DIWANI wa Unyambwa  katika Halmashauri ya Manispaa ya Singida, 
Shabani Salumu (CCM), amepandishwa  kizimbani katika Mahakama ya Hakimu 
Mkazi ya mjini Singida, akikabiliwa na  tuhuma za kuwatolea lugha ya 
matusi maofisa wa polisi ikiwemo kudai ni  ‘mizigo’.
  Mbele ya Hakimu Aisha  Mwetindwa, Mwendesha Mashitaka, Chemu Mussa, 
alidai  kuwa Januari 12, mwaka huu, saa 1.30 asubuhi  katika Kijiji cha 
Ijanuka, Kata ya Unyambwa,   mshitakiwa aliwatolea lugha ya matusi 
maofisa wa polisi kitendo  kilichoelekea kusababisha kutoweka au 
kuvunjika kwa amani.
  Alidai tukio hilo  lilitokea wakati maofisa hao wakiwa kazini kwenye 
eneo ambalo wananchi wa Kata  ya Unyambwa walichoma moto basi la Kampuni
 ya Mtei.
  Mshitakiwa alikana tuhuma hizo na yupo nje kwa  dhamana. Kesi itatajwa Februari 25, mwaka huu.
Chanzo;Tanzania  
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
0 comments:
Post a Comment