Home » » MHE. JAMES MKWEGA AZINDUA ZAHANATI YA IGENGU

MHE. JAMES MKWEGA AZINDUA ZAHANATI YA IGENGU


Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama Mhe. James Mkwega amezindua zahanati ya Igengu ikiwa ni mpango wa serikali wa kuhakikisha kila Kijiji nchini kinakuwa na zahanati.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa zahanati hiyo Julai 20,2024 katika Kijiji cha Igengu, Mhe. James Mkwega ameishukuru serikali pamoja na kwataka wananchi wa Kijiji hicho kulinda afya zao.
 
“Serikali imefanya kazi kubwa, Rais Dkt. Samia kaleta Zahanati na kaleta Umeme. Nampongeza pia Mganga Mkuu wetu Dkt. Solomon Michael kwa kazi kubwa anayofanya lakini pia niwapongeze wananchi kwa kazi kubwa mliofanya. Niwasihi tulinde afya zetu, tuzingatie ushauri wa wataalamu wetu”Mhe. Mkwega
 
Akizungumza kwa niaba ya Mkuregenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama, Dkt. Solomon Michael amewataka wajawazito wa Igengu kufika kliniki mapema ili kuepusha madhara yanayoweza jitokeza wakati wa kujifungua.
Awali akisoma taarifa kuhusu ujenzi wa zahanati hiyo, Mtendaji wa kata ya Ibaga Ndugu Abdallah Mohamedi amesema zahanati hiyo imegharimu kiasi cha shilingi milioni 110 ikiwa ni fedha kutoka Serikali Kuu, Fedha za Jimbo pamoja na nguvu za wananchi



0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2011. Singida Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogz za Mikoa