na Jumbe Ismaily, Singida
MTANDAO
wa asasi za kiraia wilaya ya Singida vijijini (SIRUNGONET) umetangaza kuanza
kuendesha midahalo ya mikakati ya kupunguza umaskini na kuongeza kipato kwa
jamii kwenye jimbo la Singida Kaskazini, Singida Magharibi na Singida
Mashariki.
Mratibu
wa Sirungonet wilayani hapa, Sombi Sombi, alisema jana kuwa leo wataanza
mdahalo katika kijiji cha Itaja, tarafa ya Mgori.
Alisema
Oktoba 23, wataendesha mdahalao kijiji cha Puma, kilichoko jimbo la Singida
Magharibi kuanzia saa tatu asubuhi ambapo wananchi watapata fursa ya kutoa
maoni yao wakati saa sita mchana wananchi wa kijiji cha Dung’unyi katika jimbo
la Singida Magharibi watapa nafasi ya kutoa maoni yao pia.
Aidha,
mratibu huyo alisema lengo la midahalo hiyo ni kuimarisha mahusiano kati ya
wananchi na wabunge au wawakilishi wao.
“Midahalo
hii inalenga kutoa fursa ya majadiliano kati ya wabunge, madiwani na watendaji
wa serikali ili kuimarisha ari ya ushiriki na ushirikishwaji wa wananchi katika
kupanga na kutekeleza mipango ya maendeleo,” alisema.
Chanzo: Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment