Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
 WAKAZI wa Mwambani, Kata ya Tangasisi, wilayani Tanga wameelezea 
kutoridhishwa  na fidia waliyolipwa ili kupisha ujenzi wa reli kwenye 
Bandari mpya ya  Mwambani.
  Wakazi hao zaidi  ya 200 wanaoishi kandokando ya bahari wamelipwa sh 
3,400 kwa mita moja ya mraba  wakati viwango vya jiji hilo kwa sasa ni 
sh 7,000 kwa ukubwa huo kitu  kinachowafanya wadai fidia zaidi.
  Kwa sababu hiyo wamemuomba  Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe
 na Waziri wa Nyumba na Maendeleo ya Makazi,  Profesa Anna Tibaijuka, 
kuingilia kati suala hilo kwa kuwa thamani ya pesa  wanayolipwa 
hailingani na mali zao.
Chanzo;Tanzania Daima  
0 comments:
Post a Comment