Home » » “WAZAZI TUNA WAJIBU WA KUMLINDA MTOTO WAKIKE” DC MACHALI

“WAZAZI TUNA WAJIBU WA KUMLINDA MTOTO WAKIKE” DC MACHALI


Mkuu wa wilaya ya Mkalama Mhe. Moses Machali amefanya ziara ya kikazi kwa ajili ya kusikiliza na kutatua kero mbalimbali zinazowakabili wananchi wa Kijiji cha Nkinto kilichopo kata ya Nkito wilayani Mkalama.

Akizungumza wakati wa mkutano wa hadhara, Leo Julai 29,2024 Mhe. Machali amewataka wazazi wa Kijiji cha Nkinto na wilayani Mkalama kwa ujumla kuwa mstari wa mbele kupinga mimba za utotoni hasa kwa wanafunzi.

“Tunawajibu mkubwa wa kumlinda mtoto wakike, wananchi wenzangu tushirikiane pamoja kupambana dhidi ya tatizo la mimba mashuleni. Nawaomba sana mtoe ushirikiano pindi kesi za mimba zinapofika Mahakamani, wanaume achaneni na wanafunzi” Mhe. Machali

Mhe. Machali amesisitiza kuwa mzazi yeyote atayebainika kuwa chanzo cha kukwamisha Ushahidi mahakamani atachukuliwa hatua za kisheria “Mtendaji kuanzia leo ikiwa kuna mzazi anahusika nayeye achukulie hatua za kisheria” Mhe. Machali

Akijibu swali kuhusu changamoto ya maji iliyoibuka wakati wa mkutano huo wa hadhara, Mhe. Machali amesema tayari serikali imeshatenga fedha kwa ajili ya kuleta maji safi na hata wataalamu kutoka Mamlaka ya Bonde la Maji mkoa wa Singida wapo Kijiji Nkinto kufuatilia vyanzo vya maji.

“Niwahikishishie wananchi wa Kijiji cha Nkinto na vijiji vya Jirani kuwa tayari watalaamu wetu wako kazini nimeambatanao hapa, mwaka huu hautaisha mtakuwa mmepata Maji” Mhe. Moses Mahali

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2011. Singida Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogz za Mikoa