TUNAOMBA RADHI KWA HII PICHA
Kamanda wa polisi mkoa wa Singida,SACP Geofrey Kamwela,akionyesha bunduki ya kijeshi aina ya SMG no.34555 iliyokuwa ikitumiwa na watu wawili wanaodhaniwa kuwa majamabazi katika kijiji cha Manga manispaa ya Singida.
WATU 
wawili wakazi wa manispaa ya Singida ambao majina yao bado 
hayajajulikana,wakiwa kwenye Jokofu la kuhifadhia maiti baada ya kuuawa 
wakati wa majibishano ya risasi na polisi.
JESHI  la Polisi mkoani Singida limewauwa watu wawili wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wakati wa kurushiana rasasi.
Kamanda
 wa Jeshi la Polisi mkoani Singida, SACP, Geofrey Kamwela amesema tukio 
hilo limetokea desemba tisa mwaka huu saa 12:00 jioni, huko katika 
kijiji cha Manga nje kidogo ya mji wa Singida.
Amesema
 watu watatu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wakiwa na bunduki moja ya 
kijeshi aina ya SMG, walifika kijijini hapo kwa lengo la kufanya 
uhalifu.
Kamanda
 Kamwela, amesema watu hao ambao miili yao imehifadhi kwenye chumba cha 
mochwari katika hospitali ya mkoa, majina na makazi yao bado 
hayajajulikana.
Akifafanua,
 amesema taarifa za siri kutoka kwa raia wema zilifikia jeshi la polisi 
na ndipo askari polisi walipofika kwenye eneo la tukio.
“Baada
 ya polisi kufika kijijini hapo watu hao walistuka kuwa wanafuatilwa na 
askari polisi na hivyo kuanza kukimbia kuelekea kijiji cha Uhamaka kwa 
kutumia pikipiki yenye namba za usajili T. 634 BTW aina ya Sanlag yenye 
rangi nyeusi”,amesema Kamwela.
Amesema walipoona Polisi wanawakaribia waliamua kutelekeza pikipiki yao hiyo na kuanza kukimbilia porini kwa miguu.
“Hali
 ilipokuwa ngumu zaidi, walianza kuwarushia polisi risasi, hivyo polisi 
nao ikwabidi kujibu mapigo.  Katika majibizao hayo ya risasi, majambazi 
mawili yaliweza kujeruhiwa huku mmoja akifanikiwa kutoroka”
Amesema
 majambazi hayo yaliyojeruhiwa yalifariki dunia wakati yanakimbizwa 
katika hospitali ya mkoa kwa matibabu,lakini yakafia njiani.
Amesema katika eneo la tukio, ilipatikana 
bunduki
 moja aina ya SMG yenye namba 34555 ikiwa na risasi saba kwenye 
magazine.  Pia pikipiki iliyokuwa iantumiwa na majambazi hayo, iliwezea 
kupatikana.
Kamwela
 alitoa wito kwamba wananchi waendelee na moyo huo huo wa kuwafichua 
watu wanaowatilia shaka ili waweze kudhibitiwa mapema kabla ya kufanya 
uhalifu.
Kwa hisani ya Mtandao wa Singida Yetu 


0 comments:
Post a Comment