Akizungumza na uongozi wa kampuni ya CHICO (hawapo pichani), Magufuli aliwataka kutekeleza mradi huo kwa kuzingatia makubaliano
 John Magufuli akizungumza na wafanyakazi wa kampuni ya CHICO
 Magufuli akikagua barabara inayokarabatiwa na kampuni ya CHICO kutoka nchini China baada ya kujenga chini ya kiwango mwaka 2008
 Meneja TANROADS mkoa Singida Yustak Kangole akitoa taarifa ya marudio ya ujenzi wa barabara Sekenke-Shelui, km 33.3, kwa waziri
Singida.   Oktoba09,2012.   Makandarasi..... WIZARA  ya Ujenzi imewakumbusha Wakandarasi nchini kujenga barabara  zinazolingana na thamani ya fedha, iliyopo kwenye mikataba yao.   Agizo  hilo limetolewa leo mkoani Singida na Waziri John Magufuli, wakati  anakagua marudio ya ujenzi wa barabara, eneo la mlima Sekenke-Shelui,  yenye urefu wa kilomita 33.3.   Amesema  serikali imetumia zaidi ya Sh.Bilioni 35, kugharamia ujenzi huo, lakini  mkandarasi China Henan International Cooparation Group Co Ltd(CHICO),  ilijenga chini ya kiwango.   Aidha ameuagiza  uongozi wa kampuni hiyo kuwapatia wafanyakazi wake vifaa vya kufanyia  kazi, hasa viatu na gloves kwa ajili ya kuvaa mikononi.  Hata  hivyo meneja TANROADS Mkoa Singida, Yustak Kangole amesema barabara  hiyo baada ya kukamilika Januari, 2008, ilichukua miezi miwili kuanza  kubomoka, kutokana na ujenzi hafifu.    Kwa  mujibu wa meneja mradi wa barabara hiyo, mhandisi Stone Chen, marudio  ya ujenzi yanaigharimu kampuni zaidi ya S h.Bilioni kumi.  Na Elisante John     | 
,+Magufuli+aliwataka+kutekeleza+mradi+huo+kwa+kuzingatia+makubaliano.jpg)




0 comments:
Post a Comment