Kamanda
wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida, SACP Geofrey Kamwela, akizungumza
na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na tukio la maafa ya
mvua kubwa iliyosababisha vifo.
Na Nathaniel Limu, Singida
MVUA
kubwa zilizoanza kunyesha mkoani Singida zimeanza kuleta maafa baada ya
watu watano kuhofiwa kufa maji kutokana na gari waliolokuwa wakisafiria
kusombwa na maji ya mto.
Kamanda
wa Jeshi la Polisi mkoani Singida, SACP Geofrey Kamwela amesema tukio
hilo limetokea Desemba saba mwaka huu saa 3:30 asubuhi huko katika mto
wa Nzalala kijiji cha Kisimba tarafa ya Kisiriri wilayani Iramba.
Amesema
siku ya tukio, abiria 16 waliokuwa wakitoka kijiji cha Doromoni kwa
kutumia Landrover 110 TDI lenye namba za usajili T.499 ATR, lilisombwa
na maji ya mto wakati dereva wake akijaribu kuvuka mto Nzalala.
Akifafanua,
amesema walimpofika kwenye mto huo abiria hao walimwomba dereva huyo
asubiri maji ya mto yapungue ili waweze kuvuka lakini dereva huyo
alikataa kwa madai maji ni machache.
“Wakati
gari hilo lilipofika katikati ya mto, lilizimika ghafla na wakati huo
huo maji ya mto yaliongezeka na kulifunika gari. Dereva na kondakta
waliweza kufanikiwa kutoka na kukimbilia kusikojulikana”
Aidha,
amesema abiria 11 waliweza kuokolewa na wamelazwa katika hospitali ya
wilaya ya Iramba na watano hadi sasa haijulikani iwapo wamekufa ndani ya
landrover au wamesomba na maji na kupelekwa kusikojulikana.
Katika
hatua nyingine, Kamanda Kamwela, ametoa wito kwa madereva wa vyomba vya
moto, baiskeli na watembea kwa miguu kuchukua tahadhari wakati wa
kuvuka mito au mabonde kipindi hiki cha mvua kubwa zinazoendelea
kunyesha.
Alitumia
fursa hiyo kushauri mamlaka zinazohusika kutengeneza madaraja kwenye
mito au mabonde badala ya kuweka zege ambalo husaidia tu katika kipindi
cha kiangazi.
“Aidha nashauri abiria nao wasikubali kujazwa kwenye vyombo vya usafiri tofauti na uwezo hali wa gari” amesema.
Na Mo Blog
0 comments:
Post a Comment