Katibu wa CCM Mkoa wa Singida
Naomi Kapambala aaizungumza na waanndishi wa habari juu ya ufafanuzi wa
maendeleo ya ujenzi wa uwanja huo.
Na Hillary Shoo, Singida
Mbunge wa Jimbo la Singida mjini
(CCM), Mohammed Dewji ameulalamikia uongozi wa Chama chake Mkoa wa
Singida kwa kitendo cha kuchelewesha mchakato wa kumalizia ujenzi wa
Uwanja wa michezo Namfua ikiwa ni moja ya ahadi zake alizotoa kwa
wananchi wakati wa Uchaguzi Mkuu mwaka 2010.
Kuchelewa huko kuanza kwa mchakato
wa ukarabati na uwekaji wa nyasi za bandia kwenye uwanja huo imeelezwa
ni kutokana na urasimu na maslahi binafsi miongozi mwa viongozi wa CCM
Mkoa wa Singida.
Katika barua yake ya Julai 31 mwaka
huu kwa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, Dewji amedai kuwa kwa
kiasi kikubwa ameweza kutekeleza Ilani ya Uchaguzi kwa vipindi vyote
viwili pamoja na ahadi zake binafsi, isipokuwa ahadi ya kumalizia ujenzi
wa michezo Namfua.
Katika barua hiyo, ambayo pia
ameinakili kwa Rais Jakaya Kikwete, Katibu Baraza la wadhamini CCM
Taifa, Katibu wa Uchumi na Fedha na Katibu wa CCM mkoa wa Singida, Dewji
amedai kuwa kila alipotaka kufanya hivyo alipata vikwazo kutoka kwa
viongozi wa CCM mkoa wa Singida.
Katikati ya kiwanja chenyewe.
Amesema kuwa matayarisho yote muhimu
kuhusiana na ujenzi huo yapo tayari, ikiwa ni pamoja na kuwepo dola za
kimarekani 880,000 (sawa na sh bilioni 1.46) ambazo kwa kushirikiana na
Rais Kikwete aliweza kuzipata kutoka Makampuni ya Airtel Tanzania na
Mohammed Ent (T) Ltd.
Dewji amesema wakati wa kampeni za
uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 yeye pamoja na Raisi Jakaya Kikwete walitoa
ahadi ya kukarabati na kuweka nyasi za bandia
kwenye uwanja huo unaomilikiwa na chama cha mapinduzi CCM.
Hili ni jukwaa kuu la uwanja wa Namfua unaomilikiwa na CCM Mkoa wa Singida.
“Baada ya uchaguzi sote wawili
tulishinda na sasa tunatumikia wananchi, na kwa kiasi kikubwa
tumefanikiwa kutekeleza ilani ya uchaguzi kwa vipindi vyote viwili,
pamoja na ahadi zetu binafsi, lakini ahadi tuliyotoa ya ukarabati wa
uwanja mpaka sasa hatujafanikiwa kuitekeleza. Alisem MO na kuongeza
Dewji amesema anasikitishwa na
uongozi wa CCM Mkoa wa Singida bila sababu za msingi wanachelewesha
kuanza kwa mchakato wa ukarabati wa uwanja huo.
Aidha amesema kuna vikao vingi
viimefanyika na makampuni hayo bila mafanikio na hivyo anaomba CCM Makao
makuu kuingilia kati ili kama kuna jambo linasababisha kusuasua kwa
mchakato huo liweze kupatiwa ifumbuzi na ukarabati ufanyike haraka
iwezekanavyo.
Vijana wakicheza mpira uwanjani humo.
Amesema suala la uchakavu wa uwanja
wa Namfua imekuwa ni kero kubwa inayowakabili wananchi wa jimbo la
singida mjini kwa sasa na hivyo kuwanyima vijana fursa za kutumia uwanja
huo ili kupata ajira na kukuza vipaji kwa vijana.
Kutokana na ukweli kwamba muda wa
kuelekea Uchaguzi Mkuu 2015 unayoyoma, Dewji maarufu kwa jina la "MO"
amemwomba Katibu Mkuu wa CCM kuingilia kati urasimu huo usio wa lazima
ili ujenzi uweze kufanyika mapema.
Akizungumzia madai hayo ya Mbunge
Dewji, Katibu wa CCM Mkoa wa Singida, Naomi Kapambala alikiri kupata
nakala ya barua hiyo na kusema kuwa wamefanya matayarisho yote muhimu
ikiwa ni pamoja na kufuatilia Airtel makao makuu juu ya suala hilo.
Aidha Kapambala amesema kuwa kamati
ya siasa imemaliza kazi na kupeleka baraza la wadhamini, na
kinachosubiriwa na baraza kukaa ili kutoka majibu.
“Mi namshangaa ni kwa nini yeye
mwenyewe Dewji hajafika hapa ofisini na kupata ufafanuzi juu ya hili
matokeo yake analeta nakala ya barua kwetu, akamwulize katibu Mkuu
ambaye amemwandikia hii barua.” Alisema Kapambala
Hata wakati katibu mkuu alipokuja
hapa tulimweleza juu ya hilo , yeye kama anaonaje ni vyema akafika
ofisini ili kujua inachoendelea.
Sehemu ya jukwaa la uwanja wa Namfua linalotumiwa na washabiki likiwa linaonekana kuchakaa.
Aidha Kapambala amesema Katibu mkuu
msaidizi yuko jijini Dar es Salaam ambapo pamoja na mambo mengine
wamemwagiza kupitia baraza la wadhamini wa CCM ili kujua hatma ya suala
hilo.
Pia Kapambala amesema pia ofisi yake
imekwishatoa notisi kwa wafanyabiashara mbalimbali kuondoka kwenye eneo
la uwanja ili kupisha ukarabati huo.
Mwenyekiti wa SIREFA Baltazari
Kimario alisema anasikitishwa kuona maendeleo ya uwanja huo bado
haujakamilika na hivyo kuathiri maendeleo ya soka katika mkoa wa
singida.
Aidha wadau mbalimbali nao wametoa
masikitiko yao kwa uongozi wa CCM Mkoa wa singida kuchelewesha mchakato
huo kwa maslahi binafsi, huku Mbunge akiwa tayari kushughulikia kero
hiyo.
Uwanja huo hivi sasa umebaki kuwa
kama eneo maarufu la vijana kuvuta bangi na wengine kujisaidia hovyo
kwenye vyoo na hivyo kutapakaa kwa vinyesi kila mahali ndani ya uwanja
huo.
Ujenzi wa Uwanja wa Namfua,ambao
ulikuwa ukienda sambamba na Jengo la CCM mkoa, ulisimama miaka ya 1990
na tangu wakati huo uwanja huo umebakia gofu na kugeuka maficho ya
wahalifu mbalimbali na eneo la choo cha jumuiya.
Baadhi ya Waandishi wa habari wa Mkoa wa Singida wakipiga picha jengo la makao makuu ya CCM Mkoa wa Singida.
Vijana hawa walikutwa wakivuta bangi kwenye majukwaa ya uwanja wa Namfua.
Hapa ndio makao makuu ya CCM Mkoa wa Singida.(Picha zote na Hillary Shoo).
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment