RAIS DKT. MAGUFULI PAMOJA NA MKEWE MAMA JANETH WASHIRIKI IBADA YA KRISMASI KATIKA KANISA KATOLIKI (KANISA KUU LA MOYO MTAKATIFU WA YESU) MKOANI SINGIDA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mke wake Mama Janeth Magufuli wakiwa katika Misa ya Krismasi katika Kanisa Kuu la Moyo Mtakatifu wa Yesu mkoani Singida.
Hapa wakiwa katika sala.
Rais Magufuli na mkewe wakisilkiliza neno

Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiwasalimia waumini wa Kanisa Kuu la Moyo Mtakatifu wa Yesu mkoani Singida mara baada ya kushiriki Misa ya Krismasi katika kanisa hilo mkoani Singida

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia waumini wa Kanisa Kuu la Moyo Mtakatifu wa Yesu mkoani Singida mara baada ya kushiriki Misa ya Krismasi katika kanisa hilo mkoani Singida.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Baba Askofu wa Jimbo la Singida Askofu Edward Mapunda mara baada ya Ibada ya Krismasi katika Kanisa Kuu la Moyo Mtakatifu wa Yesu mkoani Singida.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Baba Askofu wa Jimbo la Singida Askofu Edward Mapunda mara baada ya Ibada ya Krismasi katika Kanisa Kuu la Moyo Mtakatifu wa Yesu mkoani Singida.

Baba Askofu wa Jimbo la Singida Askofu Edward Mapunda akimuombea na kumbariki Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya Ibada ya Krismasi katika Kanisa Kuu la Moyo Mtakatifu wa Yesu mkoani Singida.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mkewe Mama Janeth Magufuli wakisalimiana na waumini wa Kanisa Kuu la Moyo Mtakatifu wa Yesu mkoani Singida mara baada ya ibada ya Krismasi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mkewe Mama Janeth Magufuli wakipunga mkono wakati wakitoka kwenye Kanisa Kuu la Moyo Mtakatifu wa Yesu mkoani Singida. PICHA NA IKULU

RC NCHIMBI ALIPONGEZA SHIRIKA LA NYUMBA; AZUNGUMZA NA WATUMISHI MANYONI NA KUWAKUMBUSHA MAADILI YA UTUMISHI WA UMMA.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 



WAZIRI MKUU ATEMBELEA KIWANDA KIKUBWA CHA KUZALISHA MAFUTA YA ALIZETI MKOANI SINGIDA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Mkurugenzi Mtendaji (Group Excutive Director) kampuni ya Mount Meru Millers, Atul Mittal (kushoto) akimwonyesha Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mashudu ya alizeti yanayonunuliwa na kampuni ya Mount Meru tawi la Singida na kusangwa upya na kutoa mafuta ya kutosha.

RC MTIGUMWE AONGOZA WAOMBOLEZAJI KUAGA MWILI WA ALIYEKUWA KAMANDA WA POLISI MKOA WA SINGIDA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.


Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew John Mtigumwe akitoa heshima zake za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Kamanda wa jeshi la polisi Mkoa wa Singida SSP Peter Charles Kakamba, baada ya mwili kuagwa Mhandisi Mtigumwe amewaongoza msafara wa waombolezaji kuelekea Mkoani Katavi, kijiji cha Kawajese kwa ajili ya mazishi. Kamanda Kakamba amefariki usiku wa kuamkia jana katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili wakati akipatiwa matibabu.(Picha na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida)

Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida Dkt. Angelina Mageni Lutambi akitoa heshima zake za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa kamanda wa jeshi la polisi Mkoa wa Singida SSP Peter Kakamba aliyefariki usiku wa kuamkia jana hospitali ya taifa ya Muhimbili. Kakamba amefariki dunia baada ya kuugua maradhi ya tumbo. Mwili huo umesafirishwa kwenda kijiji cha Kowajese Mkoani Katavi kwa ajili ya mazishi.
 

Askari polisi Mkoani Singida wakitoa heshima zao za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Kamanda wa jeshi la polisi Mkoa wa Singida SSP Peter Kakamba aliyefariki usiku wa kuamkia jana hospitali ya taifa ya Muhimbili. Kakamba amefariki dunia baada ya kuugua maradhi ya tumbo. Mwili huo umesafirishwa kwenda kijiji cha Kowajese Mkoani Katavi kwa ajili ya mazishi.

Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa kamanda jeshi la polisi Mkoa wa Singida SSP Peter Kakamba ukitolewa kwenye nyumba aliyokuwa akiishi maeneo ya VETA mjini hapa kwa ajili ya kuagwa na viongozi mbalimbali na wananchi wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew John Mtigumwe. Baada ya kuagwa kwa mwili huo umesafirishwa hadi kijiji cha Kawajese Mkoani Katavi kwa ajili ya mazishi. 
Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Kamanda jeshi la polisi Mkoa wa Singida SSP Peter Kakamba ukitolewa kwenye basi dogo lililobeba mwili huo kutoka hospitali ya taifa Muhimbili jijini Dar-es-salaam. Mwili huo umefikishwa kwenye nyumba aliyokuwa akiishi mjini Singida kwa ajili ya kuagwa leo (01/12/2016).  
Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida Dkt. Angelina Mageni Lutambi akiwashukuru wananchi waliojitokeza kwa wigni kuungana na familia kwa ajili ya kuaga mwili wa aliyekuwa kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida SSP Peter Charles Kakamba, Dkt Lutambi amesema Ofisi ya Mkuu wa Mkoa iko pamoja na wafiwa na watashiriki mazishi kijiji cha Kowajese Mkoani wa Katavi.

 Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida SSP Mayalla Towo akiwashukuru wananchi, taasisi na mashirika mbalimbali walioshiriki msiba huo, Towo amesema marehemu alikuwa kiongozi bora aliyependa kuwafundisha na kuwaelekeza ujuzi na maarifa aliyonayo watumishi walio chini yake.

Wananchi waliojitokeza wakiaga mwili wa aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida SSP Peter Charles Kakamba.
  
Na Mathias Canal

Mwili wa Aliyekuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Singida, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) EX Peter Kakamba umeagwa na wamia ya wakazi wa Mkoa wa Singida wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo Injinia Methew Mtigumwe.

Kakamba alifariki dunia alfajiri ya tarehe 30/11/2016 katika hospital ya taifa Muhimbili alipokuwa akipatiwa matibabu.

Kakamba alizaliwa mwaka 1963 katika kijiji cha Kawajense Wilayani Mpanda, mkoa wa Katavi. Alisoma shule ya msingi Shanwe Kawajense  mwaka 1973 hadi 1980, Kidato cha kwanza hadi cha nne katika shule ya Sekondari Kantalamba mwaka 1981 hadi 1984 ambapo kidato cha tano na sita alisoma katika shule ya Sekondari Umbwe mkoani Kilimanjaro mwaka 1985 hadi 1987. Mwaka 1992 hadi 1994 alisoma Astashahada ya Sheria katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Marehemu alijiunga na Jeshi la Polisi mwaka 1988 ambapo katika utumishi wake alipandishwa vyeo mbalimbali ikiwemo Konstable wa Polisi (1989), Sagenti wa Polisi (1991), Mkaguzi Msaidizi wa Polisi (1997), Mkaguzi wa Polisi (2003), Mrakibu Msaidizi wa Polisi (2006), Mrakibu wa Polisi (2008), Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (2011), Kamishna Msaidizi wa Polisi (2015) na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (2016).
 
Baadhi ya nafasi alizowahi kushika ni pamoja na kuwa  Mwendesha Mashtaka wa Polisi katika mkoa wa Iringa, Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Mufindi, Afisa mnadhimu wa Polisi katika Mikoa ya Iringa na Geita, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa na mpaka anafariki alikuwa Kamanda wa Polisi katika mkoa wa Singida.
 
