MHASHAMU BABA ASKOFU MAPUNDA AHIMIZA JUU YA UMUHIMU WA KUJITEGEMEA WENYEWE NA KUONDOKANA NA TABIA YA UTEGEMEZI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
 
Mhashamu Baba Askofu Jimbo Katoliki Singida,Edward Mapunda akiongoza misa ya ibada ya maadhimisho ya Jubilee ya miaka 50 tangu kuzaliwa kwa Parokia ya Kupaa Bwana Manyoni iliyofanyika katika viwanja vya kanisa hilo mjini Manyoni.

Na Jumbe Ismailly, MANYONI.

MHASHAMU Baba Askofu Jimbo Katoliki Singida,Edward Mapunda amewataka waumini wa madhehebu hayo kuondokana na tabia ya kutegemea wafadhili wakati wa utekelezaji na ukamilishaji wa miradi mbali mbali ya maendeleo na kuwataka watambue kuwa bwana bure amekufa na aliyebakia kwa sasa ni bwana kujitegemea peke yake. Mhashamu Baba Askofu ametoa wito huo kwenye misa takatifu aliyoiongoza wakati wa maadhimisho ya sherehe za Jubilee ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa Parokia ya Kupaa Bwana Manyoni iliyofanyika katika viwanja vya Kanisa la Parokia hiyo mjini Manyoni.

“Lakini ninachotaka kusisitiza jambo moja la kujitegemea,jambo moja la kujitegemea..enh tumesikia wazee wetu hapa walichanga hela,wazee wetu walichanga hela….wazeeeeee mlichanga hela sasa na sisi tunataka kuchanga hela ninyi mbona mlichanga tunataka kujenga Parokia.”alisisitiza baba Askofu Mapunda.
baadhi ya viongozi wa Parokia jimbo Katoliki Singida wakiwa katika maandamano ya kuadhimisha Jubilee ya miaka 50 tangu kuzaliwa kwa Parokia ya Kupaa Bwana Manyoni kwenye sherehe za maadhimisho hayo yaliyofanyika mjini,Manyoni.

Aidha Kiongozi huyo mkuu wa Kanisa hilo alisisitiza kwa wakazi wa wilaya ya Manyoni kwamba suala la kujitegemea halina budi kupatiwa kipaumbele katika shughuli za kukamilisha ujenzi wa majengo ya makanisa pamoja na vigango. Akifafanua zaidi Baba Askofu huyo aliweka bayana kuwa jukumu la kukamilisha ujenzi wa makanisa ni la waumini wenyewe na wenye moyo ambapo hata hivyo aliwatoa hofu waumini wa Manyoni kwa kuweka wazi msimamo wake kuwa anaamini kabisa waumini wa Manyoni ni waumini wenye moyo wa dhati wa kukamilisha majengo hayo.

Kutokana na moyo huo walionao wana Manyoni,Baba Askofu huyo alitumia wasaa wa maadhimisho hayo ya miaka 50 ya Jubilee kwa kuwataka waumini wa Jimbo hilo la Manyoni wajitoe bila kujibakiza,ili mipango na mikakati waliyojiwekea katika Jubilee hiyo iweze kufanikiwa zaidi.

“Namkumbuka sana Askofu Balina,askofu Balina alikuwa wa jimbo Katoliki la Shinyanga tunamuombea kwa Mungu ametangulia kwa Mungu lakini alikuwa anawaambia wasukuma wenzake maneno mazuri sana,na mimi nataka niwaambie hayo wana Manyoni kwa sababu mikakati hii ni mizito,mipango hii ni mizito,maazimio haya ni mazito tusipojitoa yote yatakwama”alisema huku akishangiliwa na waumini.


baadhi ya waumini wa kanisa hilo waliohudhuria kuadhimisha miaka 50 tangu kuzaliwa kwa Parokia ya Kupaa Bwana Manyoni,iliyofanyika mjini Manyoni.Picha zote Na Jumbe Ismailly.

