SITAKI TENA KUSIKIA MSAMIATI "MRADI UKO CHINI YA KIWANGO", RC NCHIMBI AAGIZA.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe. Dkt. Rehema Nchimbi akipanda viazi lishe katika shamba la Mkulima wa viazi katika kijiji cha Nkungi Wilayani Mkalama katika ziara yake wilayani humo.
Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dkt. Angelina Mageni Lutambi akipanda viazi lishe katika shamba la Mkulima wa viazi katika kijiji cha Nkungi Wilayani Mkalama.
Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Mhe. Jakson Masaka akishiri kupanda viazi lishe katika shamba la Mkulima katika kijiji cha Nkungi Wilayani humo.
 
Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe. Dkt. Rehema Nchimbi au “mama Nchimbi” kama anavyojulikana jana amefanya ziara ya kikazi Wilaya ya Mkalama na kuagiza watendaji kusimamia miradi kwa umakini kwakuwa hataki kusikia mradi wowote uko chini ya kiwango.

Dkt. Nchimbi amesema msamiati chini ya kiwango hataki kuusikia kwakuwa umekua ukifanya watendaji kuwa wazembe na kuongeza kuwa hatua kali zitachukulkiwa kwa viongozi wote ambao hawatasimamia ipasavyo utekelezaji wa maelekezo hayo.

Ameongeza kuwa watendaji wamekuwa wakiilalamikia serikali na kuirudisha nyuma kwa kutotekeleza majukumu yao ipasavyo na hivyo kupelekea wananchi kuona serikali haifanyi chochote wakati inaleta pesa nyingi za miradi mbalimbali ambapo jukumu la watumishi ni kusimamia miradi ili ifanye kazi ipasavyo.

Dkt. Nchimbi amesema viongozi wote kabla ya kusaini mikataba yoyote ya halmashauri wanapaswa kukiri thamani ya mali zao zinazohamishika na zisizohamishika ili kama mradi utatekelezwa chini ya kiwango, mali zao zitumike kufidia pesa ya serikali iliyopotea.

“Mradi wakati unajengwa Mkurugenzi, Mwenyekiti wa halmashauri na wataalam wanauangalia bila kusema chochote, ukikamilika ndio wanakuambia umejengwa chini ya kiwango, kuanzia sasa sitaki kusikia msamiati wa ‘chini ya kiwango’ na endapo ikitokea chini ya kiwango tutahakikisha fedha ya serikali inarudi”, amesema Dkt. Nchimbi.

Aidha katika kikao hicho na watumishi wote wa halmashauri hiyo amewaagiza wakuu wote wa shule za msingi na sekondari kuwaruhusu wanafunzi ambao hawana sare kuanza masomo huku utaratibu wa kuwafuatilia wazazi watimize majukumu yao ukiendelea.

“ Baada ya elimu kuanza kutolewa bure, changamoto nyingine iliyobakia kwa baadhi ya wazazi ni uwezo wa kuwashonea watoto wao sare za shule, sasa ninaagiza wakuu wa shule za sekondari na Msingi wote Wilayani hapa kuwaruhusu watoto hao waingine madarasani hata kama hawajavaa sare za shule ili wasikose haki yao ya msingi kwa sababu ya sare tu”, ameagiza Dkt. Nchimbi.

Awali kabla ya kuzungumza na watumishi Dkt. Nchimbi alifanya ziara katika mashamba ya wakulima ili kujionea na kushiriki na wananchi shughuli za kilimo hasa mashamba ya viazi katika kijiji cha Nkungi na mashamba ya mtama katika kijiji cha Ilunda wilayani humo.

Dkt. Nchimbi akiwa katika shamba la mkulima wa viazi lishe katika kijiji cha Nkungi alipanda viazi na kuhamasisha wananchi wengine walime mazao ambayo yanatumia maji kwa ufanisi kama vile viazi, mihogo, matama na uwele kutoka na mabadilike ya tabia nchini ili kujihakikishia uwepo wa chakula.

Amewataka watendaji hasa wa kada za kilimo na ufugaji kuacha kufanya kazi kwa mazoea hasa kuandaa taarifa za makaratasi bali wawatembelee wakulima na wafugaji katika maeneo wanayofanya shughuli zao ili waweze kutoa ushauri kwa kupata picha halisi.“Sipendi kiongozi anayesema yupo karibu na wananchi kwa sababu hatuwezi kupima ukaribu uliopo hivyo ni vyema kuanzia sasa tuache kuwa karibu na badala yake tuwe pamoja nao”, amesema Dkt. Nchimbi.
 

