MPIGIE KURA MO DEWJI KUSHINDA TUZO YA HESHIMA BARANI AFRIKA #FAPOY2015‏

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

mohammed-dewji_416x416
“NINAFURAHA KUKUARIFU KUWA NIMETEULIWA KUWANIA TUZO YA “ FORBES PERSON OF THE YEAR 2015” #FAPOY2015
KWA HESHIMA NA TAADHIMA NINAOMBA KURA YAKO; Bonyeza Link hii: [ ttp://t.co/8mPEDbghsB] KUNIPIGIA KURA ILI TUIPEPERUSHE BENDERA YA TANZANIA JUU ZAIDI NA KUIWAKILISHA VYEMA AFRIKA MASHARIKI.”
MO DEWJI
"I am humbled to be one of the nominees for Forbes Person of the Year and i hope to make Tanzania/East Africa & Africa Proud. Please share with your friends and cast your votes here: http://t.co/8mPEDbghsB

MAKAMU WA RAIS MHE. DKT. BILAL AZINDUA MRADI WA UMEME UNAOTUMIA NGUVU YA UPEPO MKOANI SINGIDA‏

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wananchi kwenye ghafla ya uwekaji wa jiwe la msingi uzinduzi wa mradi wa kuzalisha Umeme kwa njia ya Upepo Mkoani Singida, ghafla hiyo ilifanyika jana Oct 06, 2015 katika kijiji cha Irawo Unyamikumbi Mkoani Singida.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiondoa kitambaa kuweka jiwe la msingi uzinduzi wa mradi wa kuzalisha Umeme kwa njia ya Upepo katika kijiji cha Irawo Unyamikumbi Mkoani Singida jana Oct 06, 2015
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na baadhi ya wawekezaji wa kampuni ya Wind East Africa Group inayozalisha umeme unaotumia nguvu za upepo baada ya kuweka jiwe la msingi uzinduzi wa mradi huo jana Oct 06, 2015 katika kijiji cha Irawo Inyamikumi Mkoani Singida.  (Picha na OMR)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, kati kati akiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa kampuni ya Wind East Afrika Group wakati wa ghafla ya uwekaji jiwe la msingi uzinduzi wa mradi wa kuzalisha Umeme kwa njia ya Upepo katika kijiji cha Irawo Unyamikumbi Mkoani Singida jana Oct 06,2015
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipanda mti kwenye eneo la uwekezaji wa mradi wa kuzalisha umeme kwa njia ya upepo katika kijiji cha Irawo Inyamikumi Mkoani Singida baada ya kuweka jiwe la msingi uzinduzi wa mradi huo jana Oct 06,2015