Kwa mujibu wa kiongozi huyo wa madhehebu ya Kikatoliki askofu Banila alikuwa akiwaambia wanashinyanga kwamba bwana bure amekufa na kwa kutokana na kauli hiyo naye Baba Askofu Mapunda alitumia pia kauli hiyo kwa kuwaasa waumini wa jimbo hilo kwamba bwana bure amekufa na bwana misaada yupo taabani na hivyo aliyebakia ni bwana kujitegemea.
Hata hivyo Askafu Mapunda aliwatahadharisha waumini wa jimbo hilo kwamba suala la kujitegemea lina umuhimu wake na kwa hali hiyo hawana ujanja wa kulikwepa jukumu hilo la kuondokana na utegemezi na kwenda kwenye tabia ya kujitegemea wenyewe kutokana na changamoto nyingi zinazowakabili Mapadrii zikiwemo changamoto za kutokuwa na vyombo vya usafiri.

Naye Paroko wa Parokia  ya Kupaa bwana Manyoni Jimbo Katoliki Singida,Padri Thomasi Wambura  alisema mwaka jana ulikuwa mwaka wa Jubilee ya 100  wa Mapadri Tanzania mwaka huu wao nao wanaadhimisha miaka 50 ya Jubilee ya Parokia yao na mwaka ujao wa 2018 wataadhimisha Jubilee ya miaka 150 tangu ukristo ulipoingia nchini Tanzania.

Kwa mujibu wa Padri Wambura waumini wote wana wajibu wa kuyatekeleza yale yote waliyoaswa na Baba Asskofu kama mchungaji wao mkuu lakini hakusita kusisitiza kwamba wajibu walionao ni kuyatekeleza yale waliyoyapata katika ukrito. Kwa upande wao baadhi ya waumini wa Kanisa hilo,Elizabeth Mkyalu  alishauri kwamba fedha zilizochangwa na waumini wa kanisa hilo hazina budi kuanza shughuli zilizokusudiwa za ujenzi wa majengo hayo huku akionya tabia ya kusubiri wafadhili kwamba kwa namna moja au nyingine hukwamisha miradi iliyoanzishwa pale wanapojitoa au kutochangia.

Naye Flora Lyimo kwa upande wake alisema kwamba njia pekee ya kujikwamua kiuchumi na kijamii na kuhakikisha maeendeleo endelevu yanapatikana ni kujiamini na kusimama wenyewe kwa miguu yao na siyo kusubiri kusaidiw a na watu wengine kwani endapo watasubiri misaada upo uwezekano wa malengo waliyojiwekea kutokamilika.

RC NCHIMBI AAGIZA KUVUNJWA KWA BODI YA USHIRIKA MSAI WILAYANI IRAMBA, NDANI YA WIKI MBILI.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
 Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi akiwaelekeza wakulima wa pamba kijiji cha Msai wilayani Iramba, vipimo vya kati ya tuta na tuta, shimo na shimo kwa kutumia kamba na vijiti ili waweze kupanda kitaalamu na kuvuna kwa wingi.
 Wakulima wa pamba kijiji cha Msai wilayani Iramba, wakishiriki kwa vitendo mafunzo yya kupima urefu kati ya tuta na tuta, shimo na shimo kwa kutumia kamba na vijiti ili waweze kupanda kitaalamu na kuvuna kwa wingi.
 Katibu Tawala Wilaya ya Iramba Pius Songoma akishiriki kuwaelekea wakulima wa pamba kijiji cha Msai wilayani Iramba, vipimo vya kati ya tuta na tuta, shimo na shimo kwa kutumia kamba na vijiti ili waweze kupanda kitaalamu na kuvuna kwa wingi.
 Konyo Mjika ambaye ni mkulima hodari wa pamba wilaya ya Iramba kutoka kijiji cha Msai akimshukuru Mkuu wa Mkoa wa Singida kwa zawadi ya kilo tano za mbegu ya pamba aliyopewa.
Zakaria Marko Mwakilishi wa Kampuni ya Biosustain itakayosambaza mbegu za pamba tani 300 mkoani Singida akizungumza na wakulima wa zao hilo Katika kijiji cha Msai Wilayani Iramba.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Iramba Emmanuel Luhahula, asimamie kuvunjwa kwa bodi ya Ushirika wa Kijiji cha Msai Wilayani Iramba ndani ya wiki mbili, kutokana na tuhuma za ubadhirifu wa zaidi ya shilingi milioni 50.

Dkt Nchimbi ametoa agizo hilo mwishoni mwa wiki alipokuwa katika mkutano na wakulima wa Pamba wa Kijiji cha Msai, ambao wamemueleza kutokuwa na imani na viongozi wa bodi hiyo kutokana na upotevu wa fedha hizo na wakiwa hawajachukuliwa hatua yoyote.

Wakulima hao wamemueleza Mkuu wa Mkoa kuwa fedha zaidi ya milioni 50 zilitolewa na seikali kwa ajili ya ujenzi wa Jengo la ghala la ushirika wa kijijini hapo lakini hakukuwa na ujenzi wowote uliofanyika huku wakifuatilia hawapewi majibu sahihi.

Wamesema wana ushirika walijitahidi kutuma mwenyekiti wa Kijiji hicho kufuatilia upotevu huo bila mafanikio jambo lililowakatisha tamaa ya kuendelea na ushirika.

Dkt Nchimbi amesema “moja ya Muhimili wa mafanikio ya kilimo cha pamba ni ushirika ulio imara, tunakoelekea kwenye kilimo cha pamba chenye tija hawa wasiowaaminifu kwenye bodi watatukwaza na kutukwamishwa, kama bodi haifanyi kazi vizuri kwanini iendelee?, Mkuu wa Wilaya naimani kwa utendaji wako mzuri hili halitachukua zaidi ya wiki mbili”.

Aidha amemtaka Afisa Ushirika Mkoa wa Singida kusimamia na kutoa ushauri wa kitaalamu wakati wa kuvunjwa kwa bodi hiyo kwakuwa kazi ya mkoa ni kusuluhisha sio kutafuta maelezo marefu huku wananchi wanapotezewa muda.

“Afisa Ushirika hakikisha tarehe ishirini mwezi huu bodi hiyo iwe imeivunjwe na kuundwa bodi mpya ambayo itasimamia ushirika kwa umakini ili kuinua kilimo cha pamba Iramba”, amesisitiza Dkt Nchimbi.

Aidha Dkt Nchimbi amewatoa hofu wakulima kwakuwa mbegu aina ya UKM 08 za manyoya pamoja na viuatilifu zitafika na kusambazwa kwa wakati huku akiwataka kupanda kitaalamu ili kwa ekari moja iwe na miche elfu 22 na mkulima avune zaidi ya kilo elfu moja za pamba.

Pia amewaagiza maafisa ugani wote kulima pamba ili mashamba yao yawe mashamba darasa, huku wakitakiwa kuhakikisha hakuna makosa katika hatua yoyote kuanzia kwenye kuandaa mashamba, kupanda na kwenye upuliziaji dawa, bila kusahau kutoa taarifa kwa wananchi katika kila hatua.

Dkt Nchimbi amewapa wakulima wawili hodari wa zao la pamba zawadi ya kilo tano kwa kila mmoja kama kianzio huku akiwaahidi kuwa mbegu za kutosha na viuatilifu kwa ajili ya maeneo yao watapatiwa.

Akisistiza kaulimbiu ya Singida mpya kwa pamba yenye tija amewataka Wanasiasa, watendaji wa serikali na viongozi wa dini washirikiane na serikali kwa pamoja katika kutoa hamasa na elimu ya kilimo cha pamba.

Dkt Nchimbi ametoa onyo kwa wauza pembejeo na wasambaaji wasio waaminifu ambao husambaza dawa zisizo halisi kuwa serikali itawabaini na kuwapa adhabu kali huku akiwataka wakulima wasinunue dawa bila ushauri wa maafisa ugani.

“Kuna dawa nyingine ukipuliza kwenye wadudu waharibifu wa pamba badala ya kufa wananenepeana, sasa ole wako serikali ikukamate wewe unayemuuzia  mwananchi dawa feki hakika tuakushughulikia ipasavyo”, amesisitiza Dkt Nchimbi.

Kwa upande wake Konyo Mjika ambaye ni mkulima hodari wa pamba wilaya ya Iramba kutoka kijiji cha Msai amesema msimu wa mwaka jana amelima ekari nane na kupata kilo elfu sita ambapo ameweza kujenga nyumba nne za bati, kununua ng’ombe kadhaa na kuhudumia familia yake.

Mjika ameongeza kuwa ameweza kuvuna pamba nyingi kutokana na kusikiliza ushauri wa wataalamu wa kupanda kwa kufuata mistari, kuweka mbolea na viuatilifu mapema.

Kutokana na mafanikio hayo Mkulima Mjika amesema kwa msimu huu anatarajia kulima ekarini shirini pamoja na kuwashauri wanakijiji wenzake walime pamba kwa wingi huku wakifuata ushauri wa wataalamu ili waweze kuvuna kwa wingi.

Naye Zakaria Marko Mwakilishi wa Kampuni ya Biosustain inayojihusiha na kilimo cha zao la pamba kwa mkataba amesema kwa msimu huu kampuni hiyo itasambaza mbegu za pamba tani 300 mkoani Singida.

Marko ameongeza kuwa uzalishaji wa pamba mkoani Singida umekuwa mdogo ukilinganisha na mahitaji ya kiwanda chao ambapo mwaka jana zilipatitana kilo milioni 1 na mwaka huu zikaongezeka hadi kilo milioni 1.5 kutokana na jitihada za wakuu wa wilaya, Mkuu wa Mkoa na viongozi mbalimbai.

Ameongeza kuwa Kijiji cha msai chenye wakulima wa pamba zaidi ya mia tano wameweza kuzalisha kilo laki tano huku wilaya ya Iramba yote ikizalisha kilo laki nane na nusu kwa msimu wa mwaka jana na mategemeo yakiwa makubwa zaidi kwa mwaka huu.

Marko amesema kutokana na msukumo wa serikali na Viongozi wa Mkoa wa Singia ni matarajio yake kiwanda cha Bio Sustain sasa kitazalisha kwa faida kutokana na kupata pamba ya kutosha hapa Singida na sio kuifuata mikoa ya jirani kama ilivyokuwa hapo awali.

habari picha na libeneke la kaskazini blog

DC MTATURU AWATAKA WANANCHI KUHIFADHI FEDHA ZAO BENKI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akizungumza wakati akifungua wiki ya Huduma kwa mteja katika Benki ya NMB Tawi la Ikungi lililopo Wilayani humo Mkoani Singida.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akizungumza wakati akifungua wiki ya Huduma kwa mteja katika Benki ya NMB Tawi la Ikungi lililopo Wilayani humo Mkoani Singida.
Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya NMB Tawi la Ikungi wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu wakati wa ufunguzi wa wiki ya Huduma kwa mteja.
Meneja wa Benki ya NMB Wilaya ya Ikungi Ndg Wilbert Mwalusito akizungumza jambo mara baada ya ufunguzi wa wiki ya Huduma kwa mteja katika Benki ya NMB Tawi la Ikungi lililopo Wilayani humo Mkoani Singida.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akikata keki ishara ya ufunguzi wa wiki ya Huduma kwa mteja katika Benki ya NMB Tawi la Ikungi, Mkoani Singida.
Shilinde Kurwa Kasule ambaye ni mfanyabiashara akielezea namna alivyonufaika kwa kupata mikopo mbalimbali kutokana na utunzaji wa fedha zake Benki.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu (Mwenye Shati la kitenge), Kushoto kwake ni Katibu Tawala Wilaya ya Ikungi Winfrida Funto wakiwa katika picha ya pamoja na Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya NMB Tawi la Ikungi wakiongozwa na
Meneja wa Benki ya NMB Wilaya ya Ikungi Ndg Wilbert Mwalusito.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu (Kulia) akimsikiliza Meneja wa Benki ya NMB Wilaya ya Ikungi Ndg Wilbert Mwalusito akizungumza kwa niaba ya wafanyakazi wa Benki hiyo mara baada ya ufunguzi wa wiki ya Huduma kwa mteja katika Benki ya NMB Tawi la Ikungi.


Na Mathias Canal, Singida

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu amewataka wananchi kuacha tabia ya kuhifadhi fedha nyingi majumbani na badala yake wajenge utamaduni wa kuzipeleka benki ili kuepusha kuhatarisha usalama wao. 

Ametoa kauli hiyo leo Octoba 2, 2017 wakati akifungua wiki ya Huduma kwa mteja katika Benki ya NMB Tawi la Ikungi lililopo Wilayani humo Mkoani Singida.