Kufuatia kifo hicho Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu anatoa pole kwa Maofisa, Wakaguzi,Askari, ndugu, jamaa na marafiki kwa Msiba huo.
Bwana alitoa na Bwana ametwaa,
Jina la Bwana lihimidiwe - Amen.    
KAWAIDA...! RC MTIGUMWE AONGOZA WAOMBOLEZAJI KUAGA MWILI WA ALIYEKUWA KAMANDA WA POLISI MKOA WA SINGIDA Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew John Mtigumwe akitoa heshima zake za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Kamanda wa jeshi la polisi Mkoa wa Singida SSP Peter Charles Kakamba, baada ya mwili kuagwa Mhandisi Mtigumwe amewaongoza msafara wa waombolezaji kuelekea Mkoani Katavi, kijiji cha Kawajese kwa ajili ya mazishi. Kamanda Kakamba amefariki usiku wa kuamkia jana katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili wakati akipatiwa matibabu.(Picha na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida) Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida Dkt. Angelina Mageni Lutambi akitoa heshima zake za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa kamanda wa jeshi la polisi Mkoa wa Singida SSP Peter Kakamba aliyefariki usiku wa kuamkia jana hospitali ya taifa ya Muhimbili. Kakamba amefariki dunia baada ya kuugua maradhi ya tumbo. Mwili huo umesafirishwa kwenda kijiji cha Kowajese Mkoani Katavi kwa ajili ya mazishi. Askari polisi Mkoani Singida wakitoa heshima zao za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Kamanda wa jeshi la polisi Mkoa wa Singida SSP Peter Kakamba aliyefariki usiku wa kuamkia jana hospitali ya taifa ya Muhimbili. Kakamba amefariki dunia baada ya kuugua maradhi ya tumbo. Mwili huo umesafirishwa kwenda kijiji cha Kowajese Mkoani Katavi kwa ajili ya mazishi. Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa kamanda jeshi la polisi Mkoa wa Singida SSP Peter Kakamba ukitolewa kwenye nyumba aliyokuwa akiishi maeneo ya VETA mjini hapa kwa ajili ya kuagwa na viongozi mbalimbali na wananchi wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew John Mtigumwe. Baada ya kuagwa kwa mwili huo umesafirishwa hadi kijiji cha Kawajese Mkoani Katavi kwa ajili ya mazishi. Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Kamanda jeshi la polisi Mkoa wa Singida SSP Peter Kakamba ukitolewa kwenye basi dogo lililobeba mwili huo kutoka hospitali ya taifa Muhimbili jijini Dar-es-salaam. Mwili huo umefikishwa kwenye nyumba aliyokuwa akiishi mjini Singida kwa ajili ya kuagwa leo (01/12/2016). Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida Dkt. Angelina Mageni Lutambi akiwashukuru wananchi waliojitokeza kwa wigni kuungana na familia kwa ajili ya kuaga mwili wa aliyekuwa kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida SSP Peter Charles Kakamba, Dkt Lutambi amesema Ofisi ya Mkuu wa Mkoa iko pamoja na wafiwa na watashiriki mazishi kijiji cha Kowajese Mkoani wa Katavi. Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida SSP Mayalla Towo akiwashukuru wananchi, taasisi na mashirika mbalimbali walioshiriki msiba huo, Towo amesema marehemu alikuwa kiongozi bora aliyependa kuwafundisha na kuwaelekeza ujuzi na maarifa aliyonayo watumishi walio chini yake. Wananchi waliojitokeza wakiaga mwili wa aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida SSP Peter Charles Kakamba. Na Mathias Canal Mwili wa Aliyekuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Singida, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) EX Peter Kakamba umeagwa na wamia ya wakazi wa Mkoa wa Singida wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo Injinia Methew Mtigumwe. Kakamba alifariki dunia alfajiri ya tarehe 30/11/2016 katika hospital ya taifa Muhimbili alipokuwa akipatiwa matibabu. Kakamba alizaliwa mwaka 1963 katika kijiji cha Kawajense Wilayani Mpanda, mkoa wa Katavi. Alisoma shule ya msingi Shanwe Kawajense mwaka 1973 hadi 1980, Kidato cha kwanza hadi cha nne katika shule ya Sekondari Kantalamba mwaka 1981 hadi 1984 ambapo kidato cha tano na sita alisoma katika shule ya Sekondari Umbwe mkoani Kilimanjaro mwaka 1985 hadi 1987. Mwaka 1992 hadi 1994 alisoma Astashahada ya Sheria katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Marehemu alijiunga na Jeshi la Polisi mwaka 1988 ambapo katika utumishi wake alipandishwa vyeo mbalimbali ikiwemo Konstable wa Polisi (1989), Sagenti wa Polisi (1991), Mkaguzi Msaidizi wa Polisi (1997), Mkaguzi wa Polisi (2003), Mrakibu Msaidizi wa Polisi (2006), Mrakibu wa Polisi (2008), Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (2011), Kamishna Msaidizi wa Polisi (2015) na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (2016). Baadhi ya nafasi alizowahi kushika ni pamoja na kuwa Mwendesha Mashtaka wa Polisi katika mkoa wa Iringa, Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Mufindi, Afisa mnadhimu wa Polisi katika Mikoa ya Iringa na Geita, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa na mpaka anafariki alikuwa Kamanda wa Polisi katika mkoa wa Singida. Kufuatia kifo hicho Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu anatoa pole kwa Maofisa, Wakaguzi,Askari, ndugu, jamaa na marafiki kwa Msiba huo. Bwana alitoa na Bwana ametwaa, Jina la Bwana lihimidiwe - Amen.

UFAULU DARASA LA SABA WAPANDA MKOA WA SINGIDA; ELFU KUMI NA NNE KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA 2017.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Kiwango cha ufaulu wa mitihani ya kumaliza elimu ya msingi Mkoani Singida kimepanda kutoka wastani wa asilimia 58.41 mpaka asilimia 69.25 ikiwa ni ongezeko la asilimia 11 huku wanafunzi 14,759 wakichaguliwa kujiunga na masomo ya sekondari kwa kidato cha kwanza kwa mwaka 2017.

Buhacha Baltazar Kichinda akiongoza kikao cha uteuzi wa wanafunzi wa kidato cha kwanza kwa mwaka 2017 kama Kaimu Katibu Tawala Mkoa na mwenyekiti wa kikao hicho amesema mkoa umefaulisha wavulana 6,852 na wasichana7,907 huku akiwapongeza waalimu wote kwa bidii ya ufundishaji iliyopelekea mkoa wa singida kushika nafasi ya 12 kati ya Mikao 26 ya tanzania bara.

Kichinda ameipongeza halmashauri ya Itigi kwa kushika nafasi ya kwanza kati ya halmasahuri saba za mkoa wa singida na ya 38 kitaifa kati ya halmashauri 186 za Tanzania bara huku ikifaulisha kwa asilimia 80.41. Aidha amewatia moyo halmasahuri ya Mkalama kwa ufaulu hafifu wa 57.51 na kuwa nafasi ya 155  kitaifa.

Kichinda ameongeza kuwa kwa sasa kila Mkurugenzi wa halmasahuri anapaswa kukaa na wadau wake wa elimu ili kupanga mikakati ya kuboresha zaidi elimu, amesema lengo kubwa kwa sasa ni kuhakikisha kila mwanafunzi aliyefaulu anajiunga na kidato cha kwanza na kumaliza elimu ya sekondari.

Amesema sekta ya elimu inachangamoto mbalimbali ikiwemo utoro wa walimu na wananfunzi, miundombinu ya vyumba vya madarasa kutotosheleza mahitaji halisi, upungufu wa waalimu, uhaba wa nyumba za walimu pamoja na waalimu wenyewe kuwa wachache tofauti na mahitaji halisi hivyo amewata wadau wa elimu kujipanga kutatua changamoto hizo na sio kusubiria serikali kuu kufanya kila kitu.

Aidha kichinda amesema kuwepo na utaratibu wa kuwapongeza waalimu hasa kwenye shule zilizofanya vizuri ili iwe motisha kwa kazi wanayoifanya huku akiitangaza shule ya msingi Utaho ya halmasahuri ya Ikungi kuwa ya kwanza kimkoa kwa shule zenye wananfunzi zaidi ya 40 na shule ya msingi Aghondi ya Itigi kuwa ya kwanza kimkoa kwa shule ambazo zina wanafunzi chini ya 40.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Singida Elias Tarimo amesema ili kuboresha elimu mkoani Singida msisitizo uwepo wa kuhakikisha wananfunzi wote wanapata chakula shuleni ili waweze kusikiliza kwa umakini mzuri.

Tarimo ameongeza kuwa wazazi wanapaswa kutambua kuwa elimu bila malipo haiwaondolei wajibu wao kama wazazi wa kuhakikisha wanafunzi wanakula, wanalala na kuvaa hivyo hivyo watakaposhirikishwa katika kuchangia chakula, ujenzi wa mabweni au shuguli za elimu wajitoe kwani wamiliki wa shule ni wazazi.

Amesema utaratibu wa kufanya ukaguzi ili kuwatambua waalimu watoro au wazembe ufanyike katika halmashauri zote na kwa viongozi wote wanaotembelea vijijini bila ya kusubiri ziara maalumu ya ukaguzi na kuongeza kuwa hali hiyo itawaongezea umakini waalimu katika kutekeleza majukumu yao lakini pia watendaji watabaini changamoto za waalimu na shule na kuzitatua kwa uharaka.

RC SINGIDA AHIMIZA WATUMISHI KUWAJIBIKA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mkuu wa mkoa wa Singida Mhandisi Mathew Mtigumwe, amewahimiza watumishi wa umma hasa wa ngazi ya Vijiji na Kata kuwajibika  na kutimiza vyema majukumu yao kwani wao wako karibu zaidi na Wananchi, ili kutimiza adhma ya Serikali ya awamu ya tano ya kumpunguzia kama si kumuondolea kabisa kero zinazozuilika Mwananchi wa kawaida.

WANANCHI WA KITARAKA SINGIDA WAOMBA MAENEO YA UKULIMA NA UFUGAJI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399

Wananchi wa Kata ya Kitaraka iliyopo katika Halmashauri ya Itigi, Wilaya ya Manyoni, Mkoani Singida, wamemuomba Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mh. William Ole Nasha, kuwapatia shamba linalomilikiwa na Serikali la Tanganyika Packers, ambalo Serikali imeacha kulitumia kwa zaidi ya miaka 20, ili walitumie kwa shughuli za Kilimo na Ufugaji.

Wananchi hao wamefikisha maombi hayo kwa Mh. Waziri alipotembelea shamba hilo lenye ukubwa wa ekari 45,000, na kuzungumza na Wananchi wa Kata hiyo waliolalamika kuwa hawana eneo la kulima wala kufuga ilihali shamba hilo halitumiki na linafaa kwa shughuli hizo.

Nae Mh. Waziri akizungumza na Wananchi hao amesema Serikali ya awamu ya tano ni Serikali inayosikiliza kero za Wananchi na kuzishughulikia kwani ipo karibu zaidi na Wananchi na ndio sababu ya yeye kufika Kijijini hapo ili kuona namna bora ya kutatua changamoto hiyo na kuweka utaratibu jinsi shamba hilo litakavyotumika.

"Wizara inalichukua suala hili ikalitolee maamuzi, Wananchi wavute subira wakingoja Serikali itoe ufafanuzi juu ya suala hili, ni marufuku mwananchi yeyote kuvamia na kufanya shughuli za kilimo ama ufugaji kwa sasa hadi hapo Serikali itakapotoa maelekezo mapya" alisema Mh. Nasha.

Mh. Waziri pia akatoa wito kwa wafugaji wa maeneo hayo kuacha tabia ya kukata miti hovyo, kwani kwa kufanya hivyo kwani wanaharibu mazingira na watapelekea eneo lake kuwa jangwa, akawasisitiza kufuga ufugaji wa kisasa kwa kufuga madume ya kisasa, kupunguza wingi wa mifugo ili uendane na malisho waliyonayo, ukubwa wa eneo na kuendana na mabadiliko ya tabia nchi, kuitumia mifugo yao kujiendeleza kiuchumi kama kuwasaidia kujenga makazi bora na kushiriki kuchangia shughuli za maendeleo.


MKUU WA MKOA AELEKEZA HALMASHAURI YA SINGIDA KUHAMIA ILONGERO NDANI YA KIPINDI CHA MIEZI SITA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