MAGUFULI AMSHAWISHI MO KUJENGA KIWANDA SINGIDA ILI KUTOA FURSA YA AJIRA‏

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
IMG_4556
Mgombea urais kupitia tiketi ya CCM, Dkt. John Pombe Magufuli akimwaga sifa kwa aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Singida Mjini (Mbunge Mstaafu), Mohamed Dewji baada ya kutumikia vyema na kwa uadilifu kiti chake cha Ubunge jimboni humo wakati wa mkutano wa kampeni za mgombea urais huyo kwa tiketi ya CCM uliofanyika katika viwanja wa Peoples mjini humo.
Na Nathaniel Limu, Singida
MGOMBEA urais kupitia CCM Dk.John Pombe Magufuli,amemshawishi aliyekuwa mbunge wa jimbo la Singida mjini Mohammed Dewji,kujenga kiwanda mkoani humo, ili pamoja na mambo mengine,kupunguza uhaba wa ajira.
Amedai Dewji maarufu kwa jina la MO katika kipindi chake cha ubunge miaka 10 iliyopita, ameonyesha mapenzi makubwa na ya aina yake kwa wakazi wa jimbo la Singida na mkoa kwa ujumla.
Dk.Magufuli alisema kutokana na ukweli huo,sasa anapaswa kuhamishia mapenzi hayo kwa kujenga kiwanda mkoani Singida kitakachoajiri vijana, na pia kuinua pato la mkoa na taifa kwa ujumla.
Mgombea urais huyo aliyasema hayo kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya Peoples mjini Singida na kuhudhuriwa na mamia ya wakazi wa jimbo la Singida na maeneo ya jirani.
“Katika kipindi chako cha ubunge umeonyesha uzalendo wa hali ya juu,umewatumikia vema wananchi wa jimbo la Singida mjini. Ndio maana hadi sasa bado wana mapenzi makubwa sana kwako,naomba uwajengee kiwanda. Nakuhakikishia mimi binafsi napenda wawekezaji wazalendo wanaoipenda nchi yao na wewe ni mmoja wao”,alisema Dk.Magufuli.
Aidha, Dk.Magufuli amemuahidi kumpa ushirikiano pindi atakapohitaji kuwekeza katika viwanda mkoani Singida.
Akisisitiza,alisema “Dewji nakuomba sasa sana ikiwezekana jenga hata viwanda vitatu ili wananchi wa mkoa wa Singida wapate ajira. Nitakuunga mkono kwa asilimia 100.Kama ni kibali unataka,nitakupa leo hii kwa kuwa mmenihakikishia nitakuwa rais wa tano”.
Awali akizungumza kwenye mkutano huo wa kampeni, Dewji aliwaahidi wakazi wa jimbo la Singida mjini kwamba ataendelea kushirikiana nao katika kulipaisha jimbo hilo kimaendeleo.
IMG_4554
“Mimi nimezaliwa hapa nyumbani kwetu Singida mjini na kitovu changu kimezikwa hapa hapa.Kutoka chini ya sakafu ya moyo wangu,niwahakikishie kwamba nalipenda sana jimbo letu hili la Singida mjini.Nitaendelea kulisaidia kwa hali na mali kadri uwezo utakavyoniruhusu”,alisema na kushangiliwa kwa nguvu na wananchi.
Dewji alisema nia yake ya kuomba ubunge huko nyuma,lengo ilikuwa na kutaka kushirikiana na wananchi kuliletea maendeleo jimbo la Singida mjini tu, na sio kujinufaisha binafsi.
”Jimbo sasa limepiga hatua kubwa kimaendeleo katika sekta zote muhimu.Najua bado tuna mengi ya kufanya ya kimaendeleo kwa kizazi cha sasa na kile kijacho.Kwa hiyo sitowaacha,tutaendelea kushirikiana kuliendeleza jimbo la Singida mjini ili liwe mfano wa kuigwa na majimbo mengine katika masuala ya kimaendeleo”,alisema.
Baadhi ya wakazi wa jimbo la Singida mjini wamedai Dewji ataendelea kukumbukwa kwa miaka mingi ijayo, kutokana na tabia yake ya kuwapenda wananchi wote na hakuwa na chembe chembe ya ubaguzi.
“Binafsi sidhani kama jimbo letu hili litakuja kupata mbunge wa aina ya Dewji.Ukiacha misaada yake mikubwa kwenye sekta mbalimbali ikiwemo ya maji, afya, elimu na kilimo, Dewji amesaidia hata ujenzi wa misikiti na makanisa madogo na makubwa ya mjini Singida na yale ya vijijini”,alisema Limu Bunka.
Aidha,alisema Dewji amesaidia pia kugharamia matibabu ya baadhi ya wakazi ndani na nje ya mkoa na amegharamia masomo ya mamia ya wananfunzi ambao wazazi/walezi wao hawana uwezo.
_MG_2292
Aliyekuwa Mbunge wa Singida Mjini (Mbunge Mstaafu), Mohamed Dewji akimwombea kura Mgombea Urais wa CCM Dkt. John Pombe Magufuli (hayupo pichani) kwa wananchi wa Singida na vitongoji vyake katika mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa Peoples, mjini Singida, Dewji pia ametangaza kumuunga mkono aliyemrithi kiti chake cha Ubunge, Ndugu Mussa Sima.
IMG_4821
Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dkt John Magufuli akiwahesabia kupiga 'Push Up' wagombea ubunge Mwigulu Nchemba wa Iramba (kulia), Musa Sima (katikati) wa Singida Mjini na Lazaro Nyalandu wa Jimbo la Singida Kaskazini jana wakati wa mkutano wa kampeni katika Uwanja wa Peoples mjini Singida.
IMG_4214
Aliyekuwa Mbunge wa Singida Mjini (Mbunge Mstaafu), Mohamed Dewji akiteta jambo na Mgombea Ubunge jimbo la Kaskazini, Lazaro Nyalandu wakati wa mkutano wa kampeni katika Uwanja wa Peoples mjini Singida.
IMG_4182
Mtoto ambaye hakufahamika mara moja jina lake, akimsikiliza mgombea urais kupitia CCM Dk.John Pombe Magufuli uliofanyika kwenye viwanja vya Peoples mjini hapa jana,huku kando kando yake kukiwa na ujumbe maalum kwa Dkt.Magufuli.
IMG_4268
Majembe yakiwajibika kwenye mkutano wa kampeni za urais CCM katika Uwanja wa Peoples mjini Singida. Kushoto ni Mwakilishi wa Modewjiblog Singida mjini, Nathaniel Limu pamoja na Ahmad Michuzi wa Michuzijr Blog.
IMG_4856
Wakazi wa Singida mjini wakicheza na kumshangilia aliyekuwa Mbunge wa Singida Mjini (Mbunge Mstaafu), Mohamed Dewji katika mkutano wa kampeni za mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dkt. John Magufuli uliofanyika kwenye uwanja wa Peoples, mjini Singida.
IMG_4860
Umati wa wanaSingida ukimshangilia aliyekuwa Mbunge wa Singida Mjini (Mbunge Mstaafu), Mohamed Dewji mara baada ya kumalizika mkutano wa kampeni za mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dkt. John Magufuli uliofanyika kwenye uwanja wa Peoples, mjini Singida.

