Na Nathaniel Limu Singida.
Halmashauri
ya manispaa ya Singida inatarajia kutumia zaidi ya shilingi 13.1
bilioni, kwa ajili ya kugharamia miradi mitatu ya uimarishaji miji
(ULGSP) inayogharamia na benki ya dunia.
Hayo
yamesemwa juzi na Mkurugenzi wa halmashauri ya Manispaa ya Singida
Bravo Kizito Lyapembile, wakati akizungumzia kwenye hafla ya sherehe ya
kusaini mkataba baina ya manispaa, washauri na mkandarasi
atakayetekeleza miradi hiyo.
Amesema
wamefikia hatua hiyo ya kusaini mkataba baada ya taratibu zote za
kisheria za manunuzi kukamilika na kuongeza kuwa miradi hiyo ni ya
ujenzi wa barabara zenye urefu wa kilometa 5.75 kwa kiwango cha lami.
“Barabara
hizo ni pamoja na ile inayoanzia kituo cha mafuta Namfua hadi ofisi ya
Mamlaka ya mapato (TRA) ambayo itapanuliwa na kuwa mbili (double road).
Nyingine ni ile inayoanzia ofisi za TRA hadi makazi ya askofu wa kanisa
la katoliki (barabara ya Kinyeto)”, ameongeza.
Lyampembile
amesema taratibu za manunuzi katika mkataba huu zilianza mwezi Mei
mwaka jana na kukamilika Januari mwaka huu ambapo ujenzi huo utagharimu
zaidi ya shilingi 12.4 bilioni.
“Leo
hii manispaa ya Singida itatiliana saini mkataba namba
LGA/115/SMC/2016/2017 /W/NO.1 na kampuni ya China Henan International
Co-operation Group Co.LTD (CHICO) ya jijini Dar-es-salaam. Ujenzi huo
utakamilika baada ya miezi 12”, alifafanua zaidi.
Amesema
CHICO atasimamiwa na kampuni ya Luptan Consultants Ltd ya jijini
Dar-es-salaam kwa gharama ya shilingi 648.3 milioni na itakamilika baada
ya miezi 15. Mkataba wa mradi huo ni LGA/115/SWMC/2016/2017/C/No.02.
“Vile
vile tutatekeleza mradi mwingine wa uandaaji wa mpango mkakati wa miaka
mitano wa mansipaa yetu ya Singida.Mradi huu wenye mkataba
LGA/115/SMC/2016/2017/C/No.03 una thamani ya zaidi ya shilingi 55.9
milioni.Mradi huu utatekelezwa na mshauri mwelekezi chuo cha mipango
Dodoma, Titus Mwageni”,alisema.
Sherehe
hiyo ya utiaji saini mikataba hiyo,zilihudhuriwa na mkuu wa wilaya ya
Singida Elias Tarimo na mkuu wa mkoa wa Singida,Dk.Rehema Nchimbi.
Dk.Nchimbi
Alitumia fursa hiyo kuyaomba mashirika ya TANESCO,TTCL na mamlaka ya
maji (SUWASA) kutoa ushirikiano na mkandarasi,ili miundo mbinu yao
isikwamishe utekelezaji wa mradi huo mkubwa ambao
utakapokamilika,utabadilisha madhari ya mji wa Singida.
0 comments:
Post a Comment