WATU
watano wanahofiwa kufa maji na wengine 11 wamenusurika, baada ya gari
waliyokuwa wakisafiria kusombwa na maji ya mto kufuatia mvua kubwa
zinazoendelea kunyesha mkoani mkoani Singida.
Kwa
mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoa wa Singida Kamishina msaidizi
mwandamizi Geofrey Kamwela, tukio hilo limetokea jana majira ya saa
3: 30 asubuhi katika Kijiji cha Kisimba Wilayani Iramba.
Amesema watu hao waliokuwa wakisafiri kwa gari yenye namba za usajili
T.499 ATR aina ya Land rover 110 TDI, walikuwa wakijaribu kuvuka mto
Nzalala kutoka eneo Doromoni kwenda Kiomboi Mjini.
Kamanda
Kamwela amesema wakati dereva ambaye hajatambuliwa jina wala makazi
akijaribu kuvusha, gari hiyo ilizimika katikati ya mto kabla ya
kosombwa na maji ikiwa na abiria 16 ndani.
Amesema
abiria 11 kati yao wameokolewa na kupelekwa hospitali ya Wilaya ya
Iramba kwa matibabu, wakati juhudi za kufukua gari hiyo iliyofukiwa kwa
mchanga mita chache kutoka eneo la tukio na kutafuta watu wengine
watano ambao hawajulikani walipo zinaendelea kufanywa.
Dereva wa gari hiyo na kondakta wake wanasadikiwa kutoweka baada ya tukio hilo na polisi wanaendelea kuwasaka.
0 comments:
Post a Comment