DK MAGUFULI AFANYA KWELI SINGIDA MJINI‏

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

 Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk. John Magufuli akihutubia katika mkutano wa kampeni kwenye  Uwanja wa Peoples, mjini Singida jana, ambapo alilisitiza kwamba akishinda urais ataongeza ajira kwa vijana kwa kuwapa mikopo ya mitaji ya kuanzishia miradi mbalimbali ikiwemo ya ujenzi.NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli akiwahesabia kupiga Push Up wagombea ubunge Mwiguru Nchemba wa Iramba (kulia), Musa Sima (katikati) wa Singida Mjini na Lazaro Nyalandu wa Jimbo la Singida Kaskazini jana wakati wa mkutano wa kampeni katika Uwanja wa Peoples mjini Singida
 Dk Magufuli akikagua daraja la Msingi katika Kijiji cha Msingi wilayani Mkarama, Singida

 Mkazi wa Kata ya Sepuka Singida Magaribi  akiwa na mwanawe katika mkutano wa Dk Magufuli
 Wananchi wakishangilia kwa furaha baada ya kumuona Dk Magufuli akatika Kata ya Ndago, wilayani Iramba
 Mma mkazi wa Msigili akiwa na furaha baada ya kuuona Dk Magufuli
 Wananchi wakikimbia kwenda kumuona Dk Magufuli alipowasili katika Mji wa Msigili wilayani Iramba
 Nifuraha iliyoje kwa vijana hawa baada ya kumuona Dk Magufuli katika Mji wa Msigili leo
 Kijana akimshangiliAa Dk Magufuli huku akiwa amebandika picha yake mgongoni
 Baadhi ya wafanyabiashara wakishangilia baada ya kufurahishwa na hotuba ya Dk Magufuli  katika Mji wa Msigili ambapo alisema akishinda urais ataondoa kodi  kwa wafanyabiashara ndogo ndogo
 Dk Magufuli akimnadi Mgombea Ubunge Jimbo la Iramba, Mwigulu Nchemba mjini Kiomboi, Iramba
 Dk Magufuli akionesha kadi ya mmoja wa viongozi wa Chadema ambaye amaehamia CCM NA ZAIDI YA WANACHAMA 200



 Baadhi ya wananchi wakisikiliza kwa makini wakati Dk Magufuli akijinadi katika mkutano wa kampeni katika Mji wa Nduguti wilayani Mkarama
 Wanachi wakishangilia baada ya kukubali kumpigia kura Dk Magufuli katika Mji wa Nduguti wilayani Mkarama, Singida
 Wazee wakikimbilia kumuona Dk Magufuli katika Kata ya Nkungi, Jimbo la Mkarama, Singida
 Wananachi wakimshangilia Dk Magufuli alipozungumza nao katika mkutano wa kampeni Jimbo la Singida Kaskazini
 Wananchi wakimshangilia Dk Magufuli wakati wa mkutano wa kampeni  katika Mji wa Ilongelo, Jimbo la Singida Kaskazini

Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli akimnadi kwa wananchi mgombea ubunge Jimbo la Singida Kaskazini,Lazaro   Nyalandu  katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika Kata ya Ilongelo,
 Dk Magufuli akiteta jambo na Mratibu wa kampeni za CCM, Abdallah Majula muda mfupi kabla ya kuanza kuhutubia kwenye mkutano wa kampeni katika Uwanja wa Peoples mjini Singida
  Dk Magufuli akiteta jambo na Mjumbe wa Kamati ya Kampeni za CCM, Mwigulu Nchemba muda mfupi kabla ya kuanza kuhutubia kwenye mkutano wa kampeni katika Uwanja wa Peoples mjini Singida
 Wananchi wakishangilia katika mkutano wa kampeni za CCM MJINI Singida
 Nchemba akimnadi Dk Magufuli katika mkutano huo














 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2011. Singida Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogz za Mikoa