Alisema tabia ya baadhi ya wananchi kuhifadhi kiasi kikubwa cha fedha majumbani si nzuri kwa sababu wanahatarisha usalama wao, hivyo ni vyema wakatumia benki hiyo iliyoanzishwa hivi karibuni kwa ajili ya kutunza fedha zao.

Alisema mbali ya kuhatarisha usalama kwa utunzaji wa fedha ndani ya nyumba pia kuhifadhia fedha nyingi ndani Ni kosa kisheria kwani kunasababisha mzunguko wa fedha kuwa mdogo Jambo ambalo linafifihisha ukuaji wa uchumi.

Katika hatua nyingine Mhe Mtaturu aliupongeza uongozi wa benki ya NMB kwa kutii maoni ya waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa aliyoyatoa Desemba 5, 2016 wakati akifungua tawi la benki ya Biashara ya Uchumi lililopo wilayani Karatu mkoani Arusha la kupunguza kiasi cha riba wanachokitoza katika mikopo wanayoitoa ili kuwawezesha wananchi kukopa na kupata tija.

Alisema kuwa kuanzishwa kwa NMB CHAPCHAP INSTANT ACCOUNT na kupatikana kwa riba ya mpaka asilimia tano kwa wateja Ni kichocheo Cha muelekeo wa wananchi kupata Huduma laini katika Benki hiyo ikiwemo mikopo yenye riba nafuu.

Sambamba na hayo pia Mhe Mtaturu aliushauri Uongozi wa Benki hiyo kufanya Utafiti katika maeneo ya Wilaya nzima ili kuwa na namna Bora ya kuwafikia wateja wote ambao bado hawajaanza kunufaika na Huduma hiyo na Huduma za kibenki ikiwemo uhifadhi wa fedha Hizo.

Kwa upande wake Meneja wa Benki ya NMB Wilaya ya Ikungi Ndg Wilbert Mwalusito alisema kuwa wiki ya Huduma kwa mteja inawarahisishia wateja kutoa maoni yao ili kuwa na namna Bora ya kuboresha Huduma katika Benki hiyo.

Alisema kuwa Benki hiyo imeanzisha Huduma ya Akaunti ya CHAP CHAP ambayo itamuwezesha mteja kupata Huduma za kibenki na Haina kima Cha chini Cha salio kwenye Akaunti Wala makato ya mwezi.

Aliongeza kuwa NMB CHAP CHAP Akaunti Ni Huduma Bora na nafuu inayomuwezesha mteja kufanya shughuli zake zote za kibenki papo kwa papo bill shida popote alipo kwa kutumia Simu ya mkononi kupitia Huduma ya NMB Mobile.

Naye Shilinde Kurwa Kasule ambaye ni mfanyabiashara na mtumiaji mkubwa wa Huduma za Benki ya NMB aliwasihi wananchi na wafanyabishara Wilayani Ikungi kutohifadhi fedha ndani badala yake wahifadhi Benki kwa ajili ya usalama wao na fedha zao.

Shilinde alisema kuwa kuweka fedha benki Ni njia mojawapo ya wananchi na wafanyabishara kuiaminisha Benki kuwa wanakopesheka kwani watakuwa wanajua mzunguko wa biashara ya mteja wao.

