Maafisa wa mfuko wa taifa wa biwa ya afya (NHIF) wakiwa ofisini kwao katika majengo ya chuo cha VETA mjini Singida,Kulia ni afisa msimamizi wa ofisi ya mkoa wa Singida na kushoto ni afisa matekelezo Isaya Sheikifu.(Picha na Nathaniel Limu).
Nathaniel Limu.
Madiwani wa halmashauri ya wilaya na manispaa ya Singida, wamehimizwa kuongeza kasi ya kuhamasisha wananchi kujiunga na mfuko wa afya ya jamii (CHF), ili waweze kujijengea mazingira mazuri ya kupata tiba hasa kipindi hali zao kiuchumi zinapokuwa sio nzuri.
Wito huo umetolewa na Afisa Matekelezo wa mfuko wa taifa wa bima ya afya (NHIF) mkoani Singida Isaya Sheikifu wakati akizungumza kwenye kikao cha baraza la madiwani halmashauri ya wilaya ya Singida.
Amesema kutokana na kweli kwamba wananchi wengi hawawezi kuwa na fedha za matumizi mbali mbali yakiwemo ya matibabu wakati wote, njia pekee ya kuwa na uhakika wa matibabu ni pindi akiujua na mfuko wa afya ya jamii.
Sheikifu amesema ili kaya iweze kujiunga na mfuko huo, inapaswa kulipa shilingi 5,000 tu, halafu baba, mke na watoto wanne walio chini ya umri wa miaka 18, wote watatibiwa mwaka mzima bila kutoa gharama nyingine tena.
Katika hatua nyingine, Afisa huyo pia amewahamasisha madiwani kujiunga na mfuko wa taifa wa bima ya afya (NHIF), ili pamoja na mambo mengine, waweze kupata fursa ya kutibiwa hata wanapokuwa nje ya mkoa.
0 comments:
Post a Comment