Mgombea
 wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe 
Magufuli akiwahutubia wananchi  kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika 
katika uwanja wa Mnadani Ikungi mkoani Singida wakati akiwaomba  
wananchi hao kumpigia kura za ndiyo ifikapo Oktoba 25 mwaka huu katika 
uchaguzi wa Rais , Wabunge na Madiwani. 
Dk.
 Magufuli amesema serikali yake itahakikisha inazisaidia taasisi 
mbalimbali  hasa za mashirika ya  dini ambazo zinaendesha hospitali  
katika kupata vifaa, Ruzuku, na ajira kwa wafanyakazi ili   kuimarisha 
huduma  za kiafya  kwa jamii.(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE IKUNGI 
-SINGIDA)
Mgombea
 wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe 
Magufuli na mgombea ubunge wa jimbo la Singida Mashariki Jonathan Njau 
wakiwapungia  wananchi mikono  kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika 
katika uwanja wa Mnadani Ikungi leo.
Mwenyekiti
 wa UWT mkoa wa Singida Diana Chilolo akimpigia debe Mgombea wa urais wa
 Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli 
kwenye  mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Mnadani Ikungi.
Mmoja
 wa wasanii walikokuwa wakitumbiuza katika mkutano huo akiwa ameshikilia
 bango lenye picha ya mgombea ubunge wa jimbo la Singida Mashariki Ndugu
 Jonathan Njau katika mkutano wa kampeni uliofanyika uwanja wa Mnadani 
Ikungi leo.
Baadhi
 ya akina mama wakiwa wamekaa kandokando ya mkutano huo huku mmojawapo 
akiwa ameshilikilia picha ya Dk. John Pombe Magufuli wakati wa mkutano 
wa kampeni wa mgombea huyo.
Baadhi
 ya wananchi wakiwa wameshikilia vipeperushi vyenye ujumbe wa kampeni za
 mgombea Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli huku wakimsikiliza 
wakati alipokuwa akihutubia katika mkutano huo.
Mgombea
 Ubunge wa jimbo la Singida Magharibi Lazaro Nyalandu akipmigia debe 
Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John
 Pombe Magufuli  kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa 
Mnadani ambapo amewaambia wananchi wa jimbo hili kujifikiria mara bili 
na kuchagua mbunge kupitia CCM ili waweze kusonga mbele kwa maendeleo 
kutokana na kudorora kwa muda mrefu kwa sababu ya kukwamishwa na mbunge 
kupitia upinzani  aliyeshindwa kuwaletea maendeleo kwa muda wote wa 
miaka mitano.
Kada
 wa Chama cha Mapinduzi  kutoka mkoani Tabora aliyejiunga na CCM hivi 
karibuni akitokea Chadema  Mtemi Nyanda akimpigia debe Dk. John Pombe 
Magufuli.
Kundi la TOT likitumbuiza katika mkutano huo.
Chege na Temba kutoka TMK Family wakitumbuiza katika mkutano huo.
Baadhi ya wananchi waliohudhuria katika mkutano huo.
Msanii Msami pamoja na kundi lake wakitumuiza katika mkutano huo uliofanyika Ikungi kwenye uwanja wa Mnadani mkoani Singida.
Baadhi
 ya wana CCM wakifurahia jambo wakati Mgombea wa urais wa Jamhuri ya 
Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwahutubia .
Burudani zikiendelea.
Msafara
 wa Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. 
John Pombe Magufuliukiwasili kwenye  mkutano wa kampeni uliofanyika 
katika uwanja wa Mnadani Ikungi mkoani Singida.
Mgombea
 wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe 
Magufuli akizungumza jambo na mgombea ubunge wa jimbo la Singida 
Magharibi Mh. Lazaro Nyalandu katika mkutano wa kampeni uliofanyika 
Manyoni.
Baadhi
 ya wananchi wakiwa na shamrashamra wakati wakimpokea Dk. John Pombe 
Magufuli hayupo pichani alipowasili kwenye mkutano wa kampeni 
uliofanyika Manyoni mkoani Singida
Mgombea
 wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe 
Magufuli akimnadi mgombea ubunge wa jimbo la Manyoni Daniel Mtuka katika
 mkutano wa kampeni uliofanyika mjini Manyoni kushoto ni Kapteni John 
Chiligati aliyestaafu na kumwachia kijiti mgombea huyo.
Mgombea
 wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe 
Magufuli akimkabidhi ilani ya uchaguzi  mgombea ubunge wa jimbo la 
Manyoni Daniel Mtuka katika mkutano wa kampeni uliofanyika mjini Manyoni
Mwenyekiti
 wa CCM mkoa wa Dodoma Alhaji Adam Kimbisa akisalimiana na Mh. Lazaro 
Nyalandu mgombea ubunge wa jimbo la Singida Magharibi.
Mgombea
 wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe 
Magufuli akimnadi mgombea ubunge wa jimbo la Bahi Mh. Omary Ahmed Badwel
 katika mkutano wa kampeni uliofanyika mjini Bahi.
Mgombea
 wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe 
Magufuli akizungumza na mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma Alhaji Adam 
Kimbisa kulia na  mgombea ubunge wa jimbo la Bahi Mh. Omary Ahmed Badwel
 katika mkutano wa kampeni uliofanyika Babati
0 comments:
Post a Comment