Mkuu wa Mkoa wa Singida Mheshimiwa Mhandisi Mathew John Mtigumwe amemtaka Mkuu wa Wilaya ya Singida kusimamia utekelezaji wa maamuzi ya kuhamishia makao makuu ya halmashauri ya Singida katika mji mdogo wa Ilongero ndani ya kipindi cha miezi sita  ili kusogeza huduma karibu na wananchi wa halmashauri hiyo.
Mheshimiwa Mhandisi Mtigumwe amefikia uamuzi huo kutokana na taarifa za kuwepo watu wachache wanaotaka kufanya mabadiliko ya makao makuu bila ya kusikiliza mawazo ya wananchi wengi huku wananchi wakipendelea makao makuu ya halmashauri hiyo kuwa katika mji mdogo wa Ilongero.
Ameongeza kuwa baraza la madiwani la halmashauri ya Singida linapaswa kuketi tena na kufanya maamuzi sahihi kwa maslahi ya wananchi wengi huku akiongeza kuwa endapo wanataka kufanya mabadiliko wayafanye wakiwa tayari wameshahamia katika halmashauri yao tofauti na sasa ambapo bado ofisi zipo manispaa ya Singida.
Mheshimiwa Mhandisi Mtigumwe amesema wananchi wanataka kupatiwa huduma kwa ukaribu hivyo halmashauri kuhamishiwa Ilongero itasaidia kusogeza Huduma ambapo zitatolewa kwa ufanisi huku akimshauri Mkurugenzi wa halmashauri hiyo kujipanga ndani ya kipindi hicho waanze kutumia ofisi chache zilizopo.
Aidha Mheshimiwa Mhandisi Mtigumwe amewataka wananchi wa halmashauri na Mkoa mzima wa Singida kujituma na kufanya kazi kwa bidii, wakulima wajiandae FEMA kwa msimu huu wa kilimo na kujitahidi kutunza vyakula ili kujiepusha na njaa na wafanyabiashara watumie fursa mbalimbali kujiongezea kipato.
Naye Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida Martha Mlata amesema chama hicho mkono mapendekezo ya wananchi yakutaka makao makuu kuwa katika mji mdogo wa Ilongero na kuahidi kufuatilia na kusimamia utekelezaji wake.
Katika kuunga mkono mapendekezo ya wananchi Mbunge wa jumbo la Singida kaskazini la kaskazini Mhe. Lazaro Nyalandu amesema kufikia mwezi Januari ataweka ofisi za Mbunge katika mji wa  I'll wananchi wapate Huduma na kumfikishia kero kwa ukaribu zaidi.

Uongozi bora na matumizi bora ya fedha vimeiletea Tanzania maendeleo

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.



Na. Lilian Lundo – MAELEZO

Dar es Salaam

28.11.2016

IMEELEZWA kuwa Uongozi bora na matumizi bora katika usimamizi wa fedha za Serikali ni miongoni mwa sababu zilizoiletea Tanzania maendeleo tangu ilipopata uhuru mwaka 1961.

Hayo yamebainishwa leo Jijini Dar es Salaam na Spika Mstaafu, Pius Msekwa wakati wa mahojiano maalum na mwandishi wa habari hii kuhusiana na hatua ambazo Tanzania imepiga tangu ipate uhuru mwaka 1961.

Msekwa alisema kuwa uongozi bora pamoja matumizi bora ya fedha ndizo nguzo kuu zilizoiletea Tanzania maendeleo yanayoonekana leo ambapo takribani sekta zote zimepiga hatua kubwa ukilinganisha na kipindi cha uhuru mwaka 1961.

“Wakati tunapata uhuru mwaka 1961 tulirithi vitu vichache kutoka kwa wakoloni ambavyo ni shule hospitali ya Muhimbili iliyokuwa ikijulikana kama Princess Magreth ambayo kwa sasa imepiga hatua na kuweza kufanya upasuaji wa moyo ambao haukuwahi kufanyika kwa miaka ya nyuma,” alifafanua Msekwa.

Alisema kuwa maendeleo yote hayo yametoka na juhudi za marais waliopita na aliyepo, katika uongozi wao ambapo wamekuwa wakipambana na maadui watatu wa maendeleo ambao ni ujinga, maradhi na umasikini.

Aidha alisema kuwa viongozi hao wamekuwa wakipambana na maadui hao kulingana na fedha ambazo zimekuwa zikipatikana katika kipindi cha uongozi wao.

Msekwa aliwataka Watanzania kuendelea kumuenzi Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kutokana na misingi aliyoiacha ambayo imeweza kutumiwa na viongozi wa nchi na kuendelea kuleta maendeleo ambayo Tanzania inajivunia hadi sasa.

SINGIDA YATEKELEZA AGIZO LA RAIS LA USAFI WA MAZINGIRA KIKAMILIFU

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.



