Aidha afisa elimu huyo alifa
Ni
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Manyoni,Moses Matonya(wa kwanza
kutoka kushoto) akiwa na Makamu Mwenyekiti,Jumanne Mlagaza wakiongoza
mkutano wa baraza la Madiwani uliofanyika mjini Manyoni.
Na,Jumbe Ismailly MANYONI
HALMASHAURI
ya wilaya ya Manyoni,Mkoani Singida inakabiliwa na changamoto mbali
mbali katika sekta ya elimu ikiwemo uhaba wa vyumba vya madarasa huku
kukiwepo ongezeko la uandikishaji la asilimia 67 na hivyo kuchangia
kuwepo kwa msongamano wa wanafunzi madarasani.
Afisa
elimu msingi wilaya ya Manyoni,Salumu Ikambi alisema kiasi hicho cha
asilimia 67 za uandikishaji ni kikubwa kutokana na idadi ya wanafunzi walioandikishwa kufikia 7,176 kati ya lengo la kuandikisha jumla ya wanafunzi 11,000.
Aidha
afisa elimu huyo alifafanua kwamba wanafunzi hao 7,176 wakiwemo
wavulana 3,734 na wasichana 3,442 ni wengi ikilinganishwa na wanafunzi
2,967 waliohitimu elimu ya msingi mwaka jana.
“Mwaka
jana waliomaliza elimu ya msingi walikuwa 2,967 kwa idadi hiyo utaona
karibu mara tatu ya wale ambao wameandikishwa mwaka huu.”alibainisha
Ikambi.
Kwa
mujibu wa Ikambi alizitaja baadhi ya changamoto wanazokaniliana nazo
kuwa ni idadi ya vyumba vya madarasa vilivyokuwepo mwaka jana ndivyo
hivyo hivyo vilivyo mwaka huu na idadi ya wanafunzi waliomaliza elimu ya
msingi 60 lakini walioandikishwa ni 200.
Hata
hivyo alisisitza pia kwamba pamoja na upungufu wa vyumba vya madarasa
lakini kuna maeneo mengine pia bado yanakabiliwa na upungufu wa walimu
na kutoa mfano kuwa darasa lenye wanafunzi 200 haliwezi kufundishwa na
mwalimu mmoja.
Kwa
upande wake afisa elimu sekondari Halmashauri ya wilaya ya
Manyoni,Ramlah Munisi alibainisha kwamba mpaka sasa ni asilimia 14 ya
wanafunzi 2,018 bado hawajaripoti shule kuanza masomo yao ya kidato cha
kwamba kutokana na sababu mbali mbali ikiwepo kubadili vituo kutokana na
umbali wa kutoka wanapoishi hadi shule walizopangiwa.
Afisa
elimu huyo hata hivyo aliweka bayana kuwa kwa mwaka 2018 Halmashauri ya
wilaya ya Manyoni ilipokea wanafunzi 2027 waliojiunga na masomo ya
kidato cha kwanza na kati yao,wanafunzi 9 wamepangwa katika shsule za
vipaji maalumu.
Kwa
mujibu wa Munisi mwenye dhamana ya kusimamaia elimu sekondari,wanafunzi
2,018 wamepangiwa shule za kata,ambapo kati yao 1,970 sawa na asilimia
82.5 wamesharipoti shuleni na asilimia 2.8 wameenda katika shule za watu
binafsi.
Akifunga
mkutano wa kawaida wa Baraza la Madiwani,Mwenyekiti wa Halmashauri ya
wilaya ya Manyoni,Moses Matonya aliwakumbusha madiwani wajibu wao wa
kwenda kusimamia mahudhurio ya wanafunzi wa shule za msingi pamoja na
sekondari.
0 comments:
Post a Comment