OFISI ya mtendaji wa kijiji cha Salanka, kata ya Salanka, wilayani
Kondoa, imefungwa kwa kukosa mtendaji wa kijiji kwa muda wa mwaka moja
sasa.
Hali hiyo imeelezwa kuchangia wananchi kukosa huduma hivyo na
kulazimika kutembea umbali mrefu kufuata huduma hiyo kwenye ofisi ya
kata.
Mtendaji wa kijiji hicho alisimamishwa na mkutano wa kijiji kwa tuhuma za ubadhirifu wa fedha za kijiji.
Akizungumza kwenye mkutano wa kijiji, Mwenyekiti wa kijiji hicho,
Khamis Majaliwa, alisema wamekuwa wakifuatilia suala hilo kwa muda sasa
huku Ofisi ya Mkaguzi wa Hesabu za Ndani wa halmashauri hiyo akifika
mara moja na hadi sasa hajafika kijijini hapo kwa madai ya kukosa
usafiri.
Katika mkutano huo, wanakijiji hao waliazimia kwenda kuonana na Waziri
Mkuu kutatua tatizo hilo lililodumu kwa muda wa mwaka sasa licha ya
viongozi mbalimbali kuulizwa na kukosa majibu.
Alipoulizwa Mkuu wa Wilaya hiyo, Omar Kwang’, alisema kwa wakati huo
alikuwa yuko nje ya ofisi akiwa likizo na kumtaka mwandishi kusuburi
hadi atakaporudi ofisini ndipo atatoa majibu.
Chanzo;Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment