MKUTANO MKUU WA TATU WA PSPF WAFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Rais mstaafu wa awamu ya pili,Alhaj Ali Hassan Mwinyi, akizindua huduma mpya ya PSPF Pamoja nawe na PSPF call centre, itolewayo na mfuko wa Pensheni wa PSPF, baada ya kufungua Mkutano mkuu wa tatu wa wadau wa mfuko huo Feb 26.2014.
 Mgeni rasmi Rais Mstaafu wa awamu ya pili Alhaji Hassan Mwinyi, kushoto kwake ni Naibu Waziri wa Fedha, Adam Malima, kulia kwake ni Ndugu Peter Ilomo aliyemwakilisha Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya PSPF George Yembesi, Mkurugenzi Mkuu PSPF, Adam Mayingu na Katibu Mkuu MPAIC, John Haule
Wakurugenzi wa idara mbalimbali za mfuko wa Pensheni wa PSPF, mstariu wa mbele, wakiwa miongoni mwa wajumbe wanaohudhuria mkutano mkuu wa tatu wa wadau wa mfuko huo kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa julius Nyerere jijini Dar es Salaam Februari 26, 2014.

  Mkurugenzi wa Uendeshaji wa PSPF, Neema Muro akijadili jambo na mmoja wa wadau wa PSPF

Usikivu 
 Naibu Waziri wa Fedha, Adam Malima akimkaribisha Mgeni Rasmi Rais Mstaafu wa Awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi alipowasili kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimtaifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam jana, kuhudhuria mkutano mkuu wa tatu wa Mfuko wa PSPF wa wadau Februari 26.2014.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Adam Mayingu (kushoto), akimkaribisha Mgeni Rasmi Rais wa Mstaafu Ally Hassan Mwinyi kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimtaifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, kuhudhuria mkutano mkuu wa tatu wa Mfuko wa PSPF wa wadau Februari 26.2014.


 Kutoka kushoto ni Meneja wa Kitengo Mawasiliano ya simu, Fatma Elhadgy, Meneja wa Mawasiliano, Masoko na Uenezi wa PSPF, Costantina Martin na Ephraim Kibonde 

 Mgeni rasmi Rais Mstaafu wa awamu ya pili Alhaji Hassan Mwinyi 
Mgeni rasmi Rais Mstaafu wa awamu ya pili Ally Hassan Mwinyi akionyesha zawadi aliyopewa na PSPF, kushoto kwake ni Ndugu Peter Ilomo aliyemwakilisha Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya PSPF George

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

Ajali Basi la Bunda Lagongana na Treni,watu wanne wafariki dunia

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


 
Basi la Bunda Express lililokuwa likitokea Dodoma kwenda Mwanza asubuhi hii limegongana na Treni Eneo la Manyoni mkoani Singida. 
Kwa mujibu wa chanzo cha habari kutoka eneo la tukiokinasema kuwa watu wanne wamefariki dunia na kadhaa kujeruhiwa.
Majeruhi Tayari wamepelekwa kwenye Hospitali ya Wilaya ya Manyoni.

TANGASIS WASUSIA FIDIA KIDUCHU

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
WAKAZI wa Mwambani, Kata ya Tangasisi, wilayani Tanga wameelezea kutoridhishwa na fidia waliyolipwa ili kupisha ujenzi wa reli kwenye Bandari mpya ya Mwambani.
Wakazi hao zaidi ya 200 wanaoishi kandokando ya bahari wamelipwa sh 3,400 kwa mita moja ya mraba wakati viwango vya jiji hilo kwa sasa ni sh 7,000 kwa ukubwa huo kitu kinachowafanya wadai fidia zaidi.
Kwa sababu hiyo wamemuomba Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe na Waziri wa Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, kuingilia kati suala hilo kwa kuwa thamani ya pesa wanayolipwa hailingani na mali zao.
Chanzo;Tanzania Daima 

TANGAZO LA MKUTANO MKUU WA WADAU WA PSPF

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
MFUKO WA PENSHENI WA
PSPF

TANGAZO LA MKUTANO MKUU WA WADAU
Mfuko wa Pensheni wa  PSPF unatangaza kwamba kutakuwa na Mkutano Mkuu wa tatu wa wadau utakaofanyika tarehe 26 na 27  Februari 2014 kuanzia saa mbili na nusu asubuhi hadi saa kumi jioni katika Ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere uliopo barabara ya Shaban Robert  jijini Dar es salaam.
Madhumuni ya Mkutano huu ni kutoa taarifa ya hesabu ya mwaka na utendaji wa Mfuko na kutathmini mafanikio na changamoto zinazokabili Mfuko na sekta ya Hifadhi ya Jamii kwa ujumla.
“PSPF - TULIZO LA WASTAAFU”
Mkurugenzi Mkuu
Mfuko wa Pensheni wa PSPF,
Makao Makuu,Golden Jubilee Towers,  S.L.P 4843. Dar-es-Salaam.
Simu: +255222120912/52 au +255222127375 /6
 Nukushi: +255222120930

 Barua pepe:pspf@pspf.tz.org

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

DC Singida awataka Madiwani na watendaji wa kata hadi Mei 30 Ujenzi wa Maabara uwe umekamilika.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


 Mkuu wa wilaya ya Singida,Queen Mwashinga Mlozi, akizungumza na madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Singida.Pamoja na mambo mengine, aliagiza kwamba Diwani na mtendaji wake wa kata wasipomaliza ujenzi wa vyumba vitatu vya maabara kabla ya Mei 30 mwaka huu, atawachukulia hatua kali ya kisheria ikiwemo kuwafikisha mahakamani. Wa pili kulia (aliyeketi),ni Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Singida,Illuminata Mwenda na anayefuata ni mwenyekiti wa halmashauri ya Singida.