NAIBU WAZIRI ELIMU MHANDISI MANYANYA AFANYA ZIARA MKOANI SINGIDA NA KUHAMASISHA ELIMU NJE YA MFUMO RASMI YA WATU WAZIMA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Naibu Waziri Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Mhandisi Stella Manyanya akiwasili katika halmashauri ya Wilaya ya Singida ambapo alipokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Singida Elias Tarimo na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Singida Eliya Digha.
Mkuu wa Wilaya ya Singida Elias Tarimo akimkaribisha Naibu Waziri Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Mhandisi Stella Manyanya ili aweze kuzungumza na watumishi wa halmashauri ya Singida.
Naibu Waziri Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Mhandisi Stella Manyanya akizungumza na baadhi ya wanafunzi wa shule aliyoitembelea kukagua na kuhamasisha elimu ya watu wazima.
Naibu Waziri Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Mhandisi Stella Manyanya akiwa amekaa kwenye moja ya darasa lenye wanafunzi walio katika mpango ulio nje ya mfumo rasmi wa elimu ya watu wazima.
Naibu Waziri Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Mhandisi Stella Manyanya akikagua daftari la mwanafunzi wa elimu ya watu wazima.

BILIONI 13.1 KUTUMIKA KUGHARIMIA MIRADI YA MAENDELEO SINGIDA.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 



Na Nathaniel Limu Singida.
Halmashauri ya manispaa ya Singida inatarajia kutumia zaidi ya shilingi 13.1 bilioni, kwa ajili ya kugharamia miradi mitatu ya uimarishaji miji (ULGSP) inayogharamia na benki ya dunia.
  
Hayo yamesemwa juzi na Mkurugenzi wa halmashauri ya Manispaa ya Singida Bravo Kizito Lyapembile, wakati akizungumzia kwenye hafla ya sherehe ya kusaini mkataba baina ya manispaa, washauri na mkandarasi atakayetekeleza miradi hiyo.
 
Amesema wamefikia hatua hiyo ya kusaini mkataba baada ya taratibu zote za kisheria za manunuzi kukamilika na kuongeza kuwa miradi hiyo ni ya ujenzi wa barabara zenye urefu wa kilometa 5.75 kwa kiwango cha lami.
 
 “Barabara hizo ni pamoja na ile inayoanzia kituo cha mafuta Namfua hadi ofisi ya Mamlaka ya mapato (TRA) ambayo itapanuliwa na kuwa mbili (double road). Nyingine ni ile inayoanzia ofisi za TRA hadi makazi ya askofu wa kanisa la katoliki (barabara ya Kinyeto)”, ameongeza.
 
Lyampembile amesema taratibu za manunuzi katika mkataba huu zilianza mwezi Mei mwaka jana na kukamilika Januari mwaka huu ambapo ujenzi huo utagharimu zaidi ya shilingi 12.4 bilioni.
 
“Leo hii manispaa ya Singida itatiliana saini mkataba namba LGA/115/SMC/2016/2017 /W/NO.1 na kampuni ya China Henan International Co-operation Group Co.LTD (CHICO) ya jijini Dar-es-salaam. Ujenzi huo utakamilika baada ya miezi 12”, alifafanua zaidi.
 
Amesema CHICO atasimamiwa na  kampuni ya Luptan Consultants Ltd ya jijini Dar-es-salaam kwa gharama ya shilingi 648.3 milioni na itakamilika baada ya miezi 15. Mkataba wa mradi huo ni LGA/115/SWMC/2016/2017/C/No.02.
 
“Vile vile tutatekeleza mradi mwingine wa uandaaji wa mpango mkakati wa miaka mitano wa mansipaa yetu ya Singida.Mradi huu wenye mkataba LGA/115/SMC/2016/2017/C/No.03 una   thamani ya zaidi ya shilingi 55.9 milioni.Mradi huu utatekelezwa na mshauri mwelekezi chuo cha mipango Dodoma, Titus Mwageni”,alisema.
 
Sherehe hiyo ya utiaji saini mikataba hiyo,zilihudhuriwa na mkuu wa wilaya ya Singida Elias Tarimo na mkuu wa mkoa wa Singida,Dk.Rehema Nchimbi.
 
Dk.Nchimbi Alitumia fursa hiyo kuyaomba mashirika ya TANESCO,TTCL na mamlaka ya maji (SUWASA) kutoa ushirikiano na mkandarasi,ili miundo mbinu yao isikwamishe utekelezaji wa mradi huo mkubwa ambao utakapokamilika,utabadilisha madhari ya mji wa Singida.

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2011. Singida Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogz za Mikoa