Na Evelyn Mkokoi – Singida
Katika kutekeleza agizo la Serikali la usafi wa mazingira kila Jumamosi ya Mwisho wa Mwezi, wananchi wa Mkoa wa Singida wamejitokeza kwa kwingi katika zoezi hilo lililofanyika kitaifa mwezi huu mkoani humo.
Akishiriki zoezi hilo  Mkoani Singida kitaifa, Naibu waziri Ofisi ya Makamu w Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina, ameupongeza uongozi wa Mkoa wa Singida na wana  singida kwa ujumla kwa jitihada walizoonyesha kwani kila eneo la Singida Jumamosi ya leo Limeonekana kuwa nadhifu kabla hata ya muda wa kuanza kufanya usafi tofauti na mikoa mingine ambayo amewahi kushiriki zoeZi hilo.
Akiongea na Hadhara iliyojitokeza katika siku ya usafi Mjini Singida Leo, Mpina alisema kuwa usafi wa mazingira  unapunguza magonjwa yatokanayo na uchafu akitolea mfano ugonjwa wa kipindu pindu na hivyo taifa likiwa safi litaweza kuokoa ngumukazi yake, na kupunguza gharama ambazo zingetumika kutibu maradhi hayo.
“Ukiona Msichana mzuri barabarani ujue kagharamiwa ukiona kijana mtanashati vilevile ujue kagharamiwa Mkiona taifa zuri na safi ujue limegharamiwa na wananchi wake wamejipanga vizuri, hivyo wana singida Muendelee kujitahidi katika suala zima la usafiwa mazingira.” Alisisitiza Mpina.
Zoezi la usafi wa Mazingira Mkoani Singida lilienda sambamba na zoezi la upandaji miti ambapo, Naibu Waziri Mpina Pia alishiriki  na wananchi katika zoezi la kupanda miti mkoani Singida ambapo alipanda mti aina ya mpararachichi katika eneo la stand mpya ya Misuna.

WAMILIKI WA LESENI ZA UCHIMBAJI MDOGO WA MADINI MKOANI SINGIDA WAMETOZWA FAINI YA SHILINGI MILIONI 20 KWA UHARIBIFU WA MAZINGIRA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 





Na Evelyn Mkokoi-Singida
Wamilki wa Leseni za uchimaji mdogo wa madini wa Joshua Mine na Sekeknke one mine wa Sekenke Mkoani Singida, wametozwa faini ya shilingi milioni 10 kila moja kwa kosa la uchafuzi wa mazingira wa kutumia vibaya madini ya zebaki, hivyo kuhatarisha maisha ya viumbe hai.
Baraza la taifa la Hifadhi na usimamizi wa Mazingira limeitoza faini hiyo kupitia mratibuwa wa Barazakanda a Ziwa Bw. Jamali Baruti na kiwataka wamiliki hao kulipa faini hiyo ndani ya siku 14.
Adhabu hiyo inatokana na makelele katika eneo la uchimbaji, kusambaa kwa vumbi lisilovumilika, kukosekana kwa vyoo pia na matumizi mabaya ya miti katika uchimbaji wao ambao huenda sambamba na uharifu wa misitu.
Aidha Baraza limewataka wachimbaji hao kuwa na vyeti vya tathmini ya athari ya mazingira pamoja na leseni ya uchimbaji.
Kwa Upande wake Mkuu wa Wiaya ya Mkalama Injinia Joakim Masakala  akimuwaklisha mkuu wawiaya ya Iramba, alisema kuwa ni vizuri wakazi wa maeneo hayo wanavyojibidisha katika kazi lakini ni muhimu sana kuzingatia afya kwani uchimbaji wa kutumia madini aina ya zebaki bila vifaa salama kazini unaweza kuleta maradhi hususan ya saratani kwani madini hayo upenya kirahisi katika mwili wa binadamu.
Awali Katika Kikao na uongozi wa Mkoa pamoja na wadau wa Mazingira Naibu Waziri Mpina alitolea ufafanuzi masuala mbalimbali ya Mazingira ikiwemo matumizi ya Mifuko ya plastic na kuwashauri wakazi wa singida kutunza mazingira akitolea mfano wa ziwa Kitangiri lililoo Hatarini kutoweka kabisa.
 
 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2011. Singida Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogz za Mikoa