ina madawati 188, meza 12, viti 27, nyumba mbili za walimu huku kukiwa na nyumba moja iliyoanza kujengwa kwa nguvu za wananchi tangu mwaka 2006. Nyumba hii hadi bado haijakamilika na pia shule ina huduma za umeme na maji,” alisema mwalimu huyo.

Hata hivyo, alisema pamoja na mafanikio hayo, shule inakabiliwa na matatizo mbalimbali likiwamo la upungufu wa vyumba 28 vya madarasa, madawati 229, viti vitano, meza 20, nyumba za walimu 30 na chumba cha darasa la awali.

Kwa mujibu wa mwalimu mkuu huyo msaidizi, upungufu huo wa chumba cha darasa la awali umesababisha kwa sasa wanafunzi wake 173 kusomea kwenye sebule ya nyumba ya mwalimu wao.

Shule ya Minga, iliyoanza mwaka 2000 wakati huo ikijulikana kwa jina la Mughanga B, ilisajiliwa mwaka 2003 na kupewa jina hilo, ikiwa na wanafunzi 444 wa Darasa la Kwanza hadi la Nne.
 Chanzo;Tanzania Daima
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

MBUNGE ASIHI WAKAZI WA SINGIDA KUIPIGIA KURA CCM

MBUNGE wa Singida Mjini, Mohammed Dewji amewasihi wakazi wa Halmashauri ya Manispaa ya Singida kukipigia kura Chama Cha Mapinduzi wakati wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa nchini ili kukiwezesha kutekeleza Ilani yake kwa urahisi zaidi.
Mbunge huyo alitoa mwito huo juzi wakati wa uzinduzi wa kampeni za uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika hafla iliyofanyika kwenye eneo la soko la zamani la Kibaoni mjini hapa.
Alisema chaguzi za Serikali za Mitaa ni jiwe la msingi la nyumba inayojengwa na serikali yoyote ile, hivyo ili kuiwezesha nyumba hiyo kuwa imara wakazi wote wa Jimbo la Singida Mjini hasa wana- CCM, hawana budi kuipigia CCM kura nyingi ili kuiimarisha kisiasa.
Alisema kuwa kwa vile tayari Mbunge wa jimbo hilo ni wa CCM, ingekuwa vizuri zaidi iwapo wananchi wataendelea kukiamini na kukipigia kura za ndio chama hicho ili kuweka mnyororo sahihi kwa ajili ya utekelezaji wa Ilani ya Chama na maendeleo katika jimbo hilo.
Katika uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika nchini kote baadaye mwezi huu, Chama Cha Mapinduzi Singida Mjini kimejihakikishia ushindi katika mitaa 14 kati ya 50 iliyopo, vijiji sita kati ya 20 na vitongoji 36 kati ya 83 baada ya vyama pinzani kuacha kuweka mgombea.
Wakati huo huo, MO amewataka wakazi wa Singida Mjini kukamilisha ujenzi wa maabara kwa shule za sekondari na kuanza kujenga madarasa kwa ajili ya Kidato cha Tano katika shule zao ili kuwa na uhakika wa kuwapatia nafasi za kuendelea na masomo ya juu wote watakaofaulu.
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Chanzo;Habari Leo

WENYE MAAMBUKIZI YA VVU WAJIUNGA KWENYE VITUO

ZAIDI ya asilimia 69 ya watu waliobainika kuwa na maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU) mkoani Singida wamejiunga kwenye vituo vya tiba na matunzo (CTC) na kuanza kupewa dawa za kupunguza makali ya VVU katika kipindi cha miaka tisa iliyopita.
Mratibu wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) Mkoa wa Singida, Edson Mdala alisema hayo juzi wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani yaliyofanyika kimkoa katika kijiji cha Musimi kata ya Sepuka wilayani Ikungi.
Mdala alisema kuwa tangu 2005 hadi kufikia Juni mwaka huu, jumla ya watu waliopimwa VVU na kujiandikisha CTC ni 17,720, kati yao 12,286 wanapata dawa za kufubaza makali ya virusi vya Ukimwi (ARV).
Kadhalika, alisema kuwa vituo vya kutolea huduma ya dawa vimeongezeka kutoka vitatu mwaka 2005 hadi kufikia 30, mwaka huu.
Aidha, Mratibu huyo wa TACAIDS Mkoa alibainisha kuwa hali ya maambukizi mkoani Singida imepanda kutoka asilimia 2.7 mwaka 2008 hadi asilimia 3.3 mwaka 2012 ikiwa ni sawa na ongezeko la asilimia 0.6 tu.
Akihutubia kwenye Maadhimisho hayo, Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk Parseko Kone aliwataka wakazi wa Mkoa huu kupima mara kwa mara afya zao kwa hiari ili kujua kama wapo salama au la.
Katika hotuba hiyo iliyosomwa kwa niaba yake na Mkuu wa Wilaya ya Singida, Queen Mlozi, Dk Kone aliwataka wananchi wa Mkoa wa Singida kujiepusha na visababishi vinavyochochea kuongezeka kwa maambukizi ya ugonjwa huo.
Visababishi hivyo ni pamoja na kuwa na wapenzi wengi, matumizi ya pombe na dawa za kulevya na ngono zembe. Kaulimbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu ni “Kuelekea sifuri tatu za maambukizi mapya, Unyanyapaa na vifo vitokanavyo na VVU/ Ukimwi”.
Chanzo;Habari Leo

MO AZINDUA KWA KISHINDO KAMPENI ZA CCM SINGIDA‏

IMG_0216
Mbunge wa jimbo la Singida mjini Mhe. Mohammed Gulam Dewji akisalimiana na wapiga kura kura wake na wananchi wa jimbo la Singida mjini mara baada ya kuwasili kwenye viwanja vya Kibaoni tayari kuzindua kampeni za CCM uchaguzi wa serikali za mitaa katika jimbo la Singida Mjini.(Picha na Geofrey Mwakibete wa MOblog).
IMG_0223
Mbunge wa Singida MO Dewji akipata mapokezi kwenye mkutano wa uzinduzi wa kampeni zilizofanyika Kibaoni mjini Singida.
IMG_0167
Mbunge wa jimbo la Singida mjini Mhe. Mohammed Dewji akimnadi mgombe wa nafasi ya m/kiti wa mtaaa Kibaoni Timotheo Ruben John kwenye uzinduzi wa kampeni za CCM uchaguzi wa serikali za mitaa katika jimbo la Singida Mjini.
IMG_0172
Mbunge wa jimbo la Singda mjini mhe. Mohammed Dewji akizungumza kwenye uzinduzi wa kampeni za CCM uliofanyika katika viwanja vya soko la zamani la kitongoji mjini hapa.
IMG_0202
Mjumbe wa halmashauri kuu CCM (NEC) taifa manispaa ya Singida, Hassan Philip Mazala, akitoa nasaha zake kwenye uzinduzi wa kampeni za CCM zilizofanyika Kibaoni mjini hapa.
IMG_0186
Mgombea wa nafasi ya uwenyekiti wa mtaa wa Kibaoni Timotheo Ruben John akiomba kura kwa ajili ya nafasi hiyo, Mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM (NEC) taifa jimbo la Singida mjini Hassan Mazala akifurahia jambo wakati wa uzinduzi wa kampeni za CCM zilizofanyika jana.
IMG_0182
Baadhi ya wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) waliohudhuria uzinduzi huo wakimsikiliza Mbunge wao.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2011. Singida Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogz za Mikoa