MKUU wa wilaya ya Singida,Queen Mwashinga Mlozi,amewatahadharisha madiwani na watendaji kata,kwamba kabla ya mei 30 mwaka huu wawe wamekamilisha ujenzi wa vyumba vitatu vya maabara,vinginevyo watachukuliwa hatua kali za kisheria.


Mlozi ametoa agizo hilo wakati akizungumza mbele ya kikao cha kawaida cha baraza la madiwani kilichofanyika mjini Singida.


Alisema madiwani na watendaji kata ambao watashindwa kumaliza ujenzi huo kabla ya muda uliopangwa,watawajibishwa ikiwa ni pamoja na kuwafikisha mahakamani.


“Nitafanya hivyo kwa mujibu wa mamlaka niliyopewa chini ya kifungu cha 14 na 15 vya sheria za tawala za mikoa na serikali za mitaa ya mwaka 2002 ya kuvunja amri halali ya kutokujenga vyumba vitatu vya maabara”alifafanu mkuu huo wa wilaya.


Dc Mlozi alitaja shule za kata ambazo ujenzi wake

umefikia asilimia 80,kuwa ni Mdasenga,Maghojoa,Ntoge,Mughunga,Makuro,Mrama,Mwanamwema,Ngimu,Nyeri na Itaja.

Katika hatua nyingine,alisema kuwa kampuni ya bia Tanzania (TBL) kwa kushirikiana na taasisi za fedha,imeazimia kufanya zao la mtama (mweupe),kuwa zao la kutumainiwa la biashara katika mkoa wa Singida.


Akifafanua,Mlozi alisema TBL inahitaji kununua tani 7,000 na ili kufikia lengo la upatikanaji wa tani hizo,taasisi za fedha za CRDB benki na NMB,zitashirikiana na wakulima ili kuhakikisha wanalima kitaalam kwa kutumia zana bora na kilimo cha kisasa.


“Madiwani na watendaji wote tutumie fursa hii kwa kuhakikisha tunawahamasisha wakulima wetu wanufaike na kilimo hiki cha mtama mweupe.Tujipange vizuri kwa utekelezaji”,alisema Mlozi.


Na mtandao wa Singida yetu 

Ashikiliwa kwa nyara za Serikali

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Polisi Mkoa wa Singida, wanamshikilia Jafari Hamisi (23),Mkazi wa Ukombozi mjini Singida,kwa tuhuma ya kumilki kinyume cha sheria vipande 16 vya meno ya ndovu vyenye thamani ya zaidi ya Sh17milioni.

Meno hayo yamekamatwa ikiwa ni siku nne toka meno mengine vipande 21 vyenye thamani ya zaidi ya Sh43 milioni,kukamatwa kwenye eneo lile lile la kizuizi cha mazao kilichopo katika Kijiji cha Ukimbu kata ya Mgandu Wilaya ya Manyoni.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana,Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida.SSP.Cordula Lyimo,alisema meno hayo yamekamatwa Feb 16 mwaka huu saa tano usiku katika kizuizi cha mazao kilichopo Kijiji cha Ukimbu,Kata ya Mgandu Tarafa ya Itigi Wilaya ya Manyoni.
Alisema askari wakiwa katika kizuizi hicho,walifanya ukaguzi kwenye gari T.288 AJF aina ya Scania mali ya Kampuni ya Super Service likiendeshwa na Ally Hamadi,likitokea Makongorosi Chunya,kuelekea Itigi Wilaya ya Manyoni.
“Baada ya upekuzi huo,walikuta meno hayo yakiwa yamehifadhiwa ndani ya begi la nguo na kuwekwa kwenye keria za ndani ya basi.Mtuhumiwa aliweza kupatikana wakati akiwa katika juhudi za kutaka kutoka ndani ya basi ili akimbie”,alisema Lyimo.
Kaimu kamanda huyo,alisema uchuguzi zaidi unaendelea ili kubaini au kupata mtandao kamili unaojihusisha na kuwinda pamoja na kununua nyara hizo.
Chanzo;Mwananchi

Akamatwa na vipande 21 vya meno ya tembo

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


JESHI la Polisi limemkamata mtu mmoja  mkazi wa Mwamagembe, Itigi wilayani Manyoni, Singida, George James (30)  na vipande 21 vya meno  ya tembo akiwa njiani kuvisafirisha.
Kamanda wa Polisi mkoani humo (SACP) Geofrey Kamwela, alisema jeshi hilo lilifanikiwa kumkamata kijana huyo baada ya kuweka mtego wakati wakiwa ndani ya gari.
Alilitaja gari hilo kuwa ni Toyota Hiace lenye namba za usajili T 797 CQL wakati akiwa katika harakati za kusafirisha meno hayo  kwenda Itigi mjini.
Chanzo;Tanzania Daima

BREAKING NEWS TUKIO KATIKA PICHA: LORI LA MAFUTA LADONDOKA MDA HUU MLIMA SEKENKE LALIPUKA NA KUUWA WATU WA NNE HAPO HAPO.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


 Wanainchi wakiangalia Lori baada ya kuungua
 Mabaki ya Lori hilo bada ya kuteketea kabisa na moto jioni hii
 Baadhi ya wasafiri wakitazama lori lililongua jioni hii

 Bonde la mlima sekenke linavyoonekana na baadhi ya miti imeunguaa
 Hii ni njia ya mlima sekenke
 Haya ni mabaki ya mwili wa mmoja ya watu walikuwam kwenye Lori hiloo
Moto ukimalizikia kwa mbaliii kama inavyoonekana

Lori la mafuta limeanguka jioni hii katika eneo la milima ya sekenke mkoani singida na kuua watu wanne hapohapo.Chanz cha ajali hiyo ni breki kufeli kukamata wakati lori hilo lilipokuwa linashuka mlima huo.Shuhda wa ajali hiyo bwana Julius chacha alipoongea na mtandao wetu wa Dj sek blog amesema kwamba Lori hilo lilipoacha njia lilipinduka na kuingia bondeni na kushika moto.Akiendelea kuongea shuhda huyo alisema walishindwa kutoa msaada wowote kwa kwa moto uliposhika ulikuwa mkubwa na hawakuwa na vifaa vya kuokolea.Watu wanne wamekuufa papo hapo kutokana na ajali hiyo.Polisi walikuwa bado hawajafika eneoo la tukio mpaka tunaondoka eneo la tukio.

JESHI LA POLISI LAKAMATA MENO YA NDOVU YENYE THAMANI SHILINGI MILIONI 17 SINGIDA‏

Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Singida, SSP.Cordula Lyimo, akitoa taarifa kwa waandishi wa habari leo juu ya kukamtwa kwa meno ya Tembo vipande 16 vyenye thamani ya zaidi ya shilingi 17 milioni.Vipande hivyo vimekamatwa februari 16 mwaka huu saa tano usiku kwenye kizuizi cha mazao cha kijiji cha Ukimbu wilaya ya Manyoni. Siku nne zilizopita,vipande vingine 21 vya meno ya Tembo vyenye thamani ya shilingi 43 milioni,vilikamatwa eneo hilo hilo.(Picha na Nathaniel Limu).
Na Nathaniel Limu, Singida
JESHI la Polisi mkoa wa Singida limefanikiwa kukamata vipande 16 vya meno ya ndovu vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 17.
Meno hayo yamekamatwa siku nne (12/2/2014) toka meno mengine vipande 21 vyenye thamani ya zaidi ya shilingi 43 milioni, kukamatwa kwenye eneo lile lile la kizuizi cha mazao kilichopo katika kijiji cha Ukimbu kata ya Mgandu wilaya ya Manyoni.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Kaimu kamanda wa Polisi mkoa wa Singida.SSP.Cordula Lyimo amesema meno hayo yamekamatwa febr.16 saa tano usiku huko katika kizuizi cha mazao kilichopo katika kijiji cha Ukimbu,kata ya Mgandu tarafa ya Itigi wilaya ya Manyoni.
Amesema askari wakiwa katika kizuizi hicho,walifanya ukaguzi kwenye gari T.288 AJF aina ya scania mali ya kampuni ya super service likiendeshwa na dereva Ally Hamadi, likitokea Makogorosi Chunya,likielekea Itigi wilaya ya Manyoni.
“Baada ya upekuzi huo,walikuta meno hayo yakiwa yamehifadhiwa ndani ya begi la nguo na kuwekwa kwenye keria za ndani ya basi.Mtuhumiwa aliweza kupatikana wakati akiwa katika juhudi za kutaka kutoka nda ya basi ili akimbie”,amesema Lyimo.
Kaimu kamanda huyo,amesema uchuguzi zaidi unaendelea ili kubaini au kupata mtandao kamili unaojihusisha na kuwinda pamoja na kununua nyara hizo.


Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

Mt. Gaspari yatibu wagonjwa 53,000

Hospitali ya Rufaa ya Mtakatifu Gaspari ZAIDI ya wagonjwa 53,000 walipatiwa huduma za matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mtakatifu Gaspari iliyopo katika mji mdogo wa Itigi, wilayani Manyoni, Singida kwa kuanzia mwaka 2006 hadi mwaka jana.
Mkurugenzi wa hospitali hiyo, Padre Seraphine Lesiriam, alisema hayo kwenye risala aliyosoma kwa mgeni rasmi Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Kardinali Polycarp Pengo wakati wa ufunguzi wa kliniki ya upasuaji wa watoto hospitalini hapo.
Padre Seraphine alifafanua kwamba katika kipindi cha kuanzia mwaka 2006 hadi 2012 watoto waliohitaji huduma za upasuaji hususani wa moyo hupelekwa katika Hospitali ya Bambino Gesu iliyopo Italia.
Kwa mujibu wa mkurugenzi huyo, kipindi hicho jumla ya watoto 13 wamenufaika na huduma za upasuaji, kati yao 12 walifanyiwa upasuaji wa moyo na mmoja alifanyiwa ‘plastic surgery’.
Hata hivyo aliweka wazi kwamba mwaka jana jumla ya wagonjwa wa nje 9,450 wenye chini ya miaka mitano walihudumiwa wakati wagonjwa wengine wa nje 36,353 wenye zaidi ya miaka mitano walihudumiwa hospitalini hapo.
Kuhusu wagonjwa waliolazwa, alisema kwa kipindi cha mwaka uliopita jumla ya wagonjwa 8,133 ambao kati yao watoto ni 3,711 walilazwa hospitalini hapo.
Padre Lesiriam alibainisha kwamba uwepo wa huduma za upasuaji kwa watoto na tiba nyingine katika hospitali hiyo ni tunda la moyo wa ukarimu na ushirikiano kati ya hospitali ya Bambino Gesu na Shirika la Wamishenari wa Damu Azizi.
Akifafanua zaidi, mkurugenzi huyo alisisitiza kwamba hospitali ya Bambino Gesu imechangia euro 250,000 sawa na zaidi ya sh 525,000,000 ili kuanzisha huduma za upasuaji kwenye kliniki ya watoto.
“Fedha hizo zimetumika kwenye ununuzi wa vifaa na kufanya marekebisho kwenye mojawapo ya majengo katika idara ya watoto ili kuanzisha huduma hizi za upasuaji,” alisisitiza padre huyo.
Rais wa hospitali ya Bambino Gesu, Profesa Giuseppe Profiti, akinukuu maandiko matakatifu alisema: “Msifanye mambo mema kwa ajili yetu tu bali mnapaswa kufanya mambo mema kwa ajili ya wengine pia.”
Hata hivyo, aliweka bayana kwamba wao wanapenda kushirikiana nao na watafanya kila kitu ambacho wataweza kukifanya, hivyo alitumia fursa hiyo kuomba msaada kwa watendaji wa hospitali hiyo ili wafanikishe malengo yao.
Akifungua kliniki hiyo, Kardinali Pengo alitumia fursa hiyo kuwaasa viongozi wa vyama vya siasa na serikali kutoingilia na kuharibu ufanisi wa huduma zinazotolewa na wafadhili kwa Watanzania ambao kwa namna moja au nyingine hawana uwezo  wa kuzilipia.
Alifafanua kuwa huduma zinazoanzishwa kwa faida ya watu wasiokuwa na uwezo, hususani watoto, zinatakiwa zisiingiliwe na baadhi ya watu ambao wanataka kwa manufaa yao.
Awali Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida, Hassani Liana, alisema serikali inatambua ushirikiano unaofanywa na watu binafsi na mashirika ya dini hasa kwenye afya na elimu hapa nchini.
Chanzo;Tanzania Daima 
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

Halmashauri ya Manispaa ya Singida yapongezwa kwa kujenga daraja


DSC06575
Mkuu wa mkoa wa Singida, Dk.Parseko Kone,(wa kwanza kushoto) akipata maelezo kutoka mkandarasi wa daraja la Mwankoko manispaa ya Singida,Rogers Mchau(anayenyoosha mkono) juu ya maendeleo ya ujenzi wa daraja kijiji cha Mwankoko.
Dk.Kone alilikagua daraja hilo baada ya kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa, kulalamika kwamba fedha zinazotumika katika ujenzi huo ni nyingi hazifanani na daraja lenyewe. Baada ya kulikagua,alikiri kuwa daraja hilo lina thamani na fedha zilizotumika na kwamba bado kuna zaidi ya shilingi 192 milioni zinahitajika ili kukamilisha ujenzi huo.
DSC06580
Mkuu wa mkoa wa Singida, Dk. Parseko Kone,akikagua ujenzi wa daraja la kijiji cha Mwankoko manispaa ya Singida.
DSC06593
Mkuu wa mkoa wa Singida, Dk.Parseko Kone, akitoa maelekezo juu ya kuboresha ujenzi wa daraja la kijiji cha Mwankoko manispaa ya Singida.
DSC06584
Daraja la kijiji cha Mwankoko linaloendelea kujengwa na mkandarasi Rogers Mchau.
DSC06597
Mkuu wa mkoa wa Singida (kushoto) akizungumza na Meya Mstahiki wa manispaa ya Singida,Sheikh Salum Mahami wakati alipokuwa akimaliza kukagua ujenzi wa daraja la kijiji cha Mwankoko.(Picha na Nathaniel Limu).
Na Nathaniel Limu, Singida
MKUU wa mkoa wa Singida,Dk.Parseko Kone,ameipongeza Halmashauri ya Manispaa ya Singida,kwa juhudi zake za kujenga daraja linalolingana na thamani ya fedha iliyotumika.
 Dk.Kone ametoa pongezi hizo mwishoni mwa wiki wakati akikagua ujenzi wa daraja hilo, ulioanza rasmi desemba 12 mwaka 2011 na ulitarajiwa kukamilika novemba 14 mwaka 2012.Daraja hilo linaunganisha kata ya Mwankoko na kata ya Mtamaa.
Amesema kuwa fedha ambayo imetumika hadi sasa ya zaidi ya shilingi 216.1 milioni,thamani ya fedha hiyo inafafanana kabisa na kazi ya ujenzi iliyofanyika.
 “Kwa kweli mmefanya kazi nzuri pamoja na mkandarasi wenu.Fedha ambazo mmeziomba serikali kuu ili mmalizie ujenzi wa daraja hili,tutakuwa nyuma yenu katika kuhakikisha mmezipata,ili ujenzi uweze kukamilika kwa mujibu wa mkataba wenu”,amesema.
Mapema Mkurugenzi wa Manispaa hiyo,Joseph Mchina,amesema mradi huo wa ujenzi wa daraja hilo,fedha zake zimetoka katika mfuko wa barabara kupitia OWM-TAMISEMI,zikiwa ni fedha za maombi maalum ya ujenzi wa madaraja.
 Katika hatua nyingine,Mchina amesema hadi sasa ujenzi huo wa daraja,umekamilika na magari yameanza kulitumia kwa tahadharai,kwani bado kuna kazi ambazo hazijakamilika.
 Mkurugenzi huyo alitaja baadhi ya kazi ambazo bado hazijakamilika kuwa ni ujenzi wa barabara ya kuingia na kutoka,mifereji ya wazi kandokando ya barabra ya kuingia na kutoka na kuweka alama barabarani.
 Alitaja kazi zingine ambazo bado hazijakamilika,kuwa ni pamoja na kazi ya ujenzi wa kuta za kulinda daraja,kuweka bomba za pembeni na kuweka nguzo za kuonesha mwlekeo wa daraja.
 “Katika mwaka wa fedha wa 2014/2015,halmashauri ya manispaa,imeomba kiasi cha shilingi 200 milioni kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huu”,amesema.
Mkuu huyo wa mkoa,amelazimika kukagua mradi huo wa ujenzi wa daraja,baada ya ujenzi huo kulalamikiwa kuwa umetumia fedha nyingi ambazo hazilingani na kazi iliyofanyika.Mbaya zaidi ni kwamba ujenzi huo upo nyuma ya muda kwa mujibu wa mkataba.
Mo Blog

