Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Polisi Mkoa wa Singida, wanamshikilia Jafari Hamisi (23),Mkazi
wa Ukombozi mjini Singida,kwa tuhuma ya kumilki kinyume cha sheria
vipande 16 vya meno ya ndovu vyenye thamani ya zaidi ya Sh17milioni.
Meno hayo yamekamatwa ikiwa ni siku nne toka meno
mengine vipande 21 vyenye thamani ya zaidi ya Sh43 milioni,kukamatwa
kwenye eneo lile lile la kizuizi cha mazao kilichopo katika Kijiji cha
Ukimbu kata ya Mgandu Wilaya ya Manyoni.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake
jana,Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida.SSP.Cordula Lyimo,alisema
meno hayo yamekamatwa Feb 16 mwaka huu saa tano usiku katika kizuizi cha
mazao kilichopo Kijiji cha Ukimbu,Kata ya Mgandu Tarafa ya Itigi Wilaya
ya Manyoni.
Alisema askari wakiwa katika kizuizi
hicho,walifanya ukaguzi kwenye gari T.288 AJF aina ya Scania mali ya
Kampuni ya Super Service likiendeshwa na Ally Hamadi,likitokea
Makongorosi Chunya,kuelekea Itigi Wilaya ya Manyoni.
“Baada ya upekuzi huo,walikuta meno hayo yakiwa
yamehifadhiwa ndani ya begi la nguo na kuwekwa kwenye keria za ndani ya
basi.Mtuhumiwa aliweza kupatikana wakati akiwa katika juhudi za kutaka
kutoka ndani ya basi ili akimbie”,alisema Lyimo.
Kaimu kamanda huyo,alisema uchuguzi zaidi
unaendelea ili kubaini au kupata mtandao kamili unaojihusisha na kuwinda
pamoja na kununua nyara hizo.
Chanzo;Mwananchi
Chanzo;Mwananchi
0 comments:
Post a Comment