MAANDALIZI YA UTAFITI WA MAFUTA ZIWA EYASI, TANGANYIKA YAANZA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


Picha Na 1 Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani, (mbele) akiongoza kikao kilichoshirikisha wataalam kutoka Uganda,  Idara ya Nishati, Wizara ya Nishati na  Madini, Shirika la Maendeleo  ya Petroli  Tanzania (TPDC) na Mamlaka  ua Udhibiti wa Shughuli za Mkondo wa Juu wa Mafuta (PURA) kabla ya kuanza ziara katika Ziwa Eyas Wembere lililopo mkoani  Singida. Picha Na 2 Wataalam kutoka ,  Idara ya Nishati, Wizara ya Nishati na  Madini, Shirika la Maendeleo  ya Petroli  Tanzania (TPDC) na Mamlaka  ua Udhibiti wa Shughuli za Mkondo wa Juu wa Mafuta (PURA) wakifuatilia maelekezo  yaliyokuwa yanatolewa na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani (hayupo  pichani). Picha Na 3 Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Maendeleo ya Madini Nchini Uganda, Robert Kasande (kulia) pamoja na wataalam kutoka Uganda wakifuatilia ufafanuzi  uliokuwa unatolewa na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani (hayupo  pichani) Picha Na 4 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi  Juliana Pallangyo (kushoto mbele) akieleza jambo katika kikao hicho. Picha Na 5 Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani akielezea hali ya utafiti wa mafuta na gesi nchini. Picha Na 6 Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Maendeleo ya Madini Nchini Uganda, Robert Kasande akifafanua jambo katika kikao hicho. Picha Na 7 Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Nishati na Madini, Asteria Muhozya (kulia) akibadilishana mawazo na Meneja Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki, Salum Mnuna katika kikao hicho …………………
Asteria Muhozya na Greyson Mwase.
Timu ya wataalam kutoka Uganda imewasili nchini Tanzania kwa ajili ya kubadilishana uzoefu na wataalam wa Tanzania katika utafiti wa mafuta. Mbali na kubadilishana uzoefu wataalam hao watafanya ziara Ziwa Eyasi Wembere lililopo mkoani  Singida.

Kabla ya kuanza kwa ziara hiyo wataalam hao leo tarehe 2 Oktoba, 2017  wamefanya  kikao kilichoongozwa na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani na kuwashirikisha Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo pamoja na wataalam kutoka Idara ya Nishati, Wizara ya Nishati na Madini, Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) na Mamlaka ya Udhibiti wa Shughuli za Mkondo wa Juu wa Mafuta (PURA).

Akizungumza katika kikao hicho, Dkt. Kalemani amesema  maandalizi hayo ni  juhudi za Rais wa Jamhuri  ya Muungano wa  Tanzania, Dkt. John Magufuli za kuhakikisha kuwa rasilimali ya mafuta inagunduliwa na kuanza kuleta manufaa kwa wananchi, ambapo wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi la Ujenzi wa Mradi ya Bomba la Kusafirisha Mafuta  Ghafi la  Afrika Mashariki kutoka Hoima nchini Uganda hadi Tanga nchini Tanzania tarehe 5 Agosti, 2017 alieleza kuwa wataalam waliogundua mafuta katika Ziwa Abert nchini Uganda kushirikiana na wataalam wa Tanzania katika utafiti wa mafuta katika Ziwa Tanganyika na  Eyasi nchini Tanzania.

Dkt. Kalemani amesema baada ya Rais wa Uganda kukubali ombi hilo yalianza maandalizi kupitia vikao mbalimbali ambapo hatua iliyofikiwa kwa sasa ni wataalam kukutana na kubadilishana uzoefu kabla ya kuanza kwa shughuli za utafiti katika maziwa husika.

Amesema wataalam wataanza kwa kufanya ziara ya siku mbili katika Ziwa Eyasi Wembere mkoani Singida ili kupata picha halisi kabla ya kuanza kwa majadiliano ya kubadilishana mawazo ya namna bora ya utafiti katika maziwa husika.

“ Sisi kama  Tanzania  tupo  tayari kubadilishana uzoefu na wataalam wa Uganda kwenye utafiti wa mafuta na kuanza kazi mara moja;  hata hivyo pia tupo  tayari kubadilishana nao uzoefu  kwenye masuala ya  gesi kwa kuwa tuna utaalam huo, lengo likiwa ni kuimarisha sekta hizi za mafuta na gesi kwa nchi zote mbili,” amesema  Dkt. Kalemani.

Ameongeza kuwa kwa kuwa Tanzania ina uzoefu mkubwa kwenye utafiti wa gesi asilia, wapo tayari kutuma wataalam nchini Uganda kushirikiana kwenye utafiti wa gesi nchini Uganda.

Kwa upande wake Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Maendeleo ya Madini Nchini Uganda na kiongozi  wa ujumbe huo, Robert Kasande amesema kuwa wapo tayari kubalishana uzoefu ambapo watalenga katika kuangalia tafiti zilizowahi kufanyika nyuma, kutembelea maeneo husika na kuweka mikakati ya namna bora ya kufanya utafiti kwa ubora wa hali ya juu kwa kushirikiana na  Tanzania.

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2011. Singida Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogz za Mikoa