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

MIFUKO YA BIMA YA AFYA (NHIF) NA MFUKO WA AFYA YA JAMII (CHF) SINGIDA YAHIMIZWA KUWA MAKINI KWA MADAI YA KUGHUSHI‏

DSC06603
Meneja wa NHIF mkoa wa Singida, Agnes Chaki, akifungua kikao cha waratibu wa mfuko wa Taifa Bima ya Afya na wale wa mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) ambacho kilitumika kukumbushana juu ya utoaji huduma bora kwa wananchama.Kulia ni afisa matekelezo na uratibu NHIF mkoa wa Singida,Isaya Shekifu na kushoto ni Edwin Mwangajilo afisa udhibiti ubora NHIF.(Picha na Nathaniel Limu).
DSC06615
Afisa matekelezo na uratibu wa mfuko wa taifa wa Bima ya Afya (NHIF) mkoa wa Singida, Isaya Shekifu akitoa mada yake kwenye kikao cha wataribu wa mfuko wa NHIF na mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) mkoa wa Singida.Kikoa hicho kililenga kubadilishana uzoefu juu ya utendaji kazi,ili kuboresha zaidi huduma za mifuko hiyo.Kushoto ni meneja wa NHIF mkoa wa Singida, Agnes Chaki.
DSC06606
Afisa udhibiti ubora NHIF mkoa wa Singida, Edwin Mwangajilo,akitoa mada yake kwenye kikao cha waratibu wa NHIF na CHF kilichofanyika kwenye ukumbi mdogo wa mikutano wa kanisa katoliki mjini Singida.Kushoto ni meneja NHIF mkoa wa Singida, Agnes Chaki.
DSC06607
Baadhi ya waratibu wa mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya na wale wa mfuko wa Afya ya Jamii mkoa wa Singida, waliohudhuria kikao cha kubadilishana uzoefu katika utendaji kazi, ili kuboresha huduma zaidi.
DSC06616
Picha ya pamoja.
Na Nathaniel Limu, Singida
WARATIBU wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) mkoani Singida,wamehimiza kuwa makini zaidi kukabiliana na wimbi la madai ya kughushi, kwa madai kwamba vitendo hivyo,vitachangia kudhoofisha huduma zinazotolewa na mifuko hiyo.
Wito huo umetolewa na meneja wa NHIF mkoa wa Singida,Agnes Chaki,wakati akizungumza kwenye ufunguzi wa kikao cha waratibu wa NHIF na CHF mkoani hapa, kilichofanyika kwenye ukumbi mdogo wa mikutano wa kanisa katoliki mjini hapa.
Alisema kuna baadhi ya watoa huduma si waaminifu na wanaleta madai ya kugushi, na mfuko umejiandaa kikamilifu kuhakikisha unadhibiti vitendo hivi ili kutimiza lengo la msingi la kuwapa huduma bora wanachama wake
"Ninyi waratibu ninawaomba ndugu zangu, tusaidiane katika kupambana na hili tatizo.Mnapokutana na watoa huduma,naomba mjaribu kuwaelimisha kuwa wawe wanatibu kwa kuzingatia miongozo ya NHIF na ile ya wizara.Wahakikishe kile wanachokitoa kinakuwa ni sawa na wanacho wasilisha NHIF....mfano katika dawa",alisema Chaki.
Aidha,meneja huyo wa mkoa, alisema mwanachama,mratibu au kiongozi ye yote akisikia au kuona kuna vitu/vitendo vinafanyika kinyume na taratibu za NHIF,tafadhali atoe taarifa mapema ofisi za NHIF mkoani hapa,ili ziwezekufuatiliwa mapema kabla havijaleta madhara kwa mfuko.
Kwa upande wake afisa matelekezo na uratibu NHIF mkoa wa Singida,Isaya Shekifu,akitoa mada yake ya majukumu ya waratibu wa NHIF/CHF,aliwataka waratibu hao kuhakikisha wanatimiza majukumu yao kwa uadilifu na kwa ushirikiano baina yao ili kuongeza ufanisi na pia wanajitambulisha kikamilifu katika vituo vyao vya kazi,ili wanachama wa mifuko hiyo,waweze kuwafahamu na kuwatambua .
"Pia hakikisheni mnatatua mapema matatizo/kero zinazohusu wanachma wa NHIF/CHF pamoja na watoa huduma na muandae taarifa za utekelezaji kila baada ya miezi mitatu",alisema Shekifu.
Afisa huyo wa maelekezo na uratibu,alisema NHIF inategemea endapo waratibu watatimiza majibu wao kwa uhakika, malalamiko kuhusu huduma za NHIF yatapungua na huduma zitaboreka.
Pia afisa udhibiti na uhakiki ubora wa NHIF mkoa wa singida ,Dr.Edwin Mwangajilo aliwasisitizia waratibu wa NHIF kuhakikishia wanapitia madai kwa uangalifu ili kuepusha makosa ambayo yanaweza kupunguza kiasi cha malipo ya madai kwa watoa huduma.
"Tunategemea mtafanya kazi zenu kwa ufanisi na uadilifu na kuhakikisha mnasimamia vituo vyote vile vya serikali,binafsi na mashirika ya dini ili wanachama wetu wa NHIF na CHF wapate huduma bora ,alifafanua Mwangajilo.


Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

Diwani kortini kwa lugha chafu

 DIWANI wa Unyambwa katika Halmashauri ya Manispaa ya Singida, Shabani Salumu (CCM), amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi ya mjini Singida, akikabiliwa na tuhuma za kuwatolea lugha ya matusi maofisa wa polisi ikiwemo kudai ni ‘mizigo’.
Mbele ya Hakimu Aisha Mwetindwa, Mwendesha Mashitaka, Chemu Mussa, alidai  kuwa Januari 12, mwaka huu, saa 1.30 asubuhi katika Kijiji cha Ijanuka, Kata ya Unyambwa,  mshitakiwa aliwatolea lugha ya matusi maofisa wa polisi kitendo kilichoelekea kusababisha kutoweka au kuvunjika kwa amani.
Alidai tukio hilo lilitokea wakati maofisa hao wakiwa kazini kwenye eneo ambalo wananchi wa Kata ya Unyambwa walichoma moto basi la Kampuni ya Mtei.
Mshitakiwa alikana tuhuma hizo na yupo nje kwa dhamana. Kesi itatajwa Februari 25, mwaka huu.
Chanzo;Tanzania 
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

WAKATI MKUTANO WA KUPINGA UJANGILI DUNIANI KOTE: GEORGE JAMES AKAMATWA NA MENO 21 YA TEMBO YENYE THAMANI YA TSH MILIONI 43, SINGIDA


JESHI la polisi mkoani Singida limekamata vipande 21 vya meno ya Tembo vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 43. 

Nyara hizo za serikali zimekamatwa katika kijiji cha Mwamagembe  wilayani Manyoni  zikisafirishwa kwenda Itigi, mkoani Singida. 

Mtu mmoja  George James amekamatwa kwa tuhuma za kukutwa na meno  hayo ya tembo yakiwa yamehifadhiwa katika mabegi mawili ya kusafiria. 

Mtuhumiwa huyo alikamatwa katika kizuizi cha idara ya maliasili kilichoko katika kijiji Ukimbu, kata  ya Mgandu, wilayani Manyoni akiwa katika gari aina ya Toyota Hiace lenye namba za usajili T797CQL.

Kamanda wa polisi mkoa wa Singida RPC Geofrey Kamwela (katika video) amesema vipande hivyo 21 vina thmani ya zaidi ya shilingi milioni 43 na vyote vimehifadhiwa katika kituo cha polisi wilayani Itigi.

"Meno haya yanaashiria kuuwawa kwa tembo wanne", alisema Kamanda James.

Vitendo vya ujangili wilayani MANYONI vimekuwa vikiongezeka ambapo mwaka 2013 askari mmoja wa jeshi polisi alipoteza maisha katika mapambano na majangili wilayani humo.

Tukio hili la limekuja wakati leo Rais Jakaya Mrisho Kikwete amehudhuria mkutano maalumu wa kupambana na ujangili na biashara ya meno ya tembo na pembe za Faru jijini London, Uingereza.

Katika mkutano huo amependekezWAKATI MKUTANO WA KUPINGA UJANGILI DUNIANI KOTE: GEORGE JAMES AKAMATWA NA MENO 21 YA TEMBO YENYE THAMANI YA TSH MILIONI 43, SINGIDA a kupigwa marufuku biashara hiyo ili kuweza kudhibiti ujangili duniani kote.


Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

Tanesco kutumia shilingi 48 bilioni kusambaza Umeme Vijijini Singida.


Meneja wa TANESCO mkoa wa Singida, Maclean Mbonile akiwa ofisini kwake kutekeleza majukumu yake ya kila siku.

SHIRIKA la umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa singida linatarajia kutumia zaidi ya shs. 48.3 bilioni kugharamiwa awamu mbili za miradi ya usambazaji umeme vijijini chini ya mpango wa matokeo makubwa sasa (BRN).


Akizungumuza na waandishi wa habari ofisini kwake hivi karibun, Meneja wa TANESCO mkoa wa singida, Maclean Mbonile amesema miradi yote inafadhiliwa na wakala wa nishati vijijini (REA ).


Amesema awamu ya kwanza utekelezaji wake ilianza julai 2010 na kukamilika mwishoni mwa Septemba mwaka jana. Awamu hiyo imegharimu  dola za kimarekani 9.94 milioni.


Amesema awamu ya pili imeanza kutekeleza mapema oktomba jana (2013), na inatarajiwa kukamilika ndani ya miezi 24. Awamu hii ya pili, inakadiriwa kugharimu jumla ya dola za kimarekani 20 milioni.


Mbonile amesema utekelezaji wa miradi hiyo, unasimamiwa na TANESCO  pamoja na uongozi wa serikali ya mkoa wa Singida .Ujenzi wake unafanywa na mkadarasi  binafsi aliyeshinda zabuni  M/S Spencon Services Ltd.


“Awamu ya kwanza tumeweza kuwapatia huduma ya umeme wananchi /wateja

1,503 katika awamu ya pili tunataajia wananchi /wateja 8,526 wapatao huduma ya umeme katika vijiji vya mradi .Idadi hii ni sawa na ongezeko la asilimia 52 ya idadi ya wateja wote mkoani”,alifafanua Meneja Mbonile

Meneja huyo alitaja wilaya na idadi ya miradi ya umeme vijijini kwenye mabano kwani Manyoni (33) ,Mkalama(15) , Iramba ( 26 ) ,Manispaa ya singida (2), Ikungi ( 5) , na singida vijijini ( 9).


Mbonile alitumia fursa hiyo kuwahimiza wakazi wa maeneo ya miradi ya umeme vijijini kutoa ushirikiano wa dhati ili miradi hiyo iweze kukamilika katika kipindi kilichopangwa.
 
Kwa hisani ya Singida Yetu 

Bil. 1.5/- kutumika kubadili maisha ya Wahadzabe

Baadhi ya wanajamii ya Wahadzabe inayoishi Wilayan Mkalama mkoani Singida.
 
Zaidi  ya Sh. bilioni 1.5 zitatumika kusaidia jamii ya Wahadzabe inayoishi Wilayan Mkalama mkoani Singida ili ibadili maisha yao kutoka kutegemea mizizi, nyama na matunda pori kama chakula chao kikuu hadi kuwa watu wanaojishughulisha na maisha ya kisasa. 
Fedha hizo amabazo zitatokana na vyanzo mbalimbali ikiwamo serikali, wafadhili na wahisani, zitatumika kuhifadhi msitu wao wa asili, kuweka miundombinu ya maji, elimu, barabara, kilimo na ufugaji bora kulingana na mahitaji ya matumizi bora ya ardhi yao.

Kwa mujibu wa Ofisa Maendeleo wa halmashauri hiyo, Patrick Mdachi, mbele ya Baraza la Madiwani, lengo ni kunusuru kabila hilo lisipotee nchini kutokana na malezi yatakayotolewa na asasi itakayoanzishwa na kusimamiwa na Wahadzabe wenyewe.

“Wahadzabe ni kati ya makabila manane mkoani Singida, mengine ni Wanyiramba, Wanyaturu, Wakimbu, Wagogo, Wanyisanzu, Wasukuma na Wataturu (Wabarbaig)... jamii ambayo bado inaishi maisha ya  kizamani (maisha ya ujima), huku chakula chao ni nyama za porini, asali, matunda mwitu na mizizi ya miti,” alisema Mdachi.

Ofisa Maendeleo huyo alisema makabila hayo hasa Wasukuma na Wabarabaig, wamekuwa wakifanya kazi zao za ufugaji kiholela na kufyeka misitu ovyo, hivyo kusababisha wanyamapori kutoweka katika eneo lao la kijiji cha Munguli na kitongoji cha Kipamba.

Mdachi alisema uharibifu wa mazingira unachangiwa pia na baadhi ya viongozi wa vijiji na kata kukubali kupokea `kitu kidogo'  kwa maana ya fedha ili kuruhusu  jamiii ya wafugaji na wakulima kuendelea kuvamia maeneo ya Wahadzabe.

Hata hivyo, baadhi ya madiwani wakiwamo Long’ida Laiser, Hadija Kahola na Philemon Mbogo, walipongeza mpango huo kwa maelezo kuwa  mkakati huo utasaidia na kuimarisha pia sekta ya utalii kutokana na jamii ya Wahadzabe kuwa kivutio kwa wageni wa nje ya nchi.

