Msichana
 Jackline Lasway akiwa amelazwa katika wodi ya kina mama namba mbili 
katika hospitali ya Mkoa wa Singida baada ya kujeruhiwa kwa kumwagiwa 
uji wa moto wakati akiwa dukani kwa bosi wake eneo la soko kuu Manispaa 
ya Singida.
Na Mwandishi Wetu , Singida.
Msichana
 mmoja mkazi wa eneo la Minga Manispaa ya Singida amenusurika kifo baada
 ya kumwagiwa uji wa moto na mke wa tajiri wake wa dukani  kutokana na 
kile kinachosadikiwa kuwa ni wivu wa kimapenzi.
Msichana
 huyo Jackline Lasway maarufu kwa jina la Pendo amelazwa wodi namba 
mbili katika hospitali ya Mkoa wa Singida, huku akiwa na majeraha ya 
moto  sehemu ya sikio la upande wa kulia na mgongoni.
Akizungumza
 kwa taabu katika wodi hiyo, Pendo alisema kuwa tukio hilo limetokea 
juzi mchana wakati akiwa dukani kwa bosi wake aliyemtaja kwa jina la 
Charles Kamnde “Frarucha”.
Alisema
 akiwa anaendelea na kazi yake ya kuuza bidhaa mbalimbali dukani hapo 
gafla alitokea mke wa bosi wake akiwa na chupa yenye uji wa moto na 
kumtaka kumwagia usoni.
Hili ni jeraha ambalo Jackline ameumia.
Alisema
 aligeuka ili uji ule usimwagikie usoni na ndipo ulimuunguza sikio la 
kulia na mgongoni ambapo baada ya mke wa bosi wake kumkosa uso alitoa 
kisu kutaka kumchoma kifuani.
“Mimi
 sikua na ugomvi nae wala sijui chanzo cha yeye kufika dukani na kufanya
 hili tukio, maana kama ni kazi mi nafanya kulingana na maelekezo kutoka
 kwa bosi wangu Chale.” Alisema.
Alisema
 katika kurupushani za kujiokoa asichomwe kisu hicho alifanikiwa 
kumkamata mkono mwanamke huo na kupiga kelele ambapo watu walifika na 
kumwokoa.
Hata
 hivyo alisema alichukuliwa na bosi wake hadi kituo cha polisi mjini 
Singida na kupewa PF 3 kwa ajili ya matibabu na kuletwa katika hospitali
 hiyo ambako amelazwa huku akiwa na majeraha makubwa mgongoni.
Waandishi wa habari wakimchukua maelezo msichana huyo.
Muuguzi
 wa zamu katika wodi namba mbili ya wanawake, Anna Sprian alisema hali 
ya mgonjwa huyo inaendelea vizuri, na anaendelea kupatiwa matibabu ya 
majeraha ya moto aliyopata.
Kwa
 upande wake mmiliki wa duka hilo Chale Kamnde ‘Frarucha’ alikiri 
kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa hayuko tayari kulizungumzia kwani 
maelezo aliyotoa binti huyo yanajitosheleza.
Baadhi
 wa kinamama waliohojiwa kuhusiana na tukio hilo wameonesha masikitiko 
yao kutokana na hatua ya mwanamke huyo kumwagia uji msichana huyo.
Msichana Jackline akilia wakati akiwaonesha waandishi wa habari jeraha alilomwagiwa uji na mke wa bosi wake.
Amina
 Ramadhani alisema hicho ni kitendo cha kinyama kwa binti mdogo kama 
huyo na kwamba kama aliona kuna mahusiano ya kimapenzi na mumewe 
angetumia busara na kumwondoa dukani na sio kumuunguza kwa uji wa moto.
Veronika
 Masawe alisema amesikitishwa na tukio hilo na kusema kuwa hakiendani na
 haki za binadamu kwa kuwa ni kumdhalilisha msichana huyo ambaye alikuwa
 akifanya kazi kwa ajili ya kujipatia kipato.
Kamanda
 wa polisi Mkoani Singida, Geofrey Kamwela amethibitisha kutokea kwa 
tukio hilo na kwamba wanamshikilia mtuhumiwa kwa mahojiano baada ya 
upelelezi kukamilika atafikishwa mahakamani.
Muuguzi wa zamu katika wodi namba mbili Anna Sprian akizelelezea maendeleo ya Jackline.
Hawa ni majirani waliofika kumjulia hali majeruhi Jackline katika hospitali ya mkoa wakihojiwa na waandishi wa habari.
Jack akiwa wodini kabla ya kuzungumza na vyombo vya habari.
Kibao cha hospitali ya mkoa wa Singida.
Kibao cha wodi namba mbili hospitali ya mkoa wa Singida.(PICHA ZOTE NA KAMERA YA MOblog SINGIDA).
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
0 comments:
Post a Comment