Mwenyekiti
wa CCM mkoa wa Singida na mwenyekiti wa wenyeviti wa CCM mikoa
nchini,Mgana Msindai, akihutubia wananchi na wana CCM waliohudhuria
maadhimisho ya CCM kutimiza miaka 37 toka kianzishwe.
Mwenyekiti
wa CCM mkoa wa Singida, Mgana Msindai, akimkabidhi kadi mwanachama mpya
aliyejiunga na CCM kwenye maadhimisho ya CCM kutimiza miaka 37 toka
kianzishwe.Maadhimisho hayo halifanyika kimkoa katika kijiji cha
Zigiligi wilayani Iramba.
Mwenyekiti
wa CCM mkoa wa Singida, Mgana Msindai, akipanda mti ikiwa ni sehemu ya
maadhimisho ya CCM kutimiza miaka 37 toka kianzishwe.
Baadhi
ya wana CCM ana wananchi wa wilaya ya Iramba mkoa wa
Singida,waliohudhuria maadhimisho ya CCM kutimiza miaka 37 toka
kianzishwe yaliyofanyika kimkoa katika kijiji cha Zigiligi tarafa ya
Ndago wilaya ya Iramba mkoa wa Singida.(Picha na Nathaniel Limu).
Na Nathaniel Limu, Iramba
MWENYEKITI
wa CCM Mkoa wa Singida,Mgana Msindai amewaagiza wakuu wa Wilaya
kuwakamata na kuwafikisha mahakamani wazazi na walezi wote ambao watoto
wao hawajaripoti katika shule za Sekondari walizopangiwa.
Masindai
ametoa agizo hilo hivi karibuni wakati akizungumza kwenye kilele cha
sherehe za maadhimisho ya CCM kutimiza miaka 37 toka kianzishwe.Sherehe
hizo zilizofana,zilifanyikia katika kijiji cha Zigiligi Wilayani
Iramba.
Amesema kuwa zipo taarifa kwamba baadhi ya wazazi /walezi wanawazuia watoto wao kwenda shule kutokana na sababu mbalimbali.
Akifafanua,amesema
“Ndugu zetu wafugaji wamekuwa mstari wa mbele kuwazuia watoto wao
kwenda shule, ili waweze kuchunga mifugo na wengine, kuwaoza kwa nguvu
watoto wao kike tena wenye umri mdogo” .
Akisisitiza
zaidi, Msindai ambaye pia ni Mwenyekiti wa wenyeviti CCM nchini,amesema
haki za msingi ambazo mtoto anapaswa kuzipata, ni pamoja na elimu.
“Kwa
hiyo, wakuu wa Wilaya nawaomba sana,hakikisheni wanafunzi wote
waliochaguliwa kujiunga na Sekondari, wanajiunga katika shule
walizopangiwa mapema iwezekanyo, hata kama hawana ada”,amesema
mwenyekiti huyo..
Msindai
amesema endapo mwanafunzi hajajiunga na shule aliyopangiwa,ameacha
shule kwa sababu yo yote ili ikiwemo ya ukosefu wa ada, wote
wapelekwe/warudishwe shule na kuanza masomo.
Wakati
huo huo,amesema wazazi na walezi wao wafikishwe mahakamani kujibu
tuhuma ya kushindwa/kuwazuia watoto wao kupata haki yao ya msingi ya
elimu.
Kwa hisani ya Mo Blog
0 comments:
Post a Comment