JESHI la polisi mkoani Singida limekamata vipande 21 vya meno ya Tembo vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 43.
Nyara hizo za serikali zimekamatwa katika kijiji cha Mwamagembe wilayani Manyoni zikisafirishwa kwenda Itigi, mkoani Singida.
Mtu mmoja George James amekamatwa kwa tuhuma za kukutwa na meno hayo
ya tembo yakiwa yamehifadhiwa katika mabegi mawili ya kusafiria.
Mtuhumiwa huyo alikamatwa katika kizuizi cha idara ya maliasili
kilichoko katika kijiji Ukimbu, kata ya Mgandu, wilayani Manyoni akiwa
katika gari aina ya Toyota Hiace lenye namba za usajili T797CQL.
Kamanda wa polisi mkoa wa Singida RPC Geofrey Kamwela (katika video)
amesema vipande hivyo 21 vina thmani ya zaidi ya shilingi milioni 43 na
vyote vimehifadhiwa katika kituo cha polisi wilayani Itigi.
"Meno haya yanaashiria kuuwawa kwa tembo wanne", alisema Kamanda James.
Vitendo vya ujangili wilayani MANYONI vimekuwa vikiongezeka ambapo mwaka
2013 askari mmoja wa jeshi polisi alipoteza maisha katika mapambano na
majangili wilayani humo.
Tukio hili la limekuja wakati leo Rais Jakaya Mrisho Kikwete amehudhuria
mkutano maalumu wa kupambana na ujangili na biashara ya meno ya tembo
na pembe za Faru jijini London, Uingereza.
Katika mkutano huo amependekezWAKATI MKUTANO WA KUPINGA UJANGILI DUNIANI KOTE: GEORGE JAMES AKAMATWA NA MENO 21 YA TEMBO YENYE THAMANI YA TSH MILIONI 43, SINGIDA a kupigwa marufuku biashara hiyo ili kuweza kudhibiti ujangili duniani kote.
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment