Singida.Abiria watano wamekufa baada ya gari
aina ya Landrover 110 waliyokuwa wanasafiria kusombwa na maji katika
Kijiji cha Doromoni Wilaya ya Iramba.
Katika ajali hiyo iliyotolea jana, watu wengine 11 walinusurika baada ya kuruka na kuogelea mara baada ya gari hiyo kupinduka.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Geofrey Kamwela alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo.
Kamwela alisema ajali hiyo ilitokea majira ya
asubuhi wakati gari hilo likiwa linabeba abiria 16 kutoka Kijiji cha
Doromoni wilayani Iramba kuelekea Kiomboi mjini.
Alisema chanzo cha ajali hiyo ni kujaa kwa maji katika Mto Nzalala kiasi cha kulifunika daraja.
Kamwela alisema wakati dereva alipojaribu kuvuka, gari hiyo ilizidiwa nguvu na maji, hivyo kuisomba.
Baadhi ya abiria walionusurika kwenye ajali hiyo
walisema kwamba walipofika kwenye daraja hilo walimwambia dereva
asivuke, bali asubiri maji yapungue.
Walidai dereva alikaidi agizo hilo na kuamua
kuvuka na alipofika katikati alionekana kubabaika na maji kabla ya maji
kuizidi nguvu gari.
Habari ambazo pia hazijathibitishwa zilidai kuwa dereva na kondakta wa gari hilo waliruka na kukimbia eneo la ajali.
Chanzo;Mwananchi
Chanzo;Mwananchi
0 comments:
Post a Comment