Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Ni marobota ya tumbaku yaliyohifadhiwa kwenye moja ya ghala la
chama cha Msingi Mitundu,tarafa ya Itigi,wilayani Manyoni wakati wa
uzinduzi wa soko la tumbaku lililofanyika hivi karibuni katika Kijiji
cha Mitundu.
baadhi ya watendaji wa Halmashauri ya Itigi,wilayani manyoni
Mkoani Singida wakiwa kwenye ukumbi wa mikutano wa Kijiji cha
Songambele,wakati wa mkutano maalumu wa baraza la madiwani.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Itigi,wilayani Manyoni,Mkoani
Singida,Ally Minja(wa pili kutoka kushoto) akiongoza mkutano maalumu wa
baraza la madiwani uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya
Kijiji cha Songambele.
Mbunge wa jimbp la Manyoni magharibi,Yahaya
Masare akichangia baadhi ya hoja kwa kutoa ufafanuzi kwa wajumbe wenzake
wa mkutano huo.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Manyoni,Jumanne Ismaili
akiwasilisha salamu za chama kwa madiwani na watendaji wa Halmashauri ya
Itigi,kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Kijiji cha
Songambele,tarafa ya Itigi,wilayani Manyoni.(Picha zote Na Jumbe
Ismailly)
WAKULIMA
wa zao la tumbaku katika Halmashauri ya Itigi,wilayani Manyoni,Mkoani
Singida hawana soko la uhakika la kuuzia zao hilo kutokana na Makampuni
yaliyokuwa yakinunua zao hilo kushindwa kuendelea kwa sababu ya madeni
makubwa yanayovikabili vyama vya msingi vinavyolima tumbaku katika
Halmashauri hiyo.
Afisa
Maendeleo ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika wa Halmashauri
hiyo,Renatusi Mtatina aliyasema hayo kwenye mkutano maalumu wa Barazaa
la Madiwani wa Halmashauri hiyo wakati akijibu swali la diwani wa kata
ya Rungwa,Charles Machapaa ambaye alitaka kufahamishwa shilingi milioni
477 zitapatikanaji kwenye zao la tumbaku wakati serikali imeshusha
ushuru wa mazao kutoka asilimia 5 hadi 3.
Aidha
Mtatina alithibitisha kwamba ni ukweli usiopingika kwamba Halmashauri
ya Itigi kwa mwaka huu bado haaijapata mnunuzi wa tumbaaku wala kampuni
yeyote ile itakayonunua zao hilo na badala yake wakulima wataendelea
kulima zao hilo na kwenda kuuza sehemu nyingine.
“Nia
tunataraji kwamba watakuwepo wakulima ambao watalima lakini wanaweza
wakauza sehemu nyingine lakini kwa Halmashauri ya Itigi hatujapata
mnunuzi kwa hiyo patakuwa na changamoto kubwa katika kilimo cha
tumbaku.”alisisitiza afisa huyo wa kilimo,umwagiliaji na ushirika.
Kwa
mujibu wa Mtatina suala la matatizo ya vyama vya ushirika bado
halijatatuliwa kwa sababu bado wana madeni makaubwa na ndiyo maana
hawajapata mnunuzi wa zao hilo la tumbaku.
Katika
swali lake la msingi,diwani wa kata ya Rungwa,Charles Machapaa
alionyesha hofu ya kutofikiwa kwa malengo ya makusanyo ya mapato ya
Halmashauri hiyo ya shilingi milioni 477 kutokana na serikali kushusha
ushuru wa aina mbali mbali ya mazao,ikiwepo tumbaku,ushuru wa pamba
pamoja na ushuru wa mazao mengineyo.
Kwa
upande wake Mweka hazina wa Halmashauri hiyo,Charles Mnamba akitetea
hoja hiyo alisisitiza kwamba katika msimu ujao uzalishaji wa kilimo cha
zao la tumbaku utaongezeka zaidi ikilinganishwa na wa mwaka uliopita na
utaweza kufidia kiwango cha ushuru wa asilimia mbili kilichopunguzwa na
serikali.
0 comments:
Post a Comment