Kamanda wa polisi mkoa wa Singida Linus Sinzumwa akitoa taarifa kwa waandishi wa habari (hawapo kwenye picha) ya ajali iliyoua mchungaji wa kanisa la Pentekoste.
(Picha na Nathaniel Limu).
(Picha na Nathaniel Limu).
Na Nathaniel Limu.
Mtu mmoja amekufa papo hapo na wengine wanne kujeruhiwa sehemu mbalimbali za miili yao baada ya gari waliyokuwa wakisafiria kuacha njia kisha kupinduka mkoani Singida.
Kamanda wa polisi mkoa wa Singida Kamishina msaidizi Linus Sinzumwa, amesema ajali hiyo imetokea majira ya saa tano usiku katika eneo la mzunguko mjini Manyoni barabara kuu ya Dodoma-Mwanza.
Amesema wakati wa tukio hilo wachungaji wa kanisa la Pentekosti walikuwa wakisafiri kwa gari ndogo aina ya Land Cruiser yenye namba za usajili T.531 EAT wakitokea Mwanza kwenye mkutano wa injili, kurejea Dodoma.
Hata hivyo, amesema kutokana na kile kinachosadikiwa kuwa mwendo kasi baada ya kufika eneo la mzunguko Manyoni, dereva wa gari hiyo alishindwa kuilmudu kabla ya kuacha njia na kupunduka.
Kamanda Sinzumwa amesema hali hiyo ilisababisha kifo cha mchungaji Jackson Husena (58) papo hapo huku wachungaji wengine Jonas Chungu, Pasian Chiwanda na Stephano Ulaya, wakijeruhiwa.
0 comments:
Post a Comment