Aidha, Maugaza Mpanda, ambaye ni Mhadzabe wa kitongoji cha Kipamba katika kijiji cha Munguli, alieleza kufurahisha na mpango huo, lakini akaiomba serikali kuwaondoa kwa nguvu wafugaji wote waliovamia eneo lao ili kurejesha hali halisi ya uoto wa asili kwenye eneo lao la hifadhi.

Kwa mujibu wa Ofisi ya Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Mkalama, hivi sasa Wahadzabe wanafikia 352, lakini ifikapo mwaka 2022 wakati wa sensa ya watu wa  makazi, inakadiriwa jamii hiyo itaongezeka hadi kufikia watu 451.
 
CHANZO: NIPASHE

Wauguzi Kilimatinde walia ukata



index
Na Salesi Malula-Manyoni
 
Wauguzi wa Hospitai ya Kilimatinde wilayani Manyoni Mkoani Singida wako katika hali mbaya kifedha kutokana na kutolipwa mishahara yao kwa muda wa miezi mitatu ambapo hawajui hadi hivi sasa hatma yao itakuwaje.
Katika mahojiano maalum na Fullshangweblog timu ya wauguzi wanaofanyakazi kazi katika Hospitari hiyo inayomilikiwa na Kanisa la Anglicana Dayosisi ya Bonde la Ufa wamesema wanasikitishwa sana na uongozi wa Hospitari hiyo kutowathamini na kuwacheleweshea mishahara huku baadhi ya madaktari wakiwa wamelipwa huku wauguzi tukiwa tunalia njaa kwani miezi mitatu ni mingi wanafikiri tutaishije? Alihoji mmoja wa wauguzi ambaye aliomba jina lake lisiandikwe gazetini kwa kulinda kibarua chake.
Wakieleza zaidi walisema kwakweli hali ni mbaya maisha ni magumu,na hatuna wa kumkimbilia kwani tuna taarifa kuwa baadhi ya Madaktari wenzetu wamelipwa lakini sisi hatuthaminiwi hii si sawa tunamuomba Mkuu wa wilaya ya Manyoni atusaidie tupate haki yetu aingilie kati suala hili kwani tunawakati mgumu sana kimaisha.
Mganga Mkuu wa Hospitari ya kilimatinde Dk. Tittus Uggu akiongea na mwandishi kupitia simu  yake ya Mkononi ya 0763…………… alikiri kuwa tatizo la kuchelewa kwa mishahara lipo na juhudi zinaendelea kwa ajili ya kulitatua kwani kulikua na tatizo la fedha hivyo amekiri pia baadhi ya madaktari kulipwa “niseme tu mwandishi kuna madaktari ambao malipo yao yanatoka serikalini hao wanalipwa moja kwa moja na kuna hao wauguzi ambao wako chini ya hospitari hawa tunawalipa kutokana na vyanzo vya mapato vya hospitalini na nakuhakikishia ndani ya siku hizi mbili au tatu wauguzi wote tutakua tumewalipa ila nikiri kuwa kweli tatizo hilo lipo”.
Habari za Jamii Blog

Maadhimisho kupinga ukeketaji kufanyika Singida

KUKITHIRI kwa vitendo vya ukeketaji kwa watoto wachanga katika Mkoa wa Singida, kumefanya maadhimisho ya kupinga vitendo hivyo kwa mwaka huu kufanyika mkoani humo ili kutoa elimu kwa wananchi.
Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Haki za Binadamu (LHRC), Imelda Urio,  alitoa kauli hiyo jijini Dae es Salaam jana kwa niaba ya Mtandao wa Kupinga Ukeketaji unaojumuisha jumla ya mashirika 12.
Urio alisema maadhimisho hayo yanayotarajiwa kufanyika Februari 6, wanaamini wataweza kufikisha elimu  ya kupinga vitendo hivyo ambavyo vina athari kwa watoto na wanawake.
Kwa mujibu wa mkurugenzi huyo, mtandao ulishajaribu kupambana na vitendo hivyo kwa kuwakagua watoto pindi wanapopelekwa kiliniki, lakini zoezi hilo lilishindikana kutokana na kina mama kuacha kuwapeleka watoto, hivyo kuwanyima haki ya kupata chanjo nyingine zitakazosaidia kulinda afya zao.
Alitaja athari zinazotokana na ukeketaji kuwa ni fistula, kupata shida wakati wa kujifungua, kupata maumivu wakati wa tendo la ndoa na kupata athari za kisaikolojia.
Hata hivyo, kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2012 mikoa inayoongoza kwa vitendo hivyo na asilimia kwenye mabano ni  Manyara (71), Arusha (55) na Mara (40).
Kutokana na hali hiyo, waliitaka serikali kuonyesha utashi wa kisiasa kwa kutekeleza sera na mpango wa kitaifa wa kupinga na kutokomeza ukeketaji kwa kufuatilia utendaji wake ili kutokomeza mila kandamizi.
Kwa upande wa asasi, Urio alitaka ziendelee kupiga kampeni za ushawishi na inapobidi kupitia tena mikakati ili kuleta matukio mazuri na ya kudumu.
Chanzo;Tanzania Daima
 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2011. Singida Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